Waraka wa Kanisa Katoliki na Nafasi ya Kanisa Tanzania, Tutarajie...!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Nilikaa kimya kwa muda baada ya Waraka wa Kanisa Katoliki, nilifanya hivyo ili kuruhusu mitazamo ya wengine katika tafakuri za waraka huu. Kabla sijachambua Waraka huo, Kwanza nithibitishe kuwa NINAUNGA MKONO kwa 100% waraka huo. Na pia kabla sijachambua nimebini kupitia maoni ya watu mbali wengi hawafahamu Nafasi ya Kanisa Katoliki katika Uhuru wa Tanganyika na nafasi ya Kanisa katika Mwelekeo wa Nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivyo ninaomba LEO NISICHAMBUE WARAKA HUSIKA, Isipokuwa nichambue kwakueleza nafasi ya kanisa katika Tanzania ambapo kwa sehemu kubwa nilishaeleza katika kitabu cha Ujasusi.

Baada ya kulijua kanisa, makala ijayo nitachambua Waraka na tafsiri yake pana ikiwa Serikali itakomaza fuvu lake. Ifahamike wazi ni kanisa katoliki ndio wametoa tamko, Bado Waislamu (BAKWATA) hawajatoa tamko, Bado CCT (KKKT, Anglikana, nk) hawajatoa Tamko, Bado CPCT (Makanisa ya Kilokole) hawajatoa tamko. Matamko mengi mnayosikia yanayotolewa kupinga waraka wa Kanisa Katoliki ni vikundi vya wahuni tu wanaotumiwa na magenge ya kihalifu huko mitaani yenye lengo la kuiingiza serikali chakani kwania za kiasiasa au kiuchumi. Waraka wakufanana na Waraka wa Katoliki zinakuja zitasomwa kila kaya na kila familia msikitini na kanisani. Hakuna raslimali ya nchi itapotea.

Pengine ni kwa mara ya kwanza Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ndio kinaeleza uhusika kikamilifu wa Kanisa katoliki duniani katika uhuru wa Bara la Afrika na hasa Tanganyika chini ya shirika nguli la Ujasusi la Kanisa Katoliki. Utafiti wa kinyaraka na machipuzi ya nera kwa mambo anuawai, ndio yaliyonihakikishia kuhitimisha katika kitabu juu ya nafasi ya kanisa, Tunapoongelea Uhuru wa Tanganyika tunayo sababu na ni haki yetu kutambua na kuheshimu mchango wa kila mtu alivyoshiriki katika uhuru huo, haijalishi mapokeo ya makundi mengine katika nchi, Tusipoandika historia yetu, tusilaumu tukiandikiwa.

Hebu turejee kwenye Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Kwa mfano, hali ya Tanganyika kuwa eneo la kudhaminiwa, ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo, hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa, ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.

Kanisa halikuwa nyuma na mwito wa dunia, Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na mashirika yake tanzu yakiongozwa na shirika la kijasusi la kanisa hilo liitwalo (Jeisuiti) kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua. Lakini, lilikumbana na kiunzi/ukinzani hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya Ukristu, kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana).

Mgogoro huo ulikuzwa kwa kuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa shirika lao la kijasusi la Fabian Society, maalumu kwa minajili ya kuwaandaa Vijana katika makoloni Uingereza hususani barani Afrika, kukabidhiwa nchi zao na kwa Tanganyika Fabian Society wao walikuwa wamemuandaa Chifu David Kidaha Makwaia huku Jeisuti ya Katoliki wakiwa wamemuandaa Julius Nyerere. Rejea kitabu cha Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps akieleza nguvu ya Vatican katika kudhibiti ulimwengu, anakazia katika harakati za ukombozi duniani hasa Afrika na nafasi ya kanisa chini ya Jeisuti.

Barani Afrika, Jesuiti ilibadili mbinu kwa kuwa dola la Kiingereza, lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani. Haikujikita kwenye dola, bali ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri shahiri, ilikuwa lazima itimie, kama ilivyoelezwa mwanzoni kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu. Kwa hiyo, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika, chini ya Udhamini wa Shirikisho la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929, kanisa Katoliki nchini, chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi wake Tanganyika, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli. Tar. 12 Februari, mwaka 1929, Zelger alistaafu wadhifa wake kwa lazima.

Ni mwaka huohuo wa 1927, ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron, maalumu kwa minajili ya kuratibu mambo ya sherehe za watu weusi pembeni ya mji, huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na akawapa jengo la ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini, historia ya Tanganyika haiwataji kinagaubaga waasisi wa AA: Rais wa kwanza, Mwalimu, Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za Mjerumani kutoka kabila la Wayao), Katibu Mkuu wa kwanza, Klest Sykes (Mzulu, Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni kutoka Afrika Kusini), Mwekahazina, Ali Ramadhan (Mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania leo bahari ya Hindi).

Hawa ndio mwaka 1927, waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933, Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho, Bw. Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948, yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest, aliyeitwa Abdulwahid Sykes.
Abdulwahid Sykes alitoka kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huko Burma. Aliporudi, alikuwa na mawazo ya ujana kutoka vitani, akampindua baba yake kwa vurugu na ngumi. Mapinduzi yaliyoitwa ‘ondoa wazee’. Kisha chama cha AA kikabadilishwa jina na kuitwa TAA ambapo Rais wake wa Kwanza, akawa Daktari wa binadamu Vedasto Kyaruzi (Mhaya), aliyekuwa anafanya kazi Kingorwila Mkoani Morogoro.

Huyu ndie daktari wa binadamu wa kwanza kabisa wa Kiafrika, Tanganyika. Katibu Mkuu, akawa Abdulwahid Sykes mwenyewe na Mweka Hazina akawa Dosa Azizi. Miaka miwili tu ya chama kipya, yaani 1950, Daktari Vedasto Kyaruzi, kwa ghiriba za wakoloni, alihamishiwa Sengerema Mwanza, kama sehemu ya kumuondoa jijini Mzizima leo Dar es Salaam awe mbali na harakati. Nafasi ya rais wa TAA ikakaimiwa na Bw. Adbulwahid, mpaka mwaka 1953, uchaguzi ulipofanyika na Julius Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo (Mnazimoja ya leo).

Mnamo tarehe 7, mwezi wa 7, mwaka 1954, Vijana (wazee wa Kariakoo) wakiongozwa na Mwl. Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajesuiti (Askofu Maranta) na Waislamu (Sheikh Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, hekima za Sheikh huyu ziliendelea kusaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwl. Nyerere ya kwenda UNO tar. 5 Machi, mwaka 1955, kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tikiti ya ndege ya kwenda na kurudi. Lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani.

Si hivyo tu, bali katika moja ya utani wa Mwl. Nyerere wenye ukweli ndani yake, aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni mabosi wake, akikumbuka malipo ya Shilingi mia sita (600/=) angali ameacha kazi ya ualimu, akiwa kijijini Butiama. Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Nyerere kuja kuiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya Kilatini, ya kitume, Tot Tangaeque, ya Papa wa Roma, ya tar. 8 Novemba, mwaka 1984, kwenda kwa Kanisa Katoliki Tanzania, inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata.

Miaka thelethini na mbili (32) baadae, Kanisa Katoliki Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, linaijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbukumbu nambari TEC/PR/1 ya tar. 10 Novemba, mwaka 2016, likikubaliana na kuitangazia dunia kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, tarehe. 9, mwezi 12 ya kila mwaka itakuwa pia siku ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Imakulata, MSIMAMIZI wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA......

Kwaundani zaidi, Soma KITABU cha Ujasusi kwa Ofa Maalumu.

Watu 5 @ mtu atapata Kitabu cha "UJASUSI" kwa 30,000/= Badala ya 80,000

Lpia kwa:

Tigo Pesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

Kwa Dar ni free delivery

Nje ya Dar nauli ni 8,000/=


IMG_20230823_131858_408.jpg

IMG_20230823_132126_795.jpg
 
Kabla sijachambua Waraka huo, Kwanza nithibitishe kuwa NINAUNGA MKONO kwa 100% waraka huo. Na pia kabla sijachambua nimebini kupitia maoni ya watu mbali wengi hawafahamu Nafasi ya Kanisa Katoliki katika Uhuru wa Tanganyika na nafasi ya Kanisa katika Mwelekeo wa Nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivyo ninaomba LEO nichambue kwakueleza nafasi ya kanisa katika Tanzania

Tigo Pesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
(Yericko Nyerere)
Asante uchambuzi mzuri
P
 
Sasa Je ! Katika Hizo Wanazosemaga Siri-kali Za Serikali Hakuna Huo Utambulisho Wa Kuonyesha Kuwa Tanganyika Ipo Chini Ya Katoliki Ili Kila Kiongozi Mjuu Akiingia Ajue Na Kuobey Makubaliano Ya Kanisa Na Waasisi Wa Nchi ? Na Usipofuata Makubaliano Na Mwongozo Wa Katoliki Kuna Disadv Gani?

Ni Vema Tujue Hilo,Hili Mama Asipotekeleza Maoni Ya Waraka Wa Maaskofu Wa Katoliki TEC Tujue Kabisa Amekiuka Makusudi Au La Hajui,na Kama Kuna Hasara Yoyote Kama Nchi Tutaipata Tusipofuata Makubaliano Yetu Na Vatican.

Na Je Vatican Walibariki Muungano Wetu Na Zanzibar Ambayo Asilimia Kubwa Ni Muslims,na Kama Walibariki Hawakujua Madhara Yake Baadae Hasa Kwa Tanganyika? maana sitarajii kama baada ya muungano walidhani raisi na viongozi wa juu wote wangekuwa wanatoka katoliki ili waendelee ku uphold makubaliano,
na tanzania ilienda mbali zaidi na kusema nchi haina dini,wakimaanisha dini zote zinamiliki nchi,
so nafasi ya katoliki ipoje katika serikali kwasasa na wana mamlaka gani ya maamuzi ?
 
Nilikaa kimya kwa muda baada ya Waraka wa Kanisa Katoliki, nilifanya hivyo ili kuruhusu mitazamo ya wengine katika tafakuri za waraka huu. Kabla sijachambua Waraka huo, Kwanza nithibitishe kuwa NINAUNGA MKONO kwa 100% waraka huo. Na pia kabla sijachambua nimebini kupitia maoni ya watu mbali wengi hawafahamu Nafasi ya Kanisa Katoliki katika Uhuru
Bora hata wewe umetia neno maana tumechoka kuelewesha vichaa wa Twiter
 
Kuna Mzee mmoja huwa anaamini uhuru wa nchi hii, ulipiganiwa na watu wa dini yake tuu, hata maandiko yake anachuja tuu, zile za dini yake, hata picha anachagua zile za dini yake tuu. Ni Nyerere tu anashindwa kumkwepa. Lakini achilia mbali taasisi zote za kanisa Katoliki ambazo tayari walikwisha soma na walikuwa na fedha walikuwa na nafasi kubwa Sana kumpigania uhuru wa nchi hii. Lakini wapo watu wengine ambao ni Wakristu kama akina THOMAS MARIALE na MZEE MBOWE ( Senior) WALIOTOA sapoti kubwa Sana kwa uhuru wa Tanzanyika
 
Kuna Mzee mmoja huwa anaamini uhuru wa nchi hii, ulipiganiwa na watu wa dini yake tuu, hata maandiko yake anachuja tuu, zile za dini yake, hata picha anachagua zile za dini yake tuu. Ni Nyerere tu anashindwa kumkwepa. Lakini achilia mbali taasisi zote za kanisa Katoliki ambazo tayari walikwisha soma na walikuwa na fedha walikuwa na nafasi kubwa Sana kumpigania uhuru wa nchi hii. Lakini wapo watu wengine ambao ni Wakristu kama akina THOMAS MARIALE na MZEE MBOWE ( Senior) WALIOTOA sapoti kubwa Sana kwa uhuru wa Tanzanyika
kanisa liliwapingaje wakolon wakati kanisa ni moja ya vitangulizi vya ukoloni?
 
Unaniita kwenye tangazo la kitabu Tate mkuu!?..kuhusu kupigania uhuru uwongo mwingi utasemwa lakini ukweli unajulikana,kanisa lijikite kuandaa watu kwenda ufalme wa milele,kazi yake kuu na waliyoiacha,wamekua na ashki na siasa,tunajua wana mirija hazina ndiyo maana wapo macho zaidi na siasa kuliko kuwaandaa kiroho waamini
 
Kuna Mzee mmoja huwa anaamini uhuru wa nchi hii, ulipiganiwa na watu wa dini yake tuu, hata maandiko yake anachuja tuu, zile za dini yake, hata picha anachagua zile za dini yake tuu. Ni Nyerere tu anashindwa kumkwepa. Lakini achilia mbali taasisi zote za kanisa Katoliki ambazo tayari walikwisha soma na walikuwa na fedha walikuwa na nafasi kubwa Sana kumpigania uhuru wa nchi hii. Lakini wapo watu wengine ambao ni Wakristu kama akina THOMAS MARIALE na MZEE MBOWE ( Senior) WALIOTOA sapoti kubwa Sana kwa uhuru wa Tanzanyika
Unamaanisha Mzee Mohamed Said? Na yeye angekuja kutoa ya kwake, ili mwisho wa usiku tuweze kupata mwanga zaidi wa kile kilichotokea wakati huo.
 
Nilikaa kimya kwa muda baada ya Waraka wa Kanisa Katoliki, nilifanya hivyo ili kuruhusu mitazamo ya wengine katika tafakuri za waraka huu. Kabla sijachambua Waraka huo, Kwanza nithibitishe kuwa NINAUNGA MKONO kwa 100% waraka huo. Na pia kabla sijachambua nimebini kupitia maoni ya watu mbali wengi hawafahamu Nafasi ya Kanisa Katoliki katika Uhuru wa Tanganyika na nafasi ya Kanisa katika Mwelekeo wa Nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivyo ninaomba LEO NISICHAMBUE
Naona kama hapa kuna 'fallacy of association'. Kanisa Katoliki lina idara nyingi zinazohusikana na uinjilishaji na za kuliombea taifa kwa jumla (viongozi wa nchi na watu wake) na kwa namna ya pekee taifa la Mungu (wanakanisa wa Tanzania) na siyo kama state authority (mamlaka ya nchi ambayo haina dini). Kulingana na 'charisms' mbalimbali kanisa limeainisha lina maeneo mbalimbali ya uinjilishaji: mfano, kuna ecumenism (kujenga uhusiano mzuri na makanisa mengine ya Kikristo); kuna utamadunisho (kutambua na kutunza mila nzuri zinazojenga jamii na kuachana na mila mbaya); dialogue with Muslims (kujenga uhusiano mzuri na waumini wa dini ya Kiislamu kwa kutafuta maeneo ya ushirikiano na kufanya kazi pamoja); kuna idara ya majeshi (inayotoa huduma kwa askari walio mstari wa mbele au katika maeneo yale ambayo askari hao hawapati huduma ya kawaida kama waumini wa Kanisa Katoliki); kuna idara ya wakimbizi (kuna baadhi ya mapadri wanatoa huduma sehemu ambazo kuna wakimbizi au watu ambao wako internally displaced); kuna idara ya afya, Caritas, miito (ya upadri, utawa, ndoa), kuna idara ya wasomi; kuna idara ya wataalamu wa anga (astronomers) na hata Kanisa lina kituo chake cha wataalamu wa anga kwa ajili ya kukuza utafiti wa mambo ya anga na lina kionambali chake (telescope) katika Mlima wa Graham (in the US) na kuna maeneo mengi pia ambayo kanisa limewekeza kuhusiana na utafiti wa kisayansi etc. Kutokana na kujihusisha kwenye aina mbalimbali za utafiti duniani tangu miaka na miaka kanisa lina pia idadi kubwa ya wanasayansi ambao ni mapadri (List of Catholic clergy scientists - Wikipedia).

Maeneo yote haya huwa yanawekwa chini ya usimamizi wa mtakatifu fulani (patron saint). Tanzania kuwekwa chini ya usimamizi wa Bikira Maria ni desturi pia ambayo iko katika nchi mbalimbali duniani na hakuhusiani na siasa wala harakati za kisiasa za kuitawala nchi, bali ni kwa ajili ya kuliweka taifa la Mungu (Kanisa la Tanzania) chini ya patron saint na jina Tanzania kwa mantiki hii halina connotation yoyote ya kisiasa. Mfano, hata nchi zingine zina patron saints: Patron saint of Russia ni Mt Nicholas, Ireland (Mt Patrick), China (Bikira Maria), Chile (Bikira Maria), Bangladesh (Mt Fracis Xavier), Misri (Mt Marko & Marcus), Fiji (Mt Petro), Lesotho (Moyo Safi wa Maria), Madagascar (Mt Vincent de Paul), Nigeria (Mt Patrick), State of Palestine (Bikira Maria & Mt George), Sudan (Mt Josephine Bakhita), Tunisia (Mt Cyprian of Carthage), US (Bikira Maria), Vietnam (Mt Joseph & Mashahidi wa Vietnam) etc. Kwa hiyo, kuwa kwa nchi kuwa na patron saint kwa mfumo wa Kanisa Katoliki hakuhusiani na kanisa kutaka au kutawala hiyo nchi kisiasa hata kidogo. Shirika la Jesuits ni shirika linalojishughulisha na elimu na wasomi wengi wa Kanisa Katoliki (hasa kwa upande wa mapadri wanatokana na shirika hili). Kuna mashirika mengine pia kama Dominicans, Carmelites, Consolata, Salvatorians etc. Shirika la Jesuits wao uinjilishaji wao ni kupitia elimu na mapadri wengi wamebobea katika maeneo mengi - sayansi, utafiti, machapisho ya utafiti, etc. Nimependa tu nichangie eneo hili isije ikaonekana as if kuwa na patron saint inatokana na uhusiano wa moja kwa moja na influence ya kanisa kwenye siasa ya nchi, hapana ila ni kwa ajili ya huduma za kiroho zinazotokana na mahitaji ya kanisa la mahali. Asante.
 
Back
Top Bottom