Kauli ya Dr. Slaa kuhusu hoja za ccm Jangwani - CCM mna majibu ya tuhuma hizi??

WAKATI CCM, ikihaha kujaza watu kwenye mkutano wake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, amekidhihaki chama hicho kuwa hakiwezi kuendelea kutawala nchi kwa kuwalipia nauli, kuwabeba na kuwapa posho watu wanaokwenda kwenye mikutano.
Slaa, alisema ilani ya chama chochote makini inapaswa kuonekana machoni mwa wananchi na siyo kusemwa kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete na timu yake ndani ya CCM wanavyofanya.

Kauli hiyo aliitoa jana katika Uwanja wa Likangala wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati akihutubia mkutano wa hadhara, huku akitanabaisha kuwa wafuasi wanaokipenda chama chao hawawezi kubebwa na magari kwenda kwenye mikutano kwa kulipiwa nauli.
Dk. Slaa alikuwa akijibu matamshi mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa CCM katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na vituo vya redio na runinga.

Alisema mawaziri wa CCM wamekuwa makasuku kwa kushindwa kutathmini kauli zao za awali, ambazo hazijatekelezwa na kwamba sasa wanakuja na hoja nyingine zisizotekelezeka.

Akiwachambua baadhi ya mawaziri na kuanza na Jumanne Maghembe, alisema kuwa anapaswa akumbuke miaka zaidi ya kumi iliyopita serikali ilikuja na mkakati wa kilimo cha umwagiliaji na kusema imeshapata kiasi cha dola milioni 12 za Marekani kwa ajili ya shughuli hiyo.
“Tunataka watuambie hizi fedha zimeenda wapi mpaka sasa wanakuja na kauli nyingine, hivi hakumbuki tulikaa katika ukumbi wa mikutano wa Pius Msekwa wakatuambia hizi fedha zipo, sasa zimeenda wapi?” alihoji Dk. Slaa.
Kuhusu ujenzi wa barabara kilomita 11,000 zilizoelezwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Slaa alisema huo ni upuuzi kwa kufananisha hali hiyo na mahitaji mazima ya nchi.


Alisema fedha zilizoibwa na watumishi wa serikali ya CCM ni nyingi kuliko hivyo wanavyojinadi kuwa wamefanya, na kuitaka serikali ieleze dola milioni 1.5 zilizokutwa katika akaunti ya mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) zimefanyiwa nini.

Alibainisha kuwa, Serikali ya CCM inapaswa kutolea maelezo fedha za chenji ya rada zimefanya nini wakati katika mahesabu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hazionekani kutumika.

Kuhusu kauli ya Steven Wassira kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe atalaaniwa kwa kuwa baba yake aligombea uhuru na Mwalimu Nyerere, Dk. Slaa alisema viongozi hao walisimama kwa ajili ya kuwatetea Watanzania na kama watasimama leo kuna hatari ya kuwachapa viboko viongozi wa CCM kwa kushindwa kuendeleza malengo waliyofikia.

Naye Mbowe alisema anamsikitikia Wassira kwa kile alichoeleza kuwa, anashindwa kusimamia hata utendaji wa nafasi yake na badala yake anahangaika kuropoka kila wakati mambo yasiyo na tija kwa taifa.
Alibainisha kuwa, Wassira si saizi yake kwenye majukwaa ya kisiasa kwa sababu hana hadhi ya kupigania ukombozi wa kweli, hivyo akamtaka awatafute watu wenye hadhi yake.

Alisema katika hali ya sasa, CCM haioni mahaba ya wananchi, hivyo wanajitahidi kukusanya watu katika maeneo mbali mbali ya nchi ikiwa ni pamoja na kununua kadi za CHADEMA kwa ajili ya kujiaminisha mbele ya wananchi.

“Hawa watu vipi, wana nini sijui kwa kuwa wanatunga uongo wanauaminisha umma na mwisho wa siku wanauamini huo uongo walioutunga kama ambavyo wamefanya leo kule Jangwani,” alisema Mbowe.

Source: Tanzania Daima


Sasa ndio naanza kuamini dokta feki wa dini ya ukatoliki anazeeka vibaya. Fedha ya rada ilirudi mwaka Jana mwishoni, hesabu za CAG ni za mpaka 30.06.2011, sasa hapo unategemea kweli zitakuwepo? zitakuwepo kwenye taarifa ya mwaka huu unaoishia 30.06.2012. Ni aibu kwa dokta feki kuongea uongo
 
CCM imezeeka....na mashabiki wake wakubwa ni wazee au vijana ambao hawafanyi kazi (wavivu) hivyo kuwa kama wazee tu in labor force.....ndio maana hawana nauli,hawana miamvuli,hawana nguo na kula ubwabwa kwao ni nadra.
Wapiganaji na hata viongozi wa CCM wenye akili wanashabakia mageuzi ya kweli that's why kwenye makazi ya viongozi wa nchi hii mbunge anatoka upinzani.
CCM kimekuwa chama cha ahadi ambazo zina overlap kila kukicha....NAPE anaifaya CCM mali yake na kupima umaarufu wake bila makada wenye mlengo wa LOWASSA.

Mkuu ikulu na ofisi za serikali zote ziko ilala, huko kuna mbunge wa upinzani? Acha kubwabwaja aisee ni aibu na unajiaibisha
 
Hivi ni akili yako.......
Sasa ndio naanza kuamini dokta feki wa dini ya ukatoliki anazeeka vibaya. Fedha ya rada ilirudi mwaka Jana mwishoni, hesabu za CAG ni za mpaka 30.06.2011, sasa hapo unategemea kweli zitakuwepo? zitakuwepo kwenye taarifa ya mwaka huu unaoishia 30.06.2012. Ni aibu kwa dokta feki kuongea uongo
 
Ama kwa hakika akutukanae hakuchagulii tusi,hivi nyie wanaCHADEMA hamuoni haya hata kidogo kila siku kufuatilia nyumanyuma kama mkia.Halafua nyie mmekuwa mkiiga mambo mengi lakini CCM HAWASEMI CHOCHOTE.KWA MFANO UZINDUZI WA MTANDAO WENU WA KUCHANGIA CHAMA,HAPO JE,MNAWEZA SEMA LOLOTE.VILEVILE NYIE MMEKUWA MKITUHADAA KUWA NYIE NIWAADILIFU,LAKINI NYIE SI LOLOTE SI CHOCHOTE MNAULOHO WA MADLAKA.HEBU TATHMINI PALE BUNGENI VYEO VYOTE MMEJIPA WENYEWE.HALAFU HUYU SLAA AMEKOSA SERA KABISA KWANI HIVI SASA AMEKUWA KAMA MWANAMKE MMBEYAAAA...KWANI HANA JIPYA.
 
Hizi ahadi mpya za "kujenga sukari" kama alivyosema mzee wa Gombe ziko kwenye ilani gani? Zile 99 zimesha tekelezwa au hizi ni maandalizi ya ahadi mpya kwa mwaka 2015?
angesema ile kauli ya pinda kuwa bei ya sukari isizidi sh 700 iliishia wapi ningemwelewa,
 
Uchafu umeanza kusafishwa ATCL,Usafiri wa treni jijini DAR kuanza...usafiri wa majini kati kupunguza foleni!!! BANdarini wajiandae rungu la MWAKYEMBE laja
 
Haya ndo matusi ya wanaccm CHADEMA SQURE jana!Na hili semeni pia


Zungumzia pia hawa wamepatikanaje hapo Jangwani, sometimes naona adui wa Dr.Slaa& CDM ni sisi wananchi pia, haiwezekani pamoja na kula hasara miaka yote bado kuna watu kama hawa. Am sor kuna mda huwa naona ni bora Dr.Slaa angebaki na family aka-enjoy maisha yaliyobaki, hawa watu wagumu sana kuelewa! Ila hapana, Keep on going Dr
 
Ama kwa hakika akutukanae hakuchagulii tusi,hivi nyie wanaCHADEMA hamuoni haya hata kidogo kila siku kufuatilia nyumanyuma kama mkia.Halafua nyie mmekuwa mkiiga mambo mengi lakini CCM HAWASEMI CHOCHOTE.KWA MFANO UZINDUZI WA MTANDAO WENU WA KUCHANGIA CHAMA,HAPO JE,MNAWEZA SEMA LOLOTE.VILEVILE NYIE MMEKUWA MKITUHADAA KUWA NYIE NIWAADILIFU,LAKINI NYIE SI LOLOTE SI CHOCHOTE MNAULOHO WA MADLAKA.HEBU TATHMINI PALE BUNGENI VYEO VYOTE MMEJIPA WENYEWE.HALAFU HUYU SLAA AMEKOSA SERA KABISA KWANI HIVI SASA AMEKUWA KAMA MWANAMKE MMBEYAAAA...KWANI HANA JIPYA.
mkuu kama sijakosea wewe ni wasira au lusinde maana mawazo yanafanana kabisa,any way kidumu chama cha ccm
 
Kilomita zaidi ya 11,000 kwa kipindi cha Kikwete tu ni upuuzi? huyu mzee kweli hamnazo.

Amesha jiuliza, Mkoloni, Nyerere, Mwinyi na Kikwete na yeye akiwemo hukohuko kabla ya ujio wa Kikwete walitengeneza kilo mita ngapi? jumlisha zote pamoja na za Slaa, uone kama zinafika hata nuzu za hii miaka 7 tu ya Kikwete.

Kumbuka, ukitoa mkoloni, Nyerere miaka 24 KM ngapi? Mwinyi (na Slaa akiwepo)? Mkapa ngapi? Kiwete zaidi ya KM 11,000.

Amma kweli akutukanae hakuchagulii tusi.

Aisee wee mpuuzi wa kipekee.

Ebu tueleze hapa hizo km 11,000 zimeanzia wapi hadi wapi mwaka gani? Hizi barabara kwa taarifa yako ni matokeo ya ujenzi ulioanza enzi za mwinyi na prof lipumba kukubali masharti ya imf. Mkapa akaja kuutekeleza kwa sera ya uchukuzi 2003 na miradi ya TSIP iliyofuatia. Kukamilika kwa miradi hii ni wakati wa kilaza wako JK.

Ubaya wako unafikiri na unatuamisha upuuzi ambao baadhi yetu tuna taarifa kuliko wewe. Pili hao wapuuzi wako ccm wengehesimu ushauri wa wataalamu kwa asili mia 1 tu katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara, nchi nzima ingekuwa na lami 2007. Hakuna kwa sababu fedha nyingi za miradi zinainufasha ccm kupitia kwa mawakala wake ambao imewapa madaraka kupitia mamlaka za uteuzi (mfano Mrema Tanroads)

Umeniudhi sana kwa uongo huu si muungwana hata chembe ni wa kupuuzwa
 
Kilomita zaidi ya 11,000 kwa kipindi cha Kikwete tu ni upuuzi? huyu mzee kweli hamnazo.

Amesha jiuliza, Mkoloni, Nyerere, Mwinyi na Kikwete na yeye akiwemo hukohuko kabla ya ujio wa Kikwete walitengeneza kilo mita ngapi? jumlisha zote pamoja na za Slaa, uone kama zinafika hata nuzu za hii miaka 7 tu ya Kikwete.

Kumbuka, ukitoa mkoloni, Nyerere miaka 24 KM ngapi? Mwinyi (na Slaa akiwepo)? Mkapa ngapi? Kiwete zaidi ya KM 11,000.

Amma kweli akutukanae hakuchagulii tusi.


Kwa taarifa yako, Mkapa peke yake kajenga bara bara nyingi kwa kiwango cha Lami tupilia mbali hizo 11,000 unazoambiwa na Magufulli. Ukitaka figures mwulize magufuli maana yeye ndiye alikuwa waziri kipindi hicho.
 
CCM ikifikia mnaanza kujibishana badala ya kufanya kazi basi siku zenu za kuishi uongozini zinahesabika. Kwahiyo badala ya kufanya kazi nyie mtazunguka kila mkoa Chadema ilikopita?

Radhia,
Nashindwa kuamini unayoandika kama ni wewe au kuna mtu anatumia ID yako. Nasema hivyo kwasababu siku si nyingi ulikuwa ukitetea sana hoja za CCM lkn sasa naona umeamua kuwa mkweli na kusema ukweli daima. Karibu sana kwenye ukombozi wa fikra za wananchi waliowengi.

Ni kweli kabisa, CCM isingekuwa chama cha kusubiri CHADEMA wabuni kitu fulani, ndipo nao huiga hicho hicho badala ya kuleta ufumbuzi wa matatizo yanayowakumba watanzania.

Radhia, Hongera sana kwa kuliona hilo.
 
binafsi huwa namkubali sana docta tangu akiwa ndani ya bunge na hata nje ta bunge..maghembe ni mtu mchafu sana na mbaya zaidi si mwanasiasa anatakiwa akae katika utendaji ndio maana anakuja na kauli za hovyo bila kujitathimini kwanza
anyway their end is so near
 
Ama kwa hakika akutukanae hakuchagulii tusi,hivi nyie wanaCDM hamuoni haya hata kidogo kila siku kufuatilia nyumanyuma kama mkia.Halafua nyie mmekuwa mkiiga mambo mengi lakini CCM HAWASEMI CHOCHOTE.KWA MFANO UZINDUZI WA MTANDAO WENU WA KUCHANGIA CHAMA,HAPO JE,MNAWEZA SEMA LOLOTE.VILEVILE NYIE MMEKUWA MKITUHADAA KUWA NYIE NIWAADILIFU,LAKINI NYIE SI LOLOTE SI CHOCHOTE MNAULOHO WA MADLAKA.HEBU TATHMINI PALE BUNGENI VYEO VYOTE MMEJIPA WENYEWE.HALAFU HUYU SLAA AMEKOSA SERA KABISA KWANI HIVI SASA AMEKUWA KAMA MWANAMKE MMBEYAAAA...KWANI HANA JIPYA.
 
Dkt. Slaa aliposema nikikosa urais nitakijenga chama walikuwa hawajaelewa,wanaacha kutekeleza ilani ya chama chao wanahaha kujibu hoja,wameshikwa pabaya wanatapatapa na hii M4C
mkubwa! Hoja zenyewe za moto,hazijibiki.chezea chadema wewee
 
Ukweli utajulikana tu waache waendelee na mipasho yao hawa nyinyiemu, unafanya mkutano huku unatangaza ya kuwa wasanii hawa watakuwepo. Je hao kuwepo kwao kunasaidia nini?

Tangu sasa nambatiza Mzee Wasira,Jina lake sasa ni Mzee Bomba Chafu
 
Huyu mzee sio saizi ya Mbowe ni saizi ya Rusinde.Ila tusimlaumu alitoroka kwa wenzie siku ya maonyesho,sasa anacho ongea ni saizi yake mzee Nyani Bomba chafu
 
Sosi: Tanzania Daima-one sided/biased/unprofessional Newspaper

Msemaji: Slaa-Kafilisika kisiasa,mahututi wa afya.
 
Dr kawashika pabaya nyinyiemu! Le hii ukimuuliza wassira na Nape walicho kiongea jangwani nina uhakika watakuja na habari nyingine kabisa kwnani uongo na uzushi ni kazi yao.

Wanaelewa ndo maana wateuriwa kuwakilisha wanaCCm kuelezea wanachowafanyia Watanzania. Kama walivyofanya ndivyo walivyoelekezwa/kutumwa wafanye.
 
Back
Top Bottom