SoC02 Mapinduzi ya Tatu ya Internet (Web 3) na Fursa Zake kwa Kijana wa KiTanzania

Stories of Change - 2022 Competition

MnllnrD

New Member
Jul 22, 2022
1
5
Vijana wengi tunapenda kutumia internet kufanya mambo yetu mbali mbali ikiwemo, kuperuzi katika mitandao mbali mbali ya kijamii, kutumiana jumbe, kuangalia video na pia kujifunza vitu mbali pia kujiburudisha kwa kucheza michezo mbali mbali inayopatikana mitandaoni maarufu kama games.

Lakini je kama tunaweza kufanya vitu ivi vyote na bado tukapata faida kwa kuingiza pesa kwa vitu tunavyovifanya mtandaoni, tutakua tupo tayari?

Basi hii ni faida moja wapo ya mapinduzi ya tatu ya internet ambayo kwa kitaalamu tunaita web 3.

Mapinduzi ya tatu ya internet ni nini?
Mapinduzi ya tatu ya internet ni mapinduzi ambayo mtumiaji wa internet anaweza kumiliki mali mtandaoni na pia akiwa ni mmiliki wa taarifa zake binafsi bila ya kuwepo makampuni makubwa yoyote ambayo yanatoa huduma hizo kwa watu mfano Facebook, Amazon nakadhalika ambapo makampuni haya yanatabia yakutumia taarifa binafsi za watumiaje wake kupata faida. Hapa unapata faida wewe mwenyewe moja kwa moja.

Historia fupi ya Mapinduzi ya internet

Mapinduzi ya kwanza ya internet web 1

Hapa ni pale ambapo internet ilipogunduliwa katika miaka ya 1990s ambapo ilikuwa inampa mtumiaji haki ya kusoma na kuandika tu pamoja na kutumia emails. Mtumiaji kazi yake ilikuwa ni kusoma na kuandika tu na ilikuwa ngumu kubadilishana taarifa. Ugunduzi huu wa internet ulitokea katika miaka ya mapema ya 1990s na mtu aliyejulikana kama Tim Berner Lee. Kwa kipindi hicho kuna makampuni yaliona fursa na yakatumia teknoljia hiyo kuwa makubwa mfano Amazon.

Mapinduzi ya pili ya internet web 2
Hapa ni kwenye miaka ya 2000 ambapo tunaona kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii kama facebook na twiter ambapo mtumiaji alikuwa na uwezo wa kusoma na kutoa maoni yake na pia ilikuwa rahisi kubadilishana taarifa kwa haraka zaidi. Hapa tunazungumzia matumizi ya mitandao ya kijamii. Hapa ndipo internet ilipokuwa kwa kasi zaidi kuliko kipindi chochote kile na makampuni haya yalikuwa yanapat faida na kukua zaidi. Mfano wa kampuni hizi zilikuwa ni Facebook, google, Netflix nakadhalika.

Mapinduzi ya tatu ya internet web 3
Inaanza mwanzoni ya miaka ya 2010s kwanzia mwaka 2014 na kuendelea. Inahusisha ugunduzi wa sarafu ya mtandaoni kama Bitcoin iliyogunduliwa mwaka 2009 ambapo ilikuwa inatumika kama chombo cha kutuma sarafu ya mtandaoni yenye thamani halisi ya pesa pamoja na umiliki wa taarifa zako binafsi bila kuipa kampuni yoyote ile.

Mapinduzi haya ya tatu ya internet yalitiwa mwanga zaidi baada ya sarafu ya mtandaoni ijulikanayo kama bitcoin kuanzishwa na kuanza kutumika, lakini yalipata nguvu zaidi baada ya sarafu nyingine ya mtandaoni ijulikanayo kama Etherium iliyogunduliwa mwaka 2015 ambayo sarafu hii inamuwezesha mtumiaji wake kufanya mihamala na kumiliki vitu tofauti katika mtandao unaotumia blockchain.

Sifa za mapinduzi ya tatu ya mtandao wa internet.
Inahusisha na ugunduzi wa teknolojia mbali mbali ambazo ni Sarafu za mtandaoni (Cryptocurrency), Blockchain, Smartcontract, NFTs pamoja na Metaverse.

Decentralized wallet
Hizi ni application zinazo kusaidia katika kuhifadhi pesa pamoja na mali yako za mtandaoni, na pia ndio application zinazokusaidia kuingia katika blockchain. Bila hizi wallet ni ngumu kumiliki pesa au mali ya mtandaoni. Zinafanya kazi kama kihifadhio cha pesa na mali zako za mtandaoni.

Cryptocurency
Hizi ni sarafu za mtandaoni zenye thamani halisi ya pesa ambazo zinatumika katika kazi mbali mbali ikiwemo kununua na kuuza vitu mtandaoni pamoja na katika ulimwengu wa kawaida mfano wake ukiwa ni Bitcoin, Ether, Sol nakdhalika.

Blockchain
Hii ka kiswahili tunaweza kuiita kihifadhi taarifa kwa njia ya mnyororo uliokowadhi kwa watu wote unaotumika kuhifadhi taarifa mbali mbali ikiwemo mihamala inayofanywa ya sarafu za mtandaoni pamoja na mali za mtandaoni kama NFTs, Hii ni aina ya internet inyowezesha kufanya mihamala na kutunza mali za mtandaoni.

Smartcontracts
Hii ni mikataba sanifu ya mtandaoni ambayo inatumika katika blockchain pale watu wawili wanapokutana na kuhitaji kufanya biashara kama kubadilishana sarafu za mtandaoni na pesa halisi. Kazi yake kuu ikiwa ni kutoa udanganyifu kwa watu hawa wawili ambao hawajuani kubadilishana sarafu hizi bila udanganyifu wowote au utapeli.

NFTs
Hii ni mali ya mtandaoni isiyo ya kujirudia ambayo inatupa haki ya kumiliki vitu vyenye thamani halisi mtandaoni, inaweza ikawa katika mfumo wa picha, video au document. Ndio kitu pekee ambacho kinatupa daraja katika umiliki wa mali ya mtandaoni hadi kumiliki mali hiyo ya mtabndaoni katika maisha yetu halisi.

Metaverse
Huu ni ulimwengu wa mtandaoni ambapo unawezeshwa kwa kuwepo na teknolojia ya blockchain. Ni kama maisha halisi tunayoishi lakini yapo mtandaoni kukiwa na pesa kwa kupitia crytpocurrency, mali kupitia NFTs ikiwezeshwa na Blockchain na kufanya mihamala pamoja na biashara kupitia smartcontracts. Kupitia Metaverse tunaweza kufanya kila kitu tunachofanya katika maisha yetu halisi ya kawaida yakawa mtandaoni.

Kama wewe ni mpenzi wa filamu kuna filamu moja ambayo inajulikana kama Ready Player one ambapo inaelezea ulimwengu huu wa Metaverse lakini huko wameutaja kwa jina la Oasis.

Teknolojia hii na fursa kwa kijana.

Ikiwa ni mwanzoni kabisa.

Mapinduzi haya ya internet Vijana tunafursa kubwa katika mapinduzi haya hususani katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kwa sababu zifuatazo.

Kwa kupitia teknolojia hii na kuazishwa kwa metaverse tunaona makampuni makubwa yashaanza kujihusisha na teknolojia hii ambapo tunaona kampuni ya facebook ilibadilisha jina laki nakujiita Meta ilikuweza kujishughulisha zaidi na ugunduzi zaidi wa metaverse hii ikimainsha kuwa ndani ya miaka michache kila kitu kitakua ndani ya metaverse, ivyo ni muhimu sana kuijua na kuingia ndani zaidi ya mapinduzi haya ya tatu ya internet mapema.

Mpaka mwaka 2020 teknolojia ya metaverse ina thamani ya billioni 27.21 dollar za kimarekani, Inaaminika kuwa mpaka mwaka 2030 teknolojia ya metaverse itakua na thamani ya jumla ya trillion 1.6 ya dollar za kimarekani sasa tafakari ni kwa jinsi gani tutakuwa tumekabiliana na umaskini kwa kuingia mapema katika teknoljia hii miaka michache ijayo.

Ugunduzi wa biashara mpya mtandaoni.
Teknolojia hii imeleta biashara mpya mbali mbali za mtandaoni ikiwemo kuuza sarafu za mtandaoni pamoja na kuuza NFTs ambapo ndani ya muda mfupi imeweza kubadilisha maisha ya watu kutoka katika ufukara hadi utajiri, bila kuhitaji mtaji mkubwa kitu cha muhimu ikiwa ni kufanya utafiti juu ya thamani ya sarafu ya mtandaoni pamoja na NFT ambayo unatakiwa kununua kwa bei ya chini na kuiuza kwa bei ya juu na wewe kupata faida.

Inatatua matatizo yanayo sababishwa na mabenki.
Pia kupitia teknolojia ya sarafu za mtandaoni inatatua baadhi ya matatizo ya pesa ikiwemo kumiliki pesa zako binafsi bila kuwepo uwepo wa taasisi za kibenki zinazoshikilia pesa zetu nakutudhibiti sisi ilihali pesa ni zetu mfano pale tunapohifadhi pesa katika benki tunazisaidia benki hizi kutumia pesa zetu katika kutoa mikopo ya riba kwa watu mbali mbali na kupata faida zaidi huku wakiendelea kutukata pesa tunazohifadhi benki wakati wao ndio wanafaidika dhaidi wakati kupitia Web 3 tunaweza tukahifadhi pesa zetu bila makato ya aina yoyote. Lakini pia unapotaka kutoa pesa lakini benki inakukatalia kutoa pesa zako kwa sababu fulani mfano kutokana na anguko la uchumi.

Kupitia sarafu za mtandaoni unahaki ya kutoa pesa yako mwenyewe wakati wowote kwa sababu wewe ni mmiliki mwenyewe aijalishi utakua kwenye hali gani au uchumi wa nchi yako ipo katika hali gani.

Inatoa ajira kwa vijana kwa njia ya ujasiriamali wa kidigitali.
Inatoa pia ajira kwa vijana. Mfano kupitia NFT project mbali mbali unaweza kuajiriwa ili kuweza kuendesha jamii inayohusika katika utengenezaji wa project hiyo, unaweza ukawa kama moderator, project and community manager, Developer, Graphics artist, Product designer nakadhalika na kujiingizia pesa nzuri ndani ya wiki.

Inaleta fursa ya kucheza games za kulipwa.
Pia kupitia mapinduzi ya tatu ya internet kila kitu tunachokifanya kinaweza kutuingizia pesa moja kwa moja. Kwa mfano kupitia teknolojia ya Blockchain kumekuwa kukianzishwa michezo mbali mbali ya mtandaoni kama games ambapo unaweza kulipwa kwa kucheza games fulani mtandaoni ila ikiwa tu ni lazima ununue NFTs fulani itakayotumika kama moja ya mshiriki katika game hilo.

Wakati wa kipindi cha COVID biashara hii ilifanya vizuri kama katika nchi ya ufilipino kupitia game linalojulikana kama Axiel infinity watu wengi walilicheza na kuwatajirisha baadhi ya watu huku watu wengine wakiifanya ni ajira kabisa.

Afrika, Tanzania na teknojia hii tukowapi nayo.
Nchi za Afrika zimekuwa zikiachwa nyuma katika mapinduzi ya maendeleo mbali mbali, lakini teknolojia hii limekuja tukiwa na nyenzo zote zinazotuwezesha kwenda nao sambamba katika mapinduzi haya na nchi za Magharibi, Swali likiwa ni je tuko na utayari gani kuchangamkia fursa hii kama kijana wa Kitanzania, Mimi niko tayari na ninaifuatilia teknolojia hii na najaribu pia kutoa elimu kwa vijana wenzangu w Kitanzania. Swali limebaki kwako msomaji. Uko tayari kuchangamkia fursa hii ya mapinduzi ya tatu ya internet kama kijana?

Hitimisho
Ili kuweza kuelewa teknolojia hii ni lazima ufanye utafiti wa hali ya juu na kusoma ili kuweza kupata maarifa ya kujua ni jinsi gani inafanya kazi, unaweza ukaona labda ni kitu kigumu ila ni kitu cha kawaida sana, ni kama internet ya kawaida tu lakini unatakiwa kuwa na maarifa ya kawaida kuweza kujua inafanyaje kazi. Ukiweka muda wako hakika utajua inafanyaje kazi.

Angalizo
Kama unataka kufanya biashara kupitia teknolojia hii, kama biashara nyinginezo ina changamoto zake, moja wapo ikiwemo utapeli hususani kwa watu wanaoanza kujifunza, watatokea watu wengi watakaosema watakupa pesa bure ila mara nyingi wengi ni matapeli ivyo unatakiwa kuwa makini na watu kama hao pia na vitu unavyomiliki mtandaoni huko.
 
Vijana wengi tunapenda kutumia internet kufanya mambo yetu mbali mbali ikiwemo, kuperuzi katika mitandao mbali mbali ya kijamii, kutumiana jumbe, kuangalia video na pia kujifunza vitu mbali pia kujiburudisha kwa kucheza michezo mbali mbali inayopatikana mitandaoni maarufu kama games.

Lakini je kama tunaweza kufanya vitu ivi vyote na bado tukapata faida kwa kuingiza pesa kwa vitu tunavyovifanya mtandaoni, tutakua tupo tayari?

Basi hii ni faida moja wapo ya mapinduzi ya tatu ya internet ambayo kwa kitaalamu tunaita web 3.

Mapinduzi ya tatu ya internet ni nini?
Mapinduzi ya tatu ya internet ni mapinduzi ambayo mtumiaji wa internet anaweza kumiliki mali mtandaoni na pia akiwa ni mmiliki wa taarifa zake binafsi bila ya kuwepo makampuni makubwa yoyote ambayo yanatoa huduma zao kwa watu mfano Facebook, Amazon nakadhalika ambapo makampuni haya yanatabia yakutumia taarifa binafsi za watumiaje wake kupata faida. Hapa unapata faida wewe mwenyewe moja kwa moja.

Historia fupi ya Mapinduzi ya internet

Mapinduzi ya kwanza ya internet web 1

Hapa ni pale ambapo internet ilipogunduliwa katika miaka ya 1990s ambapo ilikuwa inampa mtumiaji haki ya kusoma na kuandika tu pamoja na kutumia emails. Mtumiaji kazi yake ilikuwa ni kusoma na kuandika tu na ilikuwa ngumu kubadilishana taarifa.

Mapinduzi ya pili ya internet web 2
Hapa ni kwenye miaka ya 2000 ambapo tunaona kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii kama facebook na twiter ambapo mtumiaji alikuwa na uwezo wa kusoma na kutoa maoni yake na pia ilikuwa rahisi kubadilishana taarifa kwa haraka zaidi. Hapa tunazungumzia matumizi ya mitandao ya kijamii.

Mapinduzi ya tatu ya internet web 3
Inaanza mwanzoni ya miaka ya 2010s kwanzia mwaka 2014 na kuendelea. Inahusisha ugunduzi wa sarafu ya mtandaoni kama Bitcoin iliyogunduliwa mwaka 2009 ambapo ilikuwa inatumika kama chombo cha kutuma sarafu ya mtandaoni yenye thamani halisi ya pesa pamoja na umiliki wa taarifa zako binafsi bila kuipa kampuni yoyote ile.

Sifa za mapinduzi ya tatu ya mtandao wa internet.
Inahusisha na ugunduzi wa teknolojia mbali mbali ambazo ni Sarafu za mtandaoni (Cryptocurrency), Blockchain, Smartcontract, NFTs pamoja na Metaverse.

Cryptocurency
Hizi ni sarafu za mtandaoni zenye thamani halisi ya pesa ambazo zinatumika katika kazi mbali mbali ikiwemo kununua na kuuza vitu mtandaoni pamoja na katika ulimwengu wa kawaida mfano wake ukiwa ni Bitcoin.

Blockchain
Huu ni myororo wa database uliokowadhi kwa watu wote unaotumika kuhifadhi taarifa mbali mbali ikiwemo mihamala inayofanywa ya sarafu za mtandaoni pamoja na mali za mtandaoni kama NFTs, Hii ni aina ya internet inyowezesha kufanya mihamala na kutunza mali za mtandaoni.

Smartcontracts
Hii ni mikataba ya mtandaoni ambayo inatumika pale watu wawili wanapokutana na kuhitaji kufanya biashara kama kubadilishana sarafu za mtandaoni na pesa halisi. Kazi yake kuu ikiwa ni kutoa udanganyifu kwa watu hawa wawili ambao hawajuani kubadilishana sarafu hizi bila udanganyifu wowote au utapeli.

NFTs
Hii ni mali ya mtandaoni isiyo ya kujirudia ambayo inatupa haki ya kumiliki vitu vyenye thamani halisi mtandaoni, inaweza ikawa katika mfumo wa picha, video au document.

Metaverse
Hii ni ulimwengu wa mtandaoni ambapo unawezeshwa kwa kuwepo na teknolojia tajwa hapo juu. Ni kama maisha halisi tunayoishi lakini yapo mtandaoni kukiwa na pesa kwa kupitia crytpocurrency, mali kupitia NFTs ikiwezeshwa na Blockchain na kufanya mihamala pamoja na biashara kupitia smartcontracts.

Teknolojia hii na fursa kwa kijana
Ikiwa ni mwanzoni kabisa.
 Mapinduzi haya ya internet Vijana tunafursa kubwa katika mapinduzi haya hususani katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kwa sababu zifuatazo.

Kwa kupitia teknolojia hii na kuazishwa kwa metaverse tunaona makampuni makubwa yashaanza kujihusisha na teknolojia, hii ambapo tunaona kampuni ya facebook ilibadilisha jina laki nakujiita Meta ilikuweza kujishughulisha zaidi na ugunduaji wa metaverse hii ikimainsha kuwa ndani ya miaka michache kila kitu kitakua ndani ya metaverse, ivyo ni muhimu sana kuijua na kuingia ndani zaidi ya mapinduzi haya ya tatu ya internet mapema.

Inaaminika kuwa mpaka mwaka 2030 teknolojia ya metaverse itakua na thamani ya jumla ya trillion 1.6 ya dollar za kimarekani sasa tafakari ni kwa jinsi gani tutakuwa tumekabiliana na umaskini kwa kuingia mapema katika teknoljia hii miaka michache ijayo.

Teknolojia hii imeleta biashara mbali mbali za mtandaoni ikiwemo kuuza sarafu za mtandaoni pamoja na kuuza NFTs ambapo ndani ya muda mfupi imeweza kubadilisha maisha ya watu kutoka katika ufukara hadi utajiri, bila kuhitaji mtaji mkubwa kitu cha muhimu ikiwa ni kufanya utafiti juu ya thamani ya sarafu ya mtandaoni pamoja na NFT ambayo unatakiwa kununua kwa bei ya chini na kuiuza kwa bei ya juu na wewe kupata faida.

Pia kupitia teknolojia ya sarafu za mtandaoni inatatua baadhi ya matatizo ya pesa ikiwemo kumiliki pesa zako binafsi bila kuwepo uwepo wa taasisi za kibenki zinazoshikilia pesa zetu nakutudhibiti sisi ilihali pesa ni zetu mfano pale unapotaka kutoa pesa lakini benki inakukatalia kutoa pesa zako kwa sababu fulani mfano kutokana na anguko la uchumi.
Kupitia sarafu za mtandaoni unahaki ya kutoa pesa yako mwenyewe wakati wowote kwa sababu wewe ni mmiliki mwenyewe aijalishi utakua kwenye hali gani.

Inatoa pia ajira kwa vijana. Mfano kupitia NFT project mbali mbali unaweza kuajiriwa ili kuweza kuendesha jamii inayohusika katika utengenezaji wa project hiyo, unaweza ukawa moderator na kujiingizia pesa nzuri ndani ya wiki.

Pia kupitia mapinduzi haya ya tatu ya internet kila kitu tunachokifanya kinaweza kutuingizia pesa moja kwa moja. Kwa mfano kupitia teknolojia ya Blockchain kumekuwa kukianzishwa michezo mbali mbali ya mtandaoni kama games ambapo unaweza kulipwa kwa kucheza games fulani mtandaoni ila ikiwa tu ni lazima ununue NFTs fulani itakayotumika kama moja ya mshiriki katika game hilo.

Wakati wa kipindi cha COVID biashara hii ilifanya vizuri kama katika nchi ya ufilipino kupitia game linalojulikana kama Axiel infinity watu wengi walilicheza na kuwatajirisha baadhi ya watu huku watu wengine wakiifanya ni ajira kabisa.

Kama wewe ni mpenzi wa filamu hususani za nje inawezekana ushaangalia filamu inayoitwa Ready Player One na ukafanikiwa kujionea jinsi inavyokuwa, basi kwa kupitia teknolojia hii huko ndio tunapoelekea, japokuwa sasa ivi na mapema sana kufika huko basi pia ni jambo jema kujiingiza mapema ilikufikia huko kwa pamoja.

Nchi za Afrika zimekuwa zikiachwa nyuma katika mapinduzi ya maendeleo mbali mbali, lakini ili limekuja tukiwa na mali zote zinazotuwezesha kwenda nao sambamba katika mapinduzi haya na nchi za Magharibi, Swali likiwa ni je tuko na utayari gani kuchangamkia fursa hii kama kijana wa Kitanzania, Mimi niko tayari na ninaifuatilia swali limebaki kwako msomaji. Uko tayari kuchangamkia fursa hii ya mapinduzi ya tatu ya internet kama kijana?

Hitimisho
Ili kuweza kuelewa teknolojia hii ni lazima ufanye utafiti wa hali ya juu na kusoma ili kuweza kupata maarifa ya kujua ni jinsi gani inafanya kazi, unaweza ukaona labda ni kitu kigumu ila ni kitu cha kawaida sana, ni kama internet ya kawaida tu lakini unatakiwa kuwa na maarifa ya kawaida kuweza kujua inafanyaje kazi. Ukiweka muda wako hakika utajua inafanyaje kazi.

Angalizo
Kama unataka kufanya biashara kupitia teknolojia hii, kama biashara nyinginezo ina changamoto zake, moja wapo ikiwemo utapeli hususani kwa watu wanaoanza kujifunza watatokea watu wengi watakaosema watakupa pesa bure ila mara nyingi wengi ni matapeli ivyo unatakiwa kuwa makini na watu kama hao pia na vitu unavyomiliki mtandaoni huko.
Safi...jazilia makala yako hii
 
Back
Top Bottom