Kampeni ya kutowahonga wanawake inawanufaisha wanawake wenye vipato na kuwaumiza walalahoi na fukara

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Jumapili iko Pouwa bila Shaka!

Kampeni inayoendelea Kwa Vijana isemayo "linda kibunda chako" inaratibiwa Kwa kificho na Wanawake wenye vipato au wenye kazi za kuajiriwa.

Wakati nipo chuo nilibahatika kukutana na Wanawake wenye uwezo WA kiuchumi na wenye kazi zenye Mishahara mizuri. Mara Kwa mara walikuwa wakinimbia, hivi unawezaje ku-date na Mwanamke asiye na kazi? Mwanamke ambaye hawezi hata kukununulia Zawadi.

Uzoefu wangu unaniambia kuwa, Mwanamke akiwa na Pesa ndio anakuwa mtamu na mwenye mapenzi ya kweli kuliko akiwa Hana Pesa(Hana kazi yoyote ya kumuingizia kipato).

Baada ya miaka 10 inatokea kampeni ya Linda kibunda chako, usihonge Wanawake ambayo ni maneno yaleyale niliyowahi kuyasikia Kwa wale Wanawake Enzo hizo ni kijana mdogo nasoma.

Kampeni ya Linda kibunda chako Nyuma yake kuna udhamini wa Wanawake wenye vipato ambao wanataka kuwadhalilisha na kuwatesa Wanawake wenzao wasioweza kufanya kazi.

Nawasisitiza Vijana, tafuteni Wanawake wanaowapenda, bila kujali wanakazi au Hawana, wanapesa au Hawana, kigezo kikuu kiwe ni Upendo.
Msijiingize kwenye vita ya Wanawake. Sio vita nzuri na huwaga haziishagi vizuri.

Siku hizi kuna vita vya Wanawake ambavyo wanaume wameingizwa bila ya wao kujijua.
Wanawake wenye vipato Vs Wanawake walalahoi.

Wanawake Wazuri na wenye chura Vs Wanawake Wasio na mvuto na flat screen.

Wanawake single mothers Vs Wanawake Walioolewa.

Wanaume wanaoshikilia hiyo Kampeni ya Linda Kibunda chako wengi wao ukichunguza jua kuna Wanawake ambao wanawahudumia na kuwapa Huduma iwe za kingono Bure Kabisa, wengine kuwapa kabisa na Pesa. Sasa wanaona kumbe walikuwa wamechelewa na kujihangaisha bure Wakati kuna uwezekano wa Kula raha za mapenzi pasipo kutoa Pesa.

Maneno wanayotoa Wanawake wenye vipato Kwa Wanawake wenzao pindi wakiwa na wanaume ni Makali Sana, dharau, kejeli, dhihaka na matusi ya waziwazi ndio huwapa Kiburi hawa Vijana WA siku hizi.

Vijana nawakumbusha, msiingilie ugomvi wa Wanawake. Wao wamezaliwa kugombana tuu.

Haya nipumzike sasa
 
Leo umeyumba mzee unataka kuwapa kichwa hao wanawake waendeleze ujinga wao wakuombomba pesa kama mchwa hoja yako ilibidi iwe hakikisha anakupenda tu basi
 
Leo umeyumba mzee unataka kuwapa kichwa hao wanawake waendeleze ujinga wao wakuombomba pesa kama mchwa hoja yako ilibidi iwe hakikisha anakupenda tu basi

Ni jukumu la mwanaume kumtunza MKE au Mpenzi wake.
Kwa sasa wapo Wanawake wenye uwezo wa kujitunza wenyewe na kuwasaidia wanaume zao. Hao ndio wanaotia ndimu kwenye kidonda.
 
nikuulize kwanini nawao hawapendi mwanaume masikini? ili twende 50/50 na sisi wanaume tukatae wanawake masikini
 
Ukichunguza wanawake walio wengi na wenye vipato halali niwachache na hawana mvuto wa sura kulingana na mwonaji... Hawa wengine sura au mwonekano unaovutia wanao ila hawana shule, hawana kazi na hawaijui kesho yao ..

Wengi wanapendezeshwa na madanga na kutwa kushinda saluni, au kwenye PUB wanapoyapata madanga..

Wanawake wenye vipato halali huwezi wakuta stendi wakibandika kucha au kutoga pua, utawakuta shambani au sehemu wanakofanyia shughuli halali.
 
Wanawake karibu wote vigezo vyao vya mwanaume wanaemtaka vinafanana.

Hivyo competition inawafanya wahonge

Tatizo wasio na Pesa ndio huhenyeka na kuishia kwenda kuloga na Kwa Mwamposa wanashindwa kujua siku hizi unabii wa Yeremia unaenda kutimia

Yeremia 31:22​

Utatangatanga hadi lini, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.
 
Back
Top Bottom