armanisankara
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 283
- 49
Africa hatuna utamaduni wa viongozi wetu kujiuzulu ingekua America au Europe sawaKuibuka kwa kashifa mpya inayomhusu katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini inaacha maswali mengi kuliko majibu. Katibu mkuu huyo anadaiwa kuipa tender kampuni ya PUMA ya kuiuzia IPTL mafuta mazito ya kufua umeme kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma. Taarifa zinasema aliingilia uamuzi wa TANESCO wa kuipa kampuni nyingine kazi hiyo kwa kile kinachodaiwa ni tofauti ya bei.
Hata hivyo gazeti la Nipashe la leo trh 26/07/2012 ambalo pia linapatikana online limetoa taarifa ambayo mimi imenishangaza kuwa waziri mkuu anafanya juhudi za kumtetea katibu mkuu huyo. Taarifa katika gazeti hilo zinasema Waziri Mkuu amekutana na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini akiwasihi waachane na mpango wao wa kutaka katibu mkuu huyo awajibishwe. Swali, kwanini waziri mkuu anamtetea mtu aliyevunja sheria badala ya kumshauri raisi amuwajibishe? Je ametumwa? Na kama ametumwa ni nani kamtuma na kwa faida ya nani?
Watanzania hebu tutafakari mambo haya yafuatayo alafu tujiulize ni kwanini raisi na waziri mkuu wasijiuzulu au wawajibishwe
1. Kwanini wizara hii imekuwa kinara wa ufisadi tangu Kikwete aingie madarakani na ni hatua gani za kuridhisha zimechukuliwa mpaka leo?
2. Hivi viongozi hawa wakuu na bodi ya wakurugenzi wa TANESCO hawakujua kuwa shirika linahujumiwa ktk bei ya mafuta mpaka huyu katibu mkuu mpya bwana Maswi alipoingia ufisini na kama walijua mbona walikaa kimya?Ina maana na wao wanapata taarifa hizi kupitia vyombo vya habari?
3. Ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa richmond?
4. Kwanini mamlaka ya uteuzi ambayo ni raisi huwa haichukuia hatua kwa wakati mpaka bunge limshinikize?
5. Kwanini waziri mkuu anamtetea mtu alievunja sheria badala ya kushauri awajibishwe?
6. Watendaji wa wizara na TANESCO kutokuwa na hofu ya ufisadi ni nani anawapa kiburi na kuwalinda licha ya mlolongo wa matukio ya wenzao kuwajibishwa?
7. Je, wanayafanya haya kwa maelekezo ya wakubwa na ndio maana hawana hofu licha ya kujua hatari inayowakabili?
8. Je, ni kweli wakubwa wao wa kazi wanakuwa hawajui kinachoendelea mpaka taarifa hizi zifike kwenye vyombo vya habari?
9. Waziri mkuu hata kama hana mamlaka juu yao na labda hapati ushirikiano mbona hajiuzulu?
10. Mkurugenzi mkuu TANESCO amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi; Je katibu mkuu wa wizara ambae kwa mazingira ya sasa nae ni mtuhumiwa ni sahihi kuendelea kuwepo ofisini mpaka leo? Au mpaka bunge lije juu?Hii sio aibu na fedheha kwa mamlaka ya uteuzi?
Maswali ni mengi kuliko majibu.Wahusika mjitafakari na muwajibike. Tumechoka kila siku wizara moja tu.
Unahitajika uchunguzi huru tena wa vyombo vya nje maana hata kwenye richmond uchunguzi wa ndani ulificha baadhi ya taarifa kwa kile kilichodaiwa kuokoa serikali.