Tusipopaza sauti, Viongozi wa Machinga Mwanza watadhuriwa mikononi mwa Polisi

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Mnamo tarehe 08 February 2023 kulitokea vurumai katikati ya jiji la Mwanza baada ya Mgambo wa jiji kuanza kuwashambulia wachuuzi wa biashara hapo mjini.

Wamachinga898833e2191d-780x470.jpg

Vurugu hizo zilipata upinzani kutoka kwa wamachinga ambao kimsingi ni wahanga wakubwa wa kamati za ulinzi na usalama wa mikoa na wilaya zote nchini. Sambamba na kuharibiwa mitaji yao lakini majiji na miji wamekuwa wakiwasogeza nje ya maeneo waliyopangiwa awali kama vile maeneo ya wazi mijiini na hata masoko ambayo wenye fedha wamekuwa wakimilikishwa isivyo utaratibu. Maeneo ya masoko mengi hayana miundombinu rafiki na yana ugumu kufikika na wateja

Kwa mfano, hapa juzi nikifuatilia taarifa ya habari ITV nilimuona afisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa akiwaambia wachuuzi wa Mbagala kuwa wanapaswa kuhamishia shughuli zao Machinga Complex, na kutokana na kulewa madaraka hakuna anayewaza mwananchi anayeponea siku yake kwa Ths. 1,500 kwa wamachinga anawezaje kutoka Mbagala kwenda complex kufuata nyanya za Tshs 200, vitunguu vya Tsh. 100 na kibaba cha unga Tsh. 1,000 aweze kuitabiri kuiona kesho?

Turudi Mwanza
Baada ya vurumai zile, kamanda wa polisi Mwanza alitoa taarifa kwa umma kuhusu kuwashikilia wamachinga wawili ambao amewaita Ring Leaders Leader (ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya) na wanaendelea kuwahoji kuhusu vurugu zile, lakini alienda mbali zaidi kuwaonya mgambo kuwa wao walianzisha hizo vurumai na wasijione juu ya sheria na watekeleze wajibu wao kwa haki.

Ila kwenye maelezo ya polisi hakuna mahala alipouthibitishia umma kuhusu kuwashikilia ama kuwahoji wanamgambo ambao kismingi wana timiza wajibu wao kwa namna ya kikatili na kiuhalifu.


maxresdefault.jpg


DSC01127.jpg


0c5f5-mgambo-daladala-april4-2014.jpg

Nimeona nilete hoja kwa umma, kuliangalia hili na kuwaomba watetezi wa haki za binadamu kufanya juhudi za kufuatilia yanayojiri kwenye hayo mahojiano ambayo polisi wanayafanya na hao wamachinga wawili. Na usikute labda hawakuwakamata kwenye tukio bali cold blood kama ilivyo polisi. Na tukizembea kutojali maisha, uhuru na haki zao watapachikwa kesi huku wakiwa wamesainishwa maelezo ya kukiri makosa wanayoundiwa.

Polisi imelalamikiwa hata na mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan kuhusu ukatili na ubambikiziaji wa makosa kwa wstu wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali. Hivyo kusema kuwa wsnafanya kazi kwa weledi ni mapema mno.


19223198_906.jpg

MUHIMU
Polisi iwapeleke mahakamani wahusika kwa sababu muda wa kuwashikilia haupaswi kuzidi saa 48 ama iwaachie kwa dhamana huku wakiendelea na uchunguzi wao.

Jamii tukikaa kimya, tutaendelea kushuhudia ukiukwaji wa haki za raia kila siku.

Msanii.
 
Mbona unaweka picha za zamani ambazo hazihusiani na hilo tukio la machinga?
Ndio unaombea mabaya yatokee ili upate sababu ya kuanzisha uzi za lawama humu!?
Ya kwanza ni ya juzi na zingine zingatia paragraph unayosoma.

Historia ya mgambo kushambulia wachuuzi si ya leo.

Umesahau ile video ya mgambo nyamagana wakimnyang'anya mchuuzi wa kitoroli bidhaa zake?
 
Ya kwanza ni ya juzi na zingine zingatia paragraph unayosoma.

Historia ya mgambo kushambulia wachuuzi si ya leo.

Umesahau ile video ya mgambo nyamagana wakimnyang'anya mchuuzi wa kitoroli bidhaa zake?
Sio picha zote hapo zinahusika na machinga kutolewa na mgambo
 
Sio picha zote hapo zinahusika na machinga kutolewa na mgambo
Tafuta kichaka cha kujificha. Kama zinakukera ruksa uzitoe

Hao mnaowaita ring leaders muwaachie kwa dhamana acheni kuwatesa maana taarifa zinazonifikia wanachezea kipondo cha polisi ili kuwahusisha baadhi ya viongozi wa upinzani na tukio la juzi lililosababishwa na Mgambo wa jiji
 
Kwa nilichokiona hapa Mwanza na kinachoendelea, ni viongozi. Hekima haipo, na mgambo wanaotumwa kufanya hivo hawajapewa elimu. Wanasababisha vurugu. Kuna maeneo ni afadhali wateja wanaweza kufika, sasa kule Buhongwa Dampo mwishoni mwa wilaya mteja nani aende? 😁
Hilo hawalijali kwa sababu viongozi wana magari na mafuta ya umma kuwafikisha popote pale
 
Mnamo tarehe 08 February 2023 kulitokea vurumai katikati ya jiji la Mwanza baada ya Mgambo wa jiji kuanza kuwsshambulia Wachuuzi wa biashara hapo mjini...
Kuna mwana CDM alipiga SELFIE na polisi siku ya ufunguzi wa mikutano mza aliamini polisi wamebadilika.

Polisi wanatii AMRI, wakiambiwa piga, Huwa hawaulizi kwann!!!!!

Tupambanie KATIBA mpya, tusijifariji na matukio ya kutengeneza.
 
Kuna mwana CDM alipiga SELFIE na polisi siku ya ufunguzi wa mikutano mza aliamini polisi wamebadilika.

Polisi wanatii AMRI, wakiambiwa piga, Huwa hawaulizi kwann!!!!!

Tupambanie KATIBA mpya, tusijifariji na matukio ya kutengeneza.
Katiba mpya ni suluhisho
 
Watu mbona ni wapumbavu?, hivi kila kitu ni katiba mpya?,. Katiba sio mwarobaini wa kila kitu,Tujitambue,
Upumbavu wetu ni better kuliko uwezo wako wa akili.

Wewe ni nani kutuhoji na kutuchagulia tunachokitaka?

Kwako katiba mpya ni kukuwajibisha na kukubana usiibe tena mali za umma bila kuwsjibishwa ndo maana unakuja kama mtu aliyefumaniwa akaacha nguo
 
Watu mbona ni wapumbavu?, hivi kila kitu ni katiba mpya?,. Katiba sio mwarobaini wa kila kitu,Tujitambue,
Wewe ndo hujitambui,

KATIBA mpya ni solution ya Kila kitu,

Kwa mfano, kwa KATIBA hii, Pamoja na maovu yote aliyofanya Sirrrow anastahili kuwa balozi?

Chochote unachokiona kinahusiana na KATIBA kimfumo.
 
Mnamo tarehe 08 February 2023 kulitokea vurumai katikati ya jiji la Mwanza baada ya Mgambo wa jiji kuanza kuwsshambulia Wachuuzi wa biashara hapo mjini...
Hata Yesu aliwafukuza wale wachuuzi waliofanya biashara sehemu isiyo sahihi
 
Ni Kweli, Polisi wangetusaidia kuwafukuza Bungeni wabunge wasio na CHAMA chochote.

Nchi hii Ina maajabu!!
Wanachama, chama chao ni CHADEMA, ila mdume jike ya CHADEMA yanawaonea wivu kwa vile wao walikosa ubunge kwenye majombo yao. Ni dhana ya kusema kama mimi (Mbowe et al ) siko mbungeni basi kila mtu asieende bungeni ni UJINGA NA WIVU WA KIDEMU
 
Back
Top Bottom