Wakuu magamba yanazidi kupata moto. Katibu mwenezi wa vijana wilaya ya Longido Ndugu YOHANA LAIZER ameamua kuhama ccm na bado hajaweka wazi atajiunga na chama gani. Katibu huyo anadai kachoshwa na magamba kuchanganya siasa na mila.
Pia anadai magamba wamekuwa wakidanganya wananchi kuwa alama nyekundu iliyopo kwenye bendera ya CDM inaonyesha kuwa ni chama cha hatari hivi wasijiunge nacho.
Pia imefika mahali wanatumia viongozi wa jamii ya Kimaasai kuwalaani watakaojiunga na Upinzani. Chanzo mahojiano na Sunrise Radio. Na bado!! Nawasilisha!
Ni kweli kabisa...amejivua na amehamia CDM....imeoneshwa na ITV ktk kipindi ya Habari zilizotufikia...Lakini na washauri waCDM kuwa na makini sana na hawa jamaa wanakuja na watakaoendelea kuja tena kwa speed...maana inawezekana ni janja ya wanamagamba kuujumu CDM...Nawasilisha