Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Hili la kupeleka bweni akiwa na miaka kumi na nane sidhani kama lina-apply kwa kila mtu. Sasa imagine mtoto amemaliza darasa la saba akiwa na miaka 12 anatakiwa kwenda secondari ya bweni, ndiyo amechaguliwa huko. Au katika kutafuta shule nzuri unakuta mtoto analazimika kuishi mbali na nyumbani kwako, utafanyeje? Kuna mambo hayazuiliki.Binafsi huwa napinga sana kitendo cha watoto wadogo kupelekwa shule za bweni...mtoto anatakiwa kuwaacha wazazi wake na kukaa mbali mpaka anapofikisha umri wa miaka 18.....
Lakini cha msingi hapo ni huyo daktari kuamua kuficha siri za hiyo shule na mlinzi aliyefanya kitendo hiki. Maana mtu kama huyu alitakiwa aandikwe kwenye magazeti na TV, na afungwe miaka 30 jela na kifungo chake kitangazwe all over. Kwa njia hii, wengi wangekuwa wanajifunza, lakini linapotokea jambo kama hili halafu hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, huo uozo unaendelea kukuzwa. Tutajieni japo jina la hiyo shule, and then tujue tunafanya nini for the goodness of our children.