Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

mkapa mwanzoni alifanya nchi iitwe nchi , biashara hewa ilikufa, tra ilikusanya kodi nyumba zote za serikali zikang'arishwa hadi kuwepo air condition, na kapeti, kiwango cha elimu na ajira vikapanda, kajenga shule nyingi na barabara, ila kilichomualibu ccm ambayo ni chukua chako mapema ngwe ya pili ilikuwa ni kuaribu, akaanza na epa kiwira, iptl migodi meremeta anabem, benk m akiwa ikulu, lakini ili tatizo aliletewa na mkewe kwani ni mchagga awezi acha asili yake ya wizi

lol....
 
Sio siri Mkapa alikuwa na matatizo yake ila alikuwa Rais mwenye maamuzi na msimamo. Hakuwa indecisive kama huyu tuliye nae. Natoa tu mfano mmoja. Kuna wakati Valambia aliishtaki serikali kuhusu rada na mahakama kuu ikaamrisha serikali ilipe shilingi bilioni 50 plus interest. Mkapa alikataa akasema mkataba ulikuwa wa hila na mkawaambia waziri wa fedha, gavana na mwanasheria mkuu kuwa kama pesa ikilipwa nao wajiuzulu. Ilibidi wapeleke sheria bungeni kuzuia mtu kushika mali za serikali. Pesa haikulipwa hadi leo na Valambia mwenyewe na mwanasheri wake Maira wameshafariki. Huyu ndie rais anayejua kuwa maslahi ya mafisadi hayawezi kuwa juu ya maslahi ya nchi. Kwanini Kikwete asifanye hivyo? Narudia, hii hela ikilipwa serikali itaanguka.

Mkapa ni Rais.

Tatizo lake akinywa pombe-kali anakuwa mropokaji...kama majuzi alipowaita Watz 'kokoto'

huyu mkwere tushirikiane tu kuhesabu siku zake za kuwa ikulu.
 
KIWIRA ni MAJONZI YAKE,IPTL,EPA,TRA NA KESI ZA KINA MRAMBA HAPANA ALIKUWA KIONGOZI MBAYA

Huu uchafu ulifanywa dakika za mwisho za uongozi wake. Na inasemekana alirubuniwa na wanamtandao waliokuwa wanaandaa programu nzima ya kumwingiza kikwete madarakani.

Vyovyote iwavyo, huwezi ukalinganisha kikwete na mkapa kwa kigezo chochote kile. Udhaifu wa kikwete ni wa kihistoria na sidhani kama atakuja atokee rais kituko hapa tanzania kama jk. Hata akina mugabe hawako weak kama mkwere, tuwe wakweli.
 
WanaJF,
Mnanipata hapo? Hakika pamoja na mapungufu yote mzee nkapa, bado ni kidedea kwa kikwete katika vigezo vyote vya kiongozi bora. Leo hii nchi yetu imekuwa boya linaloelea majini na kupigwa na mawimbi kila upande. Kwa trend hii, miaka 5 naona kama ni karne.
 
Back
Top Bottom