Kashfa mpya Nishati na Madini; Kikwete na Pinda wajiuzulu au wawajibishwe!

Swali nimeuliza hamkulijibu.. Why Tanesco ndio wanunue mafuta kwa ajili ya IPTL? Kwa nini IPTL wenyewe wasinunue mafuta wanakotaka wao sii lazima Puma. Mafuta is part of their expenses, wayanunue wao kisha wao wawauzie Tanesco umeme.

Jibu ni moja tu IPTL na mashirika yote ya kuzalisha umeme ni mali za viongozi wetu.. we are all paying for their expenses lakini hamtaki kutazama huko na sasa mnawavutia na

bomba la gas watumalize vizuri. Tunagom,bana na Tanesco
lakini hatutaki kutazama IPTL na Symbions na mashirika haya y
alokuwa ya dharura leo ndio yameshika uchumi wa nchi..

Wacha nikupatie Jibu!
Tatizo ni kubwa kuliko mnavyoliona vijana. Niwakumbushe kidogo history . Matatizo ya uzalishaji Umeme yalianza kujitokeza kwa Mara ya kwanza 1992 na Serikali ya CCM Waziri wa nishati alikuwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Waliamua kuagiza mitambo ya dharura ya kuzalisha Umeme kwa kutumia Jet A1 . Tatizo mitambo ya Umeme au turbines zilinunuliwa off shelf na hapo ndipo Serikali iliingia choo cha kike. Mitambo ilikuwa inaendeshwa kwa gharama kubwa sana na kwa kuwa Serikali ya Mzee Ruksa haikuwa makini na Waziri Dhaifu walibuni mpango wa kufua Umeme kwa kutumia Mwekezaji IPTL. Mkataba ulifanyika kwa njia isiyokuwa sahihi kwa maana kwamba Wizara iliingia Mkataba ambao ilikuwa na kipengele cha kuwapatia Mafuta but funny enough wakaweka na kulipwa Capacity Charge ya USD 3milioni kwa mwezi. Kwa kifupi ndilo chimbuko la kuwanunulia Mafuta IPTL . Utaratibu huu ni wizi mtupu inside out hata hivyo Serikali ya Mkapa ilifumba macho na actually ufisadi ilikuwa mbaya Zaidi kwani sehemu au nusu ya capacity charge ilikuwa inalipwa na Hazina wastani wa Tshs 1.5 Bn kwa mwezi pamoja kwamba mashine zilikuwa uazifanyi Kazi na nusu ilikuwa inalipwa na Tanesco hadi mwaka 2005.

Cha kushangaza hata mikataba ya Mhando na Symbion / Aggreko inaitaka Tanesco iwanunulie Mafuta kwenye mitambo ya hao wezi iliyopo Tegeta, Ubungo na Dodoma na hata itakayofungwa kule Arusha it's alll ulaji left and right na wanaofaidi ni watu wachache ambao ndio wanamtetea kwani ndiye last card ya mhimili wa ufisadi baada ya kuondolewa Jairo na Ngeleja. Hata Bodi huwekwa watu soft ambao hupewa mgao na kuifanya Tanesco kuwa shamba la Bibi? Wacheni kusikiliza hear say just read all these have been said and written widely including hata Songas ?
 
Pinda ningependekeza anyongwe kama yeye alivyo pendekeza kwa wengine.huyu ni mnafiki sana.

Jk afungwe maisha.
 
Lakini mimi nina tatizo moja tu ya kwamba Mhando ni sehemu tu yan matatizo yote. Utamwondoa Mghando na kumweka mtumwingine ambaye atakuta utaratibu ni ule ule. Nimesema wazi hata mimi leo ukinambia nishike nafasi hiyo Tanesco nitavuta na kuwapa ndugu na jamaa zangu tender kwa sababu tatizo zima ni la kimfumo sio nani anaweza kutokuwa na tamaa..

Huu mpango wa kukata matawi wakati unajua kabisa mti mzima umeoza ndio naupinga miye.. Viongozi wangapi wameshakuja Tanesco toka Mwinti aondoke au IPTL kuinga mkataba.. Tumebadilisha viongozi wee hadi tunaishiwa watu kwa sababu hatutaki kukubali ama ku face the real problem..

Mfumo mzima wa mikataba na utawala ni mibovu kwa nchi yote. Hapa kilichobakia ni kata mti panda mti - ndio tutaweza pata miti safi.. Kupurura matawi ya mti ulooza unauwezesha mti kukua kustawi tena japo umeoza!..Hivi mnafikiria Ufisadi kufikia stage hii iloyopo leo ni bahati mbaya?..

''INSANITY is doing the same thing, over and over again,but expecting
different results''
Quotes from Albert Einstein.

Huyu jamaa Albert Einstein alikuwa sahihi kabisa na tafsiri ya neno KICHAA. Kwamba ukichaa ni kufanya jambo lile lile kwa mara nyingi huku ukitegemea matokeo tofauti. Sasa hii maana ya UKICHAA inaeleleza vizuri sana kuhusu Serikali na TANESCO. Kinachofanyika kuhusu TANESCO ni wendawazimu au ukichaa uliopitiliza!!

Kwa mtindo huu hakika tatizo la umeme Tanzania halitaisha mpaka siku ya kiyama. Vigogo wa serikali ya CCM na mafisadi wao walishageuza TANESCO kuwa ATM yao.Kila kukicha jamaa wanaenda kuchota tu!!!Mbona kazi ipo nji hii!!!!
 
Haya ndiyo mambo yanawaumiza sana wazanzibar wanapoyasikia ndiyo wanahitaji wawe kivyao HAWATAKI MUUNGANO. Sababu mila na taratibu za kwao wizi haramu sasa wanashangaa viongozi wenye asili ya huko wamekuwa wezi wameambukizwa na washenzi wa bara! mpaka naita washenzi ni wamezidi wapumbavu kila siku nyimbo ni hiyo hiyo huo ni USHENZI, waacheni wastaarabu na nchi bora wakatawaliwe na waarabu kuliko kuishi ...................
 
Pengine mimi niulize tofauti na swala zima.. Kwa nini iwe kazi ya Tanesco ndio wachague nani awa supply mafuta IPTL iikiwa IPTL ni shirika binafsi na linajitegemea kuzalisha umeme na kuwauzia Tanesco Umeme? kwa nini iwe jukumu la Tanesco ambaye ni mnunuzi wa umeme kutoka IPTL ndiye ampe mtaji IPTL kuendesha mitambo yake?....hamuoni ubovu wa mikataba hii iloingiwa na viongozi wetu wanasiasa isipokuwa ubovu wa uongozi wa Tanesco...

Tunarudi kule kule, serikali yetu imejaa mafisadi na hauna mipaka kabisa, na ajabu kubwa ni kwamba baada ya kuona mafuta yanatugharimu zaidi kuyapa haya mashirika yaliyoletwa nchini kuzalisha umeme wa dharura..Sasa hivi ndio mpango mzima! haya ndio yamekuwa mashirika ya uzalishaji umeme nchini, hakuna mipango yetu wenyewe isipokuwa kupitia kwao. Tunawavutia bomba la gas toka Kusini kwa ajili yao!. Yaani sisi wanunuzi wa umeme toka kwao ndio pia walipaji wakubwa wa matumizi ya kuendesha mitambo yao vile vile...Hii akili kweli jamani..

Kwa nini tusiwe na mitambo yetu wenyewe ya kuzalisha umeme na tuvute bomba la gas kwa ajili ya uwekezaji wa ndani na wa kudumu ktk miradi ambayo tunaipanga sisi wenyewe. Leo tunawauliza mafuta na inatugharimu sana kesho tutawalipia gas vilevile baada ya kutugharimu kuvuta bomba la gas hadi Dar. Hizi gharama za ujenzi wa bomba lazima ziingie ktk gharama ya umeme utakao uzwa na Tanesco sio IPTL au Symbion watakaolipia ni sisi wananchi kupitia Tanesco.

Tukikataa ama mchezo wanazima machine tutawafanya nini?. hasira zetu zote tunarudi kwa Tanesco.. Actually hao IPTL, Symbion na mashirika mengine - what are their expenses for real..kuwa na generator 100mw au 45 tu basi unapewa, kiwanja, supply ya mafuta au gas bure kisha unawauzia tena Tanesco umeme kwa kutumia gharama za Tanesco!.. I mean something is very wrong here!.
Mkandara majibu ya haya yako kwenye post number 3 ya KOMBESANA hatuna budi kubadili mfumo.
 
Last edited by a moderator:
Wacha nikupatie Jibu!
Tatizo ni kubwa kuliko mnavyoliona vijana. Niwakumbushe kidogo history . Matatizo ya uzalishaji Umeme yalianza kujitokeza kwa Mara ya kwanza 1992 na Serikali ya CCM Waziri wa nishati alikuwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Waliamua kuagiza mitambo ya dharura ya kuzalisha Umeme kwa kutumia Jet A1 . Tatizo mitambo ya Umeme au turbines zilinunuliwa off shelf na hapo ndipo Serikali iliingia choo cha kike. Mitambo ilikuwa inaendeshwa kwa gharama kubwa sana na kwa kuwa Serikali ya Mzee Ruksa haikuwa makini na Waziri Dhaifu walibuni mpango wa kufua Umeme kwa kutumia Mwekezaji IPTL. Mkataba ulifanyika kwa njia isiyokuwa sahihi kwa maana kwamba Wizara iliingia Mkataba ambao ilikuwa na kipengele cha kuwapatia Mafuta but funny enough wakaweka na kulipwa Capacity Charge ya USD 3milioni kwa mwezi. Kwa kifupi ndilo chimbuko la kuwanunulia Mafuta IPTL . Utaratibu huu ni wizi mtupu inside out hata hivyo Serikali ya Mkapa ilifumba macho na actually ufisadi ilikuwa mbaya Zaidi kwani sehemu au nusu ya capacity charge ilikuwa inalipwa na Hazina wastani wa Tshs 1.5 Bn kwa mwezi pamoja kwamba mashine zilikuwa uazifanyi Kazi na nusu ilikuwa inalipwa na Tanesco hadi mwaka 2005.

Cha kushangaza hata mikataba ya Mhando na Symbion / Aggreko inaitaka Tanesco iwanunulie Mafuta kwenye mitambo ya hao wezi iliyopo Tegeta, Ubungo na Dodoma na hata itakayofungwa kule Arusha it's alll ulaji left and right na wanaofaidi ni watu wachache ambao ndio wanamtetea kwani ndiye last card ya mhimili wa ufisadi baada ya kuondolewa Jairo na Ngeleja. Hata Bodi huwekwa watu soft ambao hupewa mgao na kuifanya Tanesco kuwa shamba la Bibi? Wacheni kusikiliza hear say just read all these have been said and written widely including hata Songas ?

Mkuu sasa ni nini kifanyike? Tununue machine zetu au tu review hii mikataba ya kimangungo?
 
Taarifa zinasema aliingilia uamuzi wa TANESCO

10. Mkurugenzi mkuu TANESCO amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi; Je katibu mkuu wa wizara
Hapa ndio huwa nasema kuna administrative confusion over who should make these decisions.

Mkurugenzi wa TANESCO moja ya shutuma zake ni kukiuka maagizo ya wizara. Okay? Lakini hapa tunaambiwa Katibu Mkuu ameingilia maamuzi ya TANESCO.

Ushaona hapo? Sasa Wizara Mama na shirika la Umma nani ana mamlaka ya maamuzi?
 
Haya ndiyo mambo yanawaumiza sana wazanzibar wanapoyasikia ndiyo wanahitaji wawe kivyao HAWATAKI MUUNGANO. Sababu mila na taratibu za kwao wizi haramu sasa wanashangaa viongozi wenye asili ya huko wamekuwa wezi wameambukizwa na washenzi wa bara! mpaka naita washenzi ni wamezidi wapumbavu kila siku nyimbo ni hiyo hiyo huo ni USHENZI, waacheni wastaarabu na nchi bora wakatawaliwe na waarabu kuliko kuishi ...................
Zile meli zinazopeperusha bendera za Iran kuna wajanja wachache wamekwiba.
 
Wacha nikupatie Jibu!
Tatizo ni kubwa kuliko mnavyoliona vijana. Niwakumbushe kidogo history . Matatizo ya uzalishaji Umeme yalianza kujitokeza kwa Mara ya kwanza 1992 na Serikali ya CCM Waziri wa nishati alikuwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Waliamua kuagiza mitambo ya dharura ya kuzalisha Umeme kwa kutumia Jet A1 . Tatizo mitambo ya Umeme au turbines zilinunuliwa off shelf na hapo ndipo Serikali iliingia choo cha kike. Mitambo ilikuwa inaendeshwa kwa gharama kubwa sana na kwa kuwa Serikali ya Mzee Ruksa haikuwa makini na Waziri Dhaifu walibuni mpango wa kufua Umeme kwa kutumia Mwekezaji IPTL. Mkataba ulifanyika kwa njia isiyokuwa sahihi kwa maana kwamba Wizara iliingia Mkataba ambao ilikuwa na kipengele cha kuwapatia Mafuta but funny enough wakaweka na kulipwa Capacity Charge ya USD 3milioni kwa mwezi. Kwa kifupi ndilo chimbuko la kuwanunulia Mafuta IPTL . Utaratibu huu ni wizi mtupu inside out hata hivyo Serikali ya Mkapa ilifumba macho na actually ufisadi ilikuwa mbaya Zaidi kwani sehemu au nusu ya capacity charge ilikuwa inalipwa na Hazina wastani wa Tshs 1.5 Bn kwa mwezi pamoja kwamba mashine zilikuwa uazifanyi Kazi na nusu ilikuwa inalipwa na Tanesco hadi mwaka 2005.

Cha kushangaza hata mikataba ya Mhando na Symbion / Aggreko inaitaka Tanesco iwanunulie Mafuta kwenye mitambo ya hao wezi iliyopo Tegeta, Ubungo na Dodoma na hata itakayofungwa kule Arusha it's alll ulaji left and right na wanaofaidi ni watu wachache ambao ndio wanamtetea kwani ndiye last card ya mhimili wa ufisadi baada ya kuondolewa Jairo na Ngeleja. Hata Bodi huwekwa watu soft ambao hupewa mgao na kuifanya Tanesco kuwa shamba la Bibi? Wacheni kusikiliza hear say just read all these have been said and written widely including hata Songas ?
Ndio maana mkuu wanngu nilitaka watu warudi nyuma kufikiria kwanza tumefika fikaje hapa?..Ukisha jua tulikotoka haya yanayotokea leo hii majibu yake ni rahisi kabisa..Hakuna mtu hapa asiyejua kwamba hii mitambo yote inayotumaliza leo hii ni mitambo iliyotokana na swala la DHARURA..

Sawa ulazima wa wakati ule kuwanunulia mafuta ulionekana kwa sababu sisi ndio tulitaka umeme haraka kuziba pengo lilokuwepo hadi pale tutakapo kuwa tayari wakapiga mahesabu na kusema miaka miwili. Na ndio maana mikataba ya mwanzo ilikuwa ya muda mfupi.. Mara ghafla wajanja wakaingia, Tukapigwa na changa la IPTL, hatujakaa sawa Richmond hizi zote japokuwa ziliingia bado ktk mikataba ya dharura lakini dharura isokwisha.. Imeendelkezwa mpaka leo makusudi kabisa..Tunaendelea kuwalipia mafuta na kwa ujinga wetu tunatazama mafuta na ughali wake kumbe kinachofanyika hapa ni kuhakikisha hatuwezi kuenga miradi yetu wenyewe kuhakikisha tunafuta mikataba ya dharura..

Chief
katoa mfano wa usafiri wa kwenda Morogoro na bus la Aboud unamnunulia mafuta halafu ukisha fika Morogoro anakutoza Nauli...Chief mimi nasema sii afadhali hiyo maana ni gharama ya siku moja tu. Kilichofanyika ni sawa na kwamba wewe uliharibikiwa usafiri wako njiani, ukawaomba Aboud wakufiishe Morogoro mkakubaliana utanunua mafuta halafu utalipa nauli.. Kwa sababu ulikuwa na shida ukakubali matumizi makubwa ya siku moja tu... Ukalipa na kupewa ride hadi Moro, deal limekwisha..

Tatizo la Tanesco sasa ni kwamba lile deal la dharura watu (viongozi wa serikali) wakalichezea mchezo sasa likawa ndio mpango mzima - ndio usafiri wako kwa sababu kwanza sii hela unazotoa hazitoki mfukoni mwako halafu pili kumbe Aboud ni bus la mjomba..Kwa hiyo unaweka mkataba kuwa ni lazima usafiri uwe Aboud kila siku, lijazwe mafuta halafu tulipie kodi ya siku kama vile vile unavyokodisha Limo, usafiri usisafiri tozo la siku halishuki iwe umeenda Moro au hapana, kapanda mtu au hukupanda. IPTL ni Limousine tulokodisha kwa msiba usokuwepo..

Halafu mashirika mengine pia yanavutwa ktk kukodisha kwa safari za Mwanza, Mbeya, Arusha wote wanaahidiwa kupewa mafuta na wakati mwingine vipuli wakikwama kabisa halafu bado tunawalipa wote sii nauli bali kukodisha kwa siku nzima...Kama mnakumbuka vizuri tunavyofanya ktk maharusi au misiba huwa tunakodisha Costa kwa siku na huwa tulinalipia mafuta, dereva na cha juu kwa uukodishaji wa siku nzima au safari yenyewe.

Na tukisha maliza msiba ama shughuli za Harusi deal linakufa mwenye Costa anaendelea na biashara zake nasi tutarudi ktk usafiri wetu wa kila siku.. Tatizo la Tanesco huku kukodisha kwa dharura ya msiba huu msiba haiuishi kila siku tunamuua ndugu ili bus likodishwe..Sasa ni kiasi gani kinalipwa kwenye kukodisha bus sio tatizo mama, Tatizo lipo ktk mfumo huu wa kukodisha magari na kuendelea kuua ndugu zetu wakati hakuna msiba wowote..Hizo Costa zimekuwa sasa ndio usafiri wetu wa kudumu, tukiwanunulia mafuta na vipuli halafu sasa imefikia tunawavutia kabisa bomba la gas toka Kusini.

Halafu tunasema Kwa nini Tanesco wanashindwa kujiendesha. aaah kwa sababu mafuta yamenunuliwa ghali wangefanya hivi ama vile kwa nini hawakununua ya rahisi - guyz sisi hatukutakiwa kuwa ktk mpango huu hata kidogo..Mimi nasema hivi kwa nini bado tunakodisha hii mitambo? ilikuwa ya dharura hii dharura itakwisha lini..Hutapata jibu kwa sababu hii kitambo au hizi Costa ni za Viongozi wenyewe..Nchi haina Umeme lakini viongozi wetu wamenunua mashangingi Ma VX kila mmoja wao watu zaidi ya 500.. nina hakika wangechukua gari za thamani chini ya Usd 50,000 tu tungekuwa na mtambo mmoja mkubwa sana wa kutosheleza Dar na vitongoji vyake..
 
Jambo moja ni wazi kuwa sekta ya nishati na madini imeingiliwa left and right na kwa kuwa wanene wa awamu ya nne ni sehemu ya fikra na vitendo vilivyotufikisha hapa kwenye kasha njoo-kashfa nenda-kashfa rudi, tukubaliane kwamba kama waliokuwepo walitumia akili zao zoote za kufundishwa eti na za kwao na madini na nishati ni uozo mtupu, Taifa linahitaji mfumo mwingine na watu wengine kutuongoza

"Problems cannot be solved by the same level of thinking that created them" - Albert Einstein
 
Mkandara, nashukuru sana kwa hii analogy.Natamani mtu redioni aweze kuelezea hili tatizo namna hii ndipo hapo utaona reaction ya hao 14% wenye access ya umeme huo.
 
katibu mkuu ni mzalendo sana. Wale wachumia tumbo waliteua kampuni ya kati inayonunua mafuta kutoka puma, na hivyo kuyafanya mafuta hayo yawe na bei ya juu kwa kiasi cha tzs 3 billion.

Katibu mkuu akagoma, akailazimisha tanesco kuchukua mafuta moja kwa moja toka kwa puma bila ya mtu wa kati. Huyu ni mzalendo, ameokoa tzs 3 billion ambazo watu walitaka wazivune eti kwa kutoa mafuta puma na kuyapeleka iptl.

Kwa jinsi serikali mpaka wabunge walivyo wachumia matumbo, si kitu cha ajabu wakamng'ang'ania katibu mkuu mpaka atolewe. Maana hawa wezi ni syndicate kubwa, wana watu wao kila mahali, ndani ya bunge, ndani ya kamati za bunge, kwenye baraza la mawaziri mpaka kwa watendaji wa serikali.

Na nchi yetu hii ilivyojaa wezi ni vigumu sana mtu mwadilifu kudumu kwenye nafasi za maamuzi.
kwa wiki mbili tu zimeokolewa shs 3bn, mnataka nini tena? Hawa ni masujaa tuache majungu na propaganda za kisiasa. Big up prof na wenzako.
 
Kuibuka kwa kashifa mpya inayomhusu katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini inaacha maswali mengi kuliko majibu. Katibu mkuu huyo anadaiwa kuipa tender kampuni ya PUMA ya kuiuzia IPTL mafuta mazito ya kufua umeme kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma. Taarifa zinasema aliingilia uamuzi wa TANESCO wa kuipa kampuni nyingine kazi hiyo kwa kile kinachodaiwa ni tofauti ya bei.

Hata hivyo gazeti la Nipashe la leo trh 26/07/2012 ambalo pia linapatikana online limetoa taarifa ambayo mimi imenishangaza kuwa waziri mkuu anafanya juhudi za kumtetea katibu mkuu huyo. Taarifa katika gazeti hilo zinasema Waziri Mkuu amekutana na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini akiwasihi waachane na mpango wao wa kutaka katibu mkuu huyo awajibishwe. Swali, kwanini waziri mkuu anamtetea mtu aliyevunja sheria badala ya kumshauri raisi amuwajibishe? Je ametumwa? Na kama ametumwa ni nani kamtuma na kwa faida ya nani?

Watanzania hebu tutafakari mambo haya yafuatayo alafu tujiulize ni kwanini raisi na waziri mkuu wasijiuzulu au wawajibishwe
1. Kwanini wizara hii imekuwa kinara wa ufisadi tangu Kikwete aingie madarakani na ni hatua gani za kuridhisha zimechukuliwa mpaka leo?
2. Hivi viongozi hawa wakuu na bodi ya wakurugenzi wa TANESCO hawakujua kuwa shirika linahujumiwa ktk bei ya mafuta mpaka huyu katibu mkuu mpya bwana Maswi alipoingia ufisini na kama walijua mbona walikaa kimya?Ina maana na wao wanapata taarifa hizi kupitia vyombo vya habari?
3. Ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa richmond?
4. Kwanini mamlaka ya uteuzi ambayo ni raisi huwa haichukuia hatua kwa wakati mpaka bunge limshinikize?
5. Kwanini waziri mkuu anamtetea mtu alievunja sheria badala ya kushauri awajibishwe?
6. Watendaji wa wizara na TANESCO kutokuwa na hofu ya ufisadi ni nani anawapa kiburi na kuwalinda licha ya mlolongo wa matukio ya wenzao kuwajibishwa?
7. Je, wanayafanya haya kwa maelekezo ya wakubwa na ndio maana hawana hofu licha ya kujua hatari inayowakabili?
8. Je, ni kweli wakubwa wao wa kazi wanakuwa hawajui kinachoendelea mpaka taarifa hizi zifike kwenye vyombo vya habari?
9. Waziri mkuu hata kama hana mamlaka juu yao na labda hapati ushirikiano mbona hajiuzulu?
10. Mkurugenzi mkuu TANESCO amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi; Je katibu mkuu wa wizara ambae kwa mazingira ya sasa nae ni mtuhumiwa ni sahihi kuendelea kuwepo ofisini mpaka leo? Au mpaka bunge lije juu?Hii sio aibu na fedheha kwa mamlaka ya uteuzi?

Maswali ni mengi kuliko majibu.Wahusika mjitafakari na muwajibike. Tumechoka kila siku wizara moja tu.

Unahitajika uchunguzi huru tena wa vyombo vya nje maana hata kwenye richmond uchunguzi wa ndani ulificha baadhi ya taarifa kwa kile kilichodaiwa kuokoa serikali.
Huu ndio ubaya wa kukurupuka bila kufanya utafiti na upembuzi yakinifu kuhusu suala zima kuhusu Katibu Mkuu Maswi. Matokeo yake mtu mzima Kama wewe unakutana na Rungu la Kipepe la uso,unaanguka chini kuona minyota inakuzunguka.

Katibu Mkuu alifanya hayo maamuzi kutokana na manufaa ya Taifa na Wananchi. Sina haja ya kuandika maneno mengi,Ila Wabunge wameongea na kuweka sawa shutuma na hila mlizokuwa mnatumia MAFISADI.
MENGI TUTAYAONA MPAKA KUFIKIA 2015. Eeeeeh MUNGU TUNAOMBA UZIMA.
 
Jambo moja ni wazi kuwa sekta ya nishati na madini imeingiliwa left and right na kwa kuwa wanene wa awamu ya nne ni sehemu ya fikra na vitendo vilivyotufikisha hapa kwenye kasha njoo-kashfa nenda-kashfa rudi, tukubaliane kwamba kama waliokuwepo walitumia akili zao zoote za kufundishwa eti na za kwao na madini na nishati ni uozo mtupu, Taifa linahitaji mfumo mwingine na watu wengine kutuongoza
kwanini kuna kashfa nenda kashfa rudi?,
 
kwa wiki mbili tu zimeokolewa shs 3bn, mnataka nini tena? Hawa ni masujaa tuache majungu na propaganda za kisiasa. Big up prof na wenzako.
Mkuu wangu vipi jamani?.. Zimeokolewa Bil 3 kwa wiki mbili ambazo hatukutakiwa hata kulipa senti tano kama tusingekuwa ktk mitakaba hii leo. Wote hawa wapo ktk mfumo fisadi wakimtumikia bwana toka huyo Mhando hadi Maswi na wengine wote. Miaka saba ya JK tumeshindwa kusimamisha mitambo yetu wenyewe kutosheleza hiyo Dar tu tunaliwa sasa kweli itakuwa vipi kwa nchi nzima..

Hivi mmeshajiuliza ni kiasi gani tunapoteza kila mwaka hata iwe kwa bei nusu ya hiyo za Maswi wakati haikutakiwa, halafu unaambiwa ati Puma Energy ni shirika ambalo serikali ina hisa zake, sasa kama serikali ina hisa kwa nini serikali iwauzie tena Tanesco (shirika la Umma) mafuta waliyanunua kwa fedha za walipa kodi..halafu wao wayapeleke IPTL bure?..Eeeeh, hellooo.. is any one home?
 
Huu ndio ubaya wa kukurupuka bila kufanya utafiti na upembuzi yakinifu kuhusu suala zima kuhusu Katibu Mkuu Maswi. Matokeo yake mtu mzima Kama wewe unakutana na Rungu la Kipepe la uso,unaanguka chini kuona minyota inakuzunguka.

Katibu Mkuu alifanya hayo maamuzi kutokana na manufaa ya Taifa na Wananchi. Sina haja ya kuandika maneno mengi,Ila Wabunge wameongea na kuweka sawa shutuma na hila mlizokuwa mnatumia MAFISADI.
MENGI TUTAYAONA MPAKA KUFIKIA 2015. Eeeeeh MUNGU TUNAOMBA UZIMA.
nimeipenda sana signature yako,:A S 465:
 
Mkandara said:
Swali nimeuliza hamkulijibu.. Why Tanesco ndio wanunue mafuta kwa ajili ya IPTL? Kwa nini IPTL wenyewe wasinunue mafuta wanakotaka wao sii lazima Puma. Mafuta is part of their expenses, wayanunue wao kisha wao wawauzie Tanesco umeme.

Jibu ni moja tu IPTL na mashirika yote ya kuzalisha umeme ni mali za viongozi wetu.. we are all paying for their expenses lakini hamtaki kutazama huko na sasa mnawavutia na

bomba la gas watumalize vizuri. Tunagom,bana na Tanesco
lakini hatutaki kutazama IPTL na Symbions na mashirika haya y
alokuwa ya dharura leo ndio yameshika uchumi wa nchi..

Mkuu Mkandara, kwa jinsi ninavyoelewa ni kwamba IPTL iko chini ya RITA (mufilisi) kutokana na kesi iliyofungiliwa na TANESCO miaka kama 3-4 iliyopita. Jaji wa hiyo kesi alikubali kwamba kwa kuwa IPTL iko chini ya mfilisi wakati mitambo yao bado ni mizima hivo basi haina budi TANESCO waendelee kuitumia hiyo mitambo kuzalisha umeme lakini mafuta wanunue wao. Kumbuka pia kipindi hicho kuna baadhi ya wabunge wa CDM walioshauri kuwa serikali iitaifishe kabisa hiyo mitambo.
 
nimeipenda sana signature yako,:A S 465:
Asante sana ndugu yangu. Nafikiri tukiweka U-Tanzania mbele bila kuzingatia Itikadi za vyama vya Siasa tunaweza kulikomboa Taifa letu kwenye mikono ya MAFISADI.
YES WE CAN.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom