Kauli ya Zitto kuhusu yaliyotokea Arusha

Ndugu wana JF,

Tangu Raia wema wa Arusha waanze kudai haki yao jana asubuhi na kupelekea viongozi kadhaa wa juu wa chama hicho kuswekwa ndani sijamsikia Zitto Kabwe akiongea chochote, je yuko nchini au bado anasheherekea sikuku za christmass na Mwaka mpya?

Zitto hawezi kujiunga kwenye upuuzi walio fanya viongozi wenzake wa kutotii sheria, amejiamulia kula zake samaki mwanza huku akipunga upepo pale Tilapia
 
plastic mind wewe.

Umeolewa na mafisadi nini?
 
Ndugu zangu,
Tunalaani matumizi ya ovyo ya nguvu za dola
Kwa mara nyingine tena, jana Jumatatu tarehe 05 Januari 2010, Jeshi la Polisi lilivuruga na kusambaratisha mkutano halali wa hadhara uliondaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha. Katika kuvuruga na kusambaratisha mkutano huu, jeshi la polisi liliua na kuwaumiza vibaya baadhi ya wananchi. Miongoni mwa wananchi walioumizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe, mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA mama Josephine Slaa. Wengi wa wananchi walioumizwa ni watoto na akina mama. Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu, liliwafuata na kuwakamata Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini Mhe Philemon Ndesamburo wakiwa katika Hoteli ya Mount Meru. Wabunge hawa wamedhalilishwa na jeshi la polisi bila kujali kinga ya bunge walio nayo.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi ya ovyo ya vyombo vya dola. Tunalaani Jeshi la Polisi kuendelea kukubali kutumiwa na wanasiasa katika kuficha udhaifu wao wa kisiasa na kiuongozi. Serikali hii imeshindwa kudhibiti ujambazi nchini kwa kisingizio kuwa haina askari na vifaa vya kutosha, lakini wana askari kedekede na vifaa lukuki vya kudhibiti na kuua wananchi wasio na hatia kwa sababu tu wanaonyesha mapenzi yao kwa vyama vya upinzani badala ya chama tawala. Jeshi la Polisi limeendelea kuvunja sheria kwa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani. Badala ya kutoa ulinzi katika mikutano ya hadhara, jeshi la polisi limegeuka kuwa watoa vibali!

Watawala na jeshi la polisi watambue kuwa hakuna nguvu ya risasi itakayoshinda nguvu ya umma inayotaka mabadiliko, na wala CCM haitaweza kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya risasi. CHADEMA tutaendelea na juhudi za kuhamasisha wananchi kudai haki zao za kidemokrasia, ikiwemo kuwajibisha viongozi waliowachagua kuwaletea maendeleo. Matumizi mabovu ya nguvu za dola kunakofanywa na watawala wa CCM ni ushahidi mwingine muhimu wa kwa nini tunahitaji Katiba Mpya kwa haraka iwezekanavyo.

Katika kipindi hiki kigumu, tukiendelea na juhudi za kuwatoa nje viongozi waliowekwa ndani kwa udhalimu, ninawaomba wananchi, wapenzi na wanachama wa CHADEMA wawe wastahimilivu na waendelee na shughuli zao. CHADEMA tutahakikisha haki inatendeka na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya askari waliosababisha maafa yaliyotokea.

Zitto Zuberi Kabwe (Mb)
Naibu Katibu Mkuu (Bara)-CHADEMA
Nimetoa kauli hii Mwanza saa 1300hrs
 
JE INATOSHA?
 
Good one Zitto hongera...

lakini nina wasiwasiwasi sana, umetoa kauli kama zitto badala ya kuwasemea wenzako walio ndani... imekusoma nikajisikia kwamba bado hujaiva kwenye team or collectiveness

... hebu turudi kule PPF tugawane zile pesa ulizofaidi:hat: naskia ulikodishiwa ndege
 
Tunalaani matumizi ya ovyo ya nguvu za dola

Kwa mara nyingine tena, jana Jumatatu tarehe 05 Januari 2010, Jeshi la Polisi lilivuruga na kusambaratisha mkutano halali wa hadhara uliondaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha. Katika kuvuruga na kusambaratisha mkutano huu, jeshi la polisi liliua na kuwaumiza vibaya baadhi ya wananchi. Miongoni mwa wananchi walioumizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe, mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA mama Josephine Slaa. Wengi wa wananchi walioumizwa ni watoto na akina mama. Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu, liliwafuata na kuwakamata Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini Mhe Philemon Ndesamburo wakiwa katika Hoteli ya Mount Meru. Wabunge hawa wamedhalilishwa na jeshi la polisi bila kujali kinga ya bunge walio nayo.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi ya ovyo ya vyombo vya dola. Tunalaani Jeshi la Polisi kuendelea kukubali kutumiwa na wanasiasa katika kuficha udhaifu wao wa kisiasa na kiuongozi. Serikali hii imeshindwa kudhibiti ujambazi nchini kwa kisingizio kuwa haina askari na vifaa vya kutosha, lakini wana askari kedekede na vifaa lukuki vya kudhibiti na kuua wananchi wasio na hatia kwa sababu tu wanaonyesha mapenzi yao kwa vyama vya upinzani badala ya chama tawala. Jeshi la Polisi limeendelea kuvunja sheria kwa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani. Badala ya kutoa ulinzi katika mikutano ya hadhara, jeshi la polisi limegeuka kuwa watoa vibali!

Watawala na jeshi la polisi watambue kuwa hakuna nguvu ya risasi itakayoshinda nguvu ya umma inayotaka mabadiliko, na wala CCM haitaweza kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya risasi. CHADEMA tutaendelea na juhudi za kuhamasisha wananchi kudai haki zao za kidemokrasia, ikiwemo kuwajibisha viongozi waliowachagua kuwaletea maendeleo. Matumizi mabovu ya nguvu za dola kunakofanywa na watawala wa CCM ni ushahidi mwingine muhimu wa kwa nini tunahitaji Katiba Mpya kwa haraka iwezekanavyo.

Katika kipindi hiki kigumu, tukiendelea na juhudi za kuwatoa nje viongozi waliowekwa ndani kwa udhalimu, ninawaomba wananchi, wapenzi na wanachama wa CHADEMA wawe wastahimilivu na waendelee na shughuli zao. CHADEMA tutahakikisha haki inatendeka na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya askari waliosababisha maafa yaliyotokea.

Zitto Zuberi Kabwe (Mb)

Naibu Katibu Mkuu (Bara)-CHADEMA

Nimetoa kauli hii Mwanza saa 1300hrs

JE INATOSHA?

Bado we need more

Hii kauli haina kitu tunataka kuokoa taifa la tanzania ZID YA MAJAMBAZI
NA MIMI NAWEZA KUTOA KAULI
 
bado anahitajika zaidi na hongera kwa kuwa ulikuwa mwanza kuhamasisha ushindi wa umeya na sasa tunataka uwe wazi zaidi tunataka uje dar ufanye mkutano mkubwa au musoma
 
Sijui PPF, Sijui Kutubu, sio masuala muafaka kwa sasa. Suala la muhimu ni kuwa tuwe pamoja kupambana katika kipengele hiki cha vita dhidi ya ufisadi. Nakuunga mkono Zitto...
 
Ahsante Mh Zitto, tunakushukuru pia kwa kusaidia kupatikana Mameya wa Chadema kanda ya ziwa kwa mara ya kwanza, tunaomba huu uwe mwanzo wa halmashauri nyingine kuiga mfano wa Mwanza
 
ulikuwa wapi mkuu jana ? sikukuona kwenye libeneke! au ulikuwa unasubiri kutoa tamko ili watu warudishe matumaini walipoteza kwako? anyway tumekusikia mwayego
mix with yours
 
Back
Top Bottom