Kamati ya Bunge yabaini Mwendokasi wanajiendesha kwa hasara

ATC
TTCL
TANESCO
Mashirika ya Umma hayana ushindani na bado yanafeli
Watu wanaiba hela hapo hakuna hasara hata iweje...kampuni haina ushindani ni wao tuu wanapataje hasara wakati bus za mikoani na ushindani mkubwa na hasara sio kubwa kama za huko kila kukicha...napinga hakuna hasara ni wizi tuu maana mali ni ya umma hakuna anaejali..
 
We tiketi hawachani wanazungusha zinarudi tena kupitisha watu wengine. Lile shirika ni taka taka. Tutegemee ili pia siku sgr ikianza kufanya kazi.

Kwani serikali au shirika lisije na mfumo wa kadi ili kuingia mwendokasi lazima uwe na card, na card inakuwa buku.. then unakua una nunua tiketi kwa mfumo wa kadi na scanning zifanye kazi maana tangu max malipo aondokw ni mfu.

Waongeze ubunifu wangekuja na vip mwendokasi kama mdau mmoja alivyosema, seat safi, kiyoyozi.

Pia watazame upya swala lao wa nauli kuna mahali sio wa kuenda na 650, wapunguze na mida ya watu kungoja bus
Mkuu Maxmalipo walipigwa zengwe kwa sababu wabongo wanapenda Sana wizi, hivyo mifumo ya kuwadhibiti hawaitaki kabisa lazima waivuruge..
 
Hasara ni kwa kutokuwa Wabunifu...

Ongezeni ,Tengeni Ma-bus kadhaa kwa huduma ya VVIP zenye Kadi Maalumu ...Mbezi Kivukoni 3000/=
Ubungo - Posta 2000/=
iwe ni Level Seat- Express
Tutayaacha Magari Nyumbani
Kumbuka hiyo ni huduma ya kijamii sio sekta binafsi
 
Moja kwamoja nishindwe kulipa bus Bm au abood 8000 niaze kulipa 50000 au 30000 kufika moro ,yaan akati pesa ya lodge inabakia nikilipa 8000
Sisi wengine wenye uwezo tutalipa kwani tunajadili huduma bora na uharaka. Mbona ndege watu wanalipa mpaka laki nne kwenda Dodoma?
 
Dala dala za kawaida za watu binafsi zinagombania wateja zipate faida. Ila mwendo kasi isiyo na mshindani inapata hasara
Ilitakiwa kwenye hizo barabara waruhusu makampuni mawili au matatu yenye sifa yafanye kazi na yalipe kodi serikalini...
 
Kauli ya kamati ya bunge imeniacha hoi na mshangao sana kwamba eti kampuni ya mwendokasi inajiendesha kwa hasara.

Hili nalipinga kwa nguvu zote, kwa jinsi wanavyojaza abiria na wateja wake ni wengi hakuna muda unakuta mwendokasi haijajaa sasa hizo kauli za kwamba wanajiendesha kwa hasara zinatoka wapi?
Huu mradi umekuwa aibu kwa taifa mwanzoni ulionekana kuwa mzuri mpaka nchi nyingine zikawa zinakuja kuutembelea.

Lakini sasa mfumo wa kidigitali ulitelekezwa wakaleta scanners za mkononi hata vituo vimeanza kuchakaa mabus viti hata vya plastic wanashindwa kurepair.

Ukiaangalia mabus ya mwendokasi nchi nyingine watu hawalundikani kama hapa wakati
Mabus mengine wamepaki.

Kuingia mwendokasi na kutoka ni vurugu kubwa sana watendaji wakubwa wamekaa tu maofisini hawarekebishi hizi changamoto nyepesi.

Lengo la kupunguza foleni au decongestion ya usafiri wa Dar limefeli sababu watu inabidi tutumie magari yetu sababu watu wanajazana kupitiliza ktk mabasi na mara nyingi yanaruka vituo eti ni express ujinga huo.

Nilikuwa Nairobi majuzi wenzetu wametuacha sana mfumo wao ambao utafunguliwa karibuni baada ya kukamilika kwa Nairobi express overpass 27 km utapunguza masaa ya foleni to dakika 120 mpaka dakika 30.

Imefika wakati GVT iachie private sector kurun hii miradi kwani inashindwa vibaya sana
 
Siyo lzm wapate faida waangalie pia kurahisisha huduma iwe affordable kwa kila mtu then serkali itoe. Ruzuku kufidia hasara zilizopo
 
Nilisikia in one or 2 months watakuwa wamekamilisha mfumo wao wa malipo wa online na kutumia kadi. Wakianza matumizi yake waache kabisa suala la kutumia cash. Wote watumie kadi au smartphone.
 
Sisi wengine wenye uwezo tutalipa kwani tunajadili huduma bora na uharaka. Mbona ndege watu wanalipa mpaka laki nne kwenda Dodoma?
Uharaka kapande ndege ww ,umeme wenyewe hauna unakenua mdomo kwa Jambo lisilowezekana ....ukiachana na gharama yanauli miundombinu ya uendeshaj unaijua mwendokasi tu haitumii umeme inajiendesha kwahasara je huko mtaweza
 
Kauli ya kamati ya bunge imeniacha hoi na mshangao sana kwamba eti kampuni ya mwendokasi inajiendesha kwa hasara.

Hili nalipinga kwa nguvu zote, kwa jinsi wanavyojaza abiria na wateja wake ni wengi hakuna muda unakuta mwendokasi haijajaa sasa hizo kauli za kwamba wanajiendesha kwa hasara zinatoka wapi?
Hujui taaluma ya usafiri ndio maana unashangaa.
Wanavyojaza sana kupitiliza uwezo wa magari ni gharama kwenye uchakavu na break down. Hii ni kutokana na mwanzo kuweka mabasi machache tena madogo ambapo kwenye mfumo wa mwendo kasi unahitajoka kuweka kumbakumba yaani yale marevu tu. Kwa ufupi tunasema kwa kingereza 'underprovosion of required capacity' kuna hawaelewi hadi useme kwa kingereza.
Jambo lingine ni nauli. Huenda haitoshelezi, lakini kubwa na ndilo naamini huenda kuna ubadhilifu mkubwa. And then repairs na maintanance wako organised kivipi. Je mafuta wananunua in bulk au wanatia mafuta kwa mtu kama ilivyokua mwanzo. Je wanastock vipuri na je wanaoutsource ufundi au wana workshorp yao.
 
Hasara ni kwa kutokuwa Wabunifu...

Ongezeni ,Tengeni Ma-bus kadhaa kwa huduma ya VVIP zenye Kadi Maalumu ...Mbezi Kivukoni 3000/=
Ubungo - Posta 2000/=
Level Seat
Tutayaacha Magari Nyumbani
Pumbavu vvip ya nini,hio niia tulikuwa tunapita kwa 400 tu leo nauli 600 wanashindwa nini?
 
Back
Top Bottom