Kama MWAKYEMBE na MAGUFULI wanafanya uhuni huu basi CCM imedhamiria kuwazika Watanzania!!!

Watu mmempaka sana Paul Kijoka, lakini katika undani na mantiki ya hoja yake alikuwa na hoja yenye kuhold water. Hebu someni tena uzi wake "critically" hafu muangalie kama kweli mmemtendea haki huyu kamanda. Hoja zenyewe ni hizi Mmemtendea haki kweli? Haya aloyasema hayana ukweli au umaana katika utekelezaji? guys, you must always think big and avoid being myopic. Siyo kumshambulia tu mtu bila hoja ya maana badala ya kupangua hoja kwa kutumia hoja!!!!
[/LIST]

genekai, unajua sisi wasomi wa TZ tumelogwa! Na Ukweli ni kwamba tutalipa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kusoma tukakosa Elimu. Niliyoyasema ni kweli lakini watu hapa wanaleta mzaha na mapenzi yaliyochochewa na magazeti hasa vichwa vya magazeti kwenye vyombo vya habari vya kidaku vya Tanzania (Sijainclued MwanaHalisi hapo). Ni kweli kuwa ata kujenga Reli ni more expensive kuliko kuboresha na kuweka barabara kwenye viwango hasa zile za pembeni. Mimi nimetaja Fly Overs as only one of the solutions ila nadhani kwa udahifu mkubwa wa wachangiaji wa leo wewe ndo umesomatu wengine wamelala nadhani.
 
Mkuu hapa umenena vema kabisa na nadhani mtoa mada amekurupuka kutoa lawama zisizo na kichwa wala miguu.Lengo hapa ni kuokoa muda ambao watu wanaotumia public transport wanaupoteza kutokana na msongamano wa magari njiani.Nashangaa kwanini watu hawaishi kuleta majungu hata kwa mambo ambayo yako wazi kabisa.
myhem, Kuokoa muda kwa kinanani (wakazi wa wapi) Tegeta, Kinondoni, Tandale........ au wapi? Unajennga hoja kitoto sana mkuu!! Ebu tutajie maeneo ambayo treni hizo zinapiata.
 
Mtoa mada lazime ajue nchi zote zilioendelea hazikuanza na fly over, k hata kenya majirani zetu mwaka huu ndio wamemaliza fly over lakini hazisaidia kupunguza msongamano Nairobi, Kila jambo lina hatua zake, Wananchi waneshangilia tren kwa sababu umewarahishia usafiri asb na jioni kwenye foleni za Ubongo Kariakoo au Posta, then sema kinachofuata ni kufikiria kuwepo na flyover ili kurahisisha kwenye makutano kama ya Ubungo na magomeni Mapipa, na fire, ila kwa kiasi kikubwa tren na hayo mabasi ya mwendo kasi yatasaidia kuokoa muda wa walalahoi tunaotumia usafiri wa umma
 
Lengo la treni ni kupunguza adha kwa walala hoi hasa nyakati za asubuhi na jioni na kuhusu msongamano wa magari tatizo ni miundo mbinu na wala si kwamba eti magari ni mengi sisi Tanzania hatujafikia uwiano wa nyumba moja kwa gari moja wananchi wengi wa Tanzania hawana magari mfano pita mitaani tunapoishi angalia wanaomiliki magari na wasio miliki magari wengi ni wepi?
 
Acha chuki.....wamethubutu na wameweza.......!
  • Kama una huruma na hela iliyotumika achilia mbali haijaingia mfukoni mwao, kwanini usihoji fedha zilizopo katika mabenki uswis zisirudishwe na wahusika wenyenazo wauwawe?
  • Duniani usafiri wa treni ndio maarufu kama daladala za hapa....London wanatumia achailia mbali miji mikuu kibao kote duniani.
  • Wao wameamua kuanza na hayo walioanza nayo......kama kuna wazo au njia ingine tofauti na hii ya reli na BRT kwanini tusiwape nafasi na kuwapongeza kwa hili la awali.....!
  • Kwanini usitoe wazo kuwa, wizara zinde mikoani na hapa Dar es Salaam zibakie wizara nyeti tu. Mfano; Wizra ya Afya Dodoma, Elimu iende Lindi, Kazi ajira na Vijana Singida, Malia asili na Utalii Zanzbar, Maji Shinyanga, kilimo Kigoma nk. Sasa Tuone wangapi watakaa mjini.

Wewe mleta huu uzi, ungekuwa jirani yangu lazima ningeku-mabwepande tu. Hao uliowataja ni majembe, hata kama wanaiba kazi tunaona, sio kama ilyekutuma ambaye anaiba 90%, halafu iliobaki ndio anawekeza kwenye mradi uliokusudiwa.

Kibanga Msese
Samahani sasa kaka yangu, sijatumwa na mtu. Nimeona usanii alafu ebu soma basi posit yangu maana umechagia heading tu!!!!!! Nimesema hela hizo zingeboresha usafiri na si kutapeli usafiri kwa BRT na Reli!!!!!! Ebu soma. Acha uzembe bwn. maandishi kidogo tu yanakutoa jasho kaka!!!!!!
 
nimemuelewa point yake, kuna baadhi ya sehemu hapa dar barabara ni mbovu sana hazifai kupitishia magari na hizi barabara zingeweza kutumika kama short cut zikapunguza foleni sana maeneo mengi kwa hiyo ni kweli wizara ya ujenzi wangeweka lami au kuzifukia fukia zikawa zimenyooka zingepunguza foleni maeneo mengi sana, hizi treni tunawapongeza kwa juhudi zao lakini zinawanufaisha baadhi tu ya wakazi bado kuna sehemu nyingi sana foleni zitakuepo..TANROADS wanapokea bajeti kubwa tu ya kutengeneza barabara hapa mjini sijui hua wanazifanyia nini hizo hela
 
Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona Watanzania wanashabikia matukio haya mawili la Basi ziendazo Kasi BRT
(BRT) na uzinduzi wa
Reli kwa Jiji la Dar es Salaam. Mipango hii yote inaongozwa na watu wanaojitambulisha kuwa kuwa wachapa kazi kina Magufuli na Mwakyembe.
Ukweli kwamba ni danganya toto kwa sababu zifuatazo:

1. Tatizo la msongamano wa magari halisababishwi na kuwepo kwa gari za abiria ( public transport) bali ni private cars na maroli.
2. Msongamano huu unaletwa na kwenye junctions( nodes) mf. Ubungo mataa, Shekilango, Njia panda ya Tabata, Buguruni, Magomeni Mapipa,......
na suluhisho ni fly overs.
3. Reli hizi zinaishia pafupi sana na haziondoi au kuzuia watu binafsi kwenda na magari yao.
4. Hakuna parking Dar na watu wengi hubakia barabarani wakizunguka wkt wengine walionao wanafanya issue zilizowaletra mjini.
5. Upanuaji Barabara haupunguzi foleni bali hupunguza urefu wake na kutengeneza foleni fupi yenye mistari mingi ya magari mf. barabara ya Mwenge to Ubungo kupita Mcity.
kwa msisitizo zaidi ni sawa na kuweka maji kwnye mrija wa kunywea soda ukajaa alafu na mengine ukajaza beseni na mtoto akaulizwa maji mengi yako wapi naye akachagua mrija kisa umezidi beseni kwaurefu.

Sasa hela kubwa inayotumika kutengeneza barabara za BRT na Reli ingefanya yafuatayo kama si ufisadi:
  1. kutengeneza barabara zote mbovu za kupunguza msongamano kwemye Barabara ya Moro kwa kiwango cha lami ili kupunguza kufurika kwa magari Morogoro road mf. Barabara ya Kimara na Mbezi to Uwanja wa Ndege, Kimara na Mbezi to Tegeta........
  2. kuwekeza kwenye Fly Overs kwenye mataa yote.
  3. kuboresha na kupanua barabara hasa vituo amabvyo viko barabarani hasa mf. njia ya Tandare.

MUHIMU: wATANZANIA tunapenda kushabikia mambo bila kuyachunguza na sasa tusubiri tuone jinsi hii mipango 2 isivyo na tija bali danganya toto.

Ndugu upo sawa kabisa. Hata kama mipango mingine inakuja, huu usingetakiwa uwe mpango wa haraka. uliyasema hapo kuboresha njia zingine za pembeni ingesaidia sana. Flyovers sio nzuri sana kupunguza msongamano kutokana na Dar jinsi ililivyokaa, tatizo la flyovers itaongeza kasi kubwa magari kuongezeka mjini kabla mengine hayajafikiria kutoka, kwahiyo msongamano maeneo ya mjini unaweza kuwa mkubwa zaidi. Tatizo letu kubwa Dar ni sehemu za makazi na ofisi kuwa sehemu moja, yaani watu wakiamka asubuhi wote wanaelekea sehemu moja na jioni baada ya kazi wote wanaelekea majumbani sehemu zinazofanana. Kuna baadhi ya ofisi naona zinahama taratibu maeneo ya mijini lakini bado kuna zingine zinaongezeka na kujengwa. Kama kungekuwa na utaratibu wa kutawanya sehemu za kazi na ofisi kwa ratio nzuri foleni za magari zingeisha kabisa.
 
myhem, Kuokoa muda kwa kinanani (wakazi wa wapi) Tegeta, Kinondoni, Tandale........ au wapi? Unajennga hoja kitoto sana mkuu!! Ebu tutajie maeneo ambayo treni hizo zinapiata.

sasa mbona hata wewe mwenyewe unajichanganya? ina maana kina mwakyembe hawana akili timamu mpaka wafikirie kupunguza foleni wakati wakijua kabisa kuwa hizo treni zinakava sehemu ndogo sana ya jiji? hayo ya kupunguza foleni mawazo yako wewe na usiwabambikie mawaziri wetu wachapakazi.mkakati wa kupunguza foleni upo na sio mdogo kama huu wa matumizi ya treni.

Usione aibu kukiri kuwa umechemka katika hili na utuombe radhi kwa kutaka kutupotosha hapa jamvini.
 
aisee! makundi CCM yatawamaliza, heading na unachoandika havina ushirikiano kabisa,
sijui hata unachokusudia.............punguza mhemko ndugu.

Mimi pia naona mwajembe anakwepa lile jukumu kubwa la kurejesha reli ya kati ili isafirishe mizigo toka bandarini hadi mwanza na kigoma na kuyaondoa magari yote ya mafisadi yaliyohujumu usafiri wa reli na huku ya kiharibu barabara zetu! Hakuna nchi duniani iliyoua usafiri wa reli na kuanza kutumia reli hiyo eti kupunguzia foreni mjini! Mimi nadhani hata majirani wakitusikia eti mizigo mikubwa inasafiri kwenda mwanza na hata nchi za jirani kwa malori halafu train tunaitumia kupeleka watu mjini watatucheka na kutuona akili yetu ni fupi sana!

Mwajembe ashughulikia mambo ya msingi ya kufufua usafirishaji wa reli ya kati na kuboresha bandari haya ya jam za Dar yanatatulika ikiwa serikali ikiamua kuweka mabasi makubwa na kupiga marufuku vipanya,bajaji,pikipiki na kuweka kodi ya maegesho itakayo discourage matumizi ya magari binafisi!
 
Lengo la treni ni kupunguza adha kwa walala hoi hasa nyakati za asubuhi na jioni na kuhusu msongamano wa magari tatizo ni miundo mbinu na wala si kwamba eti magari ni mengi sisi Tanzania hatujafikia uwiano wa nyumba moja kwa gari moja wananchi wengi wa Tanzania hawana magari mfano pita mitaani tunapoishi angalia wanaomiliki magari na wasio miliki magari wengi ni wepi?
Mkuu, unalosema ni sawa. Sasa treni itafika kila sehemu? Unajua moja ya mapungufu ya reli hasa hizi zetu zenye poor technology? Is poor accessibility, lkn ujue kuwa haitapunguza foleni na haitafika mahala pote kama magari!!!!!
 
Me nafkiri sababu ya kuleta treni na mabasi yaendayo kasi ni pamoja na kupunguza msongamano wa abiria kugombania usafiri mda wa asubuh na jion had usiku, ndio maana hata ratiba ya treni iko mida hiyo, kwa hiyo pongezi kwa Mh.Mwakyembe zipo palepale, ngoja tusubiri na hizo basi
 
Ndugu upo sawa kabisa. Hata kama mipango mingine inakuja, huu usingetakiwa uwe mpango wa haraka. uliyasema hapo kuboresha njia zingine za pembeni ingesaidia sana. Flyovers sio nzuri sana kupunguza msongamano kutokana na Dar jinsi ililivyokaa, tatizo la flyovers itaongeza kasi kubwa magari kuongezeka mjini kabla mengine hayajafikiria kutoka, kwahiyo msongamano maeneo ya mjini unaweza kuwa mkubwa zaidi. Tatizo letu kubwa Dar ni sehemu za makazi na ofisi kuwa sehemu moja, yaani watu wakiamka asubuhi wote wanaelekea sehemu moja na jioni baada ya kazi wote wanaelekea majumbani sehemu zinazofanana. Kuna baadhi ya ofisi naona zinahama taratibu maeneo ya mijini lakini bado kuna zingine zinaongezeka na kujengwa. Kama kungekuwa na utaratibu wa kutawanya sehemu za kazi na ofisi kwa ratio nzuri foleni za magari zingeisha kabisa.

Thanks mkuu kwakuongeza plan nyingine ya kupunguza msongamano. Nadhani hapa watu kwenye jukwaa hili wako biased sana. Treni si suluhisho la foleni Dar. Hawa madaktari 2 WALITAKIWA kuwaza kiPHD zaidi kuliko kukurupuka.
 
Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona Watanzania wanashabikia matukio haya mawili la Basi ziendazo Kasi BRT
(BRT) na uzinduzi wa
Reli kwa Jiji la Dar es Salaam. Mipango hii yote inaongozwa na watu wanaojitambulisha kuwa kuwa wachapa kazi kina Magufuli na Mwakyembe.
Ukweli kwamba ni danganya toto kwa sababu zifuatazo:

1. Tatizo la msongamano wa magari halisababishwi na kuwepo kwa gari za abiria ( public transport) bali ni private cars na maroli.
2. Msongamano huu unaletwa na kwenye junctions( nodes) mf. Ubungo mataa, Shekilango, Njia panda ya Tabata, Buguruni, Magomeni Mapipa,......
na suluhisho ni fly overs.
3. Reli hizi zinaishia pafupi sana na haziondoi au kuzuia watu binafsi kwenda na magari yao.
4. Hakuna parking Dar na watu wengi hubakia barabarani wakizunguka wkt wengine walionao wanafanya issue zilizowaletra mjini.
5. Upanuaji Barabara haupunguzi foleni bali hupunguza urefu wake na kutengeneza foleni fupi yenye mistari mingi ya magari mf. barabara ya Mwenge to Ubungo kupita Mcity.
kwa msisitizo zaidi ni sawa na kuweka maji kwnye mrija wa kunywea soda ukajaa alafu na mengine ukajaza beseni na mtoto akaulizwa maji mengi yako wapi naye akachagua mrija kisa umezidi beseni kwaurefu.

Sasa hela kubwa inayotumika kutengeneza barabara za BRT na Reli ingefanya yafuatayo kama si ufisadi:
  1. kutengeneza barabara zote mbovu za kupunguza msongamano kwemye Barabara ya Moro kwa kiwango cha lami ili kupunguza kufurika kwa magari Morogoro road mf. Barabara ya Kimara na Mbezi to Uwanja wa Ndege, Kimara na Mbezi to Tegeta........
  2. kuwekeza kwenye Fly Overs kwenye mataa yote.
  3. kuboresha na kupanua barabara hasa vituo amabvyo viko barabarani hasa mf. njia ya Tandare.

MUHIMU: wATANZANIA tunapenda kushabikia mambo bila kuyachunguza na sasa tusubiri tuone jinsi hii mipango 2 isivyo na tija bali danganya toto.
Mkuu suala la mass transport siyo siasa na nafikiri umeandika terminologies ambazo hata matumizi yake huyajui.

Kufikiria kuwa tatizo la ques katika jiji la DSM linasababishwa tu na junctions ni upuuzi usio na kifani.Na je hiyo que ikifika kule inakoelekea nini mwisho wake?

Tatizo kubwa la watanzania walio wengi ni kujitia kujua kila kitu pamoja na ufinyu wa uelewa wa field yenyewe.

Mass transport ni pamoja na kupunguza matumizi ya usafiri binafsi, kwa hiyo kupunguza magari barabarani.
Ni ukweli usiopingika kuwa katika miji mikubwa yote duniani usafiri wa umma unapokuwa efficient watu wanaacha magari yao nyumbani.
na ndio maana utakuta vrhicle density ni ndogo hata katika miji mikubwa sana, matumizi ya magari binafsi yanapungua sana.

Uelewa finyu unakandamiza hata presentation yako kwa kulazimisha au kupindisha hiyo mada yako kuwa ni ufisadi.
if anything nenda ukasome hata certificate ya vijana wa form IV pale Chuo cha Usafirishaji ili ujiondoe kutu ya kutoelewa kitu katika mada husika.
 
Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona Watanzania wanashabikia matukio haya mawili la Basi ziendazo Kasi BRT
(BRT) na uzinduzi wa
Reli kwa Jiji la Dar es Salaam. Mipango hii yote inaongozwa na watu wanaojitambulisha kuwa kuwa wachapa kazi kina Magufuli na Mwakyembe.
Ukweli kwamba ni danganya toto
kwa sababu zifuatazo:

1. Tatizo la msongamano wa magari halisababishwi na kuwepo kwa gari za abiria ( public transport) bali ni private cars na maroli.
2. Msongamano huu unaletwa na kwenye junctions( nodes) mf. Ubungo mataa, Shekilango, Njia panda ya Tabata, Buguruni, Magomeni Mapipa,......
na suluhisho ni fly overs.
3. Reli hizi zinaishia pafupi sana na haziondoi au kuzuia watu binafsi kwenda na magari yao.
4. Hakuna parking Dar na watu wengi hubakia barabarani wakizunguka wkt wengine walionao wanafanya issue zilizowaletra mjini.
5. Upanuaji Barabara haupunguzi foleni bali hupunguza urefu wake na kutengeneza foleni fupi yenye mistari mingi ya magari mf. barabara ya Mwenge to Ubungo kupita Mcity.
kwa msisitizo zaidi ni sawa na kuweka maji kwnye mrija wa kunywea soda ukajaa alafu na mengine ukajaza beseni na mtoto akaulizwa maji mengi yako wapi naye akachagua mrija kisa umezidi beseni kwaurefu.

Sasa hela kubwa inayotumika kutengeneza barabara za BRT na Reli ingefanya yafuatayo kama si ufisadi:
  1. kutengeneza barabara zote mbovu za kupunguza msongamano kwemye Barabara ya Moro kwa kiwango cha lami ili kupunguza kufurika kwa magari Morogoro road mf. Barabara ya Kimara na Mbezi to Uwanja wa Ndege, Kimara na Mbezi to Tegeta........
  2. kuwekeza kwenye Fly Overs kwenye mataa yote.
  3. kuboresha na kupanua barabara hasa vituo amabvyo viko barabarani hasa mf. njia ya Tandare.

MUHIMU: wATANZANIA tunapenda kushabikia mambo bila kuyachunguza na sasa tusubiri tuone jinsi hii mipango 2 isivyo na tija bali danganya toto.

Na wewe ni walewale msioona hata jambo zuri ambao kila kukicha ni kulalama tu utadhani hata kwenye familia yako unatimiza wajibu na majukumu yako sawasawa, mi nilidhani kama kweli wewe ungelikuwa muungwana; japo huoni jitihada zozote za kulipatia ufumbuzi tatizo la foleni walau ungeanza hata kwa kupongeza jitihada za upanuzi wa barabara, Eti watanzania wanapenda kushabikia...

Usiwe na mpapatiko wa moyo, nyie ndo huwa mnasubiri ama kuombea mtu aharibikiwe ndo mcheke na kusema mambo kibao!! kuondoa watu elfu moja karibu na mia tano kwenye ruti za kila siku za barabarani na kuwapitisha kwenye reli unaona ni kitu kidogo? Fly overs sawa lakini unaanzia wapi kwanza? wewe mbona una hisia za kusukuma gari ukiwa umelipanda? ni laziama uwe na pa kuanzia,achana na ujinga wa kukatisha watu tamaa hata kwa juhudi thabiti zinazooonekana bayana!

Mabasi yaendayo kasi yataleta ushindani wa kibiashara hata kama hawatazuia wasafirishaji binafsi, mwisho wa siku watayapunguza magari yao kama si kuyaondoa kabisa barabarani maana kila mtu atahitaji kuwahi kazi zake hawezi kusubiri gari ambalo lina vituo lukuki.

Hapo kwenye Bluu ndo umenidhihilishia una roho ya kwanini, kumbe suala hapa si Reli au mabasi yaendayo kasi bali unaumizwa na umaarufu na utendaji unaokubalika na wengi wa hao mawaziri wawili, chuki zingine ni za kijinga, unajieleza undani wako bila kutambua YAMTOKAYO MTU KINYWANI NDIYO YAUJAZAYO MOYO WAKE!! SHAME ON YOU...
 
Hujaelewa hoja hapa. Hizo gari moshi zina route ngapi mpaka uamini hara kwamba zimepunguza msongamano?
Nadani huja soma posit nzima na hujafanya utafiti lkn kwanini hela iliyotumika hapo isiboreshe barabara kwanza? naseama hivyo kwakujua na kuwa na uhakika kuwa Reli kwa Tanzania bado bado sana. Kama ya kati imetushinda itakuwaje hizi hapa????? Road Transport kwanza.

labda jamaa yangu hujaelewa lengo la hizo treni ni watu badala ya kuhamka saa kumi na moja kwenda kazini na ktumia muda mrefu baada ya kazi kurejea nyumbani watatumia muda mfupi kwa maana ukitoka huko mbezi na kibamba na kupanda treni baada ya dakika kumi upo posta ama unatoka kazini saa kumi na moja ifikapo saa kumi na moja na nusu upo ubungo
 
Mimi pia naona mwajembe anakwepa lile jukumu kubwa la kurejesha reli ya kati ili isafirishe mizigo toka bandarini hadi mwanza na kigoma na kuyaondoa magari yote ya mafisadi yaliyohujumu usafiri wa reli na huku ya kiharibu barabara zetu! Hakuna nchi duniani iliyoua usafiri wa reli na kuanza kutumia reli hiyo eti kupunguzia foreni mjini! Mimi nadhani hata majirani wakitusikia eti mizigo mikubwa inasafiri kwenda mwanza na hata nchi za jirani kwa malori halafu train tunaitumia kupeleka watu mjini watatucheka na kutuona akili yetu ni fupi sana!

Mwajembe ashughulikia mambo ya msingi ya kufufua usafirishaji wa reli ya kati na kuboresha bandari haya ya jam za Dar yanatatulika ikiwa serikali ikiamua kuweka mabasi makubwa na kupiga marufuku vipanya,bajaji,pikipiki na kuweka kodi ya maegesho itakayo discourage matumizi ya magari binafisi!

Huyu jamaa uliyemnukuu kaka nadhanindo walewale wanaomaliza University wakiwa hawajui kusoma na kuandika!!!!! Hivi kweli Reli ni suluhu ya MSONGAMANO Dar??????? Sasa kama Issue ni kusaidia wanyonge watu wote waende zilipoanzishwa Reli??? Mwakyembe afanye moja, ashughurikie bandari na Reli ya kati na Tazara. Sio lazima kuwa na reli kama usafiri mkuu ila hapa kwanini kila usafiri shida na jamaa anakuja na weak point ya Reli kwa Dar????? Soma hapa List of countries by rail transport network size - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Hii ya treni ni hatua nzuri kwa kuanzia. Then zije hizo brt na flyovers. Kwa kuwa una wivu na Mwakyembe na Magufuli, washauri wajenge kivuko kutoka kunduchi na kuja ferry. Hapo kunduchi waweke ample parking ili tiache magari yetu kwenye usalama na tupande speed boat kuja town. Hamna haja ya mtu wa bunju kudrive kila siku kuja city centre.
maendeleo yanakuja kwa hatua mkuu.

Au wewe ni mwenyekiti wa CHAUMMA?
 
Mkuu, unalosema ni sawa. Sasa treni itafika kila sehemu? Unajua moja ya mapungufu ya reli hasa hizi zetu zenye poor technology? Is poor accessibility, lkn ujue kuwa haitapunguza foleni na haitafika mahala pote kama magari!!!!!

Tupo pamoja Mkuu, na nakubaliana wewe kwenye suala la technology ya hizi treni ni poor pia na accessibility nayo ni poor maana hizi route ambazo treni inapita zilikuwa designed kwa kazi nyingine na serikali inatakiwa kujenga njia za reli sambamba na njia za magari ili kuwe na good accessibility
 
Mkuu suala la mass transport siyo siasa na nafikiri umeandika terminologies ambazo hata matumizi yake huyajui.

Kufikiria kuwa tatizo la ques katika jiji la DSM linasababishwa tu na junctions ni upuuzi usio na kifani.Na je hiyo que ikifika kule inakoelekea nini mwisho wake?

Tatizo kubwa la watanzania walio wengi ni kujitia kujua kila kitu pamoja na ufinyu wa uelewa wa field yenyewe.

Mass transport ni pamoja na kupunguza matumizi ya usafiri binafsi, kwa hiyo kupunguza magari barabarani.
Ni ukweli usiopingika kuwa katika miji mikubwa yote duniani usafiri wa umma unapokuwa efficient watu wanaacha magari yao nyumbani.
na ndio maana utakuta vrhicle density ni ndogo hata katika miji mikubwa sana, matumizi ya magari binafsi yanapungua sana.

Uelewa finyu unakandamiza hata presentation yako kwa kulazimisha au kupindisha hiyo mada yako kuwa ni ufisadi.
if anything nenda ukasome hata certificate ya vijana wa form IV pale Chuo cha Usafirishaji ili ujiondoe kutu ya kutoelewa kitu katika mada husika.

Sasa Ebu kwa mtaalam ambaye si Mtazania na anayefikria vizuri msomi utuambie jinsi Reli zilizoanzishwa zitakavyo discourage watu kutumia private transport. Uje kwa mifano dhahiri!!!!!!!! MF. Foleni toka Kibamba mpaka Ubungo, Mwenge mpaka Tegeta...... wakt Reli iko mabibo mpaka posta......
 
We unaitwa nani vilee ....kijota aaah kijoti aaa sorry kumbe kijoka! Naonekana una wivu sana na hapa umetumwa kuwachafua hawa makamanda, acha njaa itakuuweka pabaya
 
Back
Top Bottom