Uahirishaji wa kesi ni chanzo cha kupoteza muda na fedha kwa wananchi

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
291
Je, kesi mahakamani inachukua muda gani hadi kusikilizwa? Hili ni suala linalomkabili mama mmoja mkazi wa Kawe ambaye alinunua kiwanja Mapinga kutoka kwa bodaboda mmoja anaemwamini. Hata hivyo, alipokwenda kuangalia ardhi hiyo, aligundua kwamba kuna mtu tayari ameshaanza kujenga, na baadaye akapata habari kwamba waliomuuzia ardhi hiyo hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

Mama huyo na mwenzake waliamua kupeleka malalamiko yao kituo cha polisi, na baada ya wiki tatu, mtuhumiwa mmoja alikamatwa na kufikishwa mahakamani. Hata hivyo, mchakato wa kesi umekuwa ukisuasua, na baada ya kuenda mahakamani mara kadhaa, mama huyo aliamua kuomba kesi yake isikilizwe katika jimbo la Kawe.

Tarehe 14/06/2023, kesi yake ilisomwa kwa mara ya kwanza, lakini tangu wakati huo, imekuwa ikicheleweshwa mara kwa mara na anamatumaini kesi yake kusikiliza tarehe 06/02/2024. Hata alipojaribu kuwa na mashahidi, mchakato ulionekana kusuasua zaidi. Hali hii imemlazimu kutumia gharama kubwa kwa mawakili na usafiri, na kuongeza hasara ya muda wake na fedha.

Ni wazi kuwa kuchelewesha kesi hii kunaleta changamoto kubwa kwa wananchi na inawakatisha tamaa. Hali hii inaweza kusababisha watu kuchukua sheria mkononi mwao, jambo ambalo linaweza kuleta machafuko na kutoaminiana katika jamii.

Kwa hiyo, ni muhimu kwa mahakama kuboresha michakato yake ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha kuwa kesi zinasikilizwa kwa wakati. Hii itasaidia kurejesha imani ya wananchi katika mfumo wa mahakama na kuzuia hali ya watu kuchukua hatua zisizo halali.
 
Back
Top Bottom