Kama mzazi hili limeniuma sana!

Binafsi huwa napinga sana kitendo cha watoto wadogo kupelekwa shule za bweni...mtoto anatakiwa kuwaacha wazazi wake na kukaa mbali mpaka anapofikisha umri wa miaka 18.....
Hili la kupeleka bweni akiwa na miaka kumi na nane sidhani kama lina-apply kwa kila mtu. Sasa imagine mtoto amemaliza darasa la saba akiwa na miaka 12 anatakiwa kwenda secondari ya bweni, ndiyo amechaguliwa huko. Au katika kutafuta shule nzuri unakuta mtoto analazimika kuishi mbali na nyumbani kwako, utafanyeje? Kuna mambo hayazuiliki.

Lakini cha msingi hapo ni huyo daktari kuamua kuficha siri za hiyo shule na mlinzi aliyefanya kitendo hiki. Maana mtu kama huyu alitakiwa aandikwe kwenye magazeti na TV, na afungwe miaka 30 jela na kifungo chake kitangazwe all over. Kwa njia hii, wengi wangekuwa wanajifunza, lakini linapotokea jambo kama hili halafu hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, huo uozo unaendelea kukuzwa. Tutajieni japo jina la hiyo shule, and then tujue tunafanya nini for the goodness of our children.
 
Habarini waungwana!

Jana nilikutana na jamaa yangu mmoja ambaye ni muhudumu wa afya, akanipa ofa (si kawaida yake). Kwa hali hiyo ikabidi nimdadisi, ndo akaniambia amepewa ahsante baada ya kumfanyia uchunguzi na councelling mtoto mmoja wa form 1 (13yrs) katika shule fulani ya boarding!
Baada ya kudadisi vizuri zaidi akaniambia kuwa huyo mtoto amelatiwa na mtu mzima (possibly mlinzi wa shule) ila ameambiwa amfanyie councell mtoto asije kutangaza (Shiit) ili kuharibu jina la shule hiyo!
Sasa kama mzazi najiuliza usalama wa watoto wetu huko mashuleni, tunawapeleka bado wadogo sana then inakuwa ni mbali halafu wanakaa muda mrefu,
Jambo hili limeniuma ndo maana nikalileta hapa!
Ushauri wangu Kama mzazi, muangalie watoto wenu, Msijifanye mko biiize kutafuta hela mpaka mnawatupa boarding school wakiwa wadogo(hata kujitetea hawawezi)
Naandika ikiwa bado nimeumia as if ni mtoto wangu ndo amefanyiwa hivo!

Kama imekuuma kweli kama unavyosema basi chukua hatua...hiyo ni breach ya 'medical ethics' amefanya daktari huyo. Kuanzia mlinzi, shule na daktari huyo wana kesi ya kujibu..
 
Uuuuwwwwwwiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!
Watoto wetu wa kiume, Mungu Tusaidie kuwalinda, Khaaaaaaaaaa!! Tunakuomba ututajie shule , Pls, Pls, Taja shule, ili huyo mlinzi achukuliwe Hatua pamoja na hiyo shule.
Nawaombeni wazazi wenzangu msipeleke watoto boarding school mpk wajitambue na waweze kujieleza wanapotendewa baya. Please wazazi wenzangu.

CC Smile, Nyumba kubwa, Gfsonwin
 
Nakuomba wewe ndugu urudi hapa ueleze hapa angalau hata jina la Shule hiyo ni sehemu nzuri ya kuanzia. Kwanini unawalinda? utapoteza nini? Wataje tafadhali hata na jina la huyo daktari even if it means losing your friendship why would you have such friends....................Usiporudi na kueleza hayo, Shame on you! na jua kuwa Mungu anakutazama kuna sababu hizo information zimekuja kwako
 
Ndio mimi naamini mtoto anatakiwa kuachana na wazazi kwa muda mrefu hasa shule baada ya kujitambua na kujua haki zake....Angalau from form one sio mbaya sana
 
dist111 kama mzazi na kama mwananchi mwenye kufuata maadili mema!! chukua hatua ...leo kwa mwenzio kesho kwako!! usimlee 'a defiler'...chukua hatua stahiki. huitaji kwenda polisi bali unahitaji kuanika maovu yote hadharani...shule gani hii ambayo inashiriki kuficha uovu na kumuonga 'daktari' ambaye anakaaa baa kunywa hiyo hongo akifurahia uharibifu ..kweli hizi zama za kizazi cha nyoka... jivue gamba dist111 na chukua hatua ...usimung'inye mung'unye maneno!!
Hivi nyinyi hamjui kuwa mtanzania anataka mabadiliko bila yeye mwenyewe kubadilika?
Analaani kitendo lakini yeye hataki kuwa mwanzo wa kukomesha uhalifu.
 
dist111 umekimbia wapi? huwezi kimbia kivuli chako!! mabadiliko yanaanza na wewe!!
 
Binafsi huwa napinga sana kitendo cha watoto wadogo kupelekwa shule za bweni...mtoto anatakiwa kuwaacha wazazi wake na kukaa mbali mpaka anapofikisha umri wa miaka 18.....
"
Nimeishi na wazazi wangu nikiwa bado mwanafunziii..... sikuwahi kuishi peke yangu bila kuwa na wazazi wanguuu"Ukisikiliza kionjo hicho utajua kuwa nyimbo za wakati huo zilikuwa na mafunzo ndani yake!
 
habarini waungwana!

Jana nilikutana na jamaa yangu mmoja ambaye ni muhudumu wa afya, akanipa ofa (si kawaida yake). Kwa hali hiyo ikabidi nimdadisi, ndo akaniambia amepewa ahsante baada ya kumfanyia uchunguzi na councelling mtoto mmoja wa form 1 (13yrs) katika shule fulani ya boarding!
Baada ya kudadisi vizuri zaidi akaniambia kuwa huyo mtoto amelatiwa na mtu mzima (possibly mlinzi wa shule) ila ameambiwa amfanyie councell mtoto asije kutangaza (shiit) ili kuharibu jina la shule hiyo!
Sasa kama mzazi najiuliza usalama wa watoto wetu huko mashuleni, tunawapeleka bado wadogo sana then inakuwa ni mbali halafu wanakaa muda mrefu,
jambo hili limeniuma ndo maana nikalileta hapa!
Ushauri wangu kama mzazi, muangalie watoto wenu, msijifanye mko biiize kutafuta hela mpaka mnawatupa boarding school wakiwa wadogo(hata kujitetea hawawezi)
naandika ikiwa bado nimeumia as if ni mtoto wangu ndo amefanyiwa hivo!

kama kweli wewe ni mzazi na kama kweli hili jambo limetokea basi sio kweli kuwa limekuuma hata kidogo, maana kama limekuuma kweli maumivu ya mzazi basi ungelikwenda moja kwa moja polisi kuripoti ulichosikia. Infact ungelimburuza na huyo rafiki yako pia. Hata kama polisi na wahusika wengine wakiamua kutofuatilia lakini kwa upande wako kama mzazi utakuwa umefanya wajibu wako.

timiza wajibu wako kama mzazi
 
mm Mwanamgu Kumpeleka Seminary Mwisho, Sitaki Kbs Kuckia Mambo Ya Seminary Na Boarding, Day Scholar inatosha.
 
ndo maana mambo ya boarding siyataki kabisa mie.......

Kingine ndugu walojazana majumbani hawana mwelekeo pia ni hatari kwa watoto
 
mi nashauri alieleta huu uzi kama anaogopa kuilipua shule,
atume jina la shule (PM) kwa memba kama lara 1, smile, gsfown (nimekosea sp), au mwingine ambae anaona anafaa ili tujue pa kuanzia.
 
bila shaka itakuwa shule za yule mama mtakatifu
na hiyo ndiyo tabia ya shule zake kwani hata madereva wanawabaka watoto.
 
dist111 unatafutwa hapa kwenye huu uzi, njoo na majibu ya maswali yalioibuliwa na wadau hapa. Au umeme umekatika huko uliko? :A S angry:
 
Jamani hatuwapeleki boarding kwa sababu ya ubize, mazingira yanasababisha. Sasa kwa hali hii ya usafiri Dar es salaam, mtoto kusoma day si mateso makubwa? Nina jamaa yangu anakaa Makongo juu mwanae anasoma st Anthony sijui, kila siku anarudi saa tatu usiku, si mateso hayo? Lakini ujumbe umetufikia mkuu, nina binti yupo boarding. Kila siku roho juu juu tu jinsi ya kumlinda na huu ulimwengu katili. Mpaka wakati mwingine nafikiri I worry too much. Kitaniua na presha hiki kitoto. Naomba tu waniachie walau afikishe 18!

Yaani ulivyoandika umenifanya nicheke wakati sio mahali pake kabisa.....
 
Ndio mimi naamini mtoto anatakiwa kuachana na wazazi kwa muda mrefu hasa shule baada ya kujitambua na kujua haki zake....Angalau from form one sio mbaya sana

Tatizo wengine hiyo form one ndio ana miaka 13 kama ilivyoonekana kwenye kesi hii tunayoijadili hapa.
 
dist111 pls taja hiyo shule km kweli umeumia kama mzazi,just imagine ndo kangekua hako kabinti kako ungetulia kimya na kuogopa huo urafiki wenu,damu ya huyo mtoto itadaiwa mikononi mwako kwa kukaa kimya,nami naunga hoja changes begin with you!! Mabadiliko ni mm ni ww,halafu hakuna tena siri hapo bora umalizie tu kutapika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom