Katibu wa BAKWATA Arusha alipuliwa bomu

RadioOneStereo


Breaking News:Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha ABDULKARIM CHONJO amejeruhiwa vibaya na amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru baada ya nyumba yake kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu usiku wa kuamkia leo

Asante Zanta sijasikia hii ya Radio One, basi kumbe taarifa zangu zitakuwa sahihi.
Thanks again for updates
 
Wall ya EATV kule facebook nao wanadai kuwa ni kweli huyo katibu amejeruhiwa baada ya nyumba yake kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa ni bomu
 
niko arusha ni kweli tukio hilo ni talk of the town leo na watuhumiwa na waislamu wenzake wenye siasa kali ambao kwa muda mrefu sasa "wameuteka kioungozi" msikiti mkuu wa Ijumaa wa mjini Arusha walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na Katibu huyo wa Bakwata hadi kupelekena na polisi na mahakamani zaidi tutaendelea kuwajuza
 
Kwani hao viongozi wanapatikanaje?kwa kuchaguliwa au wanateuliwa.Kama wanachaguliwa kwa nini wasiombe uchaguzi ili wawachague viongozi wanaowataka.Sasa wakiwaua au kuwaumiza itawasaidia nini sasa
 
Get well soon katibu, bila shaka watakuwa wafuasi wa sheikh ponda, maana ni maadui wa bakwata.
 
niko arusha ni kweli tukio hilo ni talk of the town leo na watuhumiwa na waislamu wenzake wenye siasa kali ambao kwa muda mrefu sasa "wameuteka kioungozi" msikiti mkuu wa Ijumaa wa mjini Arusha walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na Katibu huyo wa Bakwata hadi kupelekena na polisi na mahakamani zaidi tutaendelea kuwajuza

Asante sana mkuu kwa updates na kwakuwa uko Arusha endelea kutuarifu kinachotokea huko.

Bahati mbaya sana tukio hili linakuja siku moja kabla ya Eid el Hajj.
 
Tusubiri tamko la Shehe mkuu wa Bakwata kuhusu kadhia hii. Au ndio yupo safarini Kilimanjaro kuhudhuria swala ya Eid kitaifa?
 
Katibu wa BAKWATA mkoani Arusha bwana AbdulKarim Jonjo usiku wa kuamkia leo amelipuliwa kwa bomu nyumbani kwake eneo la Esso jijini Arusha hivi sasa yuko hoi katika hospitali ya Mount Meru.

Chanzo: Wapo Radio

Nimesikia kwenye uchambuzi wa magazeti asubugi kuwa huko huko Arusha kuna vijana wametekwa na kukatwa masikio na kisha kutishiwa kuwa Shehe wao atauawa kwenye ugomvi wa kugombea msikiti wa Mianzini kama sio Kichangani, ni sakata hili hili au jingine?

Kweli hii ni dini ya amani.
 
Walaaniwe wote wanaofanya fujo!wanaovuruga amani ya nchi,wanaofanya chokochoko,waleta fitna,wanaowapiga mabomu watu wakiwa wamelala,wanaoteka nyumba za ibada,wasiofuata utaratibu na waliokosa aibu wote.amin!
 
Mkuu sosoliso tunashukuru kwa dodoso hii kwani wengine wangeanza kuunganisha hili tukio la arusha na matukio yalitokea dar kati ya kanisa na msikiti kitu ambacho ni tofauti kabisa. ni wazi kwamba huu ni mgogoro wao wenyewe kwa wenyewe na ni muendelezo wa chuki za ndani
Hii issue ya Arusha inahusu makundi mawili yanayogambania Msikiti na mali zake.. Na ni mgogoro wa muda mrefu ambao Serikali Mkoani Arusha walikuwa wanaudharau.. Leo umefikia hapo kulipuana na mabomu.. Viongozi wa usalama wa mkoa wa Arusha wanaendelea na kazi zao..! Hii nchi haina neno la uwajibikaji kwenye kamusi yake.. Damn..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom