Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Mkapa kwangu mimi was a leader in terms of vision. Lakini ilikuwaje akaamua kuwanufaisha watu wachache kwa ubinafsi? Ilikuwaje akaruhusu wezi wa mali ya uma kuonekana ndo wafanyabiashara na matajiri wakubwa TZ? Ilikuwaje akaruhusu taasisi za serikali kuwekwa mateka na wafanyabiashara uchwara wa rada na vifaa vya kijeshi...Nina macho ya kutazama..lakini tatizo nimeamua wapi nimtazame...yule bwana mmmh sidhani. Kikwete ntamuangalia vizuri baada ya muda wake kuisha na kukaa kando.Siwezi jua bwana, bado anao muda
 
Mkapa tutamkumbuka kwa yafuatayo
1 Daraja la Mkapa la kuunganisha mikoa ya kusini

Ilikuwa ni kazi iliyoachwa na Mzee Mwinyi na akijidai kulipa jina lake

2 Uwanja wa michezo wa kisasa

Hii ilikuwa kutuziba macho tusifikirie vitu kama Kiwira na mengineyo

3 Maji ya ziwa victoria kwenda Shinyanga na Kahama

Hivi nikumbushe kuna migodi huko ama?

4 Mabarabara mengi yalijengwa kwa kiwango cha rami

Mfano barabara ya Nangukulu sijui hamna lolote mpk sasa Wizara kibao zina madeni ndio watu wanajitahidi kulipa na Wizara ya Miundombinu ndio inaongoza kwa madeni

5 Uchumi uliimalika

Baada ya kubinafsisha sana ndio tukasamehewa madeni na kuambia uchumi umeimarika wakati pato la mwananchi bado lilikuwa pale pale baraka ya kujali tumbo street

6 Mfumuko wa bei ulipungua

Ulipungua kwasababu lazima wawekezaji wapate faida hasa wa ndani kwahiyo isingekuwa rahisi kukubali bei za holela

7 Kodi ziliongezeka

Sijajua unatumia takwimu gani mkuu?

Mh. Kikwete katika miaka 4 tumkumbuke kwa yapi? Orozesha hapa!!!

Kwa mengi sana na moja kubwa ni kukubali UHURU WA VYOMBO VYA HABARI tofauti na ZAMA ZA UKWELI NA UWAZI BADALA YAKE TULIPATA UBABE NA UJEURI WA KUANZIA NGAZI YA RAIS MPK WABUNGE

Sidhani kama Kipindi cha Mkapa tungethubutu kuwagusa watu wake. ALEYENADI NENO UFISADI angekuwepo leo nafikiri angetoa ushuhuda juu ya hili hasa kwa kufananisha awamu hizi 2 Mungu amlaze mahala pema PROF CHACHAGE
 
Nitadumu kumheshimu benjamin william mkapa na kumkubali kama kiongozi pekee tanzania aliyekuwa jasiri wa "kuthubutu kufanya maendeleo" hata ktk kipindi kigumu ktk maamuzi.
 
Nasisitiza tena kwa yepi hatutamsahau kaka Ben kabla sijamwaga razi hapa.
BMW ana mengi ya kukumbukwaa..

kama hupendi kuona na kukubali hayo ni matatizo yakooo...

I do respect BWM leadership to our country and his legacy will live for ever.
 
Nitadumu kumheshimu benjamin william mkapa na kumkubali kama kiongozi pekee tanzania aliyekuwa jasiri wa "kuthubutu kufanya maendeleo" hata ktk kipindi kigumu ktk maamuzi.
FDR Jr HESHIMAA MKUUUU
 
Nitadumu kumheshimu benjamin william mkapa na kumkubali kama kiongozi pekee tanzania aliyekuwa jasiri wa "kuthubutu kufanya maendeleo" hata ktk kipindi kigumu ktk maamuzi.

Hata maamuzi ya kuibia wananchi huwa ni magumu na yanataka moyo....... endelea kudumu kumheshimu.
 
Kwa kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi wake tunayo ya kumkumbuka JK, sio lazima yawe mazuri.
Mosi tutamkumbuka kwa safari zake za nje zisizokuwa na tija kwa waTZ, na zinazowagharimu walipa kodi wa nchi hii mabilioni ya pesa. Pili tutamkumbuka pia kwa uongozi wake wa kisanii wa kuiongoza nchi kwa matukio na si kwa dira/ ilani kama alivyoahidi kwenye kampeni zake. Tatu kwa mikakati yake mibovu iliyoshindwa hata kabla ya kuanza, mfano ajira milioni moja, semina elekezi ( hazikuzaa tija katika utendaji). Lakini pia tutamkumbuka kwa kukubali baadhi ya rafiki zake wasurubiwe na vyombo vya habari kwa maovu yao (Lowassa).
 
mi namkubali sana bwana nkapa, jamaa sirias kinyama,
nchi hii ilipata heshima sana.

huyu wa sasa bado amesimama juu ya mabega ya mkapa, ndo hizo pesa alizoacha mwenzake zinamfanya hatulii nyumbani.

he cannot think beyond the next meal,
bado natafuta nauli, siku nikitokeza huko aliko udugu utakufa na anko!!
 
Mkapa tutamkumbuka kwa yafuatayo
1 Daraja la Mkapa la kuunganisha mikoa ya kusini=Alianzisha Mzee Mwinyi na kuahangaika kwa wafadhili mkapa yeye kamalizia tu

2 Uwanja wa michezo wa kisasa

3 Maji ya ziwa victoria kwenda Shinyanga na Kahama

4 Mabarabara mengi yalijengwa kwa kiwango cha rami

5 Uchumi uliimalika= mikataba mingi vimeo

6 Mfumuko wa bei ulipungua
7 Kodi ziliongezeka= baada ya wawekezaji kuchukua chao mapepa

Mh. Kikwete katika miaka 4 tumkumbuke kwa yapi? Orozesha hapa!!!
= kusafiri kwenda nje za nchi kuliko viongozi wote walio mtangulia
 
Ni wazi JK hajatupa chochote cha kuweza kumkumbuka. labda USANII wake na serikali yake.

Lakini pia BMW tunaweza kumkumbuka kwa ndege yale na rada.
 
  • LIPUMBA ASEMA MKAPA ATAKUMBUKWA KUIMARISHA UCHUMI
na Asha Bani

SHUTUMA za utendaji mbovu, ufisadi zilizokuwa zikimuandama aliyekuwa rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, zinazidi kupungua siku hadi siku ambapo sasa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, amejitosa kuelezea uimara wa serikali iliyopita huku akisema utawala wa Rais Kikwete ni dhaifu.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Profesa Lipumba, alisema Mkapa alikuwa makini katika maamuzi mazito pamoja na kusimamia uchumi ambao ulikuwa kwa kiwango cha kuridhisha huku akidhibiti mfumo wa bei za bidhaa.

Lipumba alisema Kikwete hawezi kufanana na Mkapa hata kama watampambana kwa maneno matamu kwenye vyombo vya habari au majukwaani kama wafanyavyo sasa kwa kuwa si mtu makini hasa linapofikia suala la kufanya maamuzi mazito yenye kuleta ustawi na maendeleo kwa taifa.


Alibanisha kuwa katika awamu ya kwanza ya miaka mitano ya Mkapa na hii ya Rais Kikwete mambo yanajionyesha ambapo hivi sasa umaskini unazidi kushamiri siku hadi siku huku wale walionacho wakizidi kuongezewa kiasi cha kuzidisha pengo la walionacho na wasionacho ambalo mwisho wake ni hatari kwa taifa.


Aliyataja mambo ambayo Mkapa alifanikiwa ni pamoja na suala la nidhamu serikalini, kurekebisha suala la utendaji na hata kurekebisha suala zima la mfumko wa bei ambapo wananchi waliweza kupata bidhaa kwa bei nafuu tofauti na hivi sasa ambapo hupanda kila kukicha.


“Hakuna mtu asiyefahamu wakati Mkapa anaingia madarakani kulikuwa na hali ngumu ya uchumi hasa mfumko wa bei ambapo bei za bidhaa zilipanda kwa asilimia 33 na pindi alipoingia alifanikiwa kubanana na serikali na kufikia chini ya asilimia 10 kwa hilo sina budi kumsifu,” alisema Profesa Lipumba.


Alisema, hana budi kumpongeza kwa hilo kwa kuwa alifanikiwa kuudhibiti ikiwa ni pamoja na kuweka mahusiano mazuri na wahisani jambo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuinua uchumi kwa kuuweka imara tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo imefikia wahisani wameamua kupunguza misaada yao kwenye bajeti ya mwaka 2010/2011 kiasi kisichopungua bilioni 297.


Aidha, alisema ingawa hawezi akamuunga mkono moja kwa moja kwa upande mwingine yeye aliona kuna maamuzi magumu aliyowahi kuyafanya ikiwa ni pamoja na suala zima la ubinafsishaji wa mashirika ya umma ambayo yeye ameona kuwa hayakuleta faida.


Mwanasiasa huyo ambaye ni mchumi kitaaluma alisema katika kipindi cha pili cha utawala wa Mkapa kuna mambo ambayo aliyavuruga kwa madai kuwa alinogewa na kujiingiza katika rushwa.


“Mimi nimeona katika kipindi cha pili cha lala salama Mkapa naye aliona fedha tamu akajiingiza katika masuala ya rushwa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa rada, ndege , Kiwira na hatimaye kuanzisha kwa Anben ambayo aliitumia kujipatia kipato,” alisema Profesa Lipumba.


Akizungumzia miaka mitano ya Kikwete alisema rais huyo ameshindwa kudhibiti safari za nje za mawaziri wake na yeye mwenyewe kiasi cha kusababisha kushindwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama chao na kuwaacha wananchi wakiwa katika wimbi la umaskini.


Alisema, Rais Kikwete si makini ndio maana amekuwa akishindwa kuchukua maamuzi yaliyo sahihi ili nchi iweze kuwa na maendeleo yaliyokusudiwa.


Aliongeza kuwa Kikwete amekuwa mwingi wa maneno yasiyo na utekelezaji huku akitolea mfano wa hotuba aliyoitoa Disemba 30, 2005 alipokuwa akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake ambapo aliahidi kushughulikia mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar lakini hakufanya hivyo mpaka pale Wazanzibari walipofanikiwa kuyamaliza wao wenyewe.


Alisema katika utawala wa Kikwete, kulifumka mambo mengi mabaya ya Mkapa yaliyoratibiwa na wapambe wa utawala wa sasa ili kuwafanya wananchi watumie muda mwingi wajikite kuyaangalia zaidi badala ya kufanya shughuli za maendeleo ambazo zingelikwamua taifa kiuchumi.


Anabainisha kimsingi Rais Kikwete hawezi kulinganishwa hata kidogo na Mkapa aliyefanya kazi kwa umakini zaidi bila kuyapa uzito mkubwa majungu yanayotolewa na watu mbalimbali wenye maslahi binafsi.


“Kikwete hamuwezi Mkapa hata kidogo, anayetaka ushahidi wa jambo hilo aangalie maisha ya hivi sasa na wakati ule, leo hii watu wanalala kwa njaa wengine wanapata mlo mmoja kwa siku, dukani unga, mchele, sukari havishikiki kwa bei kubwa; tunakwenda wapi?” alihoji Lipumba.


Tangu kuondoka madarakani, Mkapa amekuwa akiandamwa kwa tuhuma mbalimbali za kutumia vibaya ofisi ya umma (Ikulu) kwa kufanya biashara ambapo inadaiwa alinunua mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao hata hivyo mwaka jana serikali iliutangaza kuurejesha serikalini.


Baadhi ya wanasiasa walifikia hatua ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kushtakiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake wakati akiwa kiongozi.


Mara kadhaa viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamewataka wanasiasa na Watanzania kumuacha kiongozi huyo mstaafu apumzike kwa kuwa amelifanyia mambo mema taifa na hizo tuhuma zinazoelekezwa kwake hazina ushahidi na kamwe hawezi kushtakiwa.


Hata hivyo hivi karibuni Mkapa amejibu tuhuma hizo akisema kuwa hahusiki na umiliki wa mgodi huo na kuwashangaa wale wanaomhusisha na mgodi huku akisisitiza wana lao jambo.


Wachambuzi wa masuala ya siasa walikuwa wakizielezea tuhuma hizo zinazoelekezwa kwa Mkapa ni mbinu mbovu za kuuaminisha umma kuwa kiongozi huyo mstaafu alifanya mambo mabaya ambayo utawala wa sasa unafanya jitihada kuyarekebisha


Source:
Tanzania Daima

My take:
Nafikiri Lipumba kachemka, kuna mambo kibao hajayaongelea ambayo kwa mtazamo wangu naona kwamba Kikwete ameyafanikisha kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na Mkapa. Halafu naona ya kwamba Kikwete ni kiongozi bora sana asiyepaswa hata kidogo kulinganishwa na Mkapa.
 
Lipumba yuko sahihi kwa kiasi kikubwa. Katika kipindi chake cha kwanza, Raisi Mkapa aliongoza nchi vizuri sana; mara nyingi nimekuwa nachukulia kuwa huenda alikuwa anaogopa kufanya madudu asije kukemewa na Nyerere. Baada ya Nyerere kufariki, ndipo Mkapa akawa kichwa ngumu katika kipindi chake cha pili na kuanza kuboronga. Mabaya yote yaliyofanbywa na Mkapa ambayo ndiyo wananchi wengi wanakumbuka ni yale aliyofanya katika kipindi cha pili; alipoanza kuwa mjasiliamali basi akauza nchi yote kwa mabavu hata pale ambapo ilikuwa ni wazi kabisa kuwa uamuzi wake haukuwa na faida kwa nchi; alichjali zaidi ni msalahi yake binafsi kuliko yale ya taifa. Unfortunately, historria huwa inajua kuadhibu watu wa aina hiyo kwa sababu huwa inakumbuka zaidi mabaya yao kuliko mema yao.

Kwa upande wa Kikwete, siyo kweli kuwa hajafanya mazuri. Kikwete amefanya mambo kadhaa yanayoheshimika kimataifa; kwa mfano alikuwa msitari wa mbele katika kutatua migogoro ya kisiasa ya Kenya na Zimbabwe, amesaidia sana kujenga amani katika eneo la maziwa makubwa, na mengineyo mengi katika bara la Afrika. Utawala wake pia umeimarisha urafiki na nchi za nje hasa Marekani ambapo siku hizi tu watalii wengi wa Kimarekani wanakwenda Tanzania kuliko Kenya, kinyume na zamani. Ameiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa mwenyeji wa mkutano wa WEF ambao umekuwa ukifanyikia Davos miaka yote. Kwa hiyo ana mambo mazuri aliyofanya ingawa yote hayo hayamsaidii raia wa kawaida aliyepiga kura na kumpangisha Kikwte kwenye lile kasri la Magogoni.
 
Mkuu Kichuguu usisahau pia kwamba Mwalimu alishaanza kukemea maamuzi mengi ya Mkapa katika awamu yake ya kwanza.
 
Lipumba yuko sahihi kwa kiasi kikubwa. Katika kipindi chake cha kwanza, Raisi Mkapa aliongoza nchi vizuri sana; mara nyingi nimekuwa nachukulia kuwa huenda alikuwa anaogopa kufanya madudu asije kukemewa na Nyerere. Baada ya Nyerere kufariki, ndipo Mkapa akawa kichwa ngumu katika kipindi chake cha pili na kuanza kuboronga. Mabaya yote yaliyofanbywa na Mkapa ambayo ndiyo wananchi wengi wanakumbuka ni yale aliyofanya katika kipindi cha pili; alipoanza kuwa mjasiliamali basi akauza nchi yote kwa mabavu hata pale ambapo ilikuwa ni wazi kabisa kuwa uamuzi wake haukuwa na faida kwa nchi; alichjali zaidi ni msalahi yake binafsi kuliko yale ya taifa. Unfortunately, historria huwa inajua kuadhibu watu wa aina hiyo kwa sababu huwa inakumbuka zaidi mabaya yao kuliko mema yao.

Kwa upande wa Kikwete, siyo kweli kuwa hajafanya mazuri. Kikwete amefanya mambo kadhaa yanayoheshimika kimataifa; kwa mfano alikuwa msitari wa mbele katika kutatua migogoro ya kisiasa ya Kenya na Zimbabwe, amesaidia sana kujenga amani katika eneo la maziwa makubwa, na mengineyo mengi katika bara la Afrika. Utawala wake pia umeimarisha urafiki na nchi za nje hasa Marekani ambapo siku hizi tu watalii wengi wa Kimarekani wanakwenda Tanzania kuliko Kenya, kinyume na zamani. Ameiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa mwenyeji wa mkutano wa WEF ambao umekuwa ukifanyikia Davos miaka yote. Kwa hiyo ana mambo mazuri aliyofanya ingawa yote hayo hayamsaidii raia wa kawaida aliyepiga kura na kumpangisha Kikwte kwenye lile kasri la Magogoni.

Kichuguu nadhani pana mambo unayasahau kwanza kabisa mafanikio ya Mkapa yalikuwa katika macroeconomics ambapo mabarabara, mashirika kuuzwa kama njugu, Foreign Direct Investments,etc yalikuwa yameongezeka kwa kiwango fulani lakini kwa mwananchi wa kawaida kuna hakuwa akiyaona haya.

Maisha yalikuwa magumu, gap baina ya maskini na matajiri lilikuwa linakuwa na corruption within political system ikawa inakuwa. Haya maswala yakachangia upande fulani kurejesha maendeleo ya nchi.

Sasa, Kikwete pia lazima apewe credit for some of this issue mfano infrastructural wise anajitahidi sana tu, kupunguza gap alikuja na pesa za Kikwete zikaliwa it is a completely disaster but malengo yalikuwa mazuri. Akaja na Bailout is a good policy kwa fiscal stimul is essential to stimulate current economies sijui pesa zimeenda wapi but it is a good policy.

Let us be honest kikubwa Kikwete ana-lack ni watendaji wabovu tuseme kweli. Soga nyingi utendaji zero. Malengo mazuri but no implementation. Sasa to some extent yanazidisha matatizo ya wananchi.
 
Mkapa was the best prezda.

In what aspects???? Kwa maamuzi yes he is a good president but Kikwete sio mbaya nadhani anahitaji kuwa straight forward president ila again we go back watendaji hana akiwa nao anaweza kuwa rais mzuri.
 
Kabla ya mashirika ya umma kuuzwa mnaomlaumu Mkapa. Lakini inatakiwa pia kukumbuka ktk kipindi Cha Nyerere na Mwinyi ni makupuni mengi yalikufa kuliko aliyoyauza Mkapa.

Na makapuni mengi yaliyokufa kipindi hicho , baadhi yake Mkapa aliyafufua na kuyapiga bei. Watanzania naona wanapenda kuangalia likampuni limekufa kuliko kuliuuza kwa bei nafuu na hapo hapo likaajiri wa tanzania zaidi ya elfu kadhaa na kusongesha maisha mbele.
 
Ingawa huwa simfagili Mkapa hasa hasa kwenye suala mikataba ya madini, rada na ndege ya raisi na mengineyo ambayo yanafichika na misaada mingi tuliopewa wakati huo na kuongezeka kwa kipato kutokana na mrahaba wa asilimia 3, na fedha za kuuza mashirika ya umma, na kuuza holela kwa Nyumba za Serikali alikuwa ana nafuu kidogo kwenye suala la maamuzi magumu, nidhamu kazini etc tunaweza kusema kwamba Lipumba amechambua vizuri toauti ya ya Jakaya Kikwete na Mkapa, so kama Maksi Mkapa 51% (c) wakati Kikwete 45%
 
In what aspects???? Kwa maamuzi yes he is a good president but Kikwete sio mbaya nadhani anahitaji kuwa straight forward president ila again we go back watendaji hana akiwa nao anaweza kuwa rais mzuri.

Wakati Mkapa anaingia madarakani wafanyakazi mshahara kwa wafanyakazi wa serikali mshahara ulikua haujulikani utalipwa lini na for ur info ndo kipindi hiki vyuo vya ualimu vilifungwa na ni mda mrefu sana waalimu hawakuajiliwa. Ni wakati huu wafanyakazi waliacha kazi na NDIO WAKATI HUU elimu ilishuka na konsekwensi zake ndo tunaziona saizi, watu wanalalamika lakini source yake ni ileeeeeeee.

Kipindi hiki amini usiamini mzee wangu ali quit kazi serikalini na kwenda kuchimba madini bunyakulu ya shimo kuingia mita kadhaaaaaaa alikaa huko na hata hivyo hakuambulia hata dhahabu moja na alikaa karibu mwaka na aliporudi akarudi kazini kwake bila kuwajibishwa utoro, sasa utamwajibisha vipi utoro wakati mshahara wenyewe walikuwa hawalipi.?

Mkapa mwandameni tu, lakini ametutoa ktk BOTTLE NECK kimaajabu sana.
 
Back
Top Bottom