Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Sihitaji kuulizwa kwa nini nimewapendekeza hawa manguri kutuongoza wana JF lakin naomba kwa kweli mtuongoze maana mpo kimya sanaaa tangu hukumu imetolewa mpaka sasa hivi hatuwaoni hata maoni yenu.

Tafadhali wana JF ni vyema tumchangie ndugu Melo hasifungwe kwa makosa yetu si jambo la busara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah Melo amehukumiwa mwingine kaachiwa
Haiingii akilini
Mike uje utupe maelezo how and why! Lipo jambo tusilolijua
Pole Melo - Tunaomba muongozo wa kuchangia

Kwa nini mnasema 'Aliyekuwa Mkurugenzi? Nani Mkurugenzi sasa?! JF haiko tena kwani
Ulipo Melo nasi tutakuwepo
New JF iko pande ipi???
 
Hapa tayari kagiza kashaingia ukichangia kushoto kushoto kinanuka chapu duuuh!! Embu Jf futeni kila hoja tuanze upya maana tushamchana sana "hedi boy humu" sasa kwenda jela na haya ma korona hatari sana
 
Naomba mtujibu kwani hukumu tayari? Mbona mtoa mada haelezei kwa kirefu? Kama hukumu tayari vipi imekuwaje? Kifungo? Faini? au vyote kwa pamoja?
 
Milioni 70+ au miezi 5 jela,then milioni 3 au mwaka mmoja jela....😳ila mambo ya kisheria cyajui sana...akili yangu ndo imenifikirisha hivyo....
Sasa hivi tuna revenue authorities tatu namely Mahakama ya Kisutu, police Tanzania especially traffic police na TRA yenyewe. Tz lazima ipae
 
Naomba mtujibu kwani hukumu tayari? Mbona mtoa mada haelezei kwa kirefu? Kama hukumu tayari vipi imekuwaje? Kifungo? Faini? au vyote kwa pamoja?
samahani mkuu hukumu tayari max mello yupo sero mpaka ilipwe 3m au jela mwaka mmoka mkuu mimi nipo tayari kuchanga nasubiri mwongozo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba tujadili nini itakuwa implication ya hukumu iliyotolewa leo dhidi ya Mkurugenzi wa JamiiForums bwana Melo kwa mtandao huu wa JamiiForums na watumaji wake kwa siku za usoni na iwapo ni muhimu kukata rufaa.

Wanasheria tusaidiane.
 
Back
Top Bottom