Hapa ndipo inapotoka nguvu ya Kanisa Katoliki

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Kama ilivyo ada, kila wakati katika kila nchi kuna ajenda ama sakata linalolindima, linaweza kuwa la kisiasa, kijamii ama kiuchumi. Ikiwa sehemu ya nchi zenye Siasa za mlengo wa Kidemokrasia, Tanzania imeingia katika mjadala mkali kati ya Serikali, wadau wa uwekezaji, vyama vya upinzani, asasi na taasisi mbali mbali.

Mjadala huu unahusisha uwekezaji bandarini, Uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya kimataifa ya DP-World kutoka nchini Saudia. Kuzuka kwa mjadala mkali kati ya Serikali, taaisisi na Wadau kumetokana na baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kutoleta tija au maslahi kwa Taifa.

Lakini, hivi karibuni, kumeibuka na hisia mbali mbali baada ya Sakata hili kujadiliwa na Taasisi za kidini, hasa, baada ya Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Waraka ulioonyesha msimamo wa Baraza hilo ambao unakinzana na ule wa Serikali, wa kuruhusu uwekezaji wa kampuni ya DP-World kama ulivyoainishwa katika vipengele vya Mkataba huo (IGA)

Kati ya maswali yaliyogonga vichwa vya watu, ni wapi basi, Kanisa hili kongwe linapata Mamlaka ya kutangaza misimamo yake hadharani juu ya masuala ya Kisiasa licha ya kuwa Taasisi ya kidini.

HIZI NI SABABU KUU TATU ZINAZOIPA TAASISI HII USHAWISHI KWA SERIKALI YA TANZANIA.

  1. Mtaji watu: Historia inaonyesha, tangu kabla ya uhuru, Kanisa Katoliki nchini Tanzania, limekuwa na idadi kubwa ya waumini, ambao kimsingi ndio mtaji mkubwa wa ushawishi na nguvu ya kanisa hili kufikia 32% ya waumini mpaka 2022. Kama ujuavyo, Siasa inagusa maisha ya watu, lakini, mamlaka juu ya maisha ya watu hayaishii kwa Wanasiasa pekee. Zipo taasisi nyingine zenye nguvu juu ya maisha ya watu, nazo ni Taasisi za kidini, asasi za kiraia pamoja na mashirika. Yote haya yanagawana nguvu na Wanasiasa, lakini kwa upande wa Kanisa Katoliki, ushawishi wake ni mkubwa. Hivyo basi, si Kanisa linalohitaji Serikali ili liwe na nguvu, bali, ni Serikali kupitia Wanasiasa wake linahitaji Kanisa ili kuongeza na Kudumisha ushawishi na nguvu kwa watu linao waongoza.
  2. Mchango wa Kanisa Kanisa Katoliki katika maendeleo tangu uhuru: Kazi mojawapo kuu ya Serikali ni kutoa huduma za Kijamii, kama Elimu kupitia ujenzi wa Shule, Miundombinu na Afya kupitia ujezi wa Hospitali. Kihistoria, elimu tuliyoanza kuipata hata punde baada ya Uhuru ilikuwa ni elimu yenye chembe za Kikoloni. Lakini, mpaka inafika wakati wa Utekelezaji wa Sera za Kijamaa miaka 1967-80 Shule zilizokuwa zikimilikiwa na Kanisa Katoliki zilikuwa ni Mara tatu ya zile zilizojengwa na Serikali. Kwa kutoa fursa sawa, bila kuzingatia misingi au tamaduni za Kidini, Serikali iliamua kuzitaifisha zote, hivyo, Kanisa likapoteza Shule nyingi na Hospitali ili kutengeneza usawa. Wingi wa shule hizi, ulitokana na Uambatanishaji wa huduma za Kijamii kama Afya na Elimu uliokuwa unafanywa na Wamisionari, wa Katoliki. Jambo ambalo lilivutia watu wengi hususan wa eneo la bara kuishi karibu na maeneo hayo. Mbali na hilo, hata leo 2023 Kanisa hilo Limeendelea kuwa na umiliki wa Taasisi kama Shule, Vyuo na Hospitali nyingi zaidi nchini.
  3. Kanisa Katoliki, limelea na kukuza viongozi wengi wa Kisiasa, Kijeshi na Kijamii: Kuanzia awamu ya Kwanza mpaka awamu ya tano, Maraisi wote katika mfululizo wa maisha yao hawakuwahi kuepuka kabisa malezi ya Kanisa hili. Si tu Marais, bali hata viongozi wa ngazi za juu za Jeshi, wamelelewa na wengineo kama aliyekuwa Mkuu wa Majeshi aliyemaliza muda wake, Gen. Venance Salavatory Mabeyo. Kuna Wanasiasa wengi leo hii ambao wamelelewa na kanisa hili na kukuzwa katika malezi ya kirho, nidhamu na hata kufunzwa uongozi kupitia kanisa hili.
Hivyo basi, suala hapa si kuwa Kanisa hili linataka Ushawishi kutoka kwa Viongozi hawa, la hasha, ila kupitia Sababu hizi viongozi wa nchi hii wanaliheshimu Kanisa hili. Suala la Kanisa Katoliki kutoa Waraka na Kusomwa kwa Waumini wake, ambao kimsingi ndio Wananchi na Wateja wa Wanasiasa, ni jadi na utamaduni wake wa muda mrefu, ikiwa ni kama Itifaki ya Kanisa.

Kwa kumalizia, ndugu zangu mnaodhani Kanisa hili linatawala nchi eleweni halitawali kwa Mamlaka yake kikanisa, bali kwa ushawishi wake kama Taasisi kongwe, anayetawala nchi hii ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Raia.

Ahsanteni.

Mwl. Diwani.

Rejea makala hii kutoka Vatican News - Mchango wa Kanisa Katoliki Nchini Tanzania! Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii
 
Mkapa na Magufuli, mshauri wao mkuu alikuwa kadinali Pengo.
We unasema hao walioshauriwa na Pengo. JK alipata elimu kupitia shule za Kikatoliki na kati ya washauri wake ni Papa Benedict.
Screenshot_20230827-130719.png

Bado Rais Mwinyi alikuwa anapata madini ya ukweli kutoka kwa Papa John Paul II
Screenshot_20230827-171651.jpg

Kwa hiyo mama mkimuona anaenda Vatican kufuata ushauri msione kwamba ni jambo geni.
 
Kanisa Katoliki ni kiongozi na kioo cha jamii ya watanganyika, hasa kwa misimamo yake isiyoyumba kwenye kutetea maslahi ya mtanganyika na rasilimali zake, ni wasomi, wanaoijielewa na kujua namna ya kutumia maarifa yao kuwafaa wanaowaongoza kwenye jamii.
 
Kanisa Katoliki ndilo dhehebu tajiri kuliko madhehebu yote duniani!.
Utajiri mkubwa wa kwanza ni Warumi walivamia hekalu la Constantinople kule Uturuki waka loot kila kitu, wakaliteketeza, hizo loot wakaenda kujengea St. Peter's Basilica, Vatican!. Hiyo meza hapo ukutani ni pure gold!.

Ile fimbo ya Papa ni the oldest pure gold!.
Na kwa Tanzania ndilo dhehebu kubwa lenye waumini wengi kuliko dini zote, ni kanisa tajiri, na rais wa Tanzania anapokuwa ni Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki!.
P
 
Upande wa kanisa katoliki uliobaki kua tajiri ni wa ujerumani ndo hawa waliokuja Tanganyika ila wa Italy kwanza Ethiopia tu walimshindwa na kwa sasa Italy ni nchi ya pili kufulia baada ya ugiriki,, ndo maana matangazo ya michango makanisani na kwenye jumuiya imezidi hali ni mbaya kwa wafadhili na mapadre walishategemea kula na kulala bure yajayo yanafurahisha
 
Kanisa Katoliki ndilo dhehebu tajiri kuliko madhehebu yote duniani!.
Utajiri mkubwa wa kwanza ni Warumi walivamia hekalu la Constantinople kule Uturuki waka loot kila kitu, wakaliteketeza, hizo loot wakaenda kujengea St. Peter's Basilica, Vatican!. Hiyo meza hapo ukutani ni pure gold!.

Ile fimbo ya Papa ni the oldest pure gold!.
Na kwa Tanzania ndilo dhehebu kubwa lenye waumini wengi kuliko dini zote, ni kanisa tajiri, na rais wa Tanzania anapokuwa ni Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki!.
Kanisa Katoliki sio dhehebu. Kanisa Katoliki sio taasisi. Kanisa Katoliki ni Mamlaka.

Kanisa Katoliki ni mamlaka ya dini. Ndilo lililo na mamlaka yote duniani juu ya watu na Serikali.

Nguvu ya Kanisa Katoliki si kwa sababu ndilo lina waamini wengi duniani au kwa sababu lina nguvu za uchumi na elimu; au kwa sababu ya shughuli zake za kijami. Haya kwa yenyewe ni mambo madogo ambayo hayawezi kufanya liwe na nguvu wakati wote katika historia miaka zaidi ya elfu mbili sasa.
 
Jua pia kuna katoliki ya mashariki,,,, shida waafrika wengi wamekalilishwa mambo ya magharibi..... Kuna maeneo kanisa katoliki la roma halina nguvu kabisa na ni kama ka dhehebu fulani tu
 
Kanisa Katoliki ni kiongozi na kioo cha jamii ya watanganyika, hasa kwa misimamo yake isiyoyumba kwenye kutetea maslahi ya mtanganyika na rasilimali zake, ni wasomi, wanaoijielewa na kujua namna ya kutumia maarifa yao kuwafaa wanaowaongoza kwenye jamii.
Unakusudia kanisa hili hili liloxhochea mauaji ya kimbari?
 
Kanisa Katoliki ndilo dhehebu tajiri kuliko madhehebu yote duniani!.
Utajiri mkubwa wa kwanza ni Warumi walivamia hekalu la Constantinople kule Uturuki waka loot kila kitu, wakaliteketeza, hizo loot wakaenda kujengea St. Peter's Basilica, Vatican!. Hiyo meza hapo ukutani ni pure gold!.

Ile fimbo ya Papa ni the oldest pure gold!.
Na kwa Tanzania ndilo dhehebu kubwa lenye waumini wengi kuliko dini zote, ni kanisa tajiri, na rais wa Tanzania anapokuwa ni Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki!.
P
Sio lazima imetokea Tu . EL angeweza au Sumuyawe Ila mapungufu Yao binafsi ndio yalisababisha. Mfano Marehemu Mzee Sozigwa angekuwa MTU WA Mikakati ya cheo angeweza, na kuna wengine wengi Tu .
 
Kama ilivyo ada, kila wakati katika kila nchi kuna ajenda ama sakata linalolindima, linaweza kuwa la kisiasa, kijamii ama kiuchumi. Ikiwa sehemu ya nchi zenye Siasa za mlengo wa Kidemokrasia, Tanzania imeingia katika mjadala mkali kati ya Serikali, wadau wa uwekezaji, vyama vya upinzani, asasi na taasisi mbali mbali.

Mjadala huu unahusisha uwekezaji bandarini, Uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya kimataifa ya DP-World kutoka nchini Saudia. Kuzuka kwa mjadala mkali kati ya Serikali, taaisisi na Wadau kumetokana na baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kutoleta tija au maslahi kwa Taifa.

Lakini, hivi karibuni, kumeibuka na hisia mbali mbali baada ya Sakata hili kujadiliwa na Taasisi za kidini, hasa, baada ya Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Waraka ulioonyesha msimamo wa Baraza hilo ambao unakinzana na ule wa Serikali, wa kuruhusu uwekezaji wa kampuni ya DP-World kama ulivyoainishwa katika vipengele vya Mkataba huo (IGA)

Kati ya maswali yaliyogonga vichwa vya watu, ni wapi basi, Kanisa hili kongwe linapata Mamlaka ya kutangaza misimamo yake hadharani juu ya masuala ya Kisiasa licha ya kuwa Taasisi ya kidini.

HIZI NI SABABU KUU TATU ZINAZOIPA TAASISI HII USHAWISHI KWA SERIKALI YA TANZANIA.

  1. Mtaji watu: Historia inaonyesha, tangu kabla ya uhuru, Kanisa Katoliki nchini Tanzania, limekuwa na idadi kubwa ya waumini, ambao kimsingi ndio mtaji mkubwa wa ushawishi na nguvu ya kanisa hili kufikia 32% ya waumini mpaka 2022. Kama ujuavyo, Siasa inagusa maisha ya watu, lakini, mamlaka juu ya maisha ya watu hayaishii kwa Wanasiasa pekee. Zipo taasisi nyingine zenye nguvu juu ya maisha ya watu, nazo ni Taasisi za kidini, asasi za kiraia pamoja na mashirika. Yote haya yanagawana nguvu na Wanasiasa, lakini kwa upande wa Kanisa Katoliki, ushawishi wake ni mkubwa. Hivyo basi, si Kanisa linalohitaji Serikali ili liwe na nguvu, bali, ni Serikali kupitia Wanasiasa wake linahitaji Kanisa ili kuongeza na Kudumisha ushawishi na nguvu kwa watu linao waongoza.
  2. Mchango wa Kanisa Kanisa Katoliki katika maendeleo tangu uhuru: Kazi mojawapo kuu ya Serikali ni kutoa huduma za Kijamii, kama Elimu kupitia ujenzi wa Shule, Miundombinu na Afya kupitia ujezi wa Hospitali. Kihistoria, elimu tuliyoanza kuipata hata punde baada ya Uhuru ilikuwa ni elimu yenye chembe za Kikoloni. Lakini, mpaka inafika wakati wa Utekelezaji wa Sera za Kijamaa miaka 1967-80 Shule zilizokuwa zikimilikiwa na Kanisa Katoliki zilikuwa ni Mara tatu ya zile zilizojengwa na Serikali. Kwa kutoa fursa sawa, bila kuzingatia misingi au tamaduni za Kidini, Serikali iliamua kuzitaifisha zote, hivyo, Kanisa likapoteza Shule nyingi na Hospitali ili kutengeneza usawa. Wingi wa shule hizi, ulitokana na Uambatanishaji wa huduma za Kijamii kama Afya na Elimu uliokuwa unafanywa na Wamisionari, wa Katoliki. Jambo ambalo lilivutia watu wengi hususan wa eneo la bara kuishi karibu na maeneo hayo. Mbali na hilo, hata leo 2023 Kanisa hilo Limeendelea kuwa na umiliki wa Taasisi kama Shule, Vyuo na Hospitali nyingi zaidi nchini.
  3. Kanisa Katoliki, limelea na kukuza viongozi wengi wa Kisiasa, Kijeshi na Kijamii: Kuanzia awamu ya Kwanza mpaka awamu ya tano, Maraisi wote katika mfululizo wa maisha yao hawakuwahi kuepuka kabisa malezi ya Kanisa hili. Si tu Marais, bali hata viongozi wa ngazi za juu za Jeshi, wamelelewa na wengineo kama aliyekuwa Mkuu wa Majeshi aliyemaliza muda wake, Gen. Venance Salavatory Mabeyo. Kuna Wanasiasa wengi leo hii ambao wamelelewa na kanisa hili na kukuzwa katika malezi ya kirho, nidhamu na hata kufunzwa uongozi kupitia kanisa hili.
Hivyo basi, suala hapa si kuwa Kanisa hili linataka Ushawishi kutoka kwa Viongozi hawa, la hasha, ila kupitia Sababu hizi viongozi wa nchi hii wanaliheshimu Kanisa hili. Suala la Kanisa Katoliki kutoa Waraka na Kusomwa kwa Waumini wake, ambao kimsingi ndio Wananchi na Wateja wa Wanasiasa, ni jadi na utamaduni wake wa muda mrefu, ikiwa ni kama Itifaki ya Kanisa.

Kwa kumalizia, ndugu zangu mnaodhani Kanisa hili linatawala nchi eleweni halitawali kwa Mamlaka yake kikanisa, bali kwa ushawishi wake kama Taasisi kongwe, anayetawala nchi hii ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Raia.

Ahsanteni.

Mwl. Diwani.

Rejea makala hii kutoka Vatican News - Mchango wa Kanisa Katoliki Nchini Tanzania! Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii
Ukitaka kujua nguvu ya Kanisa Katoliki angalia kwenye uchaguzi wa Papa. Dunia nzima inasimama. Anatambulika na kuheshimika dunia nzima kuliko kiongozi yeyote wa kidini dunani.
 
Back
Top Bottom