Karibu Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro

Tuache ushabiki kwa kuwa tumesoma chuo fulani, ukweli ni kwamba wanafunzi wengi wanaodahiliwa sua ni wenye ufaulu wa division two ama three kwa course zote kwani wanaofaulu vizuri sana kwa masomo ya sayansi huwakuti sua kama ni pcb wenye division one wapo muhimbili na kwingineko wakisoma medicine and other medical courses,, pcm utawakuta coet, egm hawakimbilii agribusiness wengi wenye division one hukimbilia BAF mzumbe na economics pia actuarial science ya udsm. Wengi waendao sua kwa mapenzi na wamefaulu vizuri sana ni wale wenye masomo ya kilimo kwenye combinations zao za a-level.. Lakini pamoja na hayo bado misingi iliyopo sua inatoa vijana wenye competence ya kutosha kwenye soko la ajira kwani ufaulu wa kidato cha sita si guarantee ya kumfanya mtu awe vizuri sana chuoni na baada ya hapo. Umaarufu unakosekana kutokana na nature ya course nyingi zinazotolewa sua (course za kilimo) kuwa si zinazopendwa na kutajwa na wengi ndio maana vijana wanaomaliza kidato cha sita hawaisikii sana sua. Ukweli ni kwamba ubora wa mtu kwenye interview haubebwi na chuo alichosoma bali uwezo na vigezo alivyonavyo. Sua ni chuo kikongwe na kizuri.
 
Senetor sina hakika km unaperuzi takwimu na rank mbali mbali ya academic institutions duniani....kwa kukusaidia tu Unapozungumzia kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu vyuo na taasisi za elimu Tanzania utaanza na chuo kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo cha kilimo cha Sokoine...na ukifunua zaidi utagundua kwamba kwa Afrika SUA imesimama sana linapokuja suala la vyou vya kilimo...Fanya utafiti kabla hujaconclude jambo!
mkuu kwa rekodi ya vyuo bora afrika ya mwaka jana na mwaka 2011 udsm ilikuwa ya 12 na baada ya udsm chuo kingine kilichomo ni hebert kahiluki hicho cha sokoinne sijakiona labda we sijui unaelezea rekodi za mwaka gani
 
  • Thanks
Reactions: Wa3
kozi za sua ni maarufu kwa serikali thus hata wananchi wa kawaida hawawezi kuzifahamu mfano mtu aliyesoma bvm anaingia serikalini direct tofauti na mtu atakayesoma baf mzumbe lazima azungunge na vyeti mtaani ndo mana wanakua maarufu
 
Kama umesoma arts (ungwini) huwezi jua habari za SUA. Pale si pa-Ngwini. PCM, PCB,PGM,CBG,CBA n.k ndiyo mahali pao. Labda nikukumbushe Mzumbe siyo chuo cha hivi karibuni. Unakumbuka jina hili " IDM-mzumbe"? Long time mzumbe ipo. SUA ilikuwa ni Faculty of Agriculture of UDSM enzi hizo. labda nikupe ufafanuzi mwingine. Vyuo vilivyokuwa under UDSM enzi hizo:
1. SUA.........(Formally known as Faculty of Agriculuture of UDM)
2.MUHIMBILI univ.(Formally known as Faculty of Medicine of UDSM, later MUCHS)
3.ARDHI Univ. (Formally known as UCLAS- under UDSM)
Hivyo ndg umaarufu unaoutaka kwa wa TZ ni hasa kwa mangwini ambao kazi yao ni kuongea ongea sana. Mtu wa sayansi huwa haongei sana; intergration, differentiation, dissection (cadavor), Chemical reactions, computing science, designing, etc wee unadhani muda wa kuongea utatoka wapi?
 
mbona COET-Udsm,inajulikana na wkt wao nao wanapga sciance,tena sciance ile pure kuliko hyo ya sua ilyochakachuliwa?

pure science wakati mna crame material ya kizungu...ww ni kuku wa kisasa uwezo wako wa kufikiri ni mdogo ka bao la 3
 
kwa nyongeza tu, passmark sua ni 50% and not otherwise. huko kwingine nasikia pass ni 40%. tofauti ya ubora wa wahitimu wa sua na wengineo iko wazi, kwani wa 50% atakuwa fit kuliko wa 40%. sua hukuti walimu wakihangaika na vi-part time, ambapo unakuta eti mwalimu huyohuyo anafundisha udsm, mzumbe, saut, tumaini, mkwawa nk. walimu wa sua wanatumia mda wao kuandika projects za maana, za mabilioni ya shilingi na ku-publish papers. kwa hiyo muda mwingi walimu wa sua huutumia kusafiri sana ulaya, marekani south africa au ndani ya africa, siyo kufukuzia vipart time ambavyo kmsingi vinadhalilisha hadhi ya mwalimu wa chuo kikuu. nyie wala msijisumbuwe na kuweweseka kuhusu sua. sua iko fit sana na ina vision.
 
watu wanaijua ila wanaogopa hata kuisema maana ukienda pale we kuwa tayari kuchora ma-DNA na Prof Mzanila. Kwa sokoni mi sina la kusema maana mi nakula mafao kwa sababu ya musoma Agronomy na MBA-Agribusiness.
 
sua ni chuo bora saana pale research kuandika proposal mtu anatoka ameiva ndo maana weng wao scholarship nikugusa wengi wao wako nje sababu ya ucompitent wao...huwezi fananisha sua na ifm,mzumbe watu ambao hata research hawazijui kazi kuuza sura ..... i like sua a centre of excellence
 
Inashagaza sana wasomi wa Tz mnavyokuwa mnafagilia vyuo vyenu,siku moja nijisikia kuugua baada ya mtu mmoja humu jf kutaja vyuo vya engineering Tz na akaacha chuo mama cha engineering nikaona hata hajui engineering ni nini.Hivi unaweza kulinganisha vyuo viwili au zaidi ambavyo vinafundisha mambo tofauti?Kwa mfano SUA (mambo ya kilimo) unakilinganisha na CBE(mambo ya biashara) sidhani kama uatapata jibu kipi kizuri na akiri yako watu wataitilia mashaka.Na isitoshe chuo si majengo,chuo ni walimu na wanafunzi husika ,chuo chochote kinatangazwa na "product zake".Ulishawahi kwenda kuomba kazi sehemu wakakwambia hapa tunaajiri watu wa chuo A,B na C?Hii ipo kwa baadhi ya ofisi.
Wakati nasoma chuo nilikuwa tofauti na wenzangu ,walikuwa wanawazalau watu wa course fulani ila unajua mwisho wa mtu ni muhimu kuliko mwanzo.Haya fikiria hii,wewe umesoma chuo fulani maarufufu sana hapa Tz na course fulani ngumu sana,mwenzako amesoma huko unakokuzalau lakini amefanikiwa kimaisha zaidi yako,wewe utaendelea kujivunia chuo badala ya kuhustle utoke kimaisha.We have got only one life to live waste no time.

SUA ni chuo cha siku nyingi,nimekaa pale ,washikaji wangu wamesoma pale na wengine wamefundisha pale,kwa miaka ya nyuma,sorry wasuasa kwa kusema hili SUA wanafunzi wake kazi zilikuwa inawezekana ni chache au sijui ni nini inshort wengi walikuwa mtaani na matokeo yake walifanya kazi tofauti na field.Ila kwa sasa SUA wana kazi nyingi na inawezekana si maarufu kwa mtu(wa toto wa .com) ambaye havijui vyuo vikongwe vya Tz kwa sababu kazi zao si huko posta au mijini.Wengi wako kwenye research na vijijini,labda baadhi ya course kama food science wanaajiliwa kwenye viwanda,na tbs.

Umaarufu wa CoET kwa musioijua ,CoET ilianza FoE(Facult of engineering) then pCET(Prospective College of Engineering and Technology) na mwisho ikawa CoET(College of Engineering and technology).Kwa hiyo wote walio soma tangu miaka ile kwa sasa wengi wanajitambulisha kama CoET product.
No one knows everything,si lazima ujue kila kitu.Nilishangaa siku moja mtangazaji wa radio fulani mtu alituma salam akasema yuko DIT,mtangazaji anashangaa DIT ndiyo wapi huko,so tuache ushabiki wa ajabu ajabu tujenge taifa.
Umaarufu si issue,hata ubora wa chuo hautokani na umaarufu wa chuo kumbuka chuo kinaweza kuwa maarufu hapa Tz si academically bali kwa tabia mbaya za wanachuo hao.Ubora wa chuo unatokana na product zake ziko wapi ,zinafanya nini,na zimefanya mambo gani makubwa kwa nchi na dunia kwa ujumla.
 
Nakubaliana na wewe. Wazazi wangu ni wakulima wa matunda. Tumejaribu kutafuta research papers za maembe, machungwa ambayo walinunua sua kakuna kitu. Ilibidi tutafute from websites za kilimo kenya. Hii ni aibu sana, wakati huu wa utandawazi chuo cha kilimo hakiwezi kuwasaidia wakulima.
Nadhani hujui kutafuta research paper halafu usikariri kuwa unapo publish unaandika inchi kuna journal za kimataifa zenye impact fact kubwa ambapo ndio wengi na publish research zao japokuwa mpka ipokelewe ni kazi sana ila watu wanafanikiwa ukipublish kwenye hivyo vi journal visivyokuwa na kichwa wala miguu hakuna anaye soma paper yako karibu tuwajibike mkuu
 
sua hamna pa kwenda bana,tusidanganyane,yan unataka kunambia m2 umesomea mizizi uende kuajiriwa bank alafu ulipwe sawa na m2 mwenye profesional yake ya banking..haingii akilin kabisa.
Nilichokindua kwako hujatafuta hata muda wakujua SUA wanasoma kozi gani na zipo ngapi na zinamlengo gani, jitahidi kuwa mfatiliaji wa mambo hasa kama wewe ni msomi sifa ya msomi ni mtu wa kuongea fact, kuna kozi nyingi sana ikiwemo agricultural economics and agribussness ulizia course content zake ndio ujiulize kwanini wengi wapo CRDB plc au NMB plc n.k
 
Habari zenu wakuu!naomba leo tujadiliane kuhusu hiki chuo kikuu cha sokoine,kwa nini hiki chuo sio maarufu miongoni mwa watanzania,ukilinganisha na umri wake kuwa mkubwa{25yrs} lakn co maarufu kama vilvyo vyuo vingne vichanga kama mzumbe,ifm na iaa,je sababu ni kwamba kozi za sua haziuziki sokon,masomo ya sua ni magumu hvo wanafunz weng wanapaogopa au tatizo ni nin na nin kifanyike ili kuifanya sua iwe maarufu kama ilvo udsm?
Kwanza kabisa mkuu umedanganya hapo kwenye red,
chuo kilianza mwaka 1984,(nasoma hapa), mpaka sasa ni miaka 28, kama umeshindwa kujua hilo basi hujui hata usemalo naomba watu wakusamehe kwa uzi huu, kauze vitunguu
 
Habari wakuu,

Anaeifaham Bsc in bio-processing and post harvest engineering au kama umechaguliwa 2kutane hapa.

Natanguliza shukraan
 
anaeifaham Bsc in bio-processing and post harvest engineering au kama umechaguliwa 2kutane apa

Google - Prospectus yao utapata kila kitu, course weight, no of lectures, assignments, tests, carrier opportunity, etc
 
Nashangaa sana kwa nini SUA mnajiweka nyuma kiasi hicho yaan mpaka sasa waliochaliwa Sua hatujui hatma yetu. Yaani mnashindwa mpaka na hizi mushrooming Universities??
 
Back
Top Bottom