Kauli ya Zitto kuhusu yaliyotokea Arusha

Big up Zitto. Welcome on board.

Kama ungeonyesha negative response katika hili basi Wana-CHADEMA tungendelea kuamini kuwa wewe ulishakuwa mwasi.

Lakini let me put a question to you ,Mr. Zitto Zuberi Kabwe.Were you in Arusha yesterday during this saga? If yes how did you escape the police thugs?And if not, why not in Arusha to join your CHADEMA Leaders and colleagues in order to demonstrate a party unit?

Otherwise thanks for your good and encouranging thread.

Thanks.
 
Ni kauli nzuri kuwa nguvu ya umma haizuiliwi kwa risasi au kwa gilba za kisiasa!
 
Jamani this is pathetic kuona kwamba watanzania sasa hatuna uwezo wa kutatua tofauti zetu bila kutumia nguvu. IGP Mwema...matumizi ya dola kwa karne hii hayana nafasi tena.

Sitoi hukumu, Lakini Rais wetu na viongozi wengine wa taifa letu lazima waelewe, ukimwaga damu mara moja..ndo mwanzo wa machafuko. Jamani Polisi wafundishwe..kazi yao ni kulinda USALAMA wa raia. Sasa wakikubali kutumiwa na wanasiasa kama anavyosema mh. Zitto. Tunaelekea kwenye "polisi state".

Cha muhimu Serikali IACHE KUTOA MAJIBU RAHISI KWA MASWALI MAGUMU. Haiwezekani tuambiwe kwamba serikali inajiandaa kulipa Billions kwa DOWANS wakati wananchi hawana umeme na wanalala njaa. Kwa mwendo huu..Tujiandae kuelekea kwa machafuko makubwa. Viongozi wanahitaji kutoa majibu maridhawa. Hii siyo swala la Slaa, Zitto au Mbowe. Watanzania wote tunahitaji serekali makini. hata kama sio CHADEMA watakuja wengine.....its simple as that. Huwezi kuweka vichwa million 40..kama wajinga forever. People are simply TIRED.

Otherwise, watapiga mabomu mpaka Ocampo arudi. The world has changed, so should our government. Tuache kudhani kwamba karne hii utanyamazisha legitimate voices kwa kutumia mabomu ya machozi au kuua watu. Hata kama akitoka Slaa au Mbowe..still wanaoumia ni wananchi kwa utawala usio na vision. We need strong and understanding government. Na hapa ndo true colours za TZ kama kisiwa cha amani zinapoonekana...

Poleni watanzania wenzangu.

Ila mmukumbushe RPC na IGP Mwema. Siku hizi kuna Ocampo ambaye anaweza kudeal na wale wanaoogopwa na serikali yetu. Forewarned, is forearmed armed!
 
Polisi wa tanzania ni kama mbwa. Sheria iko wazi na waandamanaji hawakuwa na silaha kwa nini wakimbilie kuwachanganya? Tunashukuru mh.zito. Lakini badonawaomba watanganyika tuungane tudai uhuru wetu wa kweli. Polisi wote wanaotetea uovu wa aina yo yote mwenyezi mungu awalaani na wakose amani siku zote.
 
Kuna mtu kanisms kuwa wabunge waliokuwa Arusha ni watu wa kaskazini tu je, hili linaukweli? Zitto kwa nini mara kadhaa ukosekana kwenye matukio ya Chadema yanayogusa isia za watu wengi?
 
Katika kipindi hiki kigumu, tukiendelea na juhudi za kuwatoa nje viongozi waliowekwa ndani kwa udhalimu, ninawaomba wananchi, wapenzi na wanachama wa CHADEMA wawe wastahimilivu na waendelee na shughuli zao. CHADEMA tutahakikisha haki inatendeka na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya askari waliosababisha maafa yaliyotokea.
Jana tuliambiwa maandamano hayata koma hivyo nilitegemea huko kigoma, Mbeya, Dar,Mwanza, Moshi nk ungeitisha maandamano!?, na watu huku Arusha wanasubulia pamoja na kwamba wameongeza ulizi wa wilaya zote na mkoa jirani...
 
Tunalaani matumizi ya ovyo ya nguvu za dola

Kwa mara nyingine tena, jana Jumatatu tarehe 05 Januari 2010, Jeshi la Polisi lilivuruga na kusambaratisha mkutano halali wa hadhara uliondaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha. Katika kuvuruga na kusambaratisha mkutano huu, jeshi la polisi liliua na kuwaumiza vibaya baadhi ya wananchi. Miongoni mwa wananchi walioumizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe, mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA mama Josephine Slaa. Wengi wa wananchi walioumizwa ni watoto na akina mama. Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu, liliwafuata na kuwakamata Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini Mhe Philemon Ndesamburo wakiwa katika Hoteli ya Mount Meru. Wabunge hawa wamedhalilishwa na jeshi la polisi bila kujali kinga ya bunge walio nayo.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi ya ovyo ya vyombo vya dola. Tunalaani Jeshi la Polisi kuendelea kukubali kutumiwa na wanasiasa katika kuficha udhaifu wao wa kisiasa na kiuongozi. Serikali hii imeshindwa kudhibiti ujambazi nchini kwa kisingizio kuwa haina askari na vifaa vya kutosha, lakini wana askari kedekede na vifaa lukuki vya kudhibiti na kuua wananchi wasio na hatia kwa sababu tu wanaonyesha mapenzi yao kwa vyama vya upinzani badala ya chama tawala. Jeshi la Polisi limeendelea kuvunja sheria kwa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani. Badala ya kutoa ulinzi katika mikutano ya hadhara, jeshi la polisi limegeuka kuwa watoa vibali!

Watawala na jeshi la polisi watambue kuwa hakuna nguvu ya risasi itakayoshinda nguvu ya umma inayotaka mabadiliko, na wala CCM haitaweza kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya risasi. CHADEMA tutaendelea na juhudi za kuhamasisha wananchi kudai haki zao za kidemokrasia, ikiwemo kuwajibisha viongozi waliowachagua kuwaletea maendeleo. Matumizi mabovu ya nguvu za dola kunakofanywa na watawala wa CCM ni ushahidi mwingine muhimu wa kwa nini tunahitaji Katiba Mpya kwa haraka iwezekanavyo.

Zitto Zuberi Kabwe (Mb)

Naibu Katibu Mkuu (Bara)-CHADEMA

Nimetoa kauli hii Mwanza saa 1300hrs

JE INATOSHA?
We mleta mada ndiye Zito? Ulishiriki maandamano na wenzio?
 
Thanks, ni meseji mhimu kwa sasa sent ila sasa tunahitaji a cordinated effort kwa timu yote chadema nchi haiwezi kukombolewa kirahisi lazima tusonge mbele kwa nguvu zaidi wajue wamewasha moto. Zitto alikuwa mwz ktk uchaguzi wa mameya, wenginr wako ,beya etc. Uko sawa na inatosha kwa sasa
 
Hatujui moyoni anawaza nini,lakini kauli hii inatia moyo!hongera Zitto!!
 
Jana tuliambiwa maandamano hayata koma hivyo nilitegemea huko kigoma, Mbeya, Dar,Mwanza, Moshi nk ungeitisha maandamano!?, na watu huku Arusha wanasubulia pamoja na kwamba wameongeza ulizi wa wilaya zote na mkoa jirani...

Inavyoonesha ZITTO hana uchungu na nchi

Huyu NIPO(MEMBER) NI KAMA M16 ALIYELETA HABARI ZA TUNDUMA ETI WAMEWASHIKILIA POLICE

Tunalaani matumizi ya ovyo ya nguvu za dola

Kwa mara nyingine tena, jana Jumatatu tarehe 05 Januari 2010, Jeshi la Polisi lilivuruga na kusambaratisha mkutano halali wa hadhara uliondaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha. Katika kuvuruga na kusambaratisha mkutano huu, jeshi la polisi liliua na kuwaumiza vibaya baadhi ya wananchi. Miongoni mwa wananchi walioumizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe, mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA mama Josephine Slaa. Wengi wa wananchi walioumizwa ni watoto na akina mama. Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu, liliwafuata na kuwakamata Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini Mhe Philemon Ndesamburo wakiwa katika Hoteli ya Mount Meru. Wabunge hawa wamedhalilishwa na jeshi la polisi bila kujali kinga ya bunge walio nayo.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi ya ovyo ya vyombo vya dola. Tunalaani Jeshi la Polisi kuendelea kukubali kutumiwa na wanasiasa katika kuficha udhaifu wao wa kisiasa na kiuongozi. Serikali hii imeshindwa kudhibiti ujambazi nchini kwa kisingizio kuwa haina askari na vifaa vya kutosha, lakini wana askari kedekede na vifaa lukuki vya kudhibiti na kuua wananchi wasio na hatia kwa sababu tu wanaonyesha mapenzi yao kwa vyama vya upinzani badala ya chama tawala. Jeshi la Polisi limeendelea kuvunja sheria kwa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani. Badala ya kutoa ulinzi katika mikutano ya hadhara, jeshi la polisi limegeuka kuwa watoa vibali!

Watawala na jeshi la polisi watambue kuwa hakuna nguvu ya risasi itakayoshinda nguvu ya umma inayotaka mabadiliko, na wala CCM haitaweza kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya risasi. CHADEMA tutaendelea na juhudi za kuhamasisha wananchi kudai haki zao za kidemokrasia, ikiwemo kuwajibisha viongozi waliowachagua kuwaletea maendeleo. Matumizi mabovu ya nguvu za dola kunakofanywa na watawala wa CCM ni ushahidi mwingine muhimu wa kwa nini tunahitaji Katiba Mpya kwa haraka iwezekanavyo.

Katika kipindi hiki kigumu, tukiendelea na juhudi za kuwatoa nje viongozi waliowekwa ndani kwa udhalimu, ninawaomba wananchi, wapenzi na wanachama wa CHADEMA wawe wastahimilivu na waendelee na shughuli zao. CHADEMA tutahakikisha haki inatendeka na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya askari waliosababisha maafa yaliyotokea.

Zitto Zuberi Kabwe (Mb)

Naibu Katibu Mkuu (Bara)-CHADEMA

Nimetoa kauli hii Mwanza saa 1300hrs

JE INATOSHA?

NAKATAA HAYA SIO MANENO YA ZITTO

nAKATAA HAYA SIO MANENO YA ZITO

nAKATAA HAYA SIO MANENO YA ZITTO

Ndugu zangu,

Back
Top Bottom