Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Halafu unakumbuka mipira iliyokuwa inatengenezwa na manailoni halafu unaifuma na kamba? Hii ndo ilikuwa alternative yetu ya magozi kwa vile yalikuwa adimu sana. Mdingi akienda kiwanja akikuletea gozi kama zawadi basi mwenyewe unataaamba...Lol.
Mipira ya manailoni tena nisahau ndugu yangu?
Mpira wa Gozi, huko unaenda mbaaaali mno. Kitenesi tu ishu!
Kuna vile vi gofu vile, vya Tiger Woods vile. Ukikipata kile dili. Ndio kinakuwa cha ndimu mpaka kipotee!
Tulikuwa tunaambiwa kigofu ndani kimejaa raba bendi. Me and my brother tukawa tunatamani tukipasue tupate raba bendi (mwanangu, raba bendi nazo iiiiiishuu!) Sasa tulikuwa tunapenda mpira kupindukia. Tukaona tukipasua kigofu, hatuna cha ndimu. Tukibaki nacho kigofu, we'll never find out ndani kuna nini. Big dilemma!
We never cracked the golf ball or the puzzle!