Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha

Sahau habari ya uchaguzi, Hawa watakwenda mahakamani kupinga kufukuzwa, na kesi haitaisha hadi 2015.

Mie nashangaa, huyu Malla ndie nguzo ya Chadema Arusha mjini na hata mchakato wa uchaguzi uliopita alikuwa agombee yeye kabla ya cdm M/makuu kumleta Lema. tunangojea kuona reaction ya wana-Arusha juu ya maamuzi haya, lakini naona sinema ndio kwanza imeanza!

Hawa madiwani walitaka kujifanya maarufu kuliko chama na walishinda udiwani simply because wako CDM, Bayo ameshindwa mara ngapi udiwani ktk hatua za awali CCM? Ni wazi this time watu walikiamini chama wakawapa watu kura walioaminiwa na chama na tuko tayari kumpa kura zetu candidate mwingine atakayeaminiwa na watu. Hatukuandamana na kupigwa mabomu na baadhi ya ndugu zetu kufariki na kupoteza viiungo ili waje wagawane madaraka kidandara bali uchaguzi uliopotoshwa kwa kukiuka kanuni urudiwe na si vinginevyo heko chadema pamoko saaana

Sahau habari ya uchaguzi, Hawa watakwenda mahakamani kupinga kufukuzwa, na kesi haitaisha hadi 2015.

Mie nashangaa, huyu Malla ndie nguzo ya Chadema Arusha mjini na hata mchakato wa uchaguzi uliopita alikuwa agombee yeye kabla ya cdm M/makuu kumleta Lema. tunangojea kuona reaction ya wana-Arusha juu ya maamuzi haya, lakini naona sinema ndio kwanza imeanza!
Mkuu wangu ukisha fukuzwa uanachama hakuna mahakama inayoweza kukutetea kuhusiana na uanachama. Maadam sheria ya uchaguzi inakusimamisha wewe kama kiongozi kupitia CDM, chama kikikutema basi umepoteza hadi Udiwani..

Halafu walichotakiwa kujiengua ni uongozi wa jiji ambao unasemekana ni batili, hapa pengine ndipo wangeweza kuhusisha mahakama lakini wao wameng'ang'ania viti vya jiji wakasahau kwamba viti hivyo vimetokana na Udiwani wao. Kwani kama wangekubali kujiengua ili uchaguzi mpya ufanyike kungepoteza kitu gani? kulikuwepo na kasoro zipi ambazo wao wameziona!.. Binafsi sikuona sababu ya kukataa kujiuzulu kwao isipokuwa kama ilikuwa na maslahi binafsi, wakihofia hizo nafasi na viti walivyopewa ktk baraza la jiji wakihofia watu wengine watachaguliwa dhidi yao.

Labda nikwambie tu kwamba Uongozi wa diwani sio ajira kama ya msimaizi wa shirika au kiwanda..Uongozi wa nchi, mkoa au wilaya unahitaji nidhamu ya juu sana kwa chama unachokiwakilisha..Huyaoni haya yakifanyika CCM hata siku moja kwa sababu viongozi wake wana nidhamu ya chama, kanuni zinaheshimika na wanajua kutetea chama mbele ya uwezo wao binafsi..Anayepingana na maamuzi ya CC hujiengua mwenyewe mapema na ndivyo ilivyo ktk serikali zote.
Wawakilishi wote wa wananchi iwe Mabalozi, mawaziri madiwani hata iwe nchi za nje hawapindui kwa serikali wanazozitumikia..They never take side against their Party or leadership..Na siku wakipindua basi hujiengua mapema na kusimama upande wa pili lakini huwezi kupinga maamuzi ya chama chako tena kutoka kamati kuu kisha bado ukakazania kutambuliwa.

Kusema kweli imesikitisha sana kuona hawa madiwani wamekuwa na kiburi kiasi hicho, hadi kutokea maamuzi kama haya... Nitasema tena na tena kwamba Kiongozi bora has to be a visionary..Kiongozi unatakiwa kuwa mwerevu, mwenye kutazama mbali kwa kila maamuzi na matendo yako kwa sababu kila jambo lina uhusiano na jambo jingine, kiongozi mzuri hana budi kuangalia tatizo analoshughulikia leo linaweza vipi kuzua matatizo mengine na upana wa athari zake ktk jamii..Kupanga ni kuchagua na mara zote kama hukuweza kuona mbele basi tambua utakutana na red lights all the way..Haya sasa wamepoteza viti vya jiji na kisha wanapoteza Udiwani na wasiweze kurudi tena ktk uongozi ktk ngazi yoyote.. Ndio imetoka!

Hawa ndugu zetu kama viongozi wameshindwa kusoma alama za nyakati, maamuzi yao leo yamesababisha madhara makubwa kwa chama na wananchi wa Arusha kwa visingizio ambavyo vingeweza kuepukwa kirahisi sana, and for that hawakuwa viongozi to begin with.. Mtazameni Obama, ni rais ambaye angeweza kabisa kusema kwa kiburi kama cha hawa jamaa lakini mwenyewe kawa mdogo kutokana na kanuni zilizowekwa kwa sababu hakuna kitu kinapita bila kukubaliwa na wengi...

I support 100% out... Walijifanya wapo zaidi ya chama. Thanx kk bado shibuda na zitto

Uamuzi mzuri uliofanywa na kamati kuu hawa madiwani wangeachwa wangekivuruga chama siku za usoni.Afadhali chama kibaki na madiwani wachache wanaojali maslahi ya wananchi kuliko hawa wanaotumiwa na CCM a.k.a magamba. Big up kamati kuu bado Shibuda.

• Thanks
Reactions: FJM
Hayo ndio maamuzi magumu sasa, nidhamu kwanza, maana chama lazima kiwe na sauti moja, viongozi bora husema tumefanya, na wabinafsi hutumia nimefanya

Masikini CDM sifa zimewaponza wanaharibu ngome yao! Huo ndio mwanzo wa mwisho wa CHADEMA , just wait and see!

Hatua hiyo ndio wana arusha tuliitegemea wangefanya vinginevyo tungewashangaa tuliandamana kudai haki wala si madaraka na vyeo kama hao madiwani. Kwa arusha sehemu ka kimandolu, elerai, kaloleni hata jiwe likisimamishwa kwa tiketi ya CDM linashinda, sisi tunaamini umakini wa chama na tunajua chama kitateua watu makini zaidi. Kina Bayo walijiona ni maarufu kuliko chama na hii isiishie hapo yeyote akizingua tupa kule awe Lema, Slaa, Mbowe, Zitto, Lissu au yeyote yule tunachotaka ni sheria na taratibu zifuatwe tusiwe wanafiki kama magamba

Tunapoiambia serikali ichukue maamuzi magumu, ni kama haya. bado shibuda..hata zitto akisumbua fukuza..tuna vijana wazuri kushinda yeye kibao tu. Hongerea CHADEMA, hongereni makamanda wote.

• Thanks
Reactions: FJM
Shibuda aliomba radhi kwani unafikili hayajui haya? Hawa jamaa wa arusha wamelewa sifa mapema
I support 100% out... Walijifanya wapo zaidi ya chama. Thanx kk bado shibuda na zitto

Safi sana CHADEMA safisha uchafu wote, hao madiwani hawana nidhamu kabisa. Potelea mbali bora JESHI DOGO LENYE NIDHAMU KULIKO JESHI KUBWA LISILO NA NIDHAMU.... Mapambano bado yanaendelea.

Naunga hoja mkono.

What great difference between CDM and CCM! CCM mafisadi wanabembelezwa kuondoka lakini CDM wanatimuliwa bila ya kuwaonea haya. Kuna maamuzi magumu kuliko haya? Big Up CDM!!

With due respect, I beg to differ! Leo hii wapiganaji wetu wamekuwa mafisadi? Kama kila anyefanya utovu wa nidhamu kwa uongozi wa chama anakuwa fisadi wangapi watabakia chamani, au ndio tunarudishwa kwenye sera za udikteta enzi za Mwalimu?

Huu ni mojawao ya maamuzi ambayo kama chama kilihitaji kuchukua muda mrefu huko nyuma. Baada ya uongozi wa maonyo na kubembelezana chama lazima kiwe na uwezo kuchukua hatua. Siyo chama tu bali uongozi wowote uwe wa kazini au mahali popote huwezi kuongoza kwa maonyo na kuwabembeleza watu kuna wakati lazima uwe tayari kukata shauri. Katika kufanya uamuzi huu maana yake ni kuwa:

a. Hakuna mtu ambaye ni indispensable ndani ya chama hata kama uwepo wake umekipa chama sifa au kura kiasi fulani - hivyo unatoa notisi kwa viongozi wote ndani ya chama kuwa kuna wakati wa kubishana, kuzungumza na kujadiliana lakini pia kunawakati wa kukata malumbano.

b. Chadema haiogopi kulipa gharama. Kwa mfano, ukija uchaguzi na CDM ikapoteza viti vyote vitano mtu anaweza akafikiria ni loss ya chadema lakini kiukweli kabisa siyo loss kwao kwani kwa kuamua kuwatimua walishaamua kula loss ya kura, ruzuku na nafasi.

CDM imetumia muda mwingi tangu tukio la "muafaka" lilipofanyika ili kuwarudisha hao madiwani kwenye mstari. Muda wote tangu tukio hili lianze sikulitolea kwa upande wangu kauli yoyote ile. Sababu binafsi nilitaka nione CDM ina uwezo gani wa kufika mahali kuchukua uamuzi ambao ulikuwa wazi toka mwanzo. CDM wameonesha kuwa demokrasia siyo kuacha watu walumbane tu bali pia kuagana na wale ambao wanatishia demokrasia yenyewe. Kwa hili wanakuwa trail blazers katika mfumo huu wa vyama vingi.

Naamini katika hayo mawili CDM imewapa wananchi wa Arusha na sehemu nyingine TZ kuwa kuna mambo hayawezi kuvumuliwa hasa kama kuna lengo la kuja kushika madaraka. Hamuwezi kwenda vitani huku baadhi yenu mnageuza bunduki zenu kwa wapiganaji wenzenu. Katika mazingira hayo wanajeshi wa namna hiyo wanaondolewa jeshini, hawabembelezwi kwani ni hatari kwa matokeo ya vita.

Natumaini vyama vingine - hasa CCM vitakuwa na ujasiri wa hatimaye kuwa tayari kulipa gharama yoyote ili kurejesha imani, nidhamu na uongozi. Kama kuzungumza CCM wameshazungumza sana, kama ni kuitishana vikao wameitishana vingi. Natumaini kikao kijacho cha CCM kitakuwa cha kukata shauri. Wasipofanya hivyo watajionesha kuwa ni chama dhaifu kuliko tunavyofikiria.

Siafiki sana hawa jamaa kufukuzwa.. Nadhani kuna umuhimu wa kamati kuu ya chadema kwenda arusha na kumaliza hii shida..

Acheni makelele, kutimua madiwani sio uamuzi mgumu hata kidogo, Mbona ZITTO muna mgwaya kila siku? Kumbukeni madiwani wapo kwa maslahi ya wananchi sio ya chama, magwanda hamna tofauti na magamba mnaweka chama mbele nchi nyuma. Hili litawatafuna sana hakuna chakushabikia hapo..........

Bravo Cdm!bravo!that is what we wanted! hata wakaeneze sumu lkn chama kitasimama imara

Siafiki sana hawa jamaa kufukuzwa.. Nadhani kuna umuhimu wa kamati kuu ya chadema kwenda arusha na kumaliza hii shida..
How about this.."Nothing in all the world is more dangerous than sincere ignorance and conscientious stupidity."

Huu ni mojawao ya maamuzi ambayo kama chama kilihitaji kuchukua muda mrefu huko nyuma. Baada ya uongozi wa maonyo na kubembelezana chama lazima kiwe na uwezo kuchukua hatua. Siyo chama tu bali uongozi wowote uwe wa kazini au mahali popote huwezi kuongoza kwa maonyo na kuwabembeleza watu kuna wakati lazima uwe tayari kukata shauri. Katika kufanya uamuzi huu maana yake ni kuwa:

a. Hakuna mtu ambaye ni indispensable ndani ya chama hata kama uwepo wake umekipa chama sifa au kura kiasi fulani - hivyo unatoa notisi kwa viongozi wote ndani ya chama kuwa kuna wakati wa kubishana, kuzungumza na kujadiliana lakini pia kunawakati wa kukata malumbano.

b. Chadema haiogopi kulipa gharama. Kwa mfano, ukija uchaguzi na CDM ikapoteza viti vyote vitano mtu anaweza akafikiria ni loss ya chadema lakini kiukweli kabisa siyo loss kwao kwani kwa kuamua kuwatimua walishaamua kula loss ya kura, ruzuku na nafasi.

CDM imetumia muda mwingi tangu tukio la "muafaka" lilipofanyika ili kuwarudisha hao madiwani kwenye mstari. Muda wote tangu tukio hili lianze sikulitolea kwa upande wangu kauli yoyote ile. Sababu binafsi nilitaka nione CDM ina uwezo gani wa kufika mahali kuchukua uamuzi ambao ulikuwa wazi toka mwanzo. CDM wameonesha kuwa demokrasia siyo kuacha watu walumbane tu bali pia kuagana na wale ambao wanatishia demokrasia yenyewe. Kwa hili wanakuwa trail blazers katika mfumo huu wa vyama vingi.

Naamini katika hayo mawili CDM imewapa wananchi wa Arusha na sehemu nyingine TZ kuwa kuna mambo hayawezi kuvumuliwa hasa kama kuna lengo la kuja kushika madaraka. Hamuwezi kwenda vitani huku baadhi yenu mnageuza bunduki zenu kwa wapiganaji wenzenu. Katika mazingira hayo wanajeshi wa namna hiyo wanaondolewa jeshini, hawabembelezwi kwani ni hatari kwa matokeo ya vita.

Natumaini vyama vingine - hasa CCM vitakuwa na ujasiri wa hatimaye kuwa tayari kulipa gharama yoyote ili kurejesha imani, nidhamu na uongozi. Kama kuzungumza CCM wameshazungumza sana, kama ni kuitishana vikao wameitishana vingi. Natumaini kikao kijacho cha CCM kitakuwa cha kukata shauri. Wasipofanya hivyo watajionesha kuwa ni chama dhaifu kuliko tunavyofikiria.

Maamuzi kama haya huchukuliwa na administrators mahala pa kazi au kwenye ofisi za umma, kwa kifupi ni maamuzi ya kiserikali zaidi kuliko chama cha siasa.

Back
Top Bottom