Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Uongozi wa nchi ndiyo kila kitu. Hatuwezi kuendesha nchi bila uongozi. Kwa hiyo watu kuangalia uongozi umefanya nini ni haki yao kwani uongozi ndo umepewa dhamana ya kuongoza nchi. Kuongoza nchi si kazi ndogo. Ukiwa huna uwezo unatakiwa ujijue na usijiingize kabisa katika uongozi kwani ni jambo baya kuongoza wakati huna uwezo. Hakuna anayeweza kuwasaidia wananchi kwa kuzuia viongozi wabovu kuingia madarakani kama viongozi wenyewe. Hawa viongozi wakikataa kujiingiza katika madaraka ambayo hawana uwezo nao kuna uwezekano wa kuwapata viongozi bora wakaongoza, kwani mara nyingi viongozi bora hawapendi kuongoza!

Sasa nije kwenye hoja. Lipumba anaanza kumponda Kikwete possibly kuna mambo hayajaenda sawa katika mahusiano yao mapya ya CCM - CUF kwani kwa siku za hivi karibuni CUF wamekuwa karibu na CCM kwa maneno na matendo kuliko wengi tulivyotarajia. Sasa hivi sauti za kupingana zimeanza; pengine ni stunts tu baada ya Lipumba kutangaza kuwa mgombea uraisi hata kama anajua urais hawezi kuupata kamwe kwa hali ya upinzani ilivyo Tanzania hasa nguvu ya chama chake cha CUF katika maeneo mengi ya nchi. CUF wangeweza kuhamishia mafanikio yao ya Pemba katika mikoa mingine hata miwili tungeiona CUF kama nguvu inayokuja. Muungano wao na CHADEMA uliokufa pengine ilikuwa ni jambo zuri ambalo kama lingeendelezwa pengine leo CCM wangekuwa na wakati mgumu zaidi kuliko walivyo sasa.

Sasa hivi CCM si coherent na uongozi dhaifu unakitafuna kama kansa. Lakini Upinzani has ukiingalia CUF inazidi kudhoofika hivyo kauli za Lipumba kumlinganisha Kikwete na Mkapa kwa minajili ya kumuinua Mkapa dhidi ya Kikwete kunazidi kudhihirisha muflisi unaozidi ndani ya CUF.

Mkapa alikuwa kiongozi mbovu si kwa kuwa hakufanya chochote. Hata Kikwete hatutamwita kiongozi mbovu kwa sababu hakufanya chochote. Suala ni overall deliverly ya uongozi ndiyo tunachoangalia. Mkapa alijitahidi hapa na pale lakini overall ni failure kama kiongozi kutokana na misururu ya kashfa za rushwa zinazomwandama yeye na baraza lake la mawaziri. Huwezi kuwa kiongozi mzuri katika rundo la kashfa zote hizo tunazozizungumzia; Mikataba, Ununuzi wa vitu (Ndege, rada), Uuzaji wa nyumba za serikali, Ubinafsishaji holela, n.k. Kashfa ni nyingi mno. Kwa kiongozi hiyo ni failure kubwa sana na hili halina Ubishi.

Kikwete miaka yake mitano ya kwanza tayari ni uozo; ikiongozwa na richmond deal, EPA(ingawa wengi tunajua EPA ilibarikiwa wakati wa mkapa Kikwete kama beneficiary wa wizi ule hawezi kukwepa hili kwani fedha za EPA zilimwingiza madarakani). Baya zaidi ni hili la Kikwete kuitwa Satellite President, yaani kiongozi wa kukwea pipa na kuzamia ughaibuni kila kukicha huku watendaji wake ama wakifuatana naye huko safarini na waliobaki wakitanua na maposho ya juu kwa juu (Parallel allowances). Utawala wa kikwete umekuwa dhaifu hasa kwani hakuna baya la wakati wa mkapa lililorekebishwa au kuondolewa. Performance ya kiuchumi imekuwa mbovu zaidi huku kikwete akiwa anawaachia watendaji wake kugawiana fedha wapendavyo jambo linalosababisha mfumko wa bei kwa viwango vinavyoelekea kule kwa Mwinyi. Tunajua kuwa kugawiana fedha kwa watendaji wa serikali ndo balaa kwa nchi nyingi za Afrika. Kikwete hana maelezo kwa nini inflation zina spiral kila kukicha. Yote hayo yanatoa ujumuisho wa aina moja; Kikwete ni failure katika miaka mitano ya Kwanza. Anayo nafasi ya kurekebisha, ila walio wengi tumeshaona kuwa uwezo wake umeshafikia mwisho na hatutarajii muujiza miaka mitano ijayo.

Sasa akifanya mazuri madogo madogo hapa na pale; haimfanyi kuwa mzuri. Overall Mkapa na Kikwete wote ni failure na pengine inatakiwa tuangalie common denominator ambayo ni CCM. CCM is a failure and big problem kwa kipindi kinachofuata hivyo tusitarajie uongozi bora utokee CCM katika hali iliyo nayo CCM leo. Pengine hiyo ndo ilikuwa message ya lipumba ingawa haikuwa delivered kwa jinsi ambayo ingeeleweka!!
 
Abdallah Bakari
MFUMUKO wa bei ni kikwazo kikubwa cha Watanzania kuyafikia maisha bora waliyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete na chama chake mwaka 2005.

Hali ya maisha kila kukicha ni afadhali ya jana, fedha haina thamani, haipatikani na bei ya bidhaa madukani, sokoni zinapanda kila kukicha. Pengo baina wenye nacho na wasio nacho linazidi kuongezeka, idadi ya milo kwa walala hoi inazidi kupungua, siku hizi tunaita pasi ndefu, yaani ukila asubuhi hadi usiku.

Leo hii Watanzania wengi waishio vijijini wanalazimika kuishi maisha ya ujima, maisha walioishi mababu zetu kabla ya ukoloni kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa za mahitaji muhimu, zikiwemo nguo, chakula na mahitaji mengine, mianya ya kujipatia fedha imebana.

Wanalazimika kutumia mienge kujiangazia usiku kutokana na bei ya mafuta ya taa kuwa juu, kipimo cha chini ni kikopo kwa Sh150, wanatumia sabuni za asili kufulia kwani kipande cha sabuni ni Sh200, mahindi, mpunga na nafaka nyingine zinasindikwa kwa kutumia vinu vya asili badala ya mashine, kwa kuwa kusaga kilo moja ni Sh200.

Tembelea Kijiji cha Ndechela, Wilaya ya Nanyumbu, Mtwara uone watoto wanavyotembea bila ya nguo. Kama si busara za Mkuu wa Wilaya hiyo kuwapelekea msaada wa nguo zilizotolewa na waumini wa Kanisa la Anglikana Mjini Masasi, hali sijui ingekuwaje.

Matatizo hayo yote chanzo ni mfumuko wa bei, tatizo ambalo lilianza kujitokeza mapema 2006. Kwa wale wenye kumbukumbu watakubaliana nami kuwa kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Nne kuliambatana na matatizo kadhaa likiwamo la uhaba wa nisharti ya umeme, lililotupeleka kwenye Richmond.

Wakati hilo likiendelea, kuliibuka tatizo jingine la kupanda bei ya mafuta ya dizeli na petroli. Huku Mtwara, kwa mfano, lita moja ilifikia 2,500 hali iliyosababisha mfumuko wa bei kwa kila bidhaa kutokana na ukweli kuwa sekta ya usafirishaji ndiyo uti wa bei.

Tukataraji kuona serikali ikichukua hatua, lakini katika hali ya kustaajabisha Rais Jakaya Kikwete akasema tatizo la mfumuko wa bei lipo nje ya uwezo wake, hivyo Watanzania waendelee kukaza buti hadi hali itakapotengamaa yenyewe.

Kwa kuwa Rais alitoa kibali cha bidhaa kupanda bei kwa kadri ya mahitaji ya faida kwa muuzaji, huku vijijini hali ikawa mbaya zaidi hata bidhaa zinazosafirishwa kwa baiskeli zikawa zinauzwa kwa bei ya juu, ukiuliza mafuta yamepanda bei, hujamsikia Rais!

Matumaini ya wengi yakawa hali itatengamaa siku chache zijazo kwa kuwa mwanzo mgumu na sasa ni miaka mitano, tunapima utekelezaji wa ahadi na Ilani ya CCM bado mfumuko wa bei upo palepale.

Watoa takwimu wanasema uchumi unapanda. Hivi kupanda kwa uchumi kwenye kompyuta wakati maisha yetu ni magumu kunatusaidia nini?

Lakini swali la msingi ninalojiuliza ni kwamba Rais Mstaafu Benjamin Mkapa aliwezaje kudhibiti mfumuko wa bei na Rais Kikwete anashindwaje? Takwimu zinaonesha kuwa Mkapa alichukua nchi kutoka kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi mfumuko wa bei ukiwa zaidi ya asilimia 33, akapambana nao hadi kuupunguza mpaka zaidi ya asilimia nne.

Tangu Kikwete aingie madarakani mfumuko wa bei ulipaa na kufikia asilimia nane kwa kipindi cha miezi mitatu na sasa ni zaidi ya asilimia 12. Sukari tuliyokuwa tunanunua kwa Sh500 kwa kilo leo hii ni Sh1,800, sasa tunarina asali na kuunga kwenye chai.

Mavazi nayo hayakamatiki. Sisi walalahoi tunaishia kuvaa mitumba, sisemi dukani nguo hazinunuliwi, wala watu hawanywi chai ya kuunga kwa sukari, la hasha, wapo wanaofanya hivyo tena kwa kusaza. Hao ni wale wachache kati ya wengi, kwani walionacho wameongezewa na wasionacho wamepokonywa kabisa.

Nadhani kuiga jambo jema si vibaya kuliko kung'ang'ani lako hata kama ni mbaya na halina maslahi. Mkapa yupo tena kama si Lushoto, Tanga atakuwa Dar es Salaam na kama si hapo Masasi, au Lupaso kijijini alikozaliwa, nendeni mkamuulize mbinu alizotumia kudhibiti mfumuko wa bei.

Tuliendesha maisha yetu vizuri, kidogo tulichokipata kilikuwa na thamani mbele ya bidhaa kuliko zama za sasa. Hata kama hatuibiwi tunahisi maumivu ya umaskini wa kupindukia.

Pengine hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya Mkapa inayomfanya atembee kifua mbele huku akishangiliwa na Watanzania kwani wametambua kuwa aliweza kuhakikisha mtu wa chini anaweza kumudu kupata mahitaji yake muhimu kwa kipato chake kidogo.

Kwa hali ya sasa, maisha bora yataendelea kuwa msamiati mgumu kwa Watanzania, huku matumaini yakizidi kuyeyuka siku hadi siku na wengi wao kukata tamaa.

Msione magari na majumba ya ghorofa mijini mkadhani Tanzania yote ipo hivyo. Kwa mijini walio wengi wana mishahara hata kama si minono lakini walau inawawezesha kwenda sokoni kuuliza fungu la nyanya, kuna watu wanahangaika kwelikweli.

Kama Rais haamini haya niyasemayo namuomba atembelee Nanyumbu hasa Kijiji cha Ndechela, bila shaka akirudi huko atakuwa amejifunza jambo na kuchukua hatua stahiki.

Kitaaluma, Rais Kikwete ni mchumi anafahamu mfumuko wa bei unavyoweza kuathiri uchumi wa nchi, sina hakika kama wasaidizi wake wanamweleza yaliyo ya kweli. Sasa ni wakati wa ile hadithi ya mbayuwayu na kong'ota kutumiwa na kila mtu.
0787 104785

Source: MWANANCHI.

My take: JK wetu na digrii yake ya uchumi alishindwa na Mwandishi wa Habari, Ben Mkapa! Kaaazi kweli kweli!
 
Linganisha hata uzito wa hotuba zao Kikwete na Mkapa utajua tu ni nani anamaanisha anachokiongea. Zingine utakuta ni nzito zingine nyepesi nyepesi.
 
Kuna njia kadhaa za kuthibiti mfumuko wa bei; njia pekee iliyotumiwa na serikali ya Mkapa ni nidhamu ya kuthibiti mzunguko wa fedha ambapo kulikuwa na fedha chache sana kwenye mzunguko. Namna gani alidhibiti mzunguko wa fedha ni pamoja na kubana matumizi ya serikali kiasi kuwa serikali ilikuwa inaendeshwa kwa kufuata bajeti kama ilivyopitishwa na bunge mwezi June; kulikuwa hakuna upuuzi wa mini-budget kama alivyokwisha fanya Kikwete. Vile vile Mkapa alibana fedha haramu nyingi zikashindwa kuingia kwenye mzunguko; yaani kulikuwa hakuna fedha haramu za mishenitown kama ambavyo siku hizi zimezagaa tena. Fedha za mishen town ndiyo chanzo cha kukua kwa inflation wakati wa Mwinyi, na vile vile wakati huu wa Kikwete.
 
Mkapa alipunguza Inflation kwa kuongeza VAT kubwa kuliko Nchi yoyote duniani, Madhara yake yakawa kama ifuatavyo:

1- Purchersing power ikashuka, wananchi hawakuwa na uwezo wa kununua kama walivyokuwa wakinunua wakati wa Mwinyi.
Maisha yakaanza kuwa magumu zaidi kwa kila mtu as result ujambazi ukaanza kupamba moto, wafanya biashara wadogowadogo wakaanza kufilisika, kwa sababu nchi ilkuwa dry, mzunguuko wapesa ukawa mdogo.

2- Mwinyi aliweza ku-establish tax base ambayo ilimfanya Mkapa kuweza kukusanya Kodi, hence kuifanya serikali kuwa na pesa, Lakini higher VAT ilipunguza kasi kwa wananchi kuweza ku-establish business.

3- Mwinyi aliridhi nchi toka kwa (so called) Mtakatifu Nyerere ikiwa na supply push inflation zaidi ya 39% Mwinyi aliweza kuishusha inflation toka 39% mpaka kufikia demand push inflation 31% bila wananchi ku sikia maumivu, hii ni kutokana na economy policy isiyokuwa ya kukurupuka.

SO, JK anaweza kushusha inflation within a week kama atafuata sera za kukrupuka kama za Mkapa, lakini akishusha inflation haraka harak impact yake kwa uchumi itakuwa mbaya
Kwa sababu hali ya uchumi duniani ni mbovu inabidi atumie gradualy decrease on inflation, on the same time lazima Kikwete a - inject maney ili uchumi u-pick up. Kwa hiyo kupunguza inflation wakati huohuo anspeculate demand kwenye economy ndiyo policy ambayo inahitajika wakati huu

RESPECT!
 
Mbona unaongea kama enzi hizo Tanzania ulikwepo peke yako? Au ndo sasa upo kwenye mshiko hayo niliyohight yanakuendea vizuri. Mimi ninachojua ni kwamba enzi hizo mshahara wangu ulitosha kuniudumia kwa sababu vitu vilikwepo na bei vilikuwa vya chini.Leo mshahara wangu hautoshi kunihudumia.Kwetu kijijini wazazi wangu waliweza kununua nyama japo mara moja kwa wiki leo hawawezi na siwezi hata kuwapa support kwa sababu mshahara wangu haunitoshi.Au unaongelea paper work?
 
Haku-indulge kwenye profligate spending! Alitumia alichokuwa nacho. Leo badala ya ku-curb matumizi yasiyo na maaana ( safari za nje za Rais, mashangingi, kualika Brazil n.k.), tunaenda kukopa kwa loan sharks! Tunaendelea kujichimbia. Na worse kwa hawa jamaa wa sasa, hawasiti kuvitia rehani vizazi vijao. Tutamkumbuka Mkapa.

SO, JK anaweza kushusha inflation within a week kama atafuata sera za kukrupuka kama za Mkapa, lakini akishusha inflation haraka harak impact yake kwa uchumi itakuwa mbaya
Kwa sababu hali ya uchumi duniani ni mbovu inabidi atumie gradualy decrease on inflation, on the same time lazima Kikwete a - inject maney ili uchumi u-pick up. Kwa hiyo kupunguza inflation wakati huohuo anspeculate demand kwenye economy ndiyo policy ambayo inahitajika wakati huu

Kama wanajua hilo mbona hawarekebishi matumizi yao? A-inject money kutoka wapi na kwenye nini? Hatuna kitu kama industrial base na ku-inject kwenye social services kwa sasa hivi return zake zitachukua muda mrefu kutufikia. Tusipende kuiga kile kinachofanywa na wenzetu ambao uchumi wao ni tofauti kabisa na wa kwetu. Sisi ni subsistence, ukitupa mbegu tutakula badala ya kupanda!

Amandla...........
 
Mkapa alipunguza Inflation kwa kuongeza VAT kubwa kuliko Nchi yoyote duniani, Madhara yake yakawa kama ifuatavyo:

1- Purchersing power ikashuka, wananchi hawakuwa na uwezo wa kununua kama walivyokuwa wakinunua wakati wa Mwinyi.
Maisha yakaanza kuwa magumu zaidi kwa kila mtu as result ujambazi ukaanza kupamba moto, wafanya biashara wadogowadogo wakaanza kufilisika, kwa sababu nchi ilkuwa dry, mzunguuko wapesa ukawa mdogo.

2- Mwinyi aliweza ku-establish tax base ambayo ilimfanya Mkapa kuweza kukusanya Kodi, hence kuifanya serikali kuwa na pesa, Lakini higher VAT ilipunguza kasi kwa wananchi kuweza ku-establish business.

3- Mwinyi aliridhi nchi toka kwa (so called) Mtakatifu Nyerere ikiwa na supply push inflation zaidi ya 39% Mwinyi aliweza kuishusha inflation toka 39% mpaka kufikia demand push inflation 31% bila wananchi ku sikia maumivu, hii ni kutokana na economy policy isiyokuwa ya kukurupuka.

SO, JK anaweza kushusha inflation within a week kama atafuata sera za kukrupuka kama za Mkapa, lakini akishusha inflation haraka harak impact yake kwa uchumi itakuwa mbaya
Kwa sababu hali ya uchumi duniani ni mbovu inabidi atumie gradualy decrease on inflation, on the same time lazima Kikwete a - inject maney ili uchumi u-pick up. Kwa hiyo kupunguza inflation wakati huohuo anspeculate demand kwenye economy ndiyo policy ambayo inahitajika wakati huu

RESPECT!

Kwangu ina sound too personal hii comment yako maana jambo la msingi hapa ni kupunguza inflation na siyo nani alikuwa bora kati ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK maana hiyo nayo ni mada ndefu ya kujitegenmea.
Kuhusu mada, utawala uliopo ulipokea dola inflation ikiwa kiwango cha chini kabisa. Nini kimetokea mpaka turudi kule tulikotoka? Ni uongozi mbovu usio na vision, wenye kufanya mabo kwa bahati bahati ndio unaotusumbua.
 
Mkapa alipunguza Inflation kwa kuongeza VAT kubwa kuliko Nchi yoyote duniani, Madhara yake yakawa kama ifuatavyo: 1- Purchersing power ikashuka, wananchi hawakuwa na uwezo wa kununua kama walivyokuwa wakinunua wakati wa Mwinyi. Maisha yakaanza kuwa magumu zaidi kwa kila mtu as result ujambazi ukaanza kupamba moto, wafanya biashara wadogowadogo wakaanza kufilisika, kwa sababu nchi ilkuwa dry, mzunguuko wapesa ukawa mdogo. 2- Mwinyi aliweza ku-establish tax base ambayo ilimfanya Mkapa kuweza kukusanya Kodi, hence kuifanya serikali kuwa na pesa, Lakini higher VAT ilipunguza kasi kwa wananchi kuweza ku-establish business. 3- Mwinyi aliridhi nchi toka kwa (so called) Mtakatifu Nyerere ikiwa na supply push inflation zaidi ya 39% Mwinyi aliweza kuishusha inflation toka 39% mpaka kufikia demand push inflation 31% bila wananchi ku sikia maumivu, hii ni kutokana na economy policy isiyokuwa ya kukurupuka. SO, JK anaweza kushusha inflation within a week kama atafuata sera za kukrupuka kama za Mkapa, lakini akishusha inflation haraka harak impact yake kwa uchumi itakuwa mbaya Kwa sababu hali ya uchumi duniani ni mbovu inabidi atumie gradualy decrease on inflation, on the same time lazima Kikwete a - inject maney ili uchumi u-pick up. Kwa hiyo kupunguza inflation wakati huohuo anspeculate demand kwenye economy ndiyo policy ambayo inahitajika wakati huu

Hebu tuambie, wakati wa mkapa, VAT ilikuwa kiasi gani , wakati wa Mwinyi, wakati wa kikwete. Unafahamu ukiwa kama msomi unatakiwa utoe tarakimu na hoja zilizosheheni.

Pili, ninapata wasi wasi na usomi wako, ninakumbuka muhadhiri wangu mmoja aliwahi kuniambia: ''....iwapo wewe ni msomi, lakini unashindwa kukitafsiri ulichosoma na kukiweka katika mazingira yanayokuzunguka, ili wanaokuzunguka waelewe, na ulichokisoma kikusaidie kutatua matatizo yanayokukabili,...basi wewe hufai kuitwa msomi bali yakupasa ujijue kuwa wewe ni muhudhuria darasani, na ole wako maana unapoteza muda na hufai, wewe ni mzigo kwa jamii inayokuzunguka....".
Sasa ndugu yangu nakushangaa, nikiangalia hapo juu kwenye maelezo yako ninagundua yafuatayo:
1) Umetumia misamiati kibaaao ya kiuchumi na kwa lugha ya kigeni, na mwishowe unachokisema hakileti mantiki na hakieleweki. (mfano, unapozungumzia "Demand Pull Inflation" badala ya kutumia maneno hayo kwanini usitumie maneno na lugha nyepesi kama "..mfumuko wa bei usababishwao na kuzidi kwa mahitaji ya kitu...." n.k. Na isitoshe bora ungetumia neno sahihi basi, eti badala ya kutumia neno "Demand Pull Inflation" umetumia maneno "Demand Push Inflation" kitu ambacho hakipo. Na hii ni kwa elimu yangu ya Uchumi niliyoipata kidato cha tano na Sita wakati huo. Nina-shaka wewe chuo kikuu umefanya uchumi kama moja ya masomo yako, sasa tujiulize kuna ubora ulioupata chuoni ama ulikwenda kutumia fedha za watanzania bure huku ukiwa unakula maandazi na kuhudhuria darasani huku ukiendelea kukua?
2) Unatoa hoja kama vile unamshambulia mtu ama watu fulani, je kwa hali hii wewe kama msomi mtaalamu wa uchumi unadhani unasifa za kuuzungumzia uchumi iwapo maoni binafsi yanakutuma kuitumia taaluma yako isivyo? Nilitegemea kama ukiwa msomi, taaluma yako ikushawishi iongoze maoni yako. Lakini inavyoonekana katika hoja zako, nashindwa kujizuwia kugundua chembe chembe za "...umimi.." na "..u-wao..watu fulani"

Hatimaye ninajiuliza, ikiwa wewe nawe ni mmoja wa wasomi wa nchi hii, na hivi ndivyo ulivyo na unavyofanya mambo yako, Tanzania ya kesho ni salama kweli?
Hivi kweli mtu kama wewe na wengine wooote wa aina yako mkipewa jukumu la kumshauri Raisi asiyejua mambo mengi ya uchumi, unadhani hali itaacha kuwa mbaya kuliko ilivyo sasa?
Mwishowe kabisa, hebu toa ufafanuzi ama rekebisha maneno yaliyobadiliwa rangi na utuombe msamaha kwa kuleta hoja ambazo hazijachujwa hapa jamvini huku ukitumia lugha isiyo sahihi na hatimaye kuupotosha ukweli. Kwa namna hii, wewe si unaweza kuwa mmojawapo wa wale waliompa Raisi Kikwete takwimu sizizo za kweli? Ndio huwa mnaanzia hivi hivi!
Nina wasiwasi, nina mashaka, ninogopa kuhusu Tanzania yetu kesho, kwa wasomi na wanataaluma wa aina hii.

Muheshimiwa Mwenyekiti wa Thread Hii, naomba kutoa hoja!
 
Ninalojua kuwa mkapa alifanikiwa sana katika utawala wake ni nidhamu ya matumizi ya pesa. Ingawa alikuwa pia akipa pesa kwa kuuza mashirika, hakufujisha fedha hizo kuziingiza kwenye mzunguko. Sasa hivi pesa nyingi sana inaingia kwenye mzunguko ikiwamo hata ile ya kukopa. Sasa niliposoma mheshimwa hapo juu akiweka somo nikashindwa kuelewa. VAT iliyoletwa na Mkapa haijawahi kupunguzwa na Kikwete labda kama ninaisha sayari nyingine; kila mwaka kodi zinaongezeka hata kama baadhi ya kodi zitapunguzwa, ni lazima mfuko wa babu upate haki yake ambayo inakuwa kila siku.
 
Mkapa hana ujuzi wa kuzuia mfumuko wa bei, Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni? Kichwa ni Dr. Balali. Mtake msitake alidhibiti uchumi?
 
Mkapa hana ujuzi wa kuzuia mfumuko wa bei, Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni? Kichwa ni Dr. Balali. Mtake msitake alidhibiti uchumi?

Tuambie alifanyaje; haitafutwi sifa hapa ila mbinu zilizotumika ili ziweze kutumika sasa...............labda mimi sijaelewa!
 
JK wetu na digrii yake ya uchumi alishindwa na Mwandishi wa Habari, Ben Mkapa! Kaaazi kweli kweli!

Sometimes najiuliza hivi,
1) Is it a matter of a right person following a wrong route?
2)Is it a matter of a wrong person going through a right route?

Sometimes, nadhani ni matatizo ya Tanzania vile? maana tunachosoma madarasani tunataka kukileta kama kilivyo kuku ukwelini. Na, to be frank, hii inakuwa ngumu kwakuwa many of the vitabu tunavyosoma ni outdated, so by the time tunamaliza kusoma tena kwa lugha ya kigeni huku tukiamini lugha ya kigeni ni bora na sahihi zaidi kuliko yetu tunayoitumia kila siku,tunajikuta tayari mazingira yetu na ulimwengu wetu umesogea hatua moja mbele, some of what we learnt becomes irrelevant. Kama hiyo haitoshi tunakutana na tatizo jingine: To put what we learned in the clasrooms to practices in the real world, in our society, amid our problems and challenges.

Now if you want to see kichekesho, ni pale msomi huyu anavyanza kuhangaika ku-paste alichokiona kwenye makabrasha! matokeo yake..? Mtu anaanza kujibu maswali ya kiuchumi ambayo hayajaulizwa na uchumi wa nchi yetu ilhali yale yanayoulizwa na uchumi wa nchi yetu akiyapuuzia ama akiyafumbia macho na kuyakwepa. Haya yanayoulizwa na uchumi wa Nchi yetu si hajayasoma popote? Si msomi huyu anaamini katika ku-copy na ku-paste? Analysis component kwake yeye si irrelevant na imekufa?

Jumlisha hayo yote na ufahamu kuwa yeye sasa anatakiwa kuwa na nyumba nzuri, gari zuri na mali kibao ili watu wakimuona wajue kwamba yeye kweli ni msomi wa nchi hii, jawabu unalolipata ni SERA MBOVU, UCHUMI MBOVU, MATATZO LUKUKI, NA UMASIKINI WA KUTUPWA WA WANANANCHI WALIO WENGI.

Mwishowe tunakuja kugundua kumbe kuna short-cut ya kutembeza bakuli? basi bakuli linaanza kutembea, linatembea weee, hadi inakuwa tabia. Kila kitu mpaka wafadhili watoe hela. Na wafadhili wnyewe wamechoka, wakagundua kitu kumbe wanaweza kutupatia vijihela na tukawapatia rasilimali zetu? Basi anza kuchukua madini, vitalu vya uwindaji n.k.

Na zaidi sana baada ya kuona hawa wafadhili wanataka tulivyonavyo, tukaona isiwe tabu, kama tunaweza kupata pesa kwa wafadhili ya nini kujihighulisha? Uza na mashirika yote ya umma, toa yote, ili tuwe tunakuja kazini kupiga stori tangu asubuhi hadi jioni lakini hela tunapata! Basi tukaanza kuuza, uza uza uza uza....! Kutahamaki kila kitu tumeacha kufanya, tumewauzia ama tumejitoa katika uendeshaji wake.

BIMA, Shirika la Ndege, Reli, Bandari, Ranchi za taifa, mashamba ya nafaka (ambazo wakati wa Nyerere yalisaidia sana kudhibiti njaa na kazalisha kiasi cha kutosha kuuza nje ya nchi na kujipatia fedha za kigeni), Mahoteli, hadi huduma za afya.

Hebu niambie kwa picha hiyo hapo juu, Mtu anayefanya hivi ni tumwite jina gani zuri linalompendeza zaidi ya "MVIVU"?

Nani aliwahi kuona mvivu akifanikiwa? Sijawahi kuona, labda ashinde bahati nasibu!

Matokeo yake, kwa kuwa hatuna chakufanya, tunajikuta tunaanza wizi, hujuma, rushwa etc.

Tutapona Watanzania wenzangu???? Nisaidieni...!
 
Tuambie alifanyaje; haitafutwi sifa hapa ila mbinu zilizotumika ili ziweze kutumika sasa...............labda mimi sijaelewa!

Baba wa watu alijitahidi kudhibiti bei ya Bia mpaka anaondoka madarakani tulikuwa tunakunywa kwa 850/= kwa chupa huyu baba aliye ingia mmmh yaani sijui anataka kutajilikia kwenye bia mbona vyanzo vya mapato vipo vingi tu tuna dhahabu, vivutio vingi vya utalii, ardhi safi yenye rutuba sasa yeye fegi na bia anaona ndo chanzo cha mapato serikalini mweh!!!
 
Mkapa hana ujuzi wa kuzuia mfumuko wa bei, Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni? Kichwa ni Dr. Balali. Mtake msitake alidhibiti uchumi?

Nimeipenda hii sentensi, ila bado mkapa alikuwa kichwa kwa uelewa wangu mdogo tu naweza sema hivyo (kujua tu kwamba Balali alikuwa mtaalam na kumwacha afanye kazi zake mpaka mfumuko wa bei ukashuka inatosha kuonyesha Mkapa alikuwa makini)

Ila binafsi bado nakumbuka nakumbuka comments za mzee Hans Kitine kwamba "nchi inaendeshwa kienyeji"!! je kwa haya yanayotokea sisi wananchi wa kawaida je tuanze kuamini kwamba ilikuwa ni fact? I dont know nachangia tu, wachumi waendelee kutupa mambo hapa wengine sisi mbumbumbu wa uchumi!
 
Baba wa watu alijitahidi kudhibiti bei ya Bia mpaka anaondoka madarakani tulikuwa tunakunywa kwa 850/= kwa chupa huyu baba aliye ingia mmmh yaani sijui anataka kutajilikia kwenye bia mbona vyanzo vya mapato vipo vingi tu tuna dhahabu, vivutio vingi vya utalii, ardhi safi yenye rutuba sasa yeye fegi na bia anaona ndo chanzo cha mapato serikalini mweh!!!

Mkuu siku zote serikali zisizo na ubunifu hujikita kwenye Booze and fags kama source ya mapato, at the same time unawakuta tena wako kwenye kampeni ya kuwataka watu waachane na vitu hivyo! contradicting eeh!!!!!
 
Mkapa alipunguza Inflation kwa kuongeza VAT kubwa kuliko Nchi yoyote duniani, Madhara yake yakawa kama ifuatavyo:

1- Purchersing power ikashuka, wananchi hawakuwa na uwezo wa kununua kama walivyokuwa wakinunua wakati wa Mwinyi.
Maisha yakaanza kuwa magumu zaidi kwa kila mtu as result ujambazi ukaanza kupamba moto, wafanya biashara wadogowadogo wakaanza kufilisika, kwa sababu nchi ilkuwa dry, mzunguuko wapesa ukawa mdogo.

2- Mwinyi aliweza ku-establish tax base ambayo ilimfanya Mkapa kuweza kukusanya Kodi, hence kuifanya serikali kuwa na pesa, Lakini higher VAT ilipunguza kasi kwa wananchi kuweza ku-establish business.

3- Mwinyi aliridhi nchi toka kwa (so called) Mtakatifu Nyerere ikiwa na supply push inflation zaidi ya 39% Mwinyi aliweza kuishusha inflation toka 39% mpaka kufikia demand push inflation 31% bila wananchi ku sikia maumivu, hii ni kutokana na economy policy isiyokuwa ya kukurupuka.

SO, JK anaweza kushusha inflation within a week kama atafuata sera za kukrupuka kama za Mkapa, lakini akishusha inflation haraka harak impact yake kwa uchumi itakuwa mbaya
Kwa sababu hali ya uchumi duniani ni mbovu inabidi atumie gradualy decrease on inflation, on the same time lazima Kikwete a - inject maney ili uchumi u-pick up. Kwa hiyo kupunguza inflation wakati huohuo anspeculate demand kwenye economy ndiyo policy ambayo inahitajika wakati huu

RESPECT!

Ushabiki mwingine hovyo sana. Hata kama humpedi Mkapa kwa sababu zako binafsi pengine za kidini, ulichoandika is completely nonsense. Unajifanya ni kama watanzania wote walikuwa watoto wadogo wasioelewa kitu enzi hizo, isipokuwa wewe tu.

Mwinyi aliichukua nchi in a cold and post cold war erra, it was hard for him. HE DID THE BEST HE COULD
Mkapa alipochukua nchi aliendeleza pale kwa mzee mwinyi kwa kuchukua mazuri na akatengeneza vyanzo vizuri ya kukusanya kodi hasa TRA.
But JK mhh sioni cha kuandika....there is nothing, I wonder if he is real an economist....
 
Back
Top Bottom