Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Nigeria kuna makabila 371 ila kuna makabila matatu maarufu
1. Hausa = Hili ndio kabila lenye watu wengi zaidi Nigeria na Afrika, Hawa wapo nyuma sana mambo ya elimu na hata huko kwao hakuna sana maendeleo miji imejaa omba omba lakini ndio walioshikilia power ya nchi kwenye siasa, Jeshini wamejazana wao na kazi za serikali nyingi wamejaa wao. Tatizo la hili kabila ni ubinafsi mtu akipata ni yeye na ukoo wake. Wengi ni wasilamu na maeneo yao mengi huongozwa kwa mifumo ya kiarabu, machifu wa mikoa yao hujulikana kama Emir. picha ya mfano ipo chini
Nigeria imewahi kufanyiwa mapinduzi mara kadhaa, mara nyingi wahusika wakiwa kabila hili ikitokea hawajampenda rais hasa asipotokea kwao japo mara ya mwisho kufanyika mapinduzi ni miaka ya 90s.
Wananufaika sana kushika power ya nchi sababu hata kama hawana elimu hizi tenda nono huwa wanapeana wao, vyeo vinono wanapeana wao, visima vingi vya mafuta ambavyo mikoa ya mbali isio yao wanamiliki wao, Ndiko anakotokea Tajiri Aliko Dangote.
Haya ni majibu ya chat-gpt kwa swali nililoiuliza "sehemu inayoongoza umaskini Nigeria"
Kaskazini Magharibi na kaskazini mashariki zimejaa wahausa
2. Yoruba - Hawa wapo Kusini Magharibi, ndio wasomi zaidi kwenye taifa hilo, na kwa sasa hata raisi anatokea huko, wengi wanategemea ajira kuendesha maisha yao, elimu kwao ndio kipaumbele japo kuna tatizo kubwa sana la ajira huko Nigeria, Pia wasanii wengi kama kina Davido na wanamichezo wengi hutokea huko. ila udhaifu wao nao hawana umoja sana.
3. Igbo - Hawa licha ya kwamba kwao ni Nigeria ya Mashariki kusini, wametapakaa sehemu nyingi Nigeria hasa kwenye majiji yenye fursa za biashara kama Lagos na Abuja, Hawa ndio wengi tunawaona kwenye muvi, maisha yale ya muvi za kinaijeria yanaonyesga zaidi maisha na tamaduni za waigbo sio wanaijeria wote, muvi hizi zilifanya hata wengi kuamini Nigeria imejaa wakristo ilhali Nigeria ni nchi iliyojaa waislam. Nadhani hata kwenye uandishi wamo, kwa wale tulioweza kusoma mpaka sekondari nadhani mnakijua kitabu cha Things fall apart, muandishi Chinua Achebe ni wa huko na aligusia zaidi maisha ya waigbo kabla na baada ya ukoloni.
Walitaka wawe na nchi yao wenyewe na kukawa na vita ya jeshi la Nigeria dhidi yao mwaka 1970, Jeshi la Nigeria lilikuwa kubwa sana na lenye nguvu likawachapa, kuanzia hapo Serikali ya Nigeria ilihakikisha hawa watu hawaji kuinuka tena, hakuna maendeleo yanapelekwa huko kwao hata barabara ni changamoto, wana akili za darasani lakini hata wasome vipi suala la ajira wanatengwa sana, kwenye mambo ya siasa nako wanatengwa sana hawapewi vyeo vikubwa, jeshini nako wanachujwa sana.
Vita vilipoisha akaunti zote za wa igbo zilifungwa na kutaifishwa, kabla ya vita waigbo ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Nigeria na wafanyabiashara wengi walikuwa waigbo, vita ilipoanza wafanyabiashara wengi waliuawa na mali zao ziliporwa, akaunti zilifungwa, baada ya vita familia nyingi walipewa noti ya pauni 20 tu na ilibidi wasafiri umbali mrefu kuzibadili ziwe pesa za Nigeria na huko bado walipata usumbufu, hii ilikuwa ni kuwakomoa.
Lakini amini usiamini hata ushindane na samaki kuogelea kwa kumuweka kilomira nyuma bado atakupita tu, wa igbo kufikia mwaka 1990 tayari walikuwa wameshaanza kutengeneza mabilionea, hadi kufikia sasa Nigeria watu wenye pesa nyingi zaidi ni waigbo, wengi ni wamiliki wa viwanda, miji mikubwa imegeuzwa kuwa maeneo ya maduka, n.k. ni kawaida sana kukuta kijana wa Igbo mwenye miaka 35 ana utajiri wa kutisha (Ni kweli wapo wanaofanya biashara haramu lakini ni aslimia ndogo sana ya waigbo wanaofanya biashara kihalali )
Lakini kumbuka kwamba nserikali ilikuwa na lengo la kuwamaliza kabisa wasije kuinuka tena, mafanikio yao yamekuwa ni mwiba na tofauti na ilivyotegemewa, Serikali inayoongozwa na wahausa na wayoruba kwa kiasi flani inaendeleza itikadi za kuwadidimiza, wanabomoa nyumba zao kwa notisi za siku 2 kwa visingizio vya ajabu, wanachoma masoko yao, wanabomoa maduka yao, n.k. lakini hawa jamaa bado wanadunda tu, siri yao ni ushirikianao, umoja na mshikamano.
Wana akili za shuleni lakini wanakosa motisha ya kusoma sana kwasababu wanabaguliwa kwenye system, wengi husoma ili kumalizana tu na mambo ya shule waanza kujitafuta kivyao ama waongeze nguvu biashara za family. Ni tofauti kwa upande wa wayoruba wanapata motisha zaidi ya kusoma sababu wao angalau wanaweza kupata ajira kwenye system japo Nigeria ni nchi yenye tatizo kubwa sana la ajira na bado kuna wale wahausa wanapeana sana ajira za kiukoo bila kuwekea uzito elimu,
Kwa Hali hii kuna system ilianzishwa inaitwa Quota Sytem, Mitihani ya sekondari kwenda vyuoni huwa ina maksi 400 kwa ujumla, Marks za kuingia vyuoni ni tofauti kulingana na ukanda na jamii za wanaiheria, Muhausa akipata marks 150 anaingia chuo, Myoruba inabidi apate 200, kwa waigbo kamba imekazwa sana inabidi wapate kuanzia 250.
Haya ni matokeo ya mtihani wa taifa wa sekondari 2023, hao wote wanne wanoongoza ni waigbo
Mtu maarufu msomi kutoka Afrika kwenye uwanja wa computer ni Philip Emeagwali, Akiwa na miaka 13 aliwahi kusitisha masomo yake huko kijijini kwao ili aende kupigana vita iliyokuwa ikiendelea, Uwezo wale mkubwa wa hesabu ulimvusha mpaka Marekani kwenda kusomea sayansi ya computer na kuweza kubuni teknolojia inayaotwa parallel Processing, kuwezesha computer kutekeleza shughuli nyingi kwa wakati mmoja badala ya kufanya kazi moja baada ya nyingine, hata hio somu ama laptop unayotumia inatumia teknolojia aliyoigundua, Mwaka 1989 alitengeneza computer yenye spidi kubwa mno kuziunganisha processor elf 65 zilizoweza kupiga hesabu bilioni 3.1 kwa sekunde, Ni jambo lililoushangaza ulimwengu wa teknolojia na mchango wake ulitambulika kwa kupewa tuzo ya Gordon Bell ambayo ni kama Noble Prize kwenye mambo ya teknolojia, Wengine pia wanamuita ni "Father of omternet" yaani baba wa internet kwa mchango wake mkubwa kwenye mifumo ya networking.
Siri yao kubwa zaidi tofauti na wenzao ni kwamba wana umoja, wanabebana wakijua muda wowote tatizo likimtokea flani basi kesho linaweza kumkukuta mwengine na pia hawajasahau walikotoka (kila christmas wana utaratibu wa kurudi vijijini kwao), wanajua wanabaguliwa na kufanyiwa figisu hivyo inabidi waaminiane na wasaidiane sana, wana system yao imejizolea umaarudu inaitwa Igbo apprenticeship system, ni kwamba wafanyabiashara wote wa igbo wamejiwekea utaratibu wa kuchukua ndugu zao vijijini kuwaleta mjini wawafundishw biashara kisha baada ya miaka mitano hadi 10 nao wanawapa mitaji kuanzisha biashara zao, hivyo hata moja akifanyiwa figisu kuna wengine zaidi wanaendeleza mapambano na kuboresha mbinu za kibiashara.
picha hii inaonyesha mfano wa hio system, hata iwe biashara ndogo watafundishana na kushirikiana kuikuza, mtu hadi awe na kiwanda unaweza kuta alianza kutengeneza viatu kwa mikono mwenyewe ila alipoleta wenzake wa ziada ndio uzalishaji ukaongezeka, Biasahra inaendelezwa hadi kuanza kuuza viatu nje ya nchi. (Umoja ni nguvu kubwa sana)
Lagos ndio jiji kubwa zaidi Nigeria na Africa
Jiji hili kwa asili lipo Nigeria ya Kusini Magharibi walipo Wayoruba lakini ndio kimbilio la waigbo wengi kwenda kytajirikia kwa kutumia uwezo wao mkubwa waliojaliwa kibiashara, Karibu asilimia 60 za biashara katika jiji hili ni waigbo na wanaendeleza ile system yao ya apprenticeship wanazidi kukua, WANACHAPISHA PESA THEY MAKE IT RAIN!!
Sasa ubaya ni kwamba wanachapisha pesa kwenye sehemu ambayo kwa asili ni ya wayoruba ina ndio hapo sasa inachangia wachukiwe kwa kufanyiwa figisu za kubomolewa makazi, kuchomewa maduka, n.k. na hata sasa ukiingia twitter ukisechi semolition igbo unakutana na post kibaoo tu maduka yanavunjwa.
Real Estate biashara za Kujenga na kukodisha Nyumba, Hotels, n.k. jamaa wamewekeza vilivyo - Hapa sasa hata Wayoruba wanajikuta kwenye mji wao wanalipa kodi kwa wageni ili wapate pa kulala,
Viwanda vingi sanaaaa, vingi mno vinamilikiwa na hawa waigbo hapo Lagos,
Masoko makubwa ya Lagos yamejaza wa igbo kama
Baligun Market - Ni kariakoo ya Lagos ila ni kubwa sana kuzidi Kariakoo na ina msongamano sana
Idumota - Ni kariakoo nyingine ya Lagos ila bado ni kubwa kuzidi hii ya Tz
Computer Village - Hii ni kama kariakoo nzima iwe imejaza masoko maalum ya mambo ya electronics kama simu, laptops, speaker, tv, n.k.
Ladipo Market - Hii ni kama kariakoo nzima ijae maduka ya spea za magari