Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

Hii ni hatari kwa viongozi wetu kudanganya uma. Akiambiwa ushahidi hana tunategemea nn, sijui kama tutafika kwa vgoz wa aina hii!!.
 
Nimerudi na ntaendelea kurudi tenaaaaa,,,alichosema wasira hakijajibiwaa hadii sasa ni porojo tu mnajazia huku!!
 
Mujwahuzia:
Ndugu yetu S.Wassira wenzake wanapokuwa katika mijadala yeye anauchapa Usingizi akikurupuka anasema lolote lile na kwavile yeye ni kiongozi wa nchi waandishi wa Habari wataandika kile atakacho zungumza hivyo basi wakati yupo Arumeru alikurupuka usingizini akasema Dr,Slaa aliiba fedha, siajabu alitoka usingizini ndio kwa maana leo anasema Mimi nilishazungumza yakaandikwa kwenye vyombo vya habari hii leo siyo habari Tumsamehe bure mwenzetu alitoka kutafakari Usingizini.
 
Watoto wa mtu kama Wasira sijui wanajisikiaje kwa tabia za ajabu namna hii za baba yao
aibu tupu. jamaa lina wakwe na wajukuu bado linafanya mambo ya aibu ktk jamii! Nadhani mjukuu akifanya utukutu anaambiwa lione hilo kama babu yake!!
 
Maandiko yote hayo, hakuna sehemu Kanisa limekanusha, linasema tu, "leta ushahidi".

Inanikumbusha Kikwete alipotakiwa kupeleka ushahidi wa kanisa kujihusisha na madawa ya kulevya, alipokamatwa mchungaji. Likakaa kimya.

Kanisa liseme nini kilimuondoa Slaa katika uongozi wa kanisa?
Hizi akili nyingine za chini ya miembe tabu sana!!

quote_icon.png
By mayenga
Swali kwako Dk Slaa,

Je ni kweli kwamba ulipokuwa Padre wa kanisa katolilki na ukiwa kama katibu mkuu wa baraza la maaskofu uliondolewa kwa ufisadi wa kutafuna michango ya ziara ya Papa Yohane Paulo wa pili?



Mayenga,


Jibu
Asante sana kwa maswali mazuri sana. Ningependa kujibu tu kwa ufupi kama ifuatavyo:

a) Kuwa nilipokuwa Padre na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC) niliondolewa kwa Ufisadi na kutafuna michango ya Ziara ya Papa Yohane Paulo wa Pili. Ah, sijui nisemeje, anayetafuna michango na kufanya ufisadi hufikishwa kwanza mahakamani na akipatikana na hatia hufungwa gerezani kwa mujibu wa Sheria.

b) Kama hoja hii siyo ya Propaganda na kama mtoa hoja anaelewa Sheria za Kanisa Katoliki, au na wale wanaopigia debe hoja hii, basi ningelitegemea mambo kadhaa i) Wangeliweka hadharani "Hati"( Decree) ya kuondolewa kwa ufisadi. Kanisa Katoliki ina very elaborate procedure kwa mujibu wa Sheria zake, hivyo isingelimwondoa tu mtu aliyetafuna michango, na hata kumwondoa Upadre, ambao kama nilivyosema ni Sakramenti na haufutiki, isipokuwa kwa Taratibu elaborate za " Laiciztion", hati ambayo hutolewa na Papa peke yake kupitia Wizara ( Idara yake husika). Hati niliyonayo inayonirudishia hadhi ya Ulei (Laity) haitoe mahali popote process yoyote dhidi yangu, bali inajibu Maombi niliyowasilisha mwenyewe kwa mandishi yaliyosainiwa na mimi mwenyewe chini ya Kiapo, na kwa kuwa maombi yangu yalifikia viwango vinavyotakiwa nikapewa Decree husika.

c) Katika Kampeni ya 1995 ndiyo hoja kubwa iliyotumika na CCM na kwa bahati mbaya kila uchaguzi unapokuja hujaribu kufufua tena propaganda hiyo.

Hata hivyo, iwapo si propaganda, basi ningeliwategemea kwenye Jamvi hili wangeliweka angalau Indicators (viashiria) kuwa huyu bwana aliondolewa na Kanisa, aidha kwa document, au kwa kiashiria kuwa kuna chuki kati ya Dokta Slaa na Maaskofu au viongozi wa Kanisa Katoliki. Badala yake Dr. Slaa ameendelea ku enjoy uhusiano na Kanisa Katoliki katika ngazi zake zote, na hata siku wazee wa Karatu walipokuja kuniomba katika delegation kulikuwa na Mapadre wawili Fr. Reginald Barhe ( class mate wangu) na Fr. Dominick Rahhi aliyekuwa Parokia ya Karatu wakijua kuwa nikiwaona wenzangu, basi nitakubali kugombea. Nami kwa Historia yangu ndani ya CCM nikakubali na kuwaambia nitagombea kwa Tiket ya CCM kwa kuwa ndiyo chama nilichokijua hadi wakati huo. Hata ccm wenyewe katika hoja ya kuniengeua kuwa Mgombea kwa tiket ya CCM walieleza kuwa "nimesaidiwa na Kanisa Katoliki, japo hawakuweza kuonyesha uthibitisho wowote, wala sikuhojiwa kuhusu hoja hiyo) badala yake wakaamua kuniondoa kwa msingi wa "siyo mwenzetu".

Hivyo sina zaidi ya kusema hiyo ni propaganda isiyo na mshiko kwa kuwa Wananchi wa Karatu ndio walionifanyia Sherehe ya Upadre, ndio walioshiriki siku ya Upadre wangu, ndio walioniomba kugombea na kunifanya nishinde kura za maoni ndani ya CCM (kabla ya kuondolewa kwa mizengwe) na ndio walioendelea kunichagua katika chaguzi zote 3 toka 1995.

d) Kwa mtu yeyote mwenye kutaka ukweli, angelienda TEC na kuomba in confidence, Handing Over notes zangu kwa Katibu Mkuu aliyenifuata, Mhe. Methodius Kilaini, kama alikwazik na jambo lolote katika Handing over yangu kwa maana ya fedha zilizotafunwa au dosari nyingine yeyote ya kifisadi. kupenda kujenga proganda bila utafiti wa kina inaonyesha dhahiri kutokuwepo kwa dhamira safi.

Nadhani kwa ujumla maelezo haya yametoa picha kamili ambayo imeendelea kurudiwa mara kwa mara na wana CCM katika jitihada zao mbalimbali, hasa wana CCM wanaotoka nje ya Karatu, kwa kuwa Karatu hadi leo majina yangu ni Willy, Dr. na Padre kwa maana ya ukaribu wa watu wa Karatu na Dr. Slaa
 
Kha ......... hakika hata Mungu atasononeka kwa kukupa ubongo wa binadamu

Wengine wanaonekana binadamu kwa mtazamo tu, lakini akili zao na ubongo Mungu aliamua akawapa Ubongo wa SISIMIZI.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
viongozi wa ccm wazidi kuaibika, baada ya mkapa sasa ni zamu ya wasira ambapo kanisa katoliki limekana kuwepo kwa ulaji fedha wakati wa ziara ya papa na kumtaka wasira atoe ushahidi............... Sinema zaendelea.

Kanisa katoliki lamshukia wasira

lasema kama anao ushahidi wa wizi wa fedha za papa autoe, wanasiasa wanaochafua wenzao wamefilisika

na waandishi wetu

kanisa katoliki nchini limemtaka waziri wa nchi ofisi ya rais (uhusiano wa jamii), stephen wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama katibu mkuu wa chadema, dk willibrod slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa papa john paul ii, alipokuja nchini mwaka 1991.

Akizungumza kwa simu jana, rais wa baraza la maaskofu tanzania (tec), yuda thadeus ruwaichi alimtaka wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu dk slaa kwa tuhuma za wizi.

Akizungumza katika kampeni za ccm jimbo la arumeru machi 19, mwaka huu, wassira alimtupia kombora dk slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo, wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya askofu ruwaichi alijibu kwa kifupi: "mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari."

ruwaichi ambaye pia ni askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la mwanza alisema madai hayo ya wassira hayana msingi.

"kanisa halijawahi kumshutumu dk slaa kuhusu madai hayo (ya wassira). Kama wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake," alisema ruwaichi.

Askofu ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

"ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa," alisema.

Askofu ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... "watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele."

askofu ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

Kauli hiyo ya askofu ruwaichi, imekuja siku chache baada ya dk slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la arumeru na kusema wassira ni mwongo na hajui asemalo.

"kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni serikali dhaifu na ijiuzulu," alisema dk slaa.


my take:
ni aina gani ya viongozi wa ccm tulionao kila wakati maneno yao yanakanushwa na kubainika kuwa ni uongo? Alianza mkapa kudanganya sasa kafuata wasira. Who is next??


wassira na uzee wote huo bado anaendesha siasa za kipumbavu. Upumbavu kweli. Sijui viongozi kama hawa wametoka wapi? Sasa waziri mzima anaongea mambo ya kipumbavu mbele ya umma, watoto wadongo wa shule za msingi watafanya nini? Inasikitisha sana kwa kweli.
 
Maandiko yote hayo, hakuna sehemu Kanisa limekanusha, linasema tu, "leta ushahidi".

Inanikumbusha Kikwete alipotakiwa kupeleka ushahidi wa kanisa kujihusisha na madawa ya kulevya, alipokamatwa mchungaji. Likakaa kimya.

Kanisa liseme nini kilimuondoa Slaa katika uongozi wa kanisa?
Kanisa liseme nini? Wasira ambaye amekuja na madai ya kutafunwa pesa ndiye atoe ushahidi. Na ninakuhakikishia kama JK alivyoshindwa na Wasira atashindwa leta ushahidi. Mwisho utambue Kanisa Katoliki linaendesha mambo yake kwa kanuni,sheria na taratibu zinazoeleweka ndiyo maana unaona linaendesha taasisi kubwa kama vyuo.hospitali na mashule kwa mafanikio makubwa. Usifananishe kanisa Katoliki na makanisa ya wasaka tonge na wajasirimali wa dini!
 
jamani hakuna mwana CCM hata mmoja anakipenda chama hiki angalau akasimama na kukemea mambo haya

unajua tatizo si yule mzee tatizo ni ukubwa wa tumbo lake!mtu anapokua na tumbo kubwa kinachotoka humo ni uchafu tu!sasa subiri msikie udhibitisho wake!
 
Nashangaa ni aina gani ya viongozi tulio nao mtu aibe 1991 uje useme leo 2012 tena kwenye kampeni!!!! huyu mzee hana sera tena anawaza kwa kutumia ma******!!!!
 
msiumize vichwa sana wadau juu ya kiumbe huyu, type ya viongozi kama wassira, lukuvi, nundu, Mponda na kina Mwantumu Mahiza wanajulikana wazi kuwa ni janga la kitaifa, very shame to them. 2015 watajuta
 
Tanapa mnafanyaje tena wanyama (sokwe) wanatoroka mwituni kuja kufanya siasa ambazo hawazijui
 
Viongozi wa CCM wazidi kuaibika, baada ya Mkapa sasa ni zamu ya wasira ambapo Kanisa katoliki limekana kuwepo kwa ulaji fedha wakati wa ziara ya Papa na kumtaka Wasira atoe ushahidi............... Sinema zaendelea.

Kanisa Katoliki Lamshukia Wasira

LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA

Na Waandishi Wetu

KANISA Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.

Akizungumza kwa simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.

Akizungumza katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi alijibu kwa kifupi: “Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari.”

Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.

“Kanisa halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake,” alisema Ruwaichi.

Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

“Ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa,” alisema.

Askofu Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... “Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele.”

Askofu Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

Kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.

“Kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu,” alisema Dk Slaa.


MY TAKE:
Ni aina gani ya viongozi wa CCM tulionao kila wakati maneno yao yanakanushwa na kubainika kuwa ni uongo? Alianza Mkapa kudanganya sasa kafuata Wasira. Who is next??


Aina ya viongozi wa CCM tulioyonao ni: (1) Waongo, (2) Hawana uchungu na wananchi waliowachagua ili wakawawakilishe, (3) Mafisadi, (4) Hawana uchungu na mali ya nchi hii na mengine meeeeeeeeeeeengi!!!!! Kwa mtindo huu basi, hawatufai tuwachukie, (Ndiyo Mzee) Hapo naomba kwa yeyote anayesoma aitikie kwa sauti ya Joseph Haule. Si waongelee sera zao kwa nini wanapenda kumfuata fuata kamanda wangu aaaghaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
DSN na Wana JF,
Mkuu comments yako haiendani na Mada au hoja ya muhusika, ungesoma mada yote ndio u-comments, labda nimekuelewa vingine, kiujumla upo nje ya mada, labda ufafanue una maana gani.
Nawakilisha

Aksante sana, nilidhani mi ndo sikuelewa yaani nimeludia mara mbili mbili lakini bado nikawa sielewe, nilikuwa naona uvivu hata kuchangia naomba nikugongee Thanks maana hapa kwangu kile kidude chetu hakionekani barikiwa sana.
 
Tatizo CCM imejengwa kwa misingi ya propaganda za uongo! bado hawajaelewa kuwa watanzania hawako huko tena!
 
Yaliyojili ni zawadi ya shukrani kwa kanisa kuwapa nafasi viongozi wa wasio waadilifu na wasio na hofu ya Mungu wanapopewa nafasi kwenye membali za makanisa hatimae hawana aibu kutamka mambo yasiyo na pciha nzuri kwa kanisa yanayolihusu pasipo ushahidi kuhusu ukweli wa matukio hayo tajwa.Nategemea next time wahusika watakuwa ni wageni waalikwa kwenye sherehe za makanisa na misikiti.

Wakazi wa Mwanza nao wajiandae, hela alizowachangia Lowassa kamwe haziwezi kwenda bure, wamuulize Mch. Mtikila yalomkuta kwa Rostam. Sh milioni 2 ilitmokea puani Mtikila
 
Jamani anayewajua watoto wa kike wa Wassira abandike picha zao humu tuone wanafananaje sura na Baba yao, plz!
 
Aibu kubwa hii kwa ccm!
Kauli zote za kimasaburi!
1.Dr Slaa aliiba fedha za ziara ya Papa...................................................................Wassira
2.Vicent Nyerere si mtoto wa Familia ya Nyerere......................................................MkaaHapa
3.Mpeni kura Sioi ili mumfute machozi na aweze kulea Familia......................................Lusinde
4.Vicent Nyerere aende kwao Musoma, anatafuta nini huku kwa Wameru na Wamaasai....Olesendeka


Hapana NOOOOOOO! Hivi hawa CCM wao wanaona nchi hii ni yao tu. Jana kuna mmoja nusura hali ya hewa ichafuke, tulikuwa tunabishana kuwa jimbo hili lazima tulichukue sisi CHADEMA weeeeeeee!!!! aliniijia juu namna gani? Sasa hiyo ilikuwa tisa, kumi Eti anasema kuliko CHADEMA ichukue nchi, basi nchi itaongozwa na jeshi, yaani nilimwangaliaje vibaya nikataka nimtemee usoni, bahati nzuri akaingia mtu hapo mahali kwa hiyo ile kusalimiana na nini ikawa imenipunguza hasira, hivi hawa watu wanajionaje lakini, hawana haya wala hawajui kuona vibaya.
 
Back
Top Bottom