Je, kinachoendelea jiji la Arusha ni hujuma kwa serikali ya Mama Samia?

Tanzaoregano

New Member
Aug 31, 2022
3
1
Wanabodi habari ya muda huu?

Nimekua nikifuatilia kwa karibu kinachoendelea katika Jiji la Arusha kwakweli hakina Afya sana kwa siasa za awamu ya sita. Ikimbukwe kihistoria jimbo hili ni la upinzani na CCM imetumia nguvu kubwa sana kulirudisha, lakini kinachoendelea ni kama kuchezea shilingi chooni.

Nijikite kwenye mfano mmoja wa namna mgambo wa Jiji la Arusha wanavyotumika kuumiza wananchi na biashara za wananchi. Mara nyingi maelekezo yanapotoka serikali kuu utekelezaji hufanyika kwa kukiuka misingi ya utu na haki za binadamu.

Serikali ilitoa maelekezo machinga wapangwe lakini kinachofanyika Jiji la Arusha ni unyama na ukatili mpaka unahisi labda watu wanafanya makusudi kumjengea Riais Samia mazingira magumu ya kukubalika kwa wananchi wa kawaida. Hili linasemwa kwakuwa ukiangalia miaka mitatu hapo nyuma wamachinga waliachwa huru kabisa lakini baada ya kutolewa maelekezo ya kupangwa wananyanyasika na kurudishwa kwenye umaskini. Je kwa hali ya kawaida unadhani lawama zao zinaelekezwa wapi?

Hatukatai machinga kupangwa, mbona Jiji la Dodoma wamepangwa na hakuna sintofahamu kama hii inayoendelea Arusha?

Mathalani juzi hapa kumevunjwa banda maarufu la kuuza baga/burger lililokua kwa zaidi ya miaka 13 jirani na benki ya Stanbic Arusha.

Inasikitisha sana kuona madiwani wa Jiji la Arusha kupitia kikao Cha mipangomiji na vikao vingine wamepitisha kuvunjwa kwa eneo hili kwa kupewa rushwa ya laki 2 kwa kila diwani na wakuu wa idara za Sheria na mipangomiji.

Hii ni aibu kubwa sana kwa watu wanao jiita ni wawakilishi wa wananchi kukubali wananchi wateseke kwa laki

2. Hela hizo zilipokelewa na Diwani wa kata ya lemara mhe Naboth kwenye mgahawa wa uzunguni. Diwani wa kata ya Themi mhe lobora alisikitika kuona habari hizo zimevuja wakati wao walipitisha kwa Siri kwenye vikao.

Madiwani wanakiri ni kweli muuza BAGA huyu alikuwa analipa Kodi ila tatizo atoi chakula kwa madiwani ambao malipo yao ni madogo sana. Hata diwani akienda pale anauziwa BAGA badala ya kupewa bure.

Ccm msipoangalia hawa madiwani watakimaliza hiki chama Arusha mjini.

Hivi punde mtapata habari ya namna madiwani wanavyo kura rushwa kwa watu mbalimbali kupitia kamati ya mipangomiji.

Mgambo siku ya kuvunja sehemu ya BAGA walipigwa picha na kinyozi pale jirani na wakaenda kumfanyia vurugu na kufuta picha bila kujua waliopiga ni wengi. Kama ni zoezi la halali hofu ya nini?. Na ukisikiliza viongozi wanaongea as if walikua na nia njema lakini kiuhalisia ni rushwa na uonevu tu.

Mapendekezo yangu kwa serikali, wananchi kwasasa wanajua hii ni serikali ya matajiri na wanyonge hawana nafasi hivyo muangalie siasa za Arusha hazifanani na eneo lolote nchi hii, zinahitaji akili kubwa na hesabu ndefu. Mathalani unaona hata wapinzani wamekaa kimya wanasubiri CCM mharibu ili 2025 wapate sababu za kuwanyoosha kwenye uchaguzi.

Wito kwa madiwani wa Arusha, njaa zitawaponza. Waswahili wanasema bora ndege mmoja aliye mkononi kuliko wawili walio kichakani, mnatumika sana kwa maslahi ya watu wachache. Mkumbuke hawa wananchi mnaotumika kuwanyanyasa sasa wanawasubiri katika sanduku la kura.

Nimemaliza

image0.jpg
 
Madiwani wanapenda vya bure sana,wanatakaga waheshimiwe heshima yenyewe hawana,ni kujitutumua tu hamna lolote,halafu wala rushwa,japo sio wote
 
Mbunge CCM, kamati ya ulinzi na usalama CCM, meya wa jiji/mwenyekiti wa manispaa CCM, Madiwani CCM, Mwenyekiti wa CCM Mkoa naye ni CCM. Sasa hiyo ni hujuma au ni utaratibu wa CCM.
 
Hii ishu mama asipoiangalia Kwa Arusha 2025 hii Ngoma inarudi CDM,wafukuzeni ila vitu vyao wapeni jamani mnabeba Maisha ya watu...na Kuna njia zingetumika ila hii ya kuchuwachukulia vitu Wamachinga Kwa nguvu big no...hapana
 
Wanabodi habari ya muda huu?

Nimekua nikifuatilia kwa karibu kinachoendelea katika Jiji la Arusha kwakweli hakina Afya sana kwa siasa za awamu ya sita. Ikimbukwe kihistoria jimbo hili ni la upinzani na CCM imetumia nguvu kubwa sana kulirudisha, lakini kinachoendelea ni kama kuchezea shilingi chooni.

Nijikite kwenye mfano mmoja wa namna mgambo wa Jiji la Arusha wanavyotumika kuumiza wananchi na biashara za wananchi. Mara nyingi maelekezo yanapotoka serikali kuu utekelezaji hufanyika kwa kukiuka misingi ya utu na haki za binadamu.

Serikali ilitoa maelekezo machinga wapangwe lakini kinachofanyika Jiji la Arusha ni unyama na ukatili mpaka unahisi labda watu wanafanya makusudi kumjengea Riais Samia mazingira magumu ya kukubalika kwa wananchi wa kawaida. Hili linasemwa kwakuwa ukiangalia miaka mitatu hapo nyuma wamachinga waliachwa huru kabisa lakini baada ya kutolewa maelekezo ya kupangwa wananyanyasika na kurudishwa kwenye umaskini. Je kwa hali ya kawaida unadhani lawama zao zinaelekezwa wapi?

Hatukatai machinga kupangwa, mbona Jiji la Dodoma wamepangwa na hakuna sintofahamu kama hii inayoendelea Arusha?

Mathalani juzi hapa kumevunjwa banda maarufu la kuuza baga/burger lililokua kwa zaidi ya miaka 13 jirani na benki ya Stanbic Arusha.

Inasikitisha sana kuona madiwani wa Jiji la Arusha kupitia kikao Cha mipangomiji na vikao vingine wamepitisha kuvunjwa kwa eneo hili kwa kupewa rushwa ya laki 2 kwa kila diwani na wakuu wa idara za Sheria na mipangomiji.

Hii ni aibu kubwa sana kwa watu wanao jiita ni wawakilishi wa wananchi kukubali wananchi wateseke kwa laki

2. Hela hizo zilipokelewa na Diwani wa kata ya lemara mhe Naboth kwenye mgahawa wa uzunguni. Diwani wa kata ya Themi mhe lobora alisikitika kuona habari hizo zimevuja wakati wao walipitisha kwa Siri kwenye vikao.

Madiwani wanakiri ni kweli muuza BAGA huyu alikuwa analipa Kodi ila tatizo atoi chakula kwa madiwani ambao malipo yao ni madogo sana. Hata diwani akienda pale anauziwa BAGA badala ya kupewa bure.

Ccm msipoangalia hawa madiwani watakimaliza hiki chama Arusha mjini.

Hivi punde mtapata habari ya namna madiwani wanavyo kura rushwa kwa watu mbalimbali kupitia kamati ya mipangomiji.

Mgambo siku ya kuvunja sehemu ya BAGA walipigwa picha na kinyozi pale jirani na wakaenda kumfanyia vurugu na kufuta picha bila kujua waliopiga ni wengi. Kama ni zoezi la halali hofu ya nini?. Na ukisikiliza viongozi wanaongea as if walikua na nia njema lakini kiuhalisia ni rushwa na uonevu tu.

Mapendekezo yangu kwa serikali, wananchi kwasasa wanajua hii ni serikali ya matajiri na wanyonge hawana nafasi hivyo muangalie siasa za Arusha hazifanani na eneo lolote nchi hii, zinahitaji akili kubwa na hesabu ndefu. Mathalani unaona hata wapinzani wamekaa kimya wanasubiri CCM mharibu ili 2025 wapate sababu za kuwanyoosha kwenye uchaguzi.

Wito kwa madiwani wa Arusha, njaa zitawaponza. Waswahili wanasema bora ndege mmoja aliye mkononi kuliko wawili walio kichakani, mnatumika sana kwa maslahi ya watu wachache. Mkumbuke hawa wananchi mnaotumika kuwanyanyasa sasa wanawasubiri katika sanduku la kura.

Nimemaliza

View attachment 2613357
Mmezoea kuishi maeneo machafu, km hamuwezi kuishi jijini tena jiji na kitalii km Arusha rudi kijijini. Bila haya unataka kuirudisha jiji la Arusha km kambi ya wakimbizi km wakati wa mwendazake? Barabara zote katikati ya jiji zilifungwa kwa kutandaziwa bidhaa, zilijengwa vibanda mpaka juu ya mitaro ya maji, mlifukuza watalii kwanza kwa kuwatisha kubadilisha jiji kuwa kambi ya wakimbizi, pili kufunga barabara za katikati mwa jiji na kujaza mauchafu mjini. Mmejengewa masoko maeneo mbalimbali ya jiji km mtaa wa Machame, pale nyuma ya Gallaxy, Mbauda, Njiro, Kilombero, Samunge, morombo na maeneo mengine mahsusi hamtaki kutumia masoko hayo mnabanana pale stand kuu na mbele za maduka ya watu ambao wanalipa kodi kubwa.

Subiri stand ipelekwe bondeni city hamtaweza hata kuingia ndani ya stand maana itakuwa na uzio. Halafu usitishie uchaguzi we na wenzako ni manyau wadogo sana, watu wengi wanataka ustaarabu. Washamba km wewe ondokeni kwenye jiji la utalii. Naipongeza serikali ishikilie msimamo wake. Mkatii sheria ya mipango miji, mmezoea uchafu km wachawi, hiyo ni NO, never again.
 
Back
Top Bottom