Kamba shingoni mwa chadema

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
443
86
Halmashauri ambazo Chama cha Democrasia na Maendeleo kimepata ridhaa ya wananchi kuziongoza, pamoja na Majimbo ya ubunge yanaweza kuwa kitanzi dhidi ya chama hicho siku za usoni hasa kama hawatakidhi mategemeo ya wananchi.

Dalili zimeishaanza kuonekana uko nyumbani Mwanza kwenye jimbo la Nyamagana, Meya wa Jiji la Mwanza (Manyerere) ametofautiana na mbunge wa Njamagana (Wenje) kwenye namna ya kutatua tatizo la Wamachinga, Meya anadai lazima Sheria zifuatwe na hivyo Machinga ni Lazima wahame kutoka maeneo fulani fulani katikati ya jiji la Mwanza. Machinga wanamlilia Wenje aliyewaahidi kwamba hawatazumbuliwa kamwe kama wakimchagua. Katika hili wenye ameishaanza kuchanganya mambo sababu anadai hajawahi kutoka ahadi ya namna hiyo (usaliti dhidi ya wananchi).

Natambua kwamba kwa jitihada za Wenje, Jiji limeridhia kutoa baadhi ya maeneo kwa Wamachinga, lakini
tatizo bado halijatatuliwa kwa maana ya kutuliza kelele za mahitaji ya Wamachinga.

Angalizo
Viongozi wa CDM katika Halmashauri zinazoongozwa na CDM wawe makini sana katika utendaji kazi zao, wasidanganywe kukimbilia kujificha nyuma ya sheria zilizowekwa sababu nyingi ziliwekwa na CCM, wawe tayari kuzibadilisha ili kukidhi matakwa ya wapiga kura wao, na wawe makini na uswaiba wa viongozi wenye Damu ya CCM, Meya na Madiwani wa CDM Mwanza angalieni sana uswaiba wenu na sheria zilizopo, Mkurugenzi wa Jiji (Kabwe) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hawa watatu wote ni CCM, na watakuwa kamba shingoni mwenu muda si mrefu.
 
Taifa-kwanza kinehe?
unaongea ni kama upo katikati kabisa ya jiji,yaani karibu kabisa na yule samaki wa vicfish
 
dawa hapo ni kwa wafuasi wa chadema kujiapiza tu.

CCM Nooooooooooooooooooooooooooooo!!!
 
Sina shida kubwa sana na wewe kutoa angalizo kwa CDM kwa kile unachohisi kinaweza kikatokea ila tu kwamba (1) KUPINDI CHA KUANZA KUFANYIA TATHMINI YAKO ndio naona kwamba bado ni mapema mno.

Pili, kwa makusudi tu umetunyima fursa ya kujua VIGEZO VYAKO unavyokusudia kutumia kufanyia tathmini husika. Kama haitoshi, bado nako haijawa wazi sana kwamba tathmini yenyewe inafanyika ikilinganishwa na nini hasa kwa sasa.

Nitafurahi sana kusoma post yako nyingine unamojitahidi walau kujibu baadhi ya maswali yangu haya.
 
Kwa Ndugu UWEZO TUNAO
Kwa taarifa tu mi sio wakwanza kutoa angalizo la namna hii, wa kwanza ni katibu wako Mkuu, DR Slaa,
alitoa angalizo la namna hii kwa Wabunge na Madiwani wa Chadema akiwa Mkoani Mbeya katika jitihada zake za kutatua Mgogoro wa kioungozi baada ya Mh. Shitambala kuachia ngazi kupisha uchunguzi wa ushiriki wake kupoteza kimbo la ubunge Mbeya Vijijini, Aliwaonya kuwa makini na Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo kimsingi ni mvibaraka wa CCM, akasisitiza kwamba wasikubali hata kuwekewa mafuta ya bure kwenye magari yao.

Slaa alikuwa akimaanisha wajiweke mbali na rushwa,Natambu SLAA alifika mpaka Mwanza kutoa alimu ya uendeshaji wa Halmashauri kwa Madiwani wa CDM Mwanza.

Hivyo angalizo langu linafanana na kuwa la pili, Katika hili usijaribu kuficha ugonjwa huu nyuma ya michakato ya kitaalamu (ambayo imejaa CCM na setikalini).

Narudia tena, na ninapaza sauti kwamba CDM wawe makini katika hili, kama mifumo ya kudhibiti hali ipo ndani ya chama, nawatakia kila la kheri katika kuitekeleza, kama haipo basi mjipime.

hizi sio dalili nzuri, japo kwa mbali, lakini Kigezo cha angalizo langu ni kwamba, Bila kujijua Viongozi wa Chadema Mwanza wametofautiana kauli adharani, sasa jamii ya machiga mwanza inajua kwamba Msimamo wa Meya hauna tofauti na msimamo wa Kabwe na Kandoro, na wanajua kwamba yeyote anayeambatana na Kabwe na Kandoro hayuko upande wa wananchi, kama haitoshi, Wenje bila kujijua baada ya kugundua kwamba Mapenzi ya Meya, Kandoro na Kabwe ndiyo yatakayotimizwa akakimbilia kujihami kwamba hakuwahi kutoa kauli ya kwamba wamachinga hawatanyanyaswa kamwe.

Wewe na mimi tunajua kwamba alitoa ahadi hii, naongezea katika swala hili Viongozi wa Chadema muda si mrefu katika halmashauri zinazoongozwa nao watakuwa kama CUF zanzibari, Angalizo ni kwamba yeyote anayeshirikiana na CCM asipokuwa makini atachafuka kuliko CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom