DART BRT Mwendo kasi “Failure before start project “

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
875
545
DART BRT aka Mradi wa mabasi yaendayo kasi “ A failure before start project “.

Niiloandika haya 2016 wakati wa kuanza tu kwa mradi huo Na kweli imekuwa kweli BRT umefeli kabla ya kuanza Na umekuwa ni disaster.

Mradi wa mabasi ya kwenda kasi aka DART or BRT una awamu 6 . Awamu ya kwanza mkopo Kutoka World Bank wa 180M Euro , Mradi was 2016-19 uliojenga km 21 za miundo wa Barabara za mabasi ya Mwendo kasi zilizotubadilishia miundo mbinu Na kutuacha Na barabara ya hovyo kabisa kuwahi kutokea toka Kimara mpaka Kivikoni, Katiakoo Na sinza Dar es Salaam zilizojengwa Na Strabag.

Awamu ya Pili Mkopo wa ADFB wa 160M USD wa Km 20.3 Toka Mbagara mpaka posta , Mradi wa 2016-2020 .. ambao hata sijui unajengwa Na nani Na lini utakamilika , ameharibu kabisa muundo mbinu ya barabara Na kuwa acha wakazi wa maeneo hayo kutaabika kwa foleni zisizo Na maana .

Malengo ya BRT or DART or Mwendo kazi yalikuwa yafuatayo:
1. kuweka miundo mbinu ya kurahisisha Na kupunguza muda wa wasafiri kufanya shughuli zao toka Dk 120 kwa safari mpaka Dk 25.
2. Kupunguza Gharama za Usafiri kwa abiria toka 1800 Tshs kwa safari mpaka Tshs 650 kwa safari .
3. kuondoa msongamano wa magari barabarani kwa kuweka mabasi , Ambapo basi moja lingeweza kuondoa Daladala 20 barabarani.

Je Mradi umefanikiwa? Total Hapana .. Hapana Kubwa .. Mradi umeleta balaa zaidi Na kuletea watanzania wanyonge Umasikini, kuachelewesha makazinj Na haukuzingatia miundo mbinu yetu Na tabia zetu hivyo kuleta foleni zisizo za lazima , ajali Na hata kuchelewesha magari madogo kwa faida ya Mwendo kasi.

Yafuatayo ni baadhi tu ya mapungufu yanayofanya Mradi kifeli
1. Gharama za nauli hazijazingatia kuwa wakazi wengi almost 80% wa Dar es Salaam wana kipato cha Chini ya 1.5$ per day ( 3500 ) Na hivyo kuwachukulia almost 2000 kwenye Nauli ya trip 3 ni kuwachukulia kipato chao chore cha siku .. Mradi umewaacha watanzania wengi kwenye lindi la Umasikini. Kumbuka kuwa watu Hawa wangetumia 1200 kwa Daladala kwa safari hizo kama zisingetolewa.

2. Kwa sasa kutokana na uchakavu Na Uchache wa mabasi abiria wanakaa vituoni kati ya Dk 30-60 kusubiri mabasi hivyo bado safari zao zina tumia kati ya Dk 90-120 wakati wa rush hour , hivyo Lengo la kupunguza muda kutofikiwa. kumbuka Dala Dala zilikuwa zina tumia muda huo sio kutokana na wingi wao bali ufinyu wa barabara kipindi hicho , Kama Dala Dala zingekuwa zimejengewa barabara yake zingetumia muda mchache zaidi chini ya 30 minutes .

3. Mradi umeleta usumbufu kwa wenye magari mengine , Kwanza kwa barabara nyembamba , Pili kwa kona zisizo za lazima Na tatu kwa kutokuwa rafiki kwa barabara za kuchepuka.. the total design is the mess.

4. Mradi pia umekuwa usumbufu wa abiria kwa kuwekewa vituo kati kati Na kulazimika Kuvuta barabara Na pia usalama kwenye vituo bado ni changamoto .

5. Kutukuwepo kwa mabasi muda mwingine Na kupelekea abiria kuwa stranded vituo I.

6. Ujenzi wake kama wa mbagara Posta kuchukua muda mrefu Na kuwa keto kwa watumiaji wa barabara.

Adjustments.JPG
 
Mimi nachukia honi zao wanapiga kama wapumbavu vile... yaani ni kero... sijui madereva wao huwa ni mavuta bange... wajue kuwa maeneo wanayopiga honi kuna binadamu na watoto wanaishi wajue wanasumbua mno... na wanavyoendelea hakika tutawachoka....
 
Kama huo mradi wq mbagala sijui utaisha lini....na imekuwa kero kubwa ya foleni kuanzia hapo mbagala misheni kwenda rangi tatu..

Napata mashaka kama hakuna upigaji kwenye hii miradi.. Phase 1 Gharama ni almost 24B Tzs kwa km Na huu wa Phase two wa Mbagara ni Karibu 18.5B tzs kwa km ...

Lakini ukiangalia ujenzi wa Phase two ya Mbagara ulivyo wa hivyo , Huwezi ku AMINI kuwa Mradi huu ni mkopo wa AFDB ...
 
Umefanya uchambuzi mzuri, inasikitiaha kuona mradi ukiwa katika ilivyosasa.
 
Binafsi naona mradi ulijengwa wakati sahihi(kulingana na uhitaji wetu), ila haukujengwa kwa usahihi(nakuunga mkono). Sababu:
1. Barabara ni finyu sana.
2. Hakuna umadhubuti(barabara kuwa na nyufa nyingi). Imechakaa kabla ya wakati.

Kuhusu uchache wa mabasi, nadhani ni kosa la viongozi wetu upande wa mikataba na kampuni inayoendesha huo mradi. Mfano, ilibidi angalau kuwe na terms zinazombana muendesha mradi kuwa 90% ya magari yanatakiwa yawe barabarani. Au kuwe na system inayoruhusu gari kukaa kituoni kwa muda fulani, baada ya hapo gari iondoke. N.k.

Kwa ile phase 2,
Kama mikataba inaruhusu, ni bora akapewa mwingine kuona kama ataweza kutatua changamoto anazozileta UDART kwa wateja wake.
 
Hiyo phase II naona jamaa wanajenga zile stations kwa tofali (zege wanalaza juu kama jamvi) na sio zege mwanzo mwisho kama phase I...
 
DART BRT aka Mradi wa mabasi yaendayo kasi “ A failure before start project “.

Niiloandika haya 2016 wakati wa kuanza tu kwa mradi huo Na kweli imekuwa kweli BRT umefeli kabla ya kuanza Na umekuwa ni disaster.

Mradi wa mabasi ya kwenda kasi aka DART or BRT una awamu 6 . Awamu ya kwanza mkopo Kutoka World Bank wa 180M Euro , Mradi was 2016-19 uliojenga km 21 za miundo wa Barabara za mabasi ya Mwendo kasi zilizotubadilishia miundo mbinu Na kutuacha Na barabara ya hovyo kabisa kuwahi kutokea toka Kimara mpaka Kivikoni, Katiakoo Na sinza Dar es Salaam zilizojengwa Na Strabag.

Awamu ya Pili Mkopo wa ADFB wa 160M USD wa Km 20.3 Toka Mbagara mpaka posta , Mradi wa 2016-2020 .. ambao hata sijui unajengwa Na nani Na lini utakamilika , ameharibu kabisa muundo mbinu ya barabara Na kuwa acha wakazi wa maeneo hayo kutaabika kwa foleni zisizo Na maana .

Malengo ya BRT or DART or Mwendo kazi yalikuwa yafuatayo:
1. kuweka miundo mbinu ya kurahisisha Na kupunguza muda wa wasafiri kufanya shughuli zao toka Dk 120 kwa safari mpaka Dk 25.
2. Kupunguza Gharama za Usafiri kwa abiria toka 1800 Tshs kwa safari mpaka Tshs 650 kwa safari .
3. kuondoa msongamano wa magari barabarani kwa kuweka mabasi , Ambapo basi moja lingeweza kuondoa Daladala 20 barabarani.

Je Mradi umefanikiwa? Total Hapana .. Hapana Kubwa .. Mradi umeleta balaa zaidi Na kuletea watanzania wanyonge Umasikini, kuachelewesha makazinj Na haukuzingatia miundo mbinu yetu Na tabia zetu hivyo kuleta foleni zisizo za lazima , ajali Na hata kuchelewesha magari madogo kwa faida ya Mwendo kasi.

Yafuatayo ni baadhi tu ya mapungufu yanayofanya Mradi kifeli
1. Gharama za nauli hazijazingatia kuwa wakazi wengi almost 80% wa Dar es Salaam wana kipato cha Chini ya 1.5$ per day ( 3500 ) Na hivyo kuwachukulia almost 2000 kwenye Nauli ya trip 3 ni kuwachukulia kipato chao chore cha siku .. Mradi umewaacha watanzania wengi kwenye lindi la Umasikini. Kumbuka kuwa watu Hawa wangetumia 1200 kwa Daladala kwa safari hizo kama zisingetolewa.

2. Kwa sasa kutokana na uchakavu Na Uchache wa mabasi abiria wanakaa vituoni kati ya Dk 30-60 kusubiri mabasi hivyo bado safari zao zina tumia kati ya Dk 90-120 wakati wa rush hour , hivyo Lengo la kupunguza muda kutofikiwa. kumbuka Dala Dala zilikuwa zina tumia muda huo sio kutokana na wingi wao bali ufinyu wa barabara kipindi hicho , Kama Dala Dala zingekuwa zimejengewa barabara yake zingetumia muda mchache zaidi chini ya 30 minutes .

3. Mradi umeleta usumbufu kwa wenye magari mengine , Kwanza kwa barabara nyembamba , Pili kwa kona zisizo za lazima Na tatu kwa kutokuwa rafiki kwa barabara za kuchepuka.. the total design is the mess.

4. Mradi pia umekuwa usumbufu wa abiria kwa kuwekewa vituo kati kati Na kulazimika Kuvuta barabara Na pia usalama kwenye vituo bado ni changamoto .

5. Kutukuwepo kwa mabasi muda mwingine Na kupelekea abiria kuwa stranded vituo I.

6. Ujenzi wake kama wa mbagara Posta kuchukua muda mrefu Na kuwa keto kwa watumiaji wa barabara.

View attachment 1679758

Unatoa ushauri gani?
 
Ni ngumu kuona tija ya mwendo kasi kwa sasa only kwa sababu unajengwa kwa phases subiri mpaka zitakapokamilika zote 6 utakapoona makosa basi ,

Phase 1 - WB
kimara - Kivukoni - kariakoo - morocco (imeisha),

Phase 2 - AFDB
Mbagala - kariakoo (gerezani) (unaendelea) ,

Phase 3 - WB
Azikiwe/Maktaba (Posta) - gombo la moto, kipande cha kariakoo - buguruni - Tazara (utaanza karibuni)

Phase 4 - WB
Posta (maktaba junction) - morocco- mwenge - ubungo (kipande cha fly over kimeshajengwa), mwenge - bunju

Phase 5 -
mandela road- kigogo - ubungo (inaunga na BRT 4 mwenge - Ubungo), kigogo - Tabata Segerea

Phase 6
inaweza kupita old bagamoyo road, na vipande vipande vya kuziba

Ni mapema sana Kuuita Mradi wa BRT failure project, kwa sababu haujakamilika
 
Huo mradi kwa magonjwa ya mlipuko ni hatari watu ni wengi mno na mabasi ni machache.

Na hawarekebishi hilo tatizo lipo siku zote.

Kuna mambo huwa yanashangaza Sana kwakweli.

Sijui kwanini watanzania tunapenda kuishi maisha ya tabu kila siku.

Yaani mpaka mtu akukanyage shingoni ndio anajisikia kua kapanda basi, Bila hivyo haoni raha kabisa.
 
Ni ngumu kuona tija ya mwendo kasi kwa sasa only kwa sababu unajengwa kwa phases subiri mpaka zitakapokamilika zote 6 utakapoona makosa basi ,

Phase 1 - WB
kimara - Kivukoni - kariakoo - morocco (imeisha),

Phase 2 - AFDB
Mbagala - kariakoo (gerezani) (unaendelea) ,

Phase 3 - WB
Azikiwe/Maktaba (Posta) - gombo la moto, kipande cha kariakoo - buguruni - Tazara (utaanza karibuni)

Phase 4 - WB
Posta (maktaba junction) - morocco- mwenge - ubungo (kipande cha fly over kimeshajengwa), mwenge - bunju

Phase 5 -
mandela road- kigogo - ubungo (inaunga na BRT 4 mwenge - Ubungo), kigogo - Tabata Segerea

Phase 6
inaweza kupita old bagamoyo road, na vipande vipande vya kuziba

Ni mapema sana Kuuita Mradi wa BRT failure project, kwa sababu haujakamilika

Hatuwezi kuona tija yoyote maana phase 2 Na zina kuja si arudi a makosa yake yake ya phase 1 .. ni Mwendo wa copy and paste
 
Ni ngumu kuona tija ya mwendo kasi kwa sasa only kwa sababu unajengwa kwa phases subiri mpaka zitakapokamilika zote 6 utakapoona makosa basi ,

Phase 1 - WB
kimara - Kivukoni - kariakoo - morocco (imeisha),

Phase 2 - AFDB
Mbagala - kariakoo (gerezani) (unaendelea) ,

Phase 3 - WB
Azikiwe/Maktaba (Posta) - gombo la moto, kipande cha kariakoo - buguruni - Tazara (utaanza karibuni)

Phase 4 - WB
Posta (maktaba junction) - morocco- mwenge - ubungo (kipande cha fly over kimeshajengwa), mwenge - bunju

Phase 5 -
mandela road- kigogo - ubungo (inaunga na BRT 4 mwenge - Ubungo), kigogo - Tabata Segerea

Phase 6
inaweza kupita old bagamoyo road, na vipande vipande vya kuziba

Ni mapema sana Kuuita Mradi wa BRT failure project, kwa sababu haujakamilika
Nakubaliana na wewe. Phase 1 kwa mfano, mwendesha mradi alikwa ni wa muda tu, na hivyo yalikuwa mabasi 140.

Mwendesha mradi mwingine kasha patikana. Na kasign mkataba wa miaka 12.

Natayari kasha toa order ya mabasi 305 ya kutumika kwenye njia ya phase 1 pekee. Ambapo anapokea mradi kabla ya mwezi wa tano.

Phase 2 itakuwa na mabasi 372 na phase 3 itakuwa na mabasi zaidi ya 400.

Hii inamaana, baada ya muda, tutaanza kuona matunda ya huu mradi.

Matarajio yangu, hayo mabasi mapya yawe ya mfumo wa gesi. Hii itawezesha kupunguza gharama ya nauli na ikiwezekana kutumia mfumo wa AC ndani ya basi, maana kwa joto la Dar, AC ni kitu cha msingi.
 
Kwenye matumizi ya Ac sawa
Lakini kwa mjazano ule kutumia ac ngumu
Ac zitafeli

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Naona unatafuta ligi
Ila ukweli mradi umefeli wameshindwa kuendesha
Sasa huko mbagala itakuwaje?

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app

Sitafuti ligi, inajulikana kweli mradi una matatitizo lakini suluhu ni nini?

Matatizo yakijadiliwa na ushauri huwa inakua changamoto zinazotekelezeka zaidi ya malalamiko na lawama zisizo na suluhu
 
Back
Top Bottom