Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,526
- 19,381
Kabla ya mashirika ya umma kuuzwa mnaomlaumu Mkapa. Lakini inatakiwa pia kukumbuka ktk kipindi Cha Nyerere na Mwinyi ni makupuni mengi yalikufa kuliko aliyoyauza Mkapa.
Na makapuni mengi yaliyokufa kipindi hicho , baadhi yake Mkapa aliyafufua na kuyapiga bei. Watanzania naona wanapenda kuangalia likampuni limekufa kuliko kuliuuza kwa bei nafuu na hapo hapo likaajiri wa tanzania zaidi ya elfu kadhaa na kusongesha maisha mbele.
Nadhani unalokosea ni kule kuchukulia kuwa watu wanamlaumu Mkapa kwa kuuza mashirika tu; hapana,kosa lake ni lile la kuuza mashirika hayo bila kuzingatia maslahi ya Taifa. Ni kweli mashirika yote yalikuwa ni mzigo kwa serikali na ilikuwa ni lazima yauzwe. Kwa kufuata maneno ya Dr. Gates, "....there is a smart way of doing things and there is a stupid way of doing things;" Mkapa alifuata hiyo njia ya pili katika kuuza mashirika. Mkapa mwenyewe alishakiri kwa mdomo wake kuwa kweli aliboronga katika kuuza mashirika yale.