Katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita kulikuwa na tetesi kuwa baadhi ya wagombea wa ubunge walipokea fedha ila kuachia ushindi kwa kulegeza msimamo na hivyo baadhi ya majimbo kuchukuliwa na magamba na kwa kuliona hilo chadema waliona siyo vyema kufanya kazi kwa kushutumiana
baadhi ya maeneo waliunda timu kabisa kama walivyofanya mkoani mbeya kwa Shitambala na kujaribu kuwasafisha wagombea wake na kuwapa moyo wasonge mbele na kuendelea kukijenga chama lakini ukweli ulibaki pale pale kuwa kuna baadhi ya wagombea hugombea kwa masilahi yao binafsi na siyo masilahi ya Chama na ndicho kilichotokea na baadhi yao kurudi ccm na kuacha kashfa nyingi baada ya kupokea ujira wao na kuwafanya wapenda Demokrasia wengi wapoteze imani na wanasiasa.
Tukiachana na hilo nataka tuangalie namna ya mgogoro wa Arusha ulivyoshughulikiwa kwanza yalifanyika maamuzi ya awali na kutoa picha halisi hali ingekuwaje kama mambo yangekwenda vile yalivyokuwa yanapelekwa nimeshuhudia jinsi Chadema kilivyokuwa kinajitahidi kushughulikia suala hilo kwa umakini na uvumilivu wa hali ya juu kwa kuepusha mgawanyiko kwenye chama na hata kutoa fursa zaidi ya mara tatu kwa wasaliti hao kujirekebisha ili kukinusuru chama wakati wananchi tayari tulishakerwa na wao lakini Madiwani hao wasaliti hawakusikia na kuendelea hata na mchezo mchafu wa kupiga kampeni haramu ndani ya chama kwa kuwatumia badhi ya viongozi wa Chadema na ccm kwa wakati mmoja huku wasaliti hao waliokuwa wanadai wanataka kuwatumikia wananchi waliowachagua huku wakisahau kuwa umaarufu na ushindi wao ulipatikana pale walipoingia ndani ya Chadema baada ya wananchi kuchoka na ccm na ndiyo maana wananchi wa Arusha wana msemo unaosema UKIWEKA TOTH PICK KAMA MGOMBEA WA CDM. NA CCM WAWEKE MTU BORA KUCHAGUA TOTH PICK KULIKO MGOMBEA MTU WA CCM MAANA KUICHAGUA CCM NI KUCHAGUA MAAFA YA KUDUMU. Hivyo basi wasaliti walioonekana chadema hawakuwa watu bora sana kuliko wagombea wengine bali walipita kutokana quality ya chama na siyo quality ya mgombea na ndiyo maana wananchi wa Arusha tumekuwa tukifuatilia sana sakata hili kwa karibu kuona viongozi watachukua maamuzi gani baada ya kutoa fursa za kutosha kwa wasaliti hawa na nimeshukuru kwa wale ambao wamegundua makosa yao kwa kukoseshwa au kurubniwa na kurudi kwenye mstari na ninapenda kutoa angalizo hapa naomba kwa viongozi wa chadema waendelee kuwaangalia kwa karibu sana kama kweli wamejirekebisha au wanalinda udiwani wao na kesho wakuja kutugeuka tena na ninaishukuru kamati kuu wamefanya kile ambacho wengi tulikitaka na tulikuwa tayari kurudia kupiga kura hata kama tutalazimika kupiga kura mara 200 tuko tayari ili kuungana na msimamo wa viongozi wetu Mbunge Godbless Lema na viongozi kitaifa ambao walidhalilishwa, kupigwa na kuumizwa na baadhi ya wananchi kupoteza maisha yao na wengine kupata ulemavu wa kudumu na bado haikutosha wakafunguliwa kesi mahakamani kwa ajili tu ya kutetea kile kinachoaminika kuwa ni haki lakini wasaliti wachache wanakuja kuuza haki kwa bei nafuu kwa madai ya kutaka kuwajibika kwa wananchi waliowachagua!
Na kwa taarifa zilizopo kutoka kwa hawa wasaliti wenyewe wanajiandaa kuita waandishi wa habari ili kujinadi kuwa wamejiuzulu kwa masilahi ya chama na kulinda mshikamano kitu ambacho siyo kweli tunajua kuwa wamefukuzwa na chama ma sisi mitaani tutaendelea kuwaona ninyi ni wasaliti wa demokrasia ya kweli na tunawataka sasa muende mkamtumikie yule aliyewapa ile ishu na kutuletea vumbi na moshi kwenye chama.
Hongereni kamati kuu ya Chadema kwa kufanya maamuzi magumu na sahihi kwa masilahi ya Taifa na kurudisha imani ambayo ilianza kutoweka miongoni mwetu tunawatakia uchaguzi mwema wa marudio na wananchi wa Arusha tutawaonyesha hili kwa vitendo kwa kuwaunga mkono katika uchaguzi mdogo natumaini tutashinda kuliko hata awali na kurudisha viti vyote bila wasiwasi.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki Arusha
Mungu ibariki Tanzania