KITABU: Kamlete, akibisha mlipue by Hammie Rajab

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,234
12,747

SURA YA 1​

KWA mara nne mfululizo katika wiki ile, Luteni Maige alijiwa na ndoto ile ile usingizini. Aliamka kwa mshtuko, jasho likimtoka huku akihema kwa kasi.

Safari hii, hata alipofumbua macho, alikuwa na hakika kabisa kuwa risasi mbili alizofyatua zilimpata kiongozi wa nchi kichwani na hapana daktari yeyote ambaye angeweza kuzuia mauti yake. Na hata risasi hizo zisingeweza kumuua, alikuwa na hakika mwanguko wa gari lake baada ya dereva kurukwa na akili kutokana na shambulizi hilo na kulibamiza gali hilo kwenye nguzo ya taa, ungemmaliza kabisa.

Maige alifumbua macho akatikisa kichwa kwa nguvu. Alipoyafumbua, akayainua taratibu akayatuliza kwenye saa kubwa ya ukutani. Zilibaki kama dakika saba kutimia saa nane kamili.

Usingizi mzito aliokuwa nao usiku ule, baada ya kunywa pombe kali, ulimruka kabisa. Angependelea sana arudi kulala lakini maumivu ya kichwa na mchanganyiko wa mawazo mazito aliyokuwa nayo, ndivyo vilivyomfanya atoke kitandani.

“Vipi?” sauti ya mkewe, Veronika, ilimpa mshtuo mwingine.

Kwa muda wote tangu Maige alipoamka, Vero alifumbua macho akamtazama. Alimwona akitokwa jasho huku akihema kwa nguvu. Alimwona alivyoduwaa kama aliyeota ndoto ya kutisha. Alimwona pia alipofumba macho na kutikisa kichwa kwa nguvu kisha akaitazama saa ya ukutani.

Maige aligeuza macho akamtazama. “Kumbe uko macho? Unasemaje?” Alijaribu kuituliza sauti yake. Hakupenda Vero ajue lililomo moyoni mwake.

“Nimeshtuka ulipoamka,” Vero alisema kwa sauti ndogo ya uchovu. “Naona jasho linakutoka. Vipi, unajisikia vibaya?”

Maige alivuta pumzi ndefu akazishusha. “Hata, najisikia kiu imebana sana. Nipe maji baridi?”

“Kiu tu ndio ikutoe jasho namna hiyo?”

Hakujibu. Aliiendea friji, akatoa chupa ya maji baridi akajimiminia kwenye glasi na kuibugia.

Maige alikuwa na umri wa miaka thelathini na minane. Alijiunga na jeshi miaka kumi iliyopita.

Tangu utotoni, maisha ya Maige hayakuwa ya kuridhisha. Pamoja na jitihada zote walizofanya wazazi wake kumpatia elimu, hakwenda mbali zaidi ya kidato cha kwanza.

Alipofikia umri wa miaka kumi na mitano, rafiki zake walianza kumshuku kuwa Maige alikuwa na hitilafu fulani akilini. Si kwamba alidhihirisha uendawazimu kamili, lah!. Ila tabia yake ya kufurahia sana madhara yoyote ayafanyayo kwa wenzake bila ya kujali maumivu au msiba atakaosababisha ndicho kilichowatia hofu.

Kwa Maige mwenyewe hiyo haikumaanisha athari yoyote ya akili. Ilikuwa ni shauku kubwa iliyokuwa ikimjia mara kwa mara ya kufanya jambo litakalodhihirisha ujasiri wake.

Alipofikia utu uzima akaingia jeshini. Akilini mwake aliamini kuwa jeshini ndipo mahali pekee ambapo angeweza kuua au kufanya madhara yoyote bila ya kufikishwa mahakamani. Angeweza kuua bila ya kuitwa na kuhojiwa, angweza kuvunja mkono, miguu, au hata shingo ya mtu bila ya kusumbuliwa, na mengine mengi.

Alikua akiomba Mungu usiku na mchana izuke vita ili aue au atese watu kwa kuwavunja viwiliwili vyao.

Haikupita hata miaka mitano ombi lake lilikubaliwa. Iddi Amin alizusha zogo lisilomithilika kwa watanzania na watanzania wakalazimika kukata kilimilimi cha nduli huyo na kunyamazisha zogo alilolianzisha.

Zikapigwa!

Katika mapigano hayo, Maige, siku hizo akiwa askari mpiganaji wa ngazi ya chini, alionyesha miujiza. Alipigana bila woga huku akiishangilia kwa sauti kubwa kila risasi yake iliyoangusha adui. Vita ilivyopamba moto na adui alivyozidi kujiimarisha, mkuu wa kikosi chake alimpandisha cheo. Ujasiri wake uliendelea kumpandisha ngazi
hadi ngazi, hatimaye, mwaka 1984 akawa Luteni.

Lakini pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata kwa muda mfupi jeshini, Maige hakuridhika. Vita ilipomalizika na jeshi la Tanzania kurudi nyumbani na ushindi mkubwa, Maige alikuwa askari wa pekee aliyelaani kumalizika kwa vita hiyo. Angepata wapi nafasi ya kuua ili aridhishe nafsi yake?

Pamoja na kujiwa mara kwa mara na shauku hiyo, lakini alitambua ya kwamba asingeweza kuchukua bastola au bunduki kubwa na kuanza kuua watu hovyo barabarani. Angethubutu kufanya hivyo angekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kuua kwa kukusudia. Pengine angehukumiwa kifo.

Alipomaliza miezi sita huku shauku yake ya kuua ikizidi kukua, Maige alikata shauri. Aliamua kufanya shambulizi moja litakalompa nafasi ya kufanya mauaji ya kutisha yatakayokumbukwa milele. Halafu basi.

Lakini lazima yawe mauaji yatakayomtambulisha yeye kama jasiri wa kweli. Lazima yawe mauji yatakayosimuliwa usiku kucha majumbani mwa watu na mchana kutwa kusomwa magazetini na kusikilizwa redioni. Ndiyo, lazima yawe mauaji ya namna hiyo.

Watu wakubwa watatu walimjia haraka mawazoni. Aliwafikiria watu hao huku akijaribu kuunda picha tofauti za hekaheka zitakazotokea kwa kila kifo cha mmoja wao.

Akaamua wawili kati yao wasingeleta msiba mkubwa alioutarajia, wala vifo vyao visingejaza hata nusu ndoo ya machozi ya watakaowalilia endapo machozi hayo yangekusanywa pamoja. Aliwaondosha mawazoni mwake, akambakiza mmoja. Kiongozi mkuu wa nchi. Na hata kusaidia uasi na kufanya mapinduzi.

Mtu wa kwanza nje ya jeshi aliyemweleza habari hizo alikuwa bepari mmoja, mfanyabiashara maarufu, Mohsin Hilal.

“Mwendawazimu!” Ndivyo Mohsin alivyomwita Maige baada ya kumsikiliza kwa muda mfupi. “Haiwezekani.”
“Haiwezekani?” Maige alitoa macho. “Kwanini isiwezekane?”

“Kama itawezekana ni baada ya kufanya mipango mikubwa na nchi za nje ili wasaidie. Na lazima ziwe nchi ambazo hazina uhusiano wowote na Tanzania. Na mpaka wakubali, ni zaidi ya mwaka au miaka miwili. Kwanza nchi ipi itakayokubali kujikita katika janga kama hilo? Ndio sababu nakuita mwendawazimu.”

Maige alianza kupandwa na hasira ambayo alijua isingemsaidia lolote. Kitu ambacho alitambua haraka ni, angehitaji fedha. Shughuli kubwa kama hiyo huthubutu kuifanya peke yako. Lazima utahitaji watu wa kukuunga mkono na kukusaidia.

Na kupewa msaada wa kuitoa roho ya Rais wa nchi yataka kishawishi kikubwa na kilichonona. Alijua kuwa kutokana na uhusiano uliyopo kati yake na Mohsin, Mohsin angeweza kumpa Maige kiasi chochote cha fedha ili atekeleze dhamira yake. Baada ya kumpa fedha hizo, isingemwia tatizo hata kidogo kupata msaada aliouhitaji.
“Sikiliza, Mohsin,” alianza upya. “Hili si jambo la mzaha. Wala hii si ndoto niliyoota jana usiku na leo na kusimulia. Tafadhali nisikilize vizuri.”

“Nakusikiliza sana. Endelea.”

Ndipo Maige alipomweleza mipango kamili anayotarajia kuifanya ili kukamilisha mauaji hayo, na jinsi ambavyo angeweza kupata msaada kutoka kwa askari kadhaa kama yeye (Mohsin) angemwazima kiasi cha pesa ambazo kwa ajili ya maandalizi na maangamizi; pesa ambazo Maige angezilipa maradufu baada ya mambo kukamilika. Mohsin alimsikiliza Maige kwa makini sana huku akijaribu kuyapima yote aliyomweleza. Aliamini kwamba maelezo yake hayakuwa na hitilafu yoyote na wala Maige hakuonyesha kubabaika wala kuwa na dalili yoyote ya hofu alipokuwa akieleza.

Si hivyo tu, bali pia ahadi ya kumkopesha hela kisha baadae kumrejeshea faida maradufu ilikuwa kishawishi kikubwa zaidi. Isitoshe, Mohsin alikuwa na hakika endapo Maige atafanikiwa lengo lake, kwa vyovyote patakuwa na faida kubwa sana kwake kibiashara na hata kicheo. Hakutaka kujidanganya kwamba baada ya mauaji ya mkuu huyo wa nchi pasingetokea machafuko yoyote.

Alijua fika pangetokea mvurugano mkubwa ambao pengine ungefuatiwa na mauaji zaidi ya wananchi wasio na hatia. Lakini hatimaye pangekuwako utulivu na amani. Ni katika kipindi hicho cha utulivu na amani ambacho Mohsin alikuwa akitegemea na ambacho alikuwa na matumaini nacho. Pengine kutokana na msaada atakaotoa, angeweza kufikiriwa kupewa wadhifa mkubwa serikalini, baada ya kuchaguliwa kiongozi mwingine wa nchi. Au pengine, japo asipate huo wadhifa, angekuwa na uhuru mkubwa wa kupanua ubepari wake wa kueneza biashara zake za magendo nchi za nje.

Lakini Mohsin hakutaka kumuonyesha Maige kwamba alishaanza kupata moto wa tamaa. Badala yake alimtazama kama aliyekuwa na wasiwasi naye.

“Sikiliza, Maige. Kiasi unachotaka cha pesa ni kikubwa sana kwa mtu kutoa kwa mpigo kwa shughuli ambayo haijawa na uhakika wa mafanikio. Si kwamba sina kiasi hicho au labda najaribu kukupiga chenga, lah!. Huo ndio ukweli wenyewe. Sijui unanielewa?”

“Nakuelewa sana,” Maige alijibu, akachukua pakiti ya sigara ya Mohsin iliyokuwa mezani, akatoa moja akawasha. “Tatizo ni kwamba ugumu na urahisi wa shughuli hii nauelewa mimi, Bwana Mohsin. Kimaelezo mtu anaweza kudhani kuwa hii ni ndoto, kama unavyodhani hivi sasa.

Na hiyo ni kwa sababu hili si jambo tulilolizoea huku kwetu. Lakini, Bwana Mohsin, napenda uelewe kuwa kutolizoea jambo fulani si sababu hata kidogo ya kumfanya mtu ashindwe kulifanya jambo hilo. Naelewa kuwa fedha ninayohitaji ni nyingi, tena nyingi sana. Hata hivyo niazime. Matunda yake yatakuburudisha. Yatakunufaisha”

“Sikatai kukuazima” Mohsin alisema, akainamisha kichwa kwa nukta mbili tatu hivi. Alipokiinua akauliza. “Ulikua ukizitaka lini?’’

“Mapema sana. Hata kesho.’’

“Umeshaongea na hao wenzako wakukusaidia?’’

“Nimeongea na kama watano hivi.’’ “Ulikua ukihitaji wangapi?’’

“Kumi wangetosha kabisa.’’

“Basi ongea na wote kwanza mkubaliane. Usiharakishe. Hili si jambo la kuchukua wiki moja tu likakamilika. Lipe muda wa kutosha ili pasiwe na makosa madogo madogo yanayoweza kuharibu mipango kisha ikawa balaa. Utakapoona kila kitu umekinyoosha vizuri, njoo siku yoyote uchukue fedha.’’

Kwa mwezi mzima na nusu uliofuata, Maige amekuwa akifanya makutano ya siri na askari wenzake na baadhi ya watu wenye vyeo vikubwa lakini waliojawa na tamaa. Kutokana na hao alioongea nao na jinsi walivyomuunga mkono, alikua na hakika pasingekuwa na kosa lolote. Na ndio maana usiku ule, kwa mara ya nne mfululizo katika wiki ile ile, Luteni Maige alijiwa na mdoto ile ile.

Alipokuwa akirudisha chupa ya maji ya baridi ndani ya friji baada ya kunywa glasi mbili, Maige alirudi kitandani. Vero alimtazama huku akiwa na mashaka kwamba mumewe hakuwa akiumwa.

Kwa kuepuka maswali ambayo Vero alishaonyesha dalili ya kuuliza, Maige alivuta shuka akajifunika gubigubi. Moyoni aliahidi kwamba asubuhi lazima aonane na Kapteni Shaibu ili waamue lini waanze kazi.

SURA INAYOFUATA
 
Mkuu je hiki kitabu ntapata kwenye Ile app yenu
 
SURA YA PILI​

ILIKUA saa tatu na nusu wakati Luteni Maige alipofungua mlango wa ofisi ya Kapteni Shaibu na kuingia ndani. Alimkuta akiongea na simu. Shaibu alimuelekeza kwa ishara kwenye kiti kimojawapo kati ya vitano vilivyokuwa nyuma ya meza na Maige akaketi.

Alipokuwa akimsubiri Kapteni Shaibu amalize maongezi yake katika simu, Maige alijiwa tena na kumbukumbu ya ndoto ya jana usiku. Japokua ndoto hiyo haikumjia waziwazi kama jana, lakini aliliona gari alilokuwemo kiongozi wa nchi likiserereka na kupamia nguzo ya chuma baada ya yeye kulitupia risasi mbili.

Aliuma meno huku misuli ya shingo ikimchachamaa. Kwa mbali moyo wake ulipiga mshindo hafifu. Alipitisha ulimi juu ya midomo yake iliyoanza kuonyeha ukavu, akameza funda dogo la mate na papo hapo alivuta pumzi ndefu akazishusha taratibu .

Alipo maliza maongezi yake, Shaibu akaiweka simu chini.

“Habari za asubuhi Luteni?’’

Maige ambaye alikuwa bado ameyazamisha mawazo yake katika kumbukumbu yake ya ndoto ya jana, alishtuka na kumtazama.

“Nzuri mzee. Habari za kazi?’’

“Salama.’’

Yeyote asingeweza kumuelezea Kapteni huyo kwamba alikua mfupi au mrefu. Alikua ni wa wastani mwenye kuonyesha dalili ya kuanza kupata kiriba –tumbo.

Pamoja na kuwa na umri mkubwa wa miaka hamsini na miwili, hakuwa na mikunjo usoni wala mvi za kuchusha. Sharubu zake ambazo zilikaribia kuziba mdomo wake wa juu zilificha karibu kila tabasamu na kumfanya aonekane kama mtu asiyetabasamu kabisa. Mwili wake uliojaa misuli imara iliyotokana na hekaheka za jeshini, chakula bora na bia nyingi, uliwafanya wengi hata wanajeshi wenzake waamini kwamba Shaibu hakuwa mtu wa kushindana naye kwa nguvu.

“Mambo yakoje mzee?” Maige alimuuliza.

“Safi. Nimeshawasuka vijana kumi ambao wapo tayari kushirikiana nasi. Kwa kutaka kuwatumbukiza zaidi na kuwatoa wasiwasi, nimewaahidi fedha ya awali nusu ya fedha kamili ambayo wanapaswa kupata”

“Kwa watu kumi hizo ni milioni shilingi. Sawa?”

“Sawa. Unadhani Mohsin atalalamika sana?”

“Alalamike nini? Nimeshaongea naye na tumekubaliana kila kitu.”

Kapteni Shaibu alivuta pumzi ndefu akazishusha. Kisha akasema, “Habari za kuaminika kutoka kwa Silas, mwenzetu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ni kwamba mtu wetu anatazamia kwenda Ethiopia kwa ziara ya siku tano siku ya Ijumaa wiki ijayo. Itabidi tukutane mapema ili tupange jinsi ya kufanya mashambulizi ya haraka na yenye uhakika bila ya kosa lolote”

Alinyamaza, akashusha pumzi. Kisha akaitupia jicho picha kubwa ya kiongozi wa nchi iliyokuwa ukutani kushoto kwake. Alipoyaondosha macho kwenye picha hiyo, aliitazama saa yake ya mkononi yenye kuonyesha siku na tarehe.

“Leo Alhamisi” Shaibu aliendelea alipoyaondosha macho yake kwenye saa na kuyatuliza usoni kwa Luteni Maige. “Lini unatazamia kukutana naye?”

“Kukutana na Mohsin?”

“Ndiyo.”

“Itabidi nikutane naye leo au kesho ili nimweleze mapema juu ya fedha nisikie maoni yake.”

“Sawa. Lakini kwa usahihi zaidi mwambie akupe robo tatu. Mbili za vijana, moja mimi na wewe.” Sharubu zake zilichanua alipoachia tabasamu pana ambalo Maige lilimpita bila ya kuligundua. “Mkimaliziana hayo,” aliendelea, “mwambie tutakuwa na mkutano wa zaidi ya masaa mawili nyumbani kwake siku ya Jumapili jioni kufanya hitimisho.”

“Kama saa ngapi?”

“Kuanzia saa kumi mpaka saa moja inatosha. Mwambie kuna mengi ya kujadili na huenda tukahitaji fedha zaidi. Tusiongee mengi hadi hapo tutakapokutana hiyo Jumapili. Hapa si mahali pa usalama hata kidogo kwa maongezi kama haya.”

“Naelewa.” Maige alijiinua kitini, “Kwa hiyo, ni hapo Jumapili mzee!.”

Shaibu alibetua kichwa, akauegemeza mgongo wake kitini.

***

Saa kumi na nusu juu ya alama siku ya Jumapili, wote walikutana. Walikuwa kumi na sita. Mohsin, Luteni Maige na Kapteni Shaibu. Wengine ni Alfonsi ambae alikuwa comandoo, Sufiani afisa mnadhimu. Wengine ni Jeff, Nkya, Tobias, Scotto, Ismail, Nelson, Wanyika na Lazaro; ambao ni vijana nane wa jeshini waliojua vema kuitumia silaha yoyote.

Kadhalika walikuwepo mfanyabiashara Sadrudin Visram Mwasia aliyekuwa mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam na katibu mkuu wa wafanyabiashara Tanzania. Weengine ni Paskali Nyirenda, aliyekuwa Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi miaka saba iliyopita na Brown Bohari, au Big Ben, kama wengi walivyomwita, jambazi wenye mtandao mkubwa; ambalo lilikuwa namba moja katika orodha ya wahalifu wanaosakwa na Jeshi la Polisi Tanania.

Kabla ya siku hiyo ya Jumapili, Luteni Maige alikutana na Mohsin mara baada ya kuzungumza na Shaibu ofisini kwake. Maige alimweleza Mohsin yote aliyozungumza na Kapteni huyo na Mohsin aliyaafiki.

Siku iliyofuatia, Ijumaa, Mohsin alimkabidhi Luteni Maige mkoba uliosheheni fedha za kigeni na Mohsin akaahidi kutoa fedha zaidi endapo zitahitajika baada ya mkutano wa Jumapili. Alipoziwakilisha fedha hizo kwa Shaibu na kugawiwa kama ilivyopangwa, vijana kumi waliohusika walifurai kupita kiasi. Nia yao ya kujiunga katika mpango huo iliongezeka maradufu.

Ukumbi uliokuwa ndani ya banda la uani la nyumba ya Mohsin ulikuwa mpana wenye nafasi ya kusimamisha hata mabasi matano ya Mwendokasi bila ya kubanana. Watu hao kumi na sita waliketi kwa nafasi, kila mmoja akisubiri kwa hamu kusikia jinsi mambo yatakavyopangwa.

Luteni Maige ndiye aliyekuwa kama Mwenyekiti wa mkutano huo, na ndiye aliyekuwa mzungumzaji mkuu.

“Bwana Mohsin,” alianza huku macho ameyatuliza kwa Mohsin Hilal. ‘‘Kabla hatujaanza kusema lolote, mimi na wapiganaji wenzangu tungependa kwanza utufahamishe ndugu hawa watatu.” Aligeuka akawaelekezea mkono Sadrudin, Paskau na Big Ben. Kisha akaendelea “Naelewa kuwako kwao hapa katika mkutano huu wa siri kumetokana na kuwakaribisha kwako na kuwaamini kwamba ni watu wenye uwezo wa kufanya jambo bila ya woga na huna wasiwasi nao. Au sivyo, Bwana Mohsin?”

“Ndivyo hasa.”

“Kwa hiyo tujulishe tu ni akina nani ili tuendelee na mambo mengine muhimu.”

Big Ben alimtupia jicho mara moja Luteni Maige kisha akayatuliza macho yake kwa Mohsin ambaye ulishaanza kujitayarisha kutoa maelezo. Ben alijiwa na shauku ya ghafla kutaka kujua maelezo ambayo Mohsin angetoa juu yake na kama maelezo hayo yangewaridhisha Maige na wenzake.

“Waungwana hawa mnao waona ni watu mashuhuri hivyo nitawatambulisha tu kwa ulazima wa utambulisho. Huyu bwana aliye kushoto kwangu anaitwa Sadrudin Visram,” Mohsin alianza kwa sauti yenye kitetemeshi cha mbali. ‘‘Yeye, kama mimi, ni mfanyabiashara na ni rafiki yangu wa miaka mingi sana ambaye namwamini na sina wasiwasi naye kabisa. Nilimweleza juu ya jambo hili bila ya woga na akakubali kushirikiana nasi. Kwa kukufahamisha Bwana Maige, robo ya fedha nilizokupa juzi Ijumaa, alitoa Bwana Sadrudin.”

Luteni Maige na Kapteni Shaibu walimtazama Muasia huyo, wakatabasamu. Sadrudin alikenua meno yaliyojazwa dhahabu, akabetua kichwa taratibu.

“Na huyu bwana hapa,” Mohsin aliendelea, sauti yake sasa ikiwa imara, mkono wake akiuelekeza upande alioketi Paskali “Anaitwa Paskali Nyirenda, miaka ya nyuma, kama sita au saba hivi, Bwana Nyirenda alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa hapa Dar.”

“Mimi namfahamu sana,” Kapteni Shaibu alidakia huku akimtazama Paskali usoni. “Labda yeye anisahau.”

Japokuwa alijitahidi kuyakutanisha macho yake na ya Kapteni huyo na kujaribu kutabasamu, uso wa Paskali ulishindwa kuficha haya alizokuwa nazo. Hakuweza kabisa kumkumbuka Shaibu.

“Kwa kuwa mkweli nimekusahau bwana, samahani. Unaitwa ndugu nani vile? Pengine nitakukumbuka.” "

“Naitwa Shaibu Malik. Najua huwezi kunikumbuka. Polisi na Jeshi maisha hatutaelewana. Kukutana kwetu ni kwenye magwaride ya Sikukuu za Kitaifa, basi. Na tunapokutana kila mmoja anamlaani mwenzake. Lakini tuyaache hayo, tuendelee na haya yaliyotuleta. Endelea, Bwana Mohsin.”

“Asante sana. Kama nilivyosema, Bwana Paskali alikuwa Mkuu wa Polisi na akaachishwa kazi kwa manufaa ya umma. Nikisema kwa manufaa ya umma nadhani nyote mnaelewa. Sidhani kama pana haja ya kujua makosa yake. Wengi wameshaachishwa kazi kwa sababu hiyo.”

“Sawa’’Maige alimuunga mkono. “Endelea tu, Bwana Mohsin.’’

“Yeye pia ni rafiki yangu wa miaka mingi na nilipomweleza habari hizi hakusita kukubali kujiunga nasi na kusaidia kwa lolote awezalo. Maana huwenda cheo chake cha zamani kikarudi maradufu”

Mohsin alivuta pumzi ndefu akazishusha. Kisha akamtazama Big Ben. “Huyu bwana mwingine anaitwa Brown Bohari. Lakini sana anajulikana kwa jina la Big Ben. Yeye” hapa alisita kidogo, akavuta pumzi zingine na kuzishusha taratibu, “Kwa kweli si mtu wa kawaida. Shughuli zake, kwa kadri ninavyoelewa mimi, ni za kijambazi tu japokuwa ndugu zetu wa polisi hawajamtia mbaroni hata siku moja kwa kukosa ushahidi.”

Macho ya watu wote waliokuwamo mle ndani yaligeuka kwa pamoja kumtazama Big Ben. Kapteni Shaibu alijisogeza kidogo karibu ya Luteni Maige akamnong’oneza neno moja au mawili sikioni. Maige alitabasamu, akabetua kichwa mara kadhaa, kisha wote wakayaelekeza macho yao tena kwa Big Ben.

“Kutokana na hali ya shughuli hii,” Mohsin aliendelea, “Nimehisi kwamba kuwa na mtu mmoja, au hata wawili, wa aina ya Big Ben si vibaya.”

“Inaweza kuwa si vibaya na inaweza kuwa vibaya sana, Bwana Mohsin” Maige alisema huku uso wake ukionyesha kutoridhika sana na maelezo ya Mohsin. “Yote inategemea na jinsi unawomwelewa huyu na unavyomwamini. Sasa sijui wewe unamwelewaje na unamwamini kiasi gani?”

‘‘Namwelewa, japo si kwa miaka mingi. Na kumwamini kwangu kumetokana na ule ujasiri wake katika shughuli anazofanya na polisi wanaishia kummezea mate tu. Mimi nadhani atatufaa.”

Hapakuwa na yeyote kati ya waliohudhuria aliyepinga maneno ya Mohsin, Big Ben ambaye muda wote maelezo yake yalipokuwa yakitolewa, alimpa Mohsin heko ya kimyakimya.

Hatimaye Maige akasema. “Asante kwa maelezo yako, Bwana Mohsin. Tumesikia na bila ya shaka tumekubaliana kwamba hawa nao ni wenzetu”

Baada ya kushusha pumzi ndefu, akaendelea “Tumeshachukua muda mrefu katika kuwafahamu wenzetu. Ingefaa sasa tuendelee na madhumuni ya mkutano wetu. Lengo letu linafahamika. Ni kutaka kugeuza hali mbaya ya nchi hii iwe nzuri. Hatua ya kwanza katika kufikia lengo hilo ni kumwondoa kiongozi wa nchi. Na kumwondoa huko si kumhamisha kutoka hapa kumpeleka nchi nyingine ya jirani au ya mbali, hapana. Kumwondoa huko ni kumuua.”

Maige alinyamaza kwanza, akawatupia jicho raia wanne waliokuwa mbele yake.

Mohsin hakuonyesha wasiwasi wowote, labda kwa vile alishaongea mara kadhaa na Luteni Maige juu ya suala hilo. Alishalizoea. Sadrudin alibadilika rangi, uso wake ukawa kama njano iliyofifia. Mara mbili alitoa kitambaa akajifuta jasho lililokuwa likimchuruzika kwa wingi nyuma ya shingo. Maige alitambua kuwa hiyo ilikuwa dalili ya wasiwasi, lakini hakujali. Alichekea tumboni tu. Alitambua kuwa baadhi ya watu hupata wasiwasi kushiriki hata katika kuua Paka, achilia mbali kiongozi wa nchi. Paskali alibetua kichwa macho yake yalipogongana na ya Maige kama aliyekuwa akimpa ishara ya kumthibitishia kwamba hana wasiwasi kabisa.

Big Ben alitulia tuli kama maji ya mtungini. Ahofu nini? Kwake yeye kutoa roho ya mtu ni sawa na kuwasha sigara na kuizima. Utulivu wake haukumshangaza Luteni Maige bali ulimfanya awe na mashaka kama kweli mawazo yote ya Big Ben yalikuwa pale mkutanoni au nusu yalikuwa katika mipango ya kuvunja karakana mojawapo yenye bidhaa adimu huko Barabara ya Pugu.

“Sasa,” Maige aliendelea, “Kuitoa roho ya mtu mkubwa kama huyo si jambo rahisi kama hivi tusemavyo. Ni jambo gumu sana lenye kuhitaji mioyo ya kijasiri, uelewano na ushirikiano mkubwa. Kwa hiyo kwanza tukubaliane hapa hapa. Mimi na wenzangu hatuna wasiwasi. Kwetu sisi kuua si jambo geni. Tunapandishwa vyeo na kulipwa mishahara minono kwa kazi hiyo. Je, mko tayari kuwa pamoja nasi hadi hapo tutakapokamilisha kazi hii? Mwenye mashak aseme hapa hapa. Na kwa vile ameshajua kitafanyika nini, hatutampa nafasi ya kuishi zaidi ya usiku wa leo. Anaweza akatoa siri nje.” Raia wanne walitazamana kisha wote wakakubali kwa pamoja.

“Vizuri. Kwa kuwa tumekubaliana nitaeleza mpango wenyewe ulivyo. Ni hivi: Adui yetu, kutokana na taarifa tuliyopokea kutoka kwa wenzetu waliyoko Wizara ya Mambo ya Ndani, kiongozi wa nchi anatazamiwa kwenda Ethiopia siku ya Ijumaa wiki ijayo. Leo ni Jumapili. Tuna siku tano, kuanzia kesho, za kujiandaa kikamilifu. Kazi lazima ifanyike siku hiyo hiyo ya Ijumaa na ikamilike siku hiyo hiyo bila ya kufanya makosa. Mpaka hapo tumeelewana?” Wote walikubali.

“Sawa. Kwa kuwa barabara zinazotumika katika misafara ya kumsindikiza kiongozi huyo kwenda Uwanja wa Ndege zinaeleweka, ninatoa ombi la msaada wa kwanza tutakaohitaji kutoka kwenu.” Alinyamaza, akamtazama Mohsin. “Tunataka, Bwana Mohsin, ufanye mpango utupatie chumba cha juu katika jengo la ghorofa tatu chenye dirisha linalotazama barabara mojawapo inayotumiwa katika misafara ya kiongozi huyo anaposindikizwa Uwanja wa Ndege. Pengine nitakusumbua, lakini ningependa jengo hilo liwe katika Barabara ya Umoja wa Wanawake.”

“Ombi jingine?” Mohsin alisema bila kusita. “Hilo umepata.” Aligeuka mara moja akamtazama Sadrudin, kisha akamgeukia tena Maige. “Bwana Visram ana miliki hoteli mbili. Moja iko katikati ya jiji Mnazi mmoja na nyingine barabara ya Kamata lakini pia anaweza kutupatia nafasi katika jengo lolote tunalohitaji ndani ya mkoa huu Bila ya shaka tatizo hilo atalitatua. Au nakosea, Bwana Visram?”

“Hukosei,” Sadrudin alijibu, akabetua kichwa. Angalia eneo unalohitaji kwa misheni kisha nipe namna ya uhitaji wako ulivyo.” Aliyageuza macho kwa Luteni Maige. “Hata leo ukiwa na nafasi njoo uchague kipi kinachokufaa, Bwana Maige.”

“Leo hapana. Sitaki watu wanione mimi na wewe mapema. Tukutane hapa siku ya Alhamisi, tuongozane nikachague eneo lifaalo. Mazingira si hayana mushkeli?”

“Ondoa shaka juu ya hilo. Nina mtandao wa kuaminika”

“Okay. Hilo tumemaliza. Kinachofuata baada ya kupatikana eneo sahihi ni kazi yenyewe. Mpango wa kazi yenyewe uko hivi: Mimi nitakuwa katika eneo la mashambulizi masaa manne kabla msafara huo haujapita. Pirikapirika zote za wana usalama kuzuia magari nitaziona kwa usahihi kutoka eneo nitakalokuwa.

“Eneo rasmi la tukio, kama mita hamsini kushoto na kulia, nitaweka vijana wetu sita katika makundi mawili ya watatu watatu. Wao watahakikisha msafara unapata mashambulizi kutoka nyuma na mbele. Wakati mimi shabaha yangu itakuwa moja tu, kiongozi mkuu.”

Aliyazungusha macho, akayatuliza usoni kwa Big Ben. Ben alijiweka vema kitini pake, akapepesa macho kisha akameza funda kubwa la mate.

Maige akagundua haraka kuwa Big Ben naye alishaanza kupata tumbo la kuharisha. Kumuua mlinzi wa benki katika tukio la ujambazi ni suala moja tofauti sana na kufikiria kumuua kiongozi wa nchi. “Big Ben,” alimwita, akaukunja uso wake ili kumthibitishia kuwa anachosema si jambo la mzaha. “Kutokana na habari zako alizotueleza Bwana Mohsin, nitakupa kazi ngumu ambayo, ukifanya kosa dogo tu basi wote tutakuwa wakimbizi daima kama tutapata nafasi hiyo. Unanisikia vizuri?”

Ben alitoa kikohozi kidogo, akajiweka vema kitini kwa mara ya pili.

“Nakusikia,” alijibu kwa sauti ndogo, nzito. “Nieleze tu. Kuna watu wema zaidi waliokufa kwa kujenga taifa na hapana aliyejali. Kifo changu mimi si kitafanyiwa tafrija na polisi? Nafasi ya kuniua hawawezi kuipata maana sina mpango wa kufanya kosa japo dogo”

Wote waliangua kicheko.

Walipomaliza kicheko chao, Maige alisema, “Kazi yako: Mara tu ninapolirushia risasi gari la adui yetu na dereva wake anapoanza kubabaika na pengine kulibamiza kwenye nguzo ya taa au mahali popote pale, utampiga risasi yeyote atakae chomoza garini.

“Likaribie hilo gari huku ukimimina risasi. Na unapoona umefikia umbali ambao unaweza kuwaona waziwazi waliomo ndani, tafuta njia ya kummaliza adui yetu iwapo kama mimi itakuwa sijafika kummiminia risasi. Una swali lolote?”

“Hamna taabu.” Alikubali badala ya kuuliza.

Mwishowe Maige alimtazama Paskali Nyirenda. Japokuwa hakujua angempa kazi gani kwa wakati ule, lakini alimwambia kuwa angehitajika sana kuwa mfikisha taarifa kwa washirika wakuu ili kulituliza taifa baada ya kifo cha kiongozi huyo.

Mnamo saa moja na nusu, baada ya kukamilisha maongezi yao, walivunja mkutano.

SURA INAYOENDELEA
 
Umenikumbusha Mbali Sana 😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
App nimeshasau ata inaitwaje naomba nitajie nirudi kuichukua
 
SURA YA 3​

SIKU ya pili, Luteni Maige aliamua kuugua. Hakuwa na chochote kilichomsumbua ila tu alitaka apate nafasi ya siku mbili-tatu za kukamilisha mipango michache iliyosalia.

Kitu cha kwanza kilichoingia mawazoni mwa Luteni Maige ni kumrudisha Veronica Mwanza kwa wazee wake. Kilichomsumbua kichwa ni jinsi ya kumweleza mpaka akubali kuondoka kwa sababu haijapita hata miezi mitatu tangu arudi kutoka huko kumpa pole shangazi yake aliyeumwa na nyoka shambani.

Baada ya kufikiri sana na kuona umuhimu uliopo wa Vero kuondoka kabla ya Ijumaa, Maige aliamua kubuni simu ya uongo. Angemtafuta mtu na kumuambia apige simu kutoa taarifa kwamba: Baba yenu mgonjwa sana. Aliamini kuwa kwa mshtuko ambao angeupata, Vero asingekuwa na hata dakika ya kuhoji.

Mnamo saa nne za asubuhi, baada ya kumuaga Vero kwamba anakwenda Hindu Mandal kupima damu na kwamba huenda akachelewa kurudi, Maige alitoka. Lakini kabla ya kuanza safari yake ya kuelekea mjini, alimpitia Kapteni Shaibu.

Alimkuta akiyapitia mafaili matatu yaliyokuwa mezani mbele yake.

“Habari ya asubuhi, mzee?”

Shaibu alilisukuma kando moja ya mafaili matatu alilokuwa akilishughulikia wakati ule, akaketi vema kitini.

“Nzuri, Maige. Karibu.” Alimwelekeza kwa ishara kiti kilichokuwa upande wa pili wa meza yake. Maige alipoketi, Shaibu akaendelea, “Habari za tangu jana?”

“Si mbaya, mzee. Ila nimeamua kuumwa leo.”

‘‘Kwa nini?” Kwa mbali uso wa Shaibu ulionyesha mshangao.

“Kwanza nataka kwenda kwa Mohsin ili anipeleke kwa Sadrudin ili niweze kupata wasaa wa kwenda eneo la tukio nikalikague; kupanga mashambulizi vyema siku ya Ijumaa.”

Mshangao wa Kapteni Shaibu uliongezeka alipouliza, “Lakini jana si mlikubaliana na Sadru kwamba mtakutana kwa Mohsin siku ya Alhamisi ndipo akakuonyeshe mahali hapo? Au sivyo?”

“Ndivyo tulivyokubaliana. Lakini mara nyingine, kwa shughuli kama hii, ni vizuri kuepuka ahadi mkafanya mambo kwa kushtukizana. Inasaidia kuepusha mizengwe.” Shaibu alishusha pumzi.

“Na kama usipowakuta?”

Maige aliitazama saa yake ya mkononi.

“Saa hizi Mohsin huwa hatoki nyumbani. Na akitoka huwa hakawii kurudi. Nikishampata yeye, kumpata Sadrudin haitakuwa tatizo. Hilo la kwanza. La Pili, nimefikiria kumpeleka Vero kwao Sengerema, Mwanza, kabla ya Ijumaa. Akiwapo hapa atanitia wasiwasi sana… kitu ambacho sitaki.”

Shaibu alikuna kichwa.

“Si atataka kujua kwa nini anaondolewa msobemsobe? Unayo sababu ya maana ya kumweleza?”

“Hilo si tatizo. Nina sababu nzuri ya kumweleza ambayo itamwondoa huku akiwa anaomba afike upesi. Itabidi aondoke kwa ndege, tena ya kesho au keshokutwa. Nina hakika Mohsin na Sadrudin wanaweza kunipatia tiketi ya VIP maana sitaki aondoke wazi.”

“Sawa, Nami nitakuwa nikiongea na vijana mara kwa mara ili kuzidi kuwatia moyo. Nenda kashughulike.”

***

llikuwa ikikaribia saa nne kasorobo Maige alipofika nyumbani kwa Mohsin. Alimkuta ameketi sebuleni akizipitia kurasa za gazeti la Uhuru.

“Karibu, Bwana Maige,” Mohsin alisema alipomwona Luteni huyo akiingia. Kisha akalifunga gazeti alilokuwa akisoma, akaliweka pembeni. “Keti, tafadhali.”

Maige alichagua kiti kilichokuwa karibu na Mohsin, akaketi.

“Habari za tangu jana, Bwana Mohsin?”

“Si mbaya. Ana hali gani Bwana Shaibu?”

“Hajambo.” Alivuta pumzi ndefu akazishusha taratibu. Kisha akasema, “Unadhani, Bwana Mohsin, ninaweza kuonana na Bwana Sadrudin leo?”

“Asubuhi hii?” Kidogo uso na sauti ya Mohsin vilionyesha mshangao.

“İkiwezekana.”

“Kwani una shida naye sana?”

“Kwa kweli nina shida na nyote wawili.” Alijiweka vema kitini, akaendelea, ‘‘Nataka nionane naye ili anipeleke mwenyewe eneo la tukio, na pia nichague mahala rasmi tutakapo anza na shambulizi la kushtukiza. Na wewe…”

“Lakini, Bwana Maige,” Mohsin alimkatiza, “jana tulipokutana si mlikubaliana kuwa mambo hayo mtaonyeshana Alhamisi? Au sivyo?’?

‘‘Ndivyo. Lakini pia usisahau kitu kimoja, Bwana Mohsin.”

“Kipi?” Mohsin alimtumbulia macho.

“Katika mipango kama hii ya kutaka kumuua mtu, hasa kama mtu mwenyewe ni kiongozi wa nchi, hamuwezi mkatungiana sheria. Sijui unanielewa”

“Sijakuelewa.” Mohsin alitingisha kichwa. “Kutungiana sheria kwa vipi, Bwana Maige?”

Maige alivuta pumzi ndefu, akazishusha taratibu. Kisha akasema, “Jana, kwa mfano, tulikutana, tukazungumza na tukakubaliana mambo mengi. Moja ya mambo havo ni kukutana mimi na Bwana Sadrudin siku ya Alhamisi akanionyeshe eneo nililochagua.

Sawa?”

“Sawa.” “Sasa, kukubaliana kwetu hakuwezi kukawa sheria. Kwamba maadam tumesema Alhamisi - ndio baaaasi! Kwamba midhali tumepanga basi ni sheria. Kukutana kabla ya hapo ni kuvunja sheria. Hiyo si sawa, Bwana Mohsin, na haiwezekani kabisa. Huu ni mpango wetu. Tuna uwezo wa kubadili hiki au kile, au hata vyote, dakika yoyote, mradi tu mabadiliko hayo hayaharibu msimamo wetu. Nadhani umenielewa.”

Mohsin alikubali kwa kubetua kichwa. Kwa sauti ndogo, akasema, “Kwa hiyo ungependa uonane naye leo akuonyeshe sivyo?”

“Ikiwezekana.”

“Utamwona.” Alinyamaza kidogo, kisha akasema, “Enhe, na mimi ulitaka kuniona kwa shida ipi?”

Bila ya kusita, Maige alisema, “Nataka unifanyie mpango wa tiketi ya ndege ya Mwanza ya kuondoka kesho au keshokutwa. VIP. Ni muhimu sana.”

Uso wa Mohsin ulionyesha mshangao ambao hata kipofu angemudu kuutambua.

“Una safiri?”

“Hapana. Namsafirisha mke wangu. Ni hivi, Bwana Mohsin. Ijumaa haiko mbali sana. Na hicho ninachodhamiria kufanya ifikapo siku hiyo ni lawama, si kwa Watanzania tu, bali kwa ulimwengu mzima. Sitaki kuwa na mwanamke ndani ya nyumba ambaye najua atatapatapa na kuanza kubabaika, akishatambua kuwa mimi ndiye kinara wa huu mpango. Ndio maana namsafirisha mapema kabla ya hiyo siku ili pasiwepo mtu wa kunivuruga mawazo. Si umenielewa?”

“Nimekuelewa sana.” Alinyamaza kidogo, akaligeuza geuza gazeti la Uhuru lililokuwa mbele yake kama aliyekuwa akitaka kuendelea kulisoma. Kisha akasema, “Lakini, Bwana Maige, ukimsafirisha ghafla hivyo, hudhani kwamba utatia wasiwasi?”

“Hilo nilishalifikiria mapema, nitahitaji apigiwe simu ya uongo kuelezwa kwamba baba yake ni mgonjwa mahututi”

“Hapo lazima aondoke kwa haraka’

“Hili limekwisha. Twende na la kukutana na Visram.

Mohsin aliinuka akaiendea simu iliyokuwa juu ya meza ndefu iliyoegemezwa pembeni mwa ukuta. Aliinua, akazungusha nambari ya Sadrudin Visram.

Ilikuwa kama bahati. Sadrudin mwenyewe ndiye aliyepokea simu hiyo.

“Sadru. Nani mwenzangu?”

“Mohsin. Una hali gani, Bwana Visram?”

“Nzuri. Vipi shughuli?”

“Zinaendelea. Luteni yupo hapa.”

Mohsin aligeuza macho mara moja akamtazama Maige.

“Luteni Maige. Ana shida nawe. Anataka muonane ikiwezekana.” Mohsin alimsikia waziwazi Sadrudin akivuta pumzi na kuzishusha.

“Mbona ghafla? Ana shida gani?”

‘‘lle ile mipango. Nimwelekeze kwako, au akusubiri hapa?”

Palizuka kimya cha karibu nukta sita au saba hivi. Kisha Sadru akasema, “Namsubiri. Mwelekeze aje.” Akakata simu.

Taratibu, Mohsin aliiweka simu chini, akarudi kitini pake.

Maige alimtazama, kinywa wazi. “Kasemaje?’“An akusubiri wewe huko huko kwake.”

“Ahaa! Sawa.” Maige aliachia tabasamu pana. “Ukinieiekeza nadhani sitapotea.”

Mohsin alimwelekeza. Alipoakikisha kuwa amepaelewa mahali hapo vizuri, akamwambia, “Ukitoka huko pitia tiketi yako muda wowote. Itakuwa tayari. Bwana Visram ana watu muhimu kama watano wanaojuana nao ambao ni wafanyakazi wa shirika la Ndege. Nina hakika hatashindwa kukufanyia mpango wa tiketi ya Mwanza kwa ndege ya kesho mchana.”

“Nitashukuru sana. Bwana Mohsin.” Alisimama, akamnyooshea mkono. “Nitapita baadaye. Nadhani nitakukuta.”

“Sitoki. Njoo tu”

Wakaagana

Itaendelea.....
 
Kabla sijaanza kusoma, naomba nikupongeze mleta Uzi, ! Hammie Rajab one of my favourite, nakumbuka shelf home ilikuwa imejaa vitabu vyake.
Thanks for bringing back my lovely memories.
RIP mom.
 
Sura ya tatu inaendelea

Barabara ya Umoja wa wanawake ilikuwa na nyumba chache tu za kawaida. Nyingi zilikuwa za ghorofa mbili au tatu.

Jengo la ghorofa tatu alimokuwa akiishi Sadrudin lilikuwa limechomoza katikati ya majengo mawili ya ghorofa mbili. Pembeni mwa jengo hilo, sehemu ya chini, kulikuwa na banda lililokuwa na nafasi ya kutosha kuegesha hata behewa la abiria, achilia mbali Peogeot 404 iliyokuwamo mle ndani.

Mlango wa mbele wa jengo hilo ulikuwa umefungwa. Alipoufikia, Maige alikitazama kidude cha kubonyezea kengele kilichokuwa ukutani, pembeni mwa mlango, akakibonyeza.

Ukimya uliokuwapo katika jengo hilo haukuonyesha dalili yoyote kwamba mlikuwamo watu wakiishi mle ndani. Akabonyeza tena. Safari hii aliliachia dole lake liendelee kubonyeza kwa nukta kadhaa. Kisha akaliondoa. Akasubiri.

Kwa mbali alisikia nyayo za mtu aliyevaa kandambili zikija haraka. Mlango ukafunguliwa.

Mtu wa makamo asiyepungua umri wa miaka arobaini na mitano alisimama nyuma ya mlango wakitazamana. Mara moja Maige alimtambua kuwa ni mfanyakazi wa mle adani.

“Nikusaidie nini, ndugu yangu?” mtu huyo aliuliza.

“Hapa ndipo anapoishi Sadrudin?’

“Bwana Sadrudin Visram?”

“Ndiyo. Ananisubiri tuonane. Ana habari kwamba nakuja.”

“Ni hapa. Wewe ndiye Bwana… Maiko vile?”

‘‘Hapana. Sio Maiko. Maige.”

“Ee ndiyo..„ Maige. Karibu. Alinambia ukifika nikupeleke kwake. Yuko juu anakusubiri. Twende.”

Sadrudin alikuwa ameketi sebuleni akisikiliza kipindi cha Habari za Ulimwengu kutoka BBC, London, wakati mtumishi wake alipogonga mlango. Sadrudin alipunguza sauti, akauliza,

“Nani?”

“Mimi, mzee. Bwana….. Maige amekuja.” Sadrudin alifunga kabisa radio, akatoka.

“Karibu, Bwana Maige. Karibu ndani.”

Maige alimtazama mtumishi wa Sadrudin, akamshukuru, kisha akaingia. Ilikuwa sebule iliyopambika vizuri. Katika kuta zote nne kulikuwako picha kadhaa za viongozi wakuu wa dini ya Kihindu. Seti tatu za sofa zenye vitambaa vya rangi ya bluu zilizunguka sebule nzima, zikaacha nafasi ya kutosha kwa zulia jekundu lenye manyoya mafupi lisambae katikati.

Juu ya meza ndefu iliyosukumwa chini ya dirisha pana, kulikuwako runinga, radio kubwa na vitu kadhaa vya mapambano vilivyomgharimu Sadru fedha nyingi.

Sadrudin alimpa nafasi Maige ayaliwaze macho yake, kisha akamwuiiza, ‘‘Habari za tangu jana?”

Maige aliyaondosha macho yake haraka kwenye saa ya ukutani iliyokuwa ikionyesha maporomoko ya maji, akamtazama Sadru huku akitabasamu.

“Nzuri tu. Vipi shughuli?”

‘Shughuli zinaendelea. Bwana Mohsin alinipigia simu kwamba unataka tuonane.”

Maige alivuta pumzi ndefu, akazishusha

“Ndiyo, Bwana Sadru. Ni katika jumla ya mipango ile ile. Kilichonileta ni kwenda kulikagua eneo la tukio.

Sadru alikuna ncha ya kidevu chake. Akasema, ‘‘Kuhusu eneo la tukio, Bwana Maige, si tulikubaliana ulione Alhamisi?”

‘‘Nakumbuka sana. Lakini, kama nilivyomweleza Bwana Mohsin muda mfupi tu uliopita, kwamba mambo haya kwa kweli ni magumu, na si vizuri kuyatungia sheria. Mnaweza mkajikuta hamfanyi lolote.”

“Kuyapangia sheria vipi, Bwana Maige?”

“Maana yangu ni kwamba isiwe maadam tumekubaliana hiyo Alhamisi, ndio kama tumepitisha sheria. Yaani mabadiliko hayawezekani kufanyika. Mipango ya kumuua kiongozi wa nchi, Bwana Sadru, ndio mapinduzi yenyewe. Na ni mapinduzi ya kumwaga damu. Sheria zinaweza zikaja baada ya kumaliza kazi, sio kabla. Ndipo nilipoona afadhali nikalione eneo la tukio, japokuwa tulikubaliana iwe Alhamisi. Nadhani umenielewa.”

Sadrudin alikubali kwa kubetua kichwa, Kisha akasema, “Kwanza kuhusu eneo la kambi mtakayokaa kabla ya sehemu ya tukio, ni nyumba hiyo hapo ya pili ya ghorofa tatu. Ni eneo salama. Ni nyumba ambayo wanatumia watoto wanguambao hivi sasa wako shuleni. Ina ukimya wa kutosha na haiko wazi.”

“Sawa. Tena imekuwa vizuri watoto hawapo.’’

“Twende mara moja ukakague ili tuendelee na mambo mengine.”

Wakatoka.

Kati ya vyumba vitatu alivyoonyeshwa, Maige alipendezewa sana na kimoja.

“Humu huwa tunakaribisha wageni,” Sadru alimweleza juu ya chumba hicho. “Hivi sasa kiko wazi tu. Unaweza kukitumia kama ndicho unachoona kinafaa.”

Hakikuwa kipana. Kilikuwa cha wastani tu. Dirisha lake lilielekea upande mzuri wa Barabara ya Umoja wa Wanawake. Na ilikuwa rahisi kutumia dirisha hilo kupanga mchoro mzima wa tukio na mashambulizi.

Maige aliliendea dirisha hilo, akasukuma pazia upande mmoja. Sura aliyoiona chini kutoka pale aliposimama ilimpa matumaini makubwa ya kuifanya kazi yake vizuri. Alikuwa na hakika kwamba akitumia bunduki ya kulenga shabaha, umbali aliopo na umbali wa barabara na gari atakayopanda kiongozi wa nchi, abadani kutokana na ujuzi wake hawezi kushindwa hata chembe kuachia risasi itakayotoa uhai. Ilikuwa kama bahati sana kwamba eneo ambalo alilipanga kwa ajili ya kuiliza nchi, ni eneo ambalo bwana Visram ana nyumba tena iliyo na uhuru na amani ya kuweza kukamilisha mchakato.

Akakagua kwa mara ya pili huku kama akijibizana na akili yake kwamba risasi yake isingeweza kumkosa mtu yeyote aliyekuwa akisafiri ndani ya gari lililokuwa likipita kule chini hata kama gari hilo lingeendeshwa kwa kasi mithili ya jet, na madirisha yake kufungwa kwa vyuma, achilia mbali vioo.

Alilirudisha pazia mahali pake, akamgeukia Sadru.

“Hapa safi,” alisema, akaachia tabasamu pana. “Tena safi saaana.”

‘‘Vizuri. Tumia hiki.”

“Alhamisi usiku nitaleta silaha na nitataka kambi hii iwe yangu peke yangu. Nitaleta silaha yangu ilale humu humu ndani. Ijumaa, kuanzia saa mbili asubuhi, nitakuwa mgeni rasmi wa chumba hiki. Tuombe Mungu. "

“Inshaalah.”

Wakarudi sebuleni.

“Tumemaliza.” Sadru alimtazama Maige.

“Naona.” Uso wa Maige ulipambwa kwa tabasamu pana.

Mwisho wa sura ya tatu​
 
Sura ya nne​
Jumatano saa Sita na nusu mchana. Kapteni Shaibu alikuwa ameketi nyuma ya meza yake akifikiria jinsi hali itakavyokuwa keshokutwa, Ijumaa, baada ya Luteni Maige kukamilisha kazi waliyopanga.

Kwa mbali, moyo wa Shaibu ulikuwa ukidunda na kijasho kikimvuja. Wasiwasi uliokuwa ukimjia mara kwa mara ulimshawishi aachilie mbali kushiriki katika jambo hilo. Lakini kila alipowaza hivyo, onyo la wazi lilimjia akilini mwake: Ukijitoa, umejitilia saini kifo chako. Maige atakuua! Na ni nusu saa tu iliyopita, Luteni Maige alikuwa ofisini mwake wakijadili na kukubaliana kwamba silaha zote zinazohitajika zipatikane kesho, Alhamisi, kabla ya saa kumi jioni. Baada ya makubaliano hayo, Shaibu asingeweza kabisa kubadili mawazo.

Alipokuwa bado yumo katikati ya mawazo hayo, mlio mkali wa simu iliyokuwa mbele yake ukamshtua. Alinyoosha mkono, akaiinua.

“Shaibu. Nani mwenzangu?”

“Mambo ya Ndani hapa.”

Moyo wa Shaibu ukapiga kwa kasi zaidi. Hakutegemea kabisa kupata simu kutoka huko japokuwa alishaitambua sauti ya aliyempigia simu hiyo. Walishakubaliana asingempigia simu tena hadi shughuli yote imekamilika; ila kama pangekuwa na jambo Ia tahadhari.

“Vipi, Silas?” Sauti ya Shaibu haikuficha wasiwasi aliokuwa nao.

“Mpira hauchezeki! Mambo yameharibika kabisa!”

Shaibu alimeza funda kubwa la mate. Kisha akauliza, “Unazungumza kutoka wapi?”

“Kibanda kimojawapo cha simu” Silas alisema, “Sikiliza, Kapteni. Mohsin, Paskali, Nyirenda na Big Ben wametiwa mbaroni. Hivi sasa…”

“Nini? Imekuwaje? Haiwezekani? Kivipi?” Aliuliza akiwa haamini masikio yake. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka kiasi ambacho mkono wa simu uliroa ghafla.

“Yaani ni balaa. Kila kitu kimeharibika ghafla! Wamekamatwa tangu jana usiku kama saa tatu. Mohsin alifuatwa nyumbani kwake saa sita na difenda za polisi.. Mpaka hivi sasa bado wako kituo cha polisi wakihojiwa. Na kutokana na taarifa niliyonayo, leo au kesho mtaingiliwa hapo jeshini. Bwana Shaibu, nimekupa taarifa mapema, sasa akili kichwani mwako. Kwaheri.”

“Ngoja kwanza! Usikate -simu, Silas! Sasa… Nini hasa kimetokea mbona mipango ilikuwa inaenda sawa?” aliuliza kwa sauti ya kitetemeshi bado haamini alichokisikia.

“Mambo mmeyaharibu wenyewe!” Silas alilaumu. “Yule mhuni mlimshirikisha ili asaidie nini?”

“Mhuni yupi?”

“Big ben. Alikuwa afanye nini hasa?”

“Tulitaka asaidie mauaji. Kwani amefanyaje? Mbona unazidi kunichanganya?”

“Mpuuzi sana yule jamaa. Sijui hata ilikuwaje akaweza kuwa jambazi mwenye mtandao na aliyeweza kuitetemesha nchi? Kaenda kwa mwanamke wake, akalewa, akatoka hapo akaenda tena Bar akaongeza pombe, baada ya kulewa chakari akaanza kujitamba kwamba maisha ya kujificha yamekwisha na siku mbili zijazo atafanya mapinduzi kwa kumuua Rais na yeye atakuwa Waziri Mkuu. Shenzi kabisa.. Na kwani! Hivyo ndivyo mlivyomuahidi?”

“Aisee!.. Yaani.. Hivii. Mungu wangu..” Kigugumizi kikamshika.

“Na kwa vile polisi walikuwa na kiu nae muda mrefu, walimtesa, akawataja Paskali na Mohsin. Bado nyie”

“Yaani…. Wewe humo?”

“Bwana Shaibu, tafadhali sana.” Sauti ya Silas ilikuwa na hasira iliyojaa kitetemeshi. “Tusitajane! Kila mtu achukue mzigo wake mwenyewe. Kwaheri.”

Akakata simu.

Kwa nukta mbili-tatu zaidi, huku kinywa

akikiacha nusu wazi kwa mshangao uliochanganyika na hofu, Shaibu aliendelea kuishikilia simu. Kisha, kwa mkono uliokuwa ukitetemeka, akaiweka chini taratibu.

Alivuta pumzi ndefu, akazishusha.

Vitu viwili vilimjia haraka mawazoni mwake, Kwanza, ampigie simu Luteni Maige amjulishe hali ilivyo. Pili, akishamjulisha, naye afanye mipango ya kukimbia haraka iwezekanavyo.

Mawazo yote mawili aliyaafiki. Lakini angemjulishaje Maige? Alijiuliza. Alipokuwa naye ofisini mwake nusu saa iliyopita wakijadili juu ya mipango ya silaha, Maige alimuaga Shaibu kwamba angekwenda mjini kuonana na Mohsin na Sadru, kisha amalize mambo mawili-matatu muhimu ndipo arudi. Shughuli yote hiyo ingemchukua kama masaa matatu. Hivyo Shaibu hakutegemea kuonana na Maige hadi saa kumi hivi.

Shaibu alivuta pumzi zingine ndefu, akazishusha taratibu. Pamoja na hali tulivu iliyokuwamo ofisini mwake na kijibaridi kisicho madhara kilichoingizwa na mashine ya Daikin iliyochomekwa ukutani, mwili wake ulihisi joto lililomsababishia michirizi ya jasho lililotoka kwapani.

‘Lazima nikimbie haraka.’ Alijisemea moyoni. Ilimuia vigumu sana kuwaza haraka haraka akimbilie wapi, lakini hilo alilifanya anapoelekea atapajua baadae. Popote atakapokwenda ni sawa tu mradi asiwepo jeshini muda huo balaa likamkuta hapo. Hakujidanganya kabisa kuwa baada ya kuhojiwa na polisi na kupata mateso madogo tu, Mohsin, Paskali na Big Ben wangemudu kufunga midomo yao. Lazima wangewataja. Na kwa vile Silas alishamtahadharisha kuwa wangeweza kuingiliwa siku ile au kesho yake, hofu yake iliongezeka mara mbili.

Alifungua saraka ya meza, akatoa vitu vyake muhimu. Alipoífunga saraka hiyo, alijiinua kitini, akatembea kwa hatua za haraka kuelekea mlangoni.

Kabla hajafungua mlango, kama vile ilikuwa ikimwona, simu yake ikaanza kuita. Shaibu aligeuka kama aliyechomwa sindano mgongoni. Huku akihisi kizunguzungu na moyo ukimwenda mbio, aliiangalia simu hiyo huku akiilaani, akaiacha ilie mara kadhaa akitegemea anayepiga atakata tamaa. Kisha akaiendea na kuiinua.

“Kapteni Shaibu”

“Ofisini kwa Meja Jenerali Kaswiza” sauti ya mwanamke ilisema. “Tafadhali , Kapteni mzee anakuita ofisini kwake”

“Sasa hivi?”

“Acha unachofanya. Njoo haraka. Ni muhimu.” Mwanamke alikata simu.

Kwa mara nyingine, moyo wa Shaibu ukapiga kasi maradufu. Pale pale alihisi kuishiwa na nguvu mwili mzima. Aliirudisha simu, akatoka.

***

Wakati hayo yote yakitokea, Luteni Maige alimwamuru dereva wa taksi aliyokodi asimame kama hatua hamsini kutoka nyumba ya Mohsin. Alimlipa dereva huyo, akatoka.

Alitembea kama hatua tano tu kuelekea nyumba hiyo, akasita. Bila ya kusimama au kuonyesha ishara ya woga, Maige aligeuka na kuelekea upande wa kushoto lilikokuwako jengo la ghorofa moja ya nyumba ya kulala wageni.

Alipochanganyika na watu waliokuwa wakitoka na kuingia ndani ya jengo hilo, alisimama, akageuka na kuangalia nyumba ya Mohsin. Mbele ya nyumba hiyo palikuwepo watu wawili. Wote walivaa nguo za kiraia. Mmoja alikuwa akitembea huku na huku, akiokota vijiwe na kuvipiga teke. Alikuwa mrefu, mweusi fii, mwenye umbo zito lililokaribia kufanana na la mpiganaji mieleka.

Mwenzake ambaye alikuwa maji ya kunde na mwenye umbo la wastani, aliegemea ukutani akisoma gazeti.

Macho ya Maige yalimganda huyo wa ukutani, akimwangalia kwa makini jinsi alivyokuwa akiyaondosha macho yake gazetini na kuangaza kila upande, na kisha kuyarudisha tena gazetini. Mara mbili au tatu alifunga gazeti bila ya kujali alikuwa akisoma ukurasa upi, akamsemesha mwenzake aliyekuwa akipiga teke vijiwe.

Askari!

Luteni Maige alitambua hivyo haraka sana. Jinsi wailivyojiweka mbele ya nyumba hiyo, jinsi walivyokuwa wakitupa macho pande zote za mtaa huo, jinsi walivyokuwa wakiongea kwa siri na kujifanya si wamoja, mjuzi yeyote angewatambua ni askari.

Moyo wa Maige ukapiga mshindo mdogo.

Kumetokea nini, alijiuliza. Kwa nini nyumba ya Mohsin ilindwe na askari? Mohsin mwenyewe yuko wapi? Swali hilo la mwisho ndilo lililomfanya aondoke haraka mahali pale na ajaribu kuchunguza yaliyotokea.

Nyuma ya jengo la nyumba ya kulala wageni, mtaa wa pili, kulikuweko kibanda cha simu. Maige aliingia ndani ya kibanda hicho, akatoa sarafu mbili za shilingi.

Alipoinua simu na kuanza kuzunguusha nambari ya Mohsin, moyo wake ukashtuka. Hatari hiyo! Alijionya. Maadam kuna askari wakilinda nje ya nyumba ya Mohsin, kuna uwezekano kabisa kuwa hata simu yake iko chini ya ulinzi. Huenda posta wameamriwa wanase katika kanda kila simu inayoingia nyumbani kwa Mohsin, na watoe taarifa kwa polisi simu hiyo ilipigiwa kibanda kipi.

Badala yake akazungusha nambari ya Sadru.

Zilipita kama nukta sita kabla simu ya upande wa pili haijainuliwa. Ilipoinuliwa, sauti ya wazi ilisema, “Nyumbani kwa bwana Visram.”

“We nani?” Maige hakutaka kujiingiza mtegoni.

“Mfanyakazi wake.”

“Bwana Visram yupo?”

“Hayupo.”

“Amekwenda wapi?”

“Kaondoka asubuhi na watoto wake.”

“Kasema wanakwenda wapi?”

Pakazuka kimya cha nukta mbili-tatu hivi.

“Kwani… kwani we nani, mwenzangu?” mfanyakazi aliuliza.

Akili ya Maige haikukawia kuuona mtego wa swali hilo.

“Yule aliyekuja juzi ukampokea. Unamkumbuka?”

“Alaaa! Bwana Maiko!”

“Maige.”

“Ndiyo nakukumbuka. Ni hivi, Bwana Maige. Bwana Visram, mkewe na watoto wao wawili, wameondoka asubuhi sana, Mkewe na watoto wamekwenda Arusha na baba yao mdogo. Visram mwenyewe yuko Upanga kwa wakweze. Kwa sasa hivi sina hakika kama bado yupo au naye ameshaondoka.” Mtu huyo akavuta pumzi kidogo kisha akaendelea… “Aliniachia ujumbe kuwa ukipiga simu au ukija mwenyewe, nikupe nambari yake ya simu uongee naye.”

“Ndio kusema hapo nyumbani kwake kahama?”

“Sina hakika, lakini ndivyo inavyoelekea.”

“Aliwahi kukueleza kwa nini anahama?” ‘‘Hata. Unajua tena hawa wenzetu walivyo.

Hata ufanye kazi kwake miaka ishirini, maadam wewe Mswahili, hakwambii siri yake. Kwa hiyo sijui.”

“Nipe hiyo nambari aliyokuachia.” Akatoa kalamu.

“Hii hapa. Una kalamu hapo?”

“Ninayo. Nitajie tu”. Akamtajia.

Haikuchukua zaidi ya dakika mbili kuipata nambari hiyo. Ilikuwa bahati sana kwani Sadru mwenyewe ndiye aliyeipokea simu hiyo.

“Visram.” Sauti yake ilikuwa ya chini. “Nani mwenzangu?”

“Maige.”

“Oh, Maige. Uko wapi?”

‘‘Kwenye kibanda cha simu, si mbali na nyumba ya Bwana Mohsin. Mbona hivi, jamani? Vipi?”

“Huna habari?”

“Sina. Imekuwaje?”

“Limelipuka!”

“Unasemaje?” Maige hakuamini.

“Yameharibika. Mohsin, Paskali na Big Ben wametiwa mbaroni tangu jana usiku. Hivi kweli huna habari, Maige?” “Sina. Nini kimetokea? Nani amevujisha siri” akauliza mapigo ya moyo yakianza kwenda kasi.

“Kwa kweli sijui. Na sina haja ya kujua kwa sasa. Watoto wangu nimeshawasafirisha, na mimi natazamia kuondoka dakika yoyote kukimbilia mafichoni. Fanya haraka iwezekanavyo nawe upotee”

“Sina pesa, sina usafiri. Na siwezi kurudi nyumbani wala kwenda popote ninapotambulika maana itakuwa sasa hivi usalama wa Taifa wamezagaa kutusaka sehemu tunazoweza kufika.”

“Hilo si tatizo, naweza kukupa msaada. Unaujua Mtaa wa Kabwe uliyopo Upanga?”

“Siujui, lakini nitautafuta. Nielekeze ulipo.”

“Huwezi kuupotea. Nenda kwenye nyumba yenye nambari 69. Hunikuti, na sitaki tuonane. Ila mbele ya nyumba hiyo utalikuta gari dogo aina ya Toyota lenye rangi ya bluu. Ni safi na lina mafuta ya kutosha. Ufunguo wake utaukuta humo. Ndani ya kidawati cha upande wa kushoto nitakuwekea kiasi cha pesa cha kutosha. Chukua hilo gari uondoke. Omba Mungu. Kwaheri.”

Maige aliiweka simu chini akiwa amechanganyikiwa. Ni kweli au ni masihara? Kwanza akajiuliza alichokisikia amekisikia kiusahihi? Na kama ni kweli hivi amuamini au ni mtego!

Akaganda hapo nukta kadhaa kisha akaona inawezakana ni kweli na sasa si muda wa kujiuliza bali kuangalia namna ya kutoweka kabla hajaingia katika mikono ya wana usalama. Hata simu hakuirudisha mahala husika, akatoka haraka akiangalia huku na kule kuhakikisha usalama wake.

Mwisho wa sura ya nne​
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom