Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

Kanisa katoliki ni kwamba linaongozwa na KANUNI na katiba ya Kanisa. Siyo Kanisa lililoanzishwa kienyeji tu. Na ndio maana ni Kanisa lililoenea DUNIANI na lina uongozi Mkuu Ulimwenguni (PAPA, MAASKOFU, MAKADINARI, MAPADRE, MASISTA, WALEI)

Hivyo ieleweke kuwa ni kanisa lenye utaratibu wake katika kutoa madaraja ya Utumishi wa Kanisa na pia kuna utaratibu wa mtumishi kuacha Utumishi wake. Huwa wanaweka NADHIRI za utumishi wao.

Hivyo kwa Dr. Slaa kutokuendelea na UPADRE ni kutokana na kanuni na katiba za kanisa Katoliki; na ndio maana RAISI wa Baraza la MAASKOFU ametoa kauli hii ya kutaka ushahidi kwa hili.

Kama upo basi uwasilishwe ili hata na mimi niweze kuujua.

WEKENI USHAHIDI HAPA JF TUONE, ACHENI KUKURUPUKA NA KUSIKILIZA MANENO YA VIJIWENI. ni aibu KWA KIONGOZI WA JUU KAMA WASSIRA KUTOA TAMKO KUTOKANA na MANENO YA VIJIWE VYA WANYWA KAHAWA.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

“Mkimchagua Sioi…(1) kura zenu zitamfuta machozi ya kufiwa na baba yake, (2) Atapata mshahara ili kulea familia yake, (3)Mtamfurahisha Rais Kikwete, Alisema Lusinde.," :rant:Signature yako mkuu, mi hoooooohooooooooooooooooooiiiii Yaani nani anataka kumfurahisha kikwete, hapo ndo kaharibu kabisa, maana umo,umo ndani ya CCM kuna watu hawamtaki/hawampendi kikwete, kwa hiyo kwa kuwaambia kura ya mtu itamfurahisha kikwete kwa kweli huyo lusinde amechemka mbaya kabisa, maana wana ccm wengine watatupigia sisi kwa hasira ya kutotaka kumfurahisha kikwete, maana hiyo ndo itakuwa njia nzuri ya kumkasirisha, kama kumpigia sioi kura ndo kutamfurahisha. Jamani JF, kwa kweli sijutii kuwa mwanafamilia wa hapa.
 
Tanapa mnafanyaje tena wanyama (sokwe) wanatoroka mwituni kuja kufanya siasa ambazo hawazijui

huwa nina mazoea ya kuwa serious pale ninapoanza kuperuzi nyuzi za JF, ila hii yako imeifanya misuli 43 ya uso wangu iliyokuwa imekakamaa kuwa ya ucheshi.
 
Malale ni ugonjwa mbaya sana unaoletwa na mbung'o na dalili zake zote anazo mheshimiwa mwenye tumbo namba mbili baada ya yule mbunge anayeimba nyimbo za chama cha kijani!!
 
Kuna kitu kinaitwa dispensation! Kama we ni padre na unataka uache inatakiwa uandike barua kwa pope ukiomba uache.....and this wil take years hadi ukubaliwe kuacha na utafanyiwa uchunguzi mkali na lazima utoe convincing reasons za kuacha. Ndicho alichokifanya dr na his letter was answered after 12 years tangu aandike xo hakufukuzwa kama baadh ya members wanavyodai! Angekua amefanya ufisadi asingekubaliwa ku hand over the office ya TEC akiwa kama katibu. Catholic church ni kanisa lenye sheria zake cio linajiendea tu!!
 
Tanapa mnafanyaje tena wanyama (sokwe) wanatoroka mwituni kuja kufanya siasa ambazo hawazijui

huwa nina mazoea ya kuwa serious pale ninapoanza kuperuzi nyuzi za JF, ila hii yako imeifanya misuli 43 ya uso wangu iliyokuwa imekakamaa kuwa ya ucheshi.

wAJAMENI Mbavu ZANGU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! KICHEKOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!! MMESABABISHA NIMEVUNJA MBAVU KWA KUCHEKA; MMESHANIPA KILEMA WAJAMENI!!!!!!!!!!!!!!!!!!! AAAhahahahahahahahahaahahahhah!!!!!!!!!!!


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
" Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kupona" LK 5"32, Mt. 9:13, Mark 2:17.Hayo ni maneno ya Bwana Yesu. Hainingii akilini jinsi unavyoweza kuwabainisha kuwa hawa ndio wenye wema na uwape mwaliko halafu wengiene useme ni mafisadi ili uwanyime mwaliko. ……..

Kwa lugha fupi tu yesu aliwatia viboko mafisadi ndani ya nyumba ya baba yake,hivi leo swala la uadilifu kwa Watanzania juu ya viongozi wao tena kwa majina acha ya sura linaitaji cheti cha dalasa la saba kuwa na ufahamu kujua nani ni nani na ana sifa gani kwenye jamii.Ebu acha siasa za kizamani tena acha kabisa usiembe kuuliza mkeka au jamvi kwenye msiba wa kitanzania.Tufike sehemu hakika nazi iwe nazi na si nazi iitwe dafu.Leo kanisa la Roman Cathoric duniani linaomba msamaha kwa baadhi ya matendo ambayo yalitendwa ndivyo sivyo miaka ya nyuma ndani ya kanisa,na hiyo ni kuonyesha kuwa kanisa nalo ambalo linaongozwa na binadmu na sio maraika linautashi wa kuona na ndio maana leo hii Papa anathubutu kuomba msamaha na kutembelea hata maeneo yalioyaathirika na matendo hayo yaliyotokea pengine chini ya kanisa.

Leo wewe karne ya ishirini na moja unaendekeza kuwa ni sawa kupokea wanasiasa wasio na sifa njema kwenye umma mbele ya hadhara kubwa ya shughuri muhimu ya Kanisa.

Mie sipingi mafisaid kwenda kanisani kwenye ibada zao siku zao za kawaida kwenye makanisa yao husika,nachopinga ni kanisa kuwa na shughuri yake kitaifa [kama vile kuvika Uaskofu wajimbo,Upadilisho, au sherehe nyingine yoyote ya Kanisa kitaifa] kualika wanasiasa wasio safi kwenye jamii ambao wewe mwenyewe umekili wapo ndio hao unasema protocol haiwezi kuingilia wakiwa wanaongea yasiyostahiki,wakaalikwa kuhudhulia kama wageni rasmi au vinginevyo na hatimae mbele ya vyombo vya habari ambavyo ni muhimli mwingine wa nne wa jamii,wanawashudia kwa kalamu,camera na picha za video kwenye television kisha kuwa taarifa ya umma basi madhara yake ni kanisa kuchafuka kwa kuwa Mwanadamu kama Mwanadamu atatoweka kila mmoja kwa wakati wake lakini kanisa kama kanisa litabaki daima.Ndio maana kuna miji kama bagamoyo na ushirombo kahama kuna madhehebu yalijenga makanisa miaka mia hamsini [150] iliyopita leo hii makanisa hayo yapo na waumini wapya vizazi na vizazi vimepita.

Usiangalie athari za kuwafurahisha wanadamu wachache kuwa wataonekana wametengwa nani aliyewatuma kuwa mafisadi kisha waaende makanisani kuuza sura kuonekana watakatifu.Ebu acha injili za mwaka alobaini na saba.Yesu [Masia] alipowakuta wanafanya biashara ndani ya nyumba ya baba yake [Kwenye sinagogi ] kwa lugha ya sasa tunasema alitembeza kichapo na kisago kwa wote na akuangalia fisadi huyu anamchango wa kuuza sura kuwa kwenye jamii.

Hayo unayoyasema ndio yameliponza kanisa wengine wakadandia misemo hiyo kuhalalisha mialiko ya watu wasio na sifa njema kwenye jamii.Ndio maana leo baadhi yao hawalioni kanisa ni eneo takatifu na sehemu muhimu ya imani ya mwanadamu ambako hakuna binadamu anaengia humo akapimwa kuwa anastahiki kuingia kwa kuwa ana mali au hana, bali kwa kuwa sote ni viumbe wa Mungu mmoja.Kanisa lilikosea ni vyema nao wakajua na kujua nao ni binadamu na kama walitafsiliwa vibaya na baadhi ya waumini, basi waludi kwenye msimamo ule wa Yesu na kuweka mambo sawa kama walivyomwambia Wasira ili kesho na keshokutwa viongozi wa kisiasa wajue kanisa ni zaidi ya siasa,na sio siasa zinaweza kuendesha kanisa ila kanisa linaweza kuendesha siasa, japo kwa mfumo wa Taifa letu mfumo huo hatuku uchagua kutuendeshea Nchi na hivyo Serikali haifungamani na dini yoyote.

Big acha propaganda za kizamani,dunia ya leo so ile ya mwaka alobaini na saba ukishaanga hayo nenda China ukashangae mtoto wa miaka tisa kazaa mtoto mwenzie,kiasi kuwa mtoto aliyezaliwa kashindwa kupitia kwenye njia yake ikabidi afanyie upasuaji kumtoa mtoto mwenzie, Je nani kampa mimba mtoto huyo aliyezaa mtoto mwenzie?

Hakika ukikosa mwongozo wa kitu kama kanisa [Dini] basi si ajabu ukasikia Tanzania mtoto wa miaka sita kazaa kichanga.Ndio maana umhimu wa kanisa [Dini] kwenye mwongozo wa maisha ya binadamu si wa kutiliwa shaka hata kidogo,tuna uwezo wa kutilia shaka siasa na wanasiasa lakini kamwe hatupaswi kutilia shaka madhehebu na viongozi wake kwa kuwa hakika tutakuwa tumemkosea Mungu na pengine tukiwa na hofu na mashaka juu ya dini kwa kuwa dini ni hatua ya mwisho ya imani ya binadamu.

Tunaweza kuyumbishwa na imani za kisiasa za CDM na CCM,kwa kuwa hivi vipo ni vilevi [opium] ambavyo unaweza kubadilisha kesho ukawa CDM keshokutwa ukaludi CCM.Lakini nenda kafanye hivyo kwenye dini kacheze na imani uone madhara yake kwako na kwa wenzio itakavyo kughalimu wewe na wanajamii yako.
 
Hivi huyo Wassira (Mike Tyson) , si ni waziri katika serikali ya JK?
Huyu si ndio shoga mkubwa wa Warioba, aliyemnyang'anya ubunge hadi akaenda Upinzani?
Leo amesahau kwamba hata yeye aliwahi kuwa Mpinzani ananasimama na kukashifu wapinzani?

Hawa ndio viongozi tuliono leo!
Wasimamizi wa Kilimo Kwanza!


Si mnamjua mnyama pekee ambaye akisha kutapika anakula matapishi yake? Pamoja na sura fulani aliyo nayo, tabia zake hazitofautiani na "mbwa koko"
 
Sijui kama wana jamvi mnakumbuka statement hii kutoka kwa Muheshimiwa Steven Wassira enzi hizo akiwa NCCR Mageuzi, "Mimi kurudi tena CCM ni bora nikalale na mama yangu"

Hizo ndio akili za huyu mzee, anyway ndio aina ya viongozi waliopo ccm na ndio policy makers wetu halafu mnategemea kupitia kwao mpate umeme wa uhakika, shule/elimu bora, mipango endelevu n.k, Hakika kama ambavyo yule mzee ambaye huandika makara katika Gazeti la Tanzanina Daima (I think mzee mahega) huwa anasema, "Ni mikosi tu kuwa na viongozi wa namna hii"
 
Jamani!! sasa Wassira naye ni mtu wa kutuumiza vichwa vyetu? tunajua huyu ni hamnazo siku zote, hapo alipo anaelewa kwa kutumia nguvu kubwa, anaelimisha kwa kutumia nguvu kubwa ina maana hatumii akili kamwe!!!
 
Viongozi wa CCM wazidi kuaibika, baada ya Mkapa sasa ni zamu ya wasira ambapo Kanisa katoliki limekana kuwepo kwa ulaji fedha wakati wa ziara ya Papa na kumtaka Wasira atoe ushahidi............... Sinema zaendelea.

Kanisa Katoliki Lamshukia Wasira

LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA

Na Waandishi Wetu

KANISA Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.

Akizungumza kwa simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.

Akizungumza katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi alijibu kwa kifupi: “Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari.”

Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.

“Kanisa halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake,” alisema Ruwaichi.

Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

“Ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa,” alisema.

Askofu Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... “Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele.”

Askofu Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

Kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.

“Kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu,” alisema Dk Slaa.


MY TAKE:
Ni aina gani ya viongozi wa CCM tulionao kila wakati maneno yao yanakanushwa na kubainika kuwa ni uongo? Alianza Mkapa kudanganya sasa kafuata Wasira. Who is next??


Bora baba askofu umeliumbua ilo zee,ni kweli ni watu waliofilisika kifikra ndio uwa wanatunga uongo na kuwachafua wenzao!jitu zee zima linakua liongo
 
dk-slaa-top-safi.jpg
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa​

LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA, NEC YAVIONYA CCM, CHADEMA
Na Waandishi Wetu
KANISA Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.Akizungumza kwa simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.

Akizungumza katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi alijibu kwa kifupi: "Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari."
Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.

"Kanisa halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake," alisema Ruwaichi.

Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

"Ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa," alisema.

Askofu Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... "Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele."

Askofu Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

Kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.

"Kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu," alisema Dk Slaa.

NEC yavionya CCM, Chadema

Katika hatua nyingine, Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeonya vyama vya CCM na Chadema kuacha kampeni chafu baada ya kuthibitika kuwa vimekiuka sheria na maadili ya uchaguzi kutokana na vitendo vya uvunjifu wa amani ambavyo vinafanywa na wafuasi wao.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Trasias Kagenzi akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema vyama hivyo vimeandikiwa barua hizo baada ya kukamilika kwa kikao cha kamati ya maadili ambacho kilipokea barua za malalamiko matano kuhusu mwenendo usioridhisha katika kampeni.

Kagenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, alisema CCM kimepewa barua ya onyo kutokana kitendo cha wafuasi wake kuchana picha na mgombea wa ubunge wa Chadema, Joshua Nassari siku ya uzinduzi wa kampeni zake katika Uwanja wa Ngaresero.

Mwenyekiti huyo alisema Chadema nacho kimepewa onyo kutokana na wafuasi wake kuwakashifu viongozi wa CCM katika eneo la Meru Garden ambako viongozi hao na mgombea wao, Sioi Sumari walisimama kupata chakula.

Alisema malalamiko yaliyojadiliwa ni ya Chadema na CCM na kwamba vyama hivyo viwili vinatuhumiana kwa ukiukwaji wa sheria na maadili ya uchaguzi.

Alisema Chadema katika barua yao ya Machi 12 mwaka huu, kililalamikia wafuasi wa CCM kung'oa picha za mgombea wao wakati wa uzinduzi wa kampeni zao ambazo zilikuwa zimebandikwa katika kontena lilipo jirani na uwanja kulipozinduliwa kampeni.

Alisema malalamiko mengine ya Chadema yaliwasilishwa Machi 14, mwaka huu kuhusu kukashifiwa kwa mgombea wao na CCM kwa matusi mbalimbali na Machi 19 walilalamika kutekwa kwa Mwenyekiti wao wa Kitongoji cha Magadirisho, Nuru Maeda na wafuasi wa CCM na kupigwa.

Kwa upande wa CCM, Kagenzi alisema kiliwasilisha barua ya malalamiko kwamba Machi 12 wafuasi wa Chadema walikaa njia panda kutoka eneo palipofanyika uzinduzi wa kampeni za CCM na kuanza kuwazomea viongozi wa chama hicho na kung'oa bendera za chama hicho kwenye magari na kuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema.

Alisema pia Machi 18 wafuasi wa Chadema waliufanyia vurugu
msafara wa mgombea ubunge wa CCM, katika eneo la Meru Garden na kushambulia magari kwa mawe na gari moja la CCM lilivunjwa vioo.

Kagenzi alisema ni busara vyama vyenye wagombea katika
uchaguzi huo kufanya kampeni kwa kunadi sera za kutoa ahadi wagombea wao wakichaguliwa watafanya nini, badala ya kutoa matusi wakati wote na kashfa dhidi ya wengine.

Pia amepiga marufuku machapisho yote kusambazwa katika jimbo hilo bila ridhaa yake... "Napenda kukumbusha kuwa ni marufuku kwa chama au mtu kusambaza machapisho katika kampeni bila kuwasilisha chapisho hilo ofisi yake ili yaidhinishwe."

Tamko hilo limekuja wakati Chadema wakiwa wanalalamikia kusambazwa kwa nyaraka za uchochezi na kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk Slaa wamekuwa wakilalamikia polisi kusambaza vipeperushi kwenye mikutano yake ambavyo alisema vinalenga kuwatisha raia.

CCM wamgomea msimamizi
Akizungumza na gazeti Dada la The Citizen jana, Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba alisema chama chake hakiwezi kuacha kujibu mapigo ya Chadema na kuongeza kuwa kitaacha kufanya hivyo endapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakiandikia Chadema kukanusha kashfa kilizozitoa dhidi ya mgombea wa CCM Sioi.

"Tunachokifanya sisi ni kuwaeleza wananchi ukweli dhidi ya wapinzani wetu hatutukani watu hapa… hatuwezi kubadili staili hii ya kampeni mpaka tume iwaambie Chadema wafute matusi hadharani dhidi ya mgombea wetu," alisema Nchemba.

Alisema tume inatakiwa kutenda haki kwa vyama vyote huku pia akiwataka wapinzani kutolia katika harakati za mashambulizi ambazo wamezianzisha wenyewe.

Meneja wa Kampeni wa Chadema, Vincent Nyerere alisema chama chake hakijapokea barua yoyote kutoka tume huku akionya kwamba hata kama kutakuwa na barua hiyo, basi walengwa wake ni CCM na siyo chama chake.



Alisema amekuwa mmoja kati ya watu waliokashifiwa na viongozi wa CCM huku akiitaka Tume kuacha upendeleo na badala yake itoe adhabu stahiki kwa chama hicho tawala.

"Hebu tuwaache Sioi na Nassari wapambane katika majukwaa na sio mzee Wassira, Mkapa na Ole Sendeka kutushambulia badala ya kutangaza sera za chama chao, sisi tunaendelea na kampeni za kistaarabu," alisema Nyerere.
Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang'oro Dar, Neville Meena na Mussa Juma, Arumeru.

Chanzo. Kanisa Katoliki lamshukia Wassira kuhusu Dk Slaa
 







  • [h=6]Chris Mahali
    [/h] [h=6]KUNA SIRI GANI ILIYOJIFICHA KATI YA DR WILBROAD PETER SLAA NA ROMAN CATHOLIC??? JE YUPO KWA AJILI YA WATANZANI? KWA AJILI YA CHADEMA? AU ROMAN CATHOLIC?[/h]


 
  • Amin Nguluma Swali langu nililouliza masaa 72 yaliyopita halikujibiwa na tayari ile agenda ya wizi wa Dr slaa imebadilika na sasa kuna agenda ya uhusiano kati ya Slaa na Katoliki.Nilipowataka mueleze agenda yenu ya msingi hamkuwa tayari kukubali kuelewa... kuwa hamjui mumlaumu ama mumchafue dr kwa kutumia agenda gani kati ya yeye kuwa mwizi ama yeye kutumwa na kanisa katoliki.Kinachoonekana hapa wakosoaji wa dr slaa mmeshindwa kumchafua kama mlivyokusudia na sasa mnahangaika kutumia kila njia kutafuta upenyo. Sasa nawapa tena mbinu nyingine ya kumchafua.Dr slaa ni mzinzi,kazini na Rose Kamili mpaka kapata watoto naye,kisha kamchukua mke wa wajina wangu Amin na sasa wanaishi pamoja.Halafu labda wajina wangu AMIN KAJIRU (labda) dr kahonga na ile kesi aliyofunguliwa na wajina wangu imeyeyuka.Mna jingine la kumbambikizia DR.See More
    2 hours ago · LikeUnlike · 1




  • Chris Mahali ‎@amin hakuna aliyembambikiza hapa na punguza jaziba kidogo kaka pamoja na zefania pia swala la mke ni agenda ya nje hapa lijazungumzwa ndani ya hili swali . kwani ni uongo dr ayupo kwa ajili ya roman na ndo mana hata kanisa limemtetea unataka nini tena mkuu zaid ya kubabaika 54 minutes ago · LikeUnlike




  • Chris Mahali ‎@bruno umeona picha iliyowazi na kanisa limembea dr sasa mnabisha nini??
 
Naona wana ccm wameamua kuwa wapuliza vuvuzela wa nguvu. Kila mtu anazuka na uongo wake. Mwishae siku wakisema jambo la kweli watu hawatazingatia kwa kudhani ni uongo wao wa siku zote.
 
kila ninapojaribu kutafiti vigezo vinavyotumika na CCM kuandaa timu zake za kampeni nagundua kuwa sifa ya kwanza ni kuwa mtaalam wa muongo, mwenye siasa za kuchafuana, na uwezo wa kuandaa mikakati ya kuchakachua kura, hao ndio kina wassira, hivi kwa akili ya kawaida tu, wassira ana mtaji gani wa kisiasa, ukiachilia mbali mvuto kwa wananchi mpaka atumike kwenye kampeni?
 
haihitaji uwe umekwenda shule saaana kujua dr slaa yuko kwa ajili ya nani, utafiti mdogo tu wa kawaida utakupa majibu kuwa watanzania walio wengi wanamkubali, bila kujali dini...acha maswali ya kuchochea udini hapa
 
Back
Top Bottom