Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

sie wengine internet cafe ilikuwa ni centre ya kucjeza games za mortal combat,need for speed na mpira tu
wanaopenda kucheza games utawajua tu, yani wanaminya keyboard kwa nguvu sana hata wakiwa computer ya umbali mita 5 unaskia tu ka ka ka ka ka
 
Kulikuwa na Dar talk(something km hivi),kabla ya facebook kulikuwa na Skype..kulikuwa na BBM MESSENGER ilikuwa kama WhatsApp vile,thanks kwa mchina kuleta hizi cmu maana ilikuwa ukidownlpad hata media yenye mb 10 tu inakuandikia 36 years to complete!!πŸ˜‚
BBM MESSENGER au sio. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mimi nilikuwa nalipia saa moja kwaajili ya kuangalia xxx tu
wazee wa pilau utawajua tu, walikuwa wanapenda kujibanza computer za mwisho mwisho ukutani ,

internet ikiwa ina vipazia ama kuna miundombinu ta privacy hapo mwenye cafe kafanya maksudi kurahisisha πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
MUHIMU: UZI HUU SIO WA KUKUMBUSHANA COMPUTER GAMES

View attachment 2648381


Pengine unaweza kuona ni rahisi kwa sasa upo na smartphone au laptop yako unaingia net, Hali haikuwa hivyo kwa miaka ya nyuma kabla ya 2010s, Kipindi hicho tulikuwa tunaenda internet cafes kupata huduma ya internet, ni watu wachache sana hasa vigogo ndio walikuwa na internet majumbani.

Miaka ya 2007 angalau tulianza kutumia internet kwenye simui za Nokia batani (tovuti maarufu ilikuwa waptrick) lakini hii internet ilikuwa ni kituko ,bado tulilazimika kwenda internet cafes kupata mambo kamili,

2010 Modems za kutumia kwenye laptops na simu za kisasa zaidi zenye uwezo mkubwa wa kuperuzi internet zilipoanza kujaa sokoni ndipo wengi tukaacha kwenda internet cafe na hii ikapelekea cafes nyingi kufungwa ama kugeuzwa kuwa stationery.

Haya sasa tukumbushane hali ilivyokuwa kwenye internet cafes

Binafsi nilianza kwenda Internet cafe 2002.

Tulikuwa tunatumia computer za meza zenye visogo πŸ˜‚ .

Mitanado maarufu kwa hapa bongo ilikuwa ni Marafiki.com na DarHotwire, baadae zikaja Jamboforums (kwa sasa jamiiforums), Hi5, Bongo 5,

tulikuwa tunalipia kwa muda kuanzia nusu saa, Ukilipia wanawasha program ya kuhesabu muda, iliitwa time watcher muda ukiisha inaloki computer, Wajanja walikuja na mbinu za kuruka hiki kiunzi πŸ˜‚

Speed ilikuwa chini sana, Yani kufungua ukurasa wenye picha unaweza subiri dakika nzima.

Kuwa na email ilikuwa ndio ujanja wa enzi hizo, Tulichat kwa kutumia emaail pamoja na kutumiana barua. email maaarufu ilikuwa hotmail, yahoo na msn.

Enzi hizo bado tunatumia floppy disk kuhifadhi mafaili, ni kipindi ambacho bado cd na flash hazijawa common.
Kicheko.com pale moshi nimewaibia sana muda wao nilikua na kidemu kinafanya kazi pale nadhani kilikua na undugu na mwenye ofisi kikanipaga pin za muda nilikua nakaa kwenye kona mwisho najipakulia madude tu.
 
Kicheko.com pale moshi nimewaibia sana muda wao nilikua na kidemu kinafanya kazi pale nadhani kilikua na undugu na mwenye ofisi kikanipaga pin za muda nilikua nakaa kwenye kona mwisho najipakulia madude tu.
Tulisechi huko yahoo namna ya kuiruka. ilikuwa unaminya kwenye keyboard ctrl, alt na delete kwa mpigo, unaitoa,

mhudumu akija unairudisha fasta inaendelea ilipoishia, kuna mwamba mchezo ulimkolea wakamtegea mtego akadakwa ilibidi alipe kila kilichomo mfukoni na wakampiga marufuku kurudi
 
wanaopenda kucheza games utawajua tu, yani wanaminya keyboard kwa nguvu sana hata wakiwa computer ya umbali mita 5 unaskia tu ka ka ka ka ka
Wakati zile keys zikishafika mwisho haijalishi unatumia nguvu gani sema ndio hivyo mizuka ya game πŸ˜ƒ
 
Dah 2002 nikiwa bwana mdogo, kuna mbunge mmoja nilimfunza ku www.manchester United.com na www.arsenal.com. Basi alikuwa anasearch,mkibishana hata kuhuhu miji au Nchi anakwambia nta www tu we nitajie.
Si mchezo, enzi hizo ilibidi uwe uweziweka kichwani tovuti / website www.-----.com, watu walikuwa na vidaftari kabisa maalum .

Siku hizi ukiingia google tu ukiandika unachotaka zinakuja website kibao unachagua ipi uingie
 
HAPA KWETU TEGETA, I C ZILIKUWA CHACHE SANA. PALE TGT PK BAR, NJIA PANDA KWA MASISTA, KIBAONI NA WAZO MAGHOROFANI. NILIJIFUNZA MAMBO MENGI YA DUNIANI KUPITIA HIZO I C. NILISOMA SANA BBC, VOA NA DW. SIKUWA MPNZ SANA WA XXX. NILICHAT NA MARAFIKI WENGI NA HASWA WA NJE YA NCHI. HAPO MATUMIZI YA CM ZA MKONONI HAYAJASHAMIRI SANA. MWALIMU WANGU WA INTERNET BAADAE AKAWA MY WANGU. KWA7BU NILIKUWA NINA VIJISENT, NALIPIA MASAA MAWILI, HALAFU NATUMIA SAA MOJA, NA YEYE NAMUACHIA SAA MOJA. HOTMAIL AU YAHOO NDIYO ILIKUWA HABARI YA MJINI. UKIWA NA E-MAIL, HUKO SKONGA MADUU KAMA WOTE. KTK MAGAZETI KUNA UKURASA WA KUTAFUTA MARAFIKI, UNACHUKUA E-MAIL, UNACHAT NAYE THROUGH INTERNET. KINACHOENDELEA HAPO MTAJUA WENYEWE. KTKT YA KUNDI LA WATU WENGI HAWANA NA HAWAJUI MATUMIZI YA E-MAIL, WEWE MWNY E-MAIL UNAJIONA MTU WA PEKEE SANA.
Hapo pk bar ndio nlifungulia email yangu na fb account....2005 hiyo
 
2007
Nilikuwa DESKTOP
hp COMPAQ pentium 3 speed 900mhz
Ram 512sdr HDD 20gb(IDE) ikiwa na DVDrom CDwriter
Then mwaka 2008 nikaupgrade kwenda 80gb IDE
dah ! Unajua 80gb nilinunua sh ngapi nilinunua 120000/= aisee kwakuwa nilikuwa nishaanza michezo ya torrent MOVIE sikuwa na namna nikalipia tu mana storage ilikuwa haitoshi
Nlimiliki mashine hii pia mwaka 2006 nikiwa chuo mlimani
 
Naona wahenga mnakumbushana zama zenu za MB ngumu kuisha.
Nawadeiz ukikanyaga enter narudi Jumbe umetumia 75% ya kifurushi chako.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Yaan niliendaga internet cafe kusoma lyrics za NSYNC this i promise u, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nikamwambia mhudumu aniprintie shaa nikarudi home na karatasi ya nyimbo mkononiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom