Katibu mwenezi wa CCM Longido ajivua gamba

Lakini mbona wanaojivua uanachama ni Arusha tu? Je kuna msukumo au nguvu " push strategy"? People's Power- tuwe makini, isije ikawa mkakati wa Raila Odinga, akiingia katika chama anaingia na watu wake, akitoka anatoka na watu na kukiacha chama kikiwa dhaifu kuliko mwanzo!!!!
 
Mwenye habari za uhakika plse tupe kuhusu diwani sombetini na longido

Maana imekaa vizuri hii

Lema bado hajamaliza mafungo hadi wiki ijayo
 
Lakini mbona wanaojivua uanachama ni Arusha tu? Je kuna msukumo au nguvu " push strategy"? People's Power- tuwe makini, isije ikawa mkakati wa Raila Odinga, akiingia katika chama anaingia na watu wake, akitoka anatoka na watu na kukiacha chama kikiwa dhaifu kuliko mwanzo!!!!

Mkuu Newazz, hata mimi nimekuwa nikijiuliza hilo na bado naendelea kutafakari. Au ndio katika mapambano ya raisi ajae hawezi kutoka kaskazini against lile suala la jina la raisi likoni mezani kwa mkulu?
 
Mkuu huyu jamaa kujivua Gamba lake inaweza kuwa ni ndoto za mchana lakini itakuwa vizuri endapo zitatimia. Mpaka sasa naamini waumi wamagamba wana vibrate na yana pukutika yenyewe! Hapa jambo la msingi ni mikakati ya kuvuna zaidi wapiganaji majasili waku itetea nchi yetu."salamu zenu mafisadi wote wa CCM siku zenu zinakaribia mtabaki Jivu"
 
Utawala wa Mali uliangushwa na Jeshi ndani ya masaa.Utawala wa magamba ndani ya AR utaangushwa na walioamua kujivua magamba na nguvu ya uma kwa siku chache zijazo.peoplessssssssssssssssssssssss.M4C.
 
Magamba yanaungua lakini yanaacha magamba ya mpingo na baada ya kuungua nini kitafuata je yataanza kuunguza na yale ya mpingo?
 
Mwenye habari za uhakika plse tupe kuhusu diwani sombetini na longido

Maana imekaa vizuri hii

Lema bado hajamaliza mafungo hadi wiki ijayo

Na kama hatakatiza mafungo huenda magamba wakapatwa na Entamoeba dysentry au E.histolytica na wote watapoteza vizibo
 
Katibu mwenezi wa vijana wilaya ya Longido Ndugu YOHANA LAIZER ameamua kuhama ccm na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Katibu huyo anadai kachoshwa na CCM kuchanganya siasa na mila. Pia anadai wamekuwa wakidanganya wananchi kuwa alama nyekundu iliyopo kwenye bendera ya CDM inaonyesha kuwa ni chama cha hatari hivi wasijiunge nacho. Pia imefika mahali wanatumia viongozi wa jamii ya Kimaasai kuwalaani watakaojiunga na Upinzani.Taarifa zaidi tukithibitisha.​
 
Wenye kuona mbali washaanza kuona kwamba meli inazama kwa hiyo wanaanz kuchukua maboya mapema ili wajiokoe. ila hilo akina NAPE hawawezi kuliona maana mamekua na vichwa vigumu kama wapiga vinubi wa TITANIC meli inazama wenyewe bado wanaendelea kupiga vinubi mpaka umauti unawakuta.
 
Whilethis is certainly an exciting news for CDM lakini lazima tupozi, tustep pembeni tuchungulie kwa jicho la tatu tutafakari kwa kina whats going on!!!! I dont believe in coincidence kwamba mtu anaamua tu kujivua gamba na yote haya yanatokea too fast after recent elections. Tunahitaji inteligensia unit ya CDM ifanye kazi kwa makini and do proper screening ya hawa ndugu wa gafla siyo kushangilia tu. Kumbukeni kwamba chama cha magamba kilishaanza kampeni za siri za ku inflitrate CHADEMA. Jamani sijapinga kuwa wasijivue gamba na kuingia CDM what am saying we should take extra precautions especially now wakat CCM wanajipanga kwa siri for 2015!.


ni mawazo tu wakubwa!!
 
Safi sana ni bora ajivue gamba hasipojivua atavuliwa,ujue huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CCM na uchaguzi ulivyo wagombea wanajaza form baada ya hapo zile form zinachambuliwa na ngazi husika wale wenye sifa nzuiri majina yao yanarudi kupigiwa kura sasa hao jamaa wanakimbia kuhaibika ni miongoni mwa magamba msishangae mtaona wengi tu kama mnafuatilia kwa ukaribu taarifa alizokuwa anatoa Mh Nape toka falsafa ya kujivua gamba imeanza pale waandishi walipomuuliza hawa jamaa ambao ni magamba mmewapa muda wa kujitathmini na kujivua gamba muda umekwisha hawajajivua CCM mnachukua atua gani? Mh Nape aliwajibu wasipojivua wakati utafika watavuliwa sasa kama unafuatilia huu ni mwaka wa uchaguzi kuanzia shina mpaka taifa ndani ya CCM,taratibu za chaguzi zimeanza toka mwanzoni mwa mwaka huu 2012 zinatarajiwa kuisha kwenye mwezi wa kumi mwaka huu 2012 na ndiyo maana mmeanza kuwaona wanakimbia kwa mfano James Ole Millya ni gamba na ndiyo maana aliomba ubunge wa EAC kupitia CCM mchujo ukafanyika ndani ya CCM jina lake halikurudi katoswa kwa kuwa ni gamba anaendekeza siasa za kibaguzi,kimakundi na ni mtovu wa nidhamu amepewa onyo mara nyingi sasa wana jamii ebu fikirieni endapo jina lake lingepitishwa na CCM kugombea ubunge wa EAC je angeama CCM? fikirieni nadhani mtajua huyu ni mtu wa namna gani!
 
Back
Top Bottom