Taifa_Kwanza
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 443
- 86
Halmashauri ambazo Chama cha Democrasia na Maendeleo kimepata ridhaa ya wananchi kuziongoza, pamoja na Majimbo ya ubunge yanaweza kuwa kitanzi dhidi ya chama hicho siku za usoni hasa kama hawatakidhi mategemeo ya wananchi.
Dalili zimeishaanza kuonekana uko nyumbani Mwanza kwenye jimbo la Nyamagana, Meya wa Jiji la Mwanza (Manyerere) ametofautiana na mbunge wa Njamagana (Wenje) kwenye namna ya kutatua tatizo la Wamachinga, Meya anadai lazima Sheria zifuatwe na hivyo Machinga ni Lazima wahame kutoka maeneo fulani fulani katikati ya jiji la Mwanza. Machinga wanamlilia Wenje aliyewaahidi kwamba hawatazumbuliwa kamwe kama wakimchagua. Katika hili wenye ameishaanza kuchanganya mambo sababu anadai hajawahi kutoka ahadi ya namna hiyo (usaliti dhidi ya wananchi).
Natambua kwamba kwa jitihada za Wenje, Jiji limeridhia kutoa baadhi ya maeneo kwa Wamachinga, lakini
tatizo bado halijatatuliwa kwa maana ya kutuliza kelele za mahitaji ya Wamachinga.
Angalizo
Viongozi wa CDM katika Halmashauri zinazoongozwa na CDM wawe makini sana katika utendaji kazi zao, wasidanganywe kukimbilia kujificha nyuma ya sheria zilizowekwa sababu nyingi ziliwekwa na CCM, wawe tayari kuzibadilisha ili kukidhi matakwa ya wapiga kura wao, na wawe makini na uswaiba wa viongozi wenye Damu ya CCM, Meya na Madiwani wa CDM Mwanza angalieni sana uswaiba wenu na sheria zilizopo, Mkurugenzi wa Jiji (Kabwe) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hawa watatu wote ni CCM, na watakuwa kamba shingoni mwenu muda si mrefu.