Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza majeruhi wote waliotokana na ajali iliyoua watu 25 mkoani Arusha watibiwe bure
Dkt Godwin Mollel amesema hayo leo Februari, 25, 2024 alipowajulia hali majeruhi wa ajali hiyo iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, Mkoani Arusha waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru.
Dkt. Mollel amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja ndo kapewa Rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC Mkoani Moshi.
"Rais Samia Suluhu Hassan ametuelekeza majeruhi wote wa ajali hii kupatiwa matibabu bila kulipa gharama zozote"
Dkt. Mollel ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu wakati wakiendelea kuwatibia majeruhi na kwa wale waliopoteza ndugu zao utaratibu wakupatiwa miili unaandaliwa na wataalamu.
Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 25 na majeruhi 21.
Credit - EastAfricaTV