Dkt. Nchimbi aonya viongozi wa CCM kuwavaa wa Serikali

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,822
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake.

“Hatuwezi kusimamia Serikali kwa kuwa tunawatukana tukana watu, wewe hapa, kwa nini, mshenzi sana wewe, ahaa hiyo mshenzi haipo katika Ilani ya CCM , lazima tuwaheshimu watumishi wa Serikali, tuongoze kwa weledi.”

Alisema Dkt. Nchimbi
---

NCHIMBII.png
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuael Nchimbi ni kama ametupa jiwe gizani akiwaonya baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotumia mamlaka yao kudhalilisha viongozi wa Serikali.

Bila kutaja majina, Dk Nchimbi amesema kumekuwa na utamaduni wa viongozi wa chama hicho kutoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali.

Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake.

Januari 15, mwaka huu, chama hicho kilitangaza kumteua Nchimbi aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri kushika nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya Daniel Chongolo kujiuzulu kwa madai ya kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Chama chetu kisikwepe wajibu wake wa kuisimamia Serikali, ni wajibu wa kikatiba na kikanuni. Sisi ndio tulichaguliwa na wananchi. Mkataba ni kati ya CCM na wananchi na mtekelezaji wa mkataba ni Serikali, lakini tusimamie bila kuwa na kiburi, tusimamie kwa weledi,’’ amesema.

Bila kutaja jina la mhusika anayetukana viongozi wa Serikali, Nchimbi alisema: “Hatuwezi kusimamia Serikali kwa kuwa tunawatukana tukana watu, wewe hapa, kwa nini, mshenzi sana wewe, ahaa hiyo mshenzi haipo katika Ilani ya CCM , lazima tuwaheshimu watumishi wa Serikali, tuongoze kwa weledi.”
 
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ....
Paul Makonda, hili tamko linakuhusu wewe bila shaka. Kumbuka ccm kwa sasa inamilikiwa na wenye chama chao (yaani watoto wa mjini). Kwa hiyo nyinyi wakuja mjitahidi kuwa makini aisee. Hakuna tena kufanya ile mikwara yako kuanzia sasa.
 
Ujumbe kwa Makonda
“Hatuwezi kusimamia Serikali kwa kuwa tunawatukana tukana watu, wewe hapa, kwa nini, mshenzi sana wewe, ahaa hiyo mshenzi haipo katika Ilani ya CCM , lazima tuwaheshimu watumishi wa Serikali, tuongoze kwa weledi.”
Nda
 
Sasa hivi watabadilika kuwa hawana Imani na Nchimbi hahahaha
 
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake...
Yupo jamaa fulani alikuwa Benchi ile kuingia tu anamwagiza Eti Waziri Mkuu amalize Migogoro ya Ardhi

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake...
Wa Chato inamhusu
 
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake..
Paka kafungwa kengele, whooooiiiii. Ni ahueni.
 
Bashite ni mjinga sana, hajui utofauti wa uongozi wa kichama na serikali. Alafu eti ndio atake mdahalo na akili kubwa CHADEMA

CHADEMA wamekosea sana kumpa masharti ya kuwa na mdahalo naye ni kama wamempa maujiko

Bashite hata mimi haniwezi ktk mdahalo na kama anataak aje hapa Jf tuweke mdahalo na mada iwe

NI HALALI KWA MDAU WA UCHAGUZI KUTEUWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI?
 
Nimeona DAB leo anamdhalilisha DED wa Pangani kwa Kweli haijakaa Poa kabisa hata kama nikutafuta Publicity ile imekuwa too Much ni Ushamba fulani ivi
 
Back
Top Bottom