Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha

Kamati kuu Chadema leo tarehe 7/8/2011 majira ya saa saba usiku imefikia maamuzi magumu baada ya kuwafuta uanachama madiwani wasaliti watano ambao ni kama ifuatvyo , John Bayo kata ya Elirai , Estomih Malah ( Kimandolu ) , Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed wa viti maalumu. Hawa ni wale baadhi ya madiwani walioingia kihuni bila kufuata utaratibu wa Chama .

Kutokana na uamuzi huu Tume ya Uchaguzi italazimika kupanga tarehe ya uchaguzi mdogo.

what a bold move by chadema!

hii ni culture mpya kwenye siasa zetu....haswa ikizingatiwa kuwa kwenye siasa (za uchwara) QUANTITY ni zaidi kuliko QUALITY.

• Thanks
Reactions: LAT
big up cdm!! Huu ndiyo uongozi imara na makini!! Lazima uwe tayari kuchukua maamuzi magumu lkn yenye faida kwa chama na nchi!! Ukiogopa kufanya hivyo chama na nchi vitakuwa lege lege. Kikwete anaogopa kuchukuwa maamuzi mazito matokeo yake chama na nchi vimemshinda!! Amebakia kutishia tu kwa kutoa siku 90 tu bila kufanya lolote.

Kuta wakati alisema ana majina ya wauza madawa ya kulevya na anawapa muda waache, lkn mpaka sasa hajawafanya chochote!! Huu siyo uongozi wenye tija kwa chama.

Nyerere alikuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi mazito ndiyo maana chama na nchi vilikuwa imara.

Hongera sana chadema. Potelea mbali tukipoteza majimbo yale

hii inaonyesha ndani ya chadema kuna watu wenye uroho wa pesa na hawana uchungu na nchi hii..,hivyo hata kama chadema itapewa nchi 2015 yatazuka yaleyale tu ya kashfa nyingi..,

achana na hoja za rejareja.ndo maana wamefukuzwa ili huo utumbo walioufanya ucrudiwe!

chadema ni chama dume kwa kweli.
Ingekuwa CCM wangeanza kupeana siku 90 au kuogopa kupoteza nafasi hizo za udiwani.

ili uwe msafi mbele ya jamii unayohitaji waamini kuwa wewe ni msafi basi ni lazima ujisafishe.

Na ni lazima uchukue maamuzi magumu kama haya bila kujali kama uchaguzi ukirudiwa utashinda tena au la

Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, kuna wakati wa kupanda na wakati wa kushuka. Hawa madiwani walibweteka sana, wakajiona wao ni bora kuliko chama. Wakatafute chama kinachowafaa pumbav zao

ndio chama kinaelekea kaburini hivyo, vyama vyote hufa kwa tabia hii ya kufukuzana
Hayo ni mawazo yako pia...tulize sisi hapa arusha..nilipoona habari hii nikasema ngoja niende maeneo ya stand kuu nikipitia na soko kuu..ee bwanaee watu wa arusha wana msimamo..kule stand wanasema kama cdm wangekubali huo mwafaka wakati watu walikufa, walikuwa wanawasubiria kina Dr Slaa wakija kwenye kesi yao wao(wananchi) ndio wangewahukumu..wanasema huo mwafaka ni batili kwani Pesa ya ccm imetumika sana..hapa sokoni nilimkuta mama mmoja akiwa na skafu ya cdm shingoni mwake,..anasema ''hii ni alama ya ushindi'' jinsi akikumbuka mtoto wake alivyojeruhiwa na risasi mpaka sasa ni kilema,..nilishindwa kumpiga picha akihofia usalama wake...wakuu wananchi wana uchungu sana na nchi yao hapa arusha.......nde maeneo ya stand kuu nikipitia na soko kuu..ee bwanaee watu wa arusha wana msimamo..kule stand wanasema kama cdm wangekubali huo mwafaka wakati watu walikufa, walikuwa wanawasubiria kina Dr Slaa wakija kwenye kesi yao wao(wananchi) ndio wangewahukumu..wanasema huo mwafaka ni batili kwani Pesa ya ccm imetumika sana..hapa sokoni nilimkuta mama mmoja akiwa na skafu ya cdm shingoni mwake,..anasema ''hii ni alama ya ushindi'' jinsi akikumbuka mtoto wake alivyojeruhiwa na risasi mpaka sasa ni kilema,..nilishindwa kumpiga picha akihofia usalama wake...wakuu wananchi wana uchungu sana na nchi yao hapa arusha.......

Sahau habari ya uchaguzi, Hawa watakwenda mahakamani kupinga kufukuzwa, na kesi haitaisha hadi 2015.

Mie nashangaa, huyu Malla ndie nguzo ya Chadema Arusha mjini na hata mchakato wa uchaguzi uliopita alikuwa agombee yeye kabla ya cdm M/makuu kumleta Lema. tunangojea kuona reaction ya wana-Arusha juu ya maamuzi haya, lakini naona sinema ndio kwanza imeanza!

sheria gani watakayotumia? Wao wamevuliwa uanachama,hawajavuliwa udiwani. Lakini kwa upande mngine sheria inahitaji uwe na chama ndo ucmame,hivo hawana budi kuondoka!..

ndio chama kinaelekea kaburini hivyo, vyama vyote hufa kwa tabia hii ya kufukuzana

wasi wasi wangu ni kwamba unatumia ubongo wa kuazima tena wa kichaa. Ukweli unaujua hutaki kuusema. Be transparent Mkuu, saying something just to please the person's mind does'nt help you.

Swali ni jamaa wataamua kuingia CCM ili wajaribu kugombea tena?

@Mwanakijiji, hao 'jamaa' waingie CCM, waigie CCJ, waingie TLP, waingie kokote wanakota but not CHADEMA. Watanzania tumechoka na viongozi VISHOKA. Hatutaki tena kusikia mtu anatumbia 'kijiko' kumbe alimaanisha 'lebeshi'.

CCM wawachukue - for free, they behave like them! Na ccm wajifunze kuwa Jairo Foundation will not be tolerated in CHADEMA.

Huu ndio mfano wa maamuzi mangu, nadhani kwa historia yalitoke miaka 60, kuna wabunge, kama sikosei mzee masha alitumuliwa ndani tanu na wenzake, msimamo wao ulikuwa wabunge wahihoji serikari, wakatolewa, likaja la jumbe. Sasa ccm ya leo inatoa siku mjifikilie!

leo mwendo ni nyamachoma na ndovu baridi kusherehekea masnitch kutoka kwenye chama chetu.
Kimsingi tumewavumilia sana. Tunahitaji kuwa na wanachama wanaoheshimu mising ya chama na siyo wasaliti kwa pesa mbuzi ya magamba.

Chama chetu kitazidi kujijenga na ndicho kitakachoiua magamba

Uamuzi wa kuwafukuza madiwani hao unaungwa mkono na walio wengi.

Ngoja niende na maeneo ya disemba kule garage kijiwe kikuu cha Lema nione na wao wana react vipi na hii habari leo ni full ukweli hakuna porojo hapa...subirieni ukweli wakuu..

Ni maamuzi ya kishujaa, nayaunga mkono. Nisingependelea chadema kuwa chama lege lege, hivyo kimetuhakikishia sisi raia kuwa kipo imara na tunaahidi kushikamana na chama hatua kwa hatua.

Peoples power!!

Back
Top Bottom