Kama MWAKYEMBE na MAGUFULI wanafanya uhuni huu basi CCM imedhamiria kuwazika Watanzania!!!

Nilipokusoma kwenye hizo quotes hao juu........NIKAJUA umevamia FANI za watu......na hata kama wewe upo kwenye fani hiyo basi........experience yako ni ndogo.......halafu usijidanganye ukifikir maamuzi wanayofanya Mwakyembe na Magufuli ni ya kwao binafsi.........kwa taarifa yako.....wameshauriwa na wataalamu waliopo kwenye Wizara zao............

Nevertheless.....Nakupongeza kwa kuwa Umejaribu!!.............BTW....hizi fani zina wenyewe aisee........wapi Morani75 .....wapi Fundi Mchundo ....
 
kwa hili la reli tupongeze kwa dhati kabisa kelele zisizochoka za chadema kuisukuma serikali hii Vivu ya ccm na kikwete hadi kimeelewka.
 
Hujaelewa hoja hapa. Hizo gari moshi zina route ngapi mpaka uamini hara kwamba zimepunguza msongamano?
Nadani huja soma posit nzima na hujafanya utafiti lkn kwanini hela iliyotumika hapo isiboreshe barabara kwanza? naseama hivyo kwakujua na kuwa na uhakika kuwa Reli kwa Tanzania bado bado sana. Kama ya kati imetushinda itakuwaje hizi hapa????? Road Transport kwanza.

Mkuu naona umechanganya. Reli ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi na Barabara zipo chini ya Wizara ya Ujenzi na kila moja ina bajeti yake serikalini. Huwezi kuhamisha pesa za kukarabati reli toka wizara ya Uchukuzi kuzipeleka Wizara ya Ujenzi eti wakajengee Flyovers au Feeder roads. Kila mmoja anajaribu kuangalia kwa upande wake ni jinsi gani anapambana na tatizo hili la Usafiri/ foleni jijini.
Pakusifu, Sifu.
 
Mkuu Paul Kijoka naona dhamira yako ni nzuri na kuna baadhi ya vitu umetaja vina pointi ila unasahau kitu kimoja. Hoja yako kuu imeelemea kwenye swala la kupunguza foleni ya magari wakati lengo kuu ya hii miradi miwili ni kuwapa unafuu na kuleta usafiri mbadala kwa walio wengi (wapanda daladala) yaani commuters na zaidi wakati wa peak hours. Na hii ndio hali iliyopo kwenye nchi zote zilizoendelea kuna systems za mass transportation ambazo watu wanakuwa wanasafiri kwa amani na si kubanana na kukatishwa safari kama ilivyo sasa kwa daladala bongo.

Kwa wale wenye umri fulani watakumbuka Dar enzi za UDA kulikuwa na mabasi makubwa pamoja na Icarus zile ambazo zilikuwa more comfortable kuliko daladala za sasa na zilikuwa hazikatizi safari. Sasa kama hii miradi itasaidia kupunguza foleni ni bonus lakini lengo kuu ni kuwapa unafuu wasafiri wa mabasi.

Nakubaliana na wewe kuwa kwenye foleni moja ya ufumbuzi wake ni kujenga flyover na kuboresha feeder roads na hata kina Magufuli wanalijua hilo na naamini wanalifanyia kazi.

Kwa sasa tuwape ushirikiano kwenye hii miradi miwili na naamini itapunguza bughudha ya sisi wasafiri wa daladala.
 
Nilipokusoma kwenye hizo quotes hao juu........NIKAJUA umevamia FANI za watu......na hata kama wewe upo kwenye fani hiyo basi........experience yako ni ndogo.......halafu usijidanganye ukifikir maamuzi wanayofanya Mwakyembe na Magufuli ni ya kwao binafsi.........kwa taarifa yako.....wameshauriwa na wataalamu waliopo kwenye Wizara zao............

Nevertheless.....Nakupongeza kwa kuwa Umejaribu!!.............BTW....hizi fani zina wenyewe aisee........wapi Morani75 .....wapi Fundi Mchundo ....
Mkuu huyo jamaa ni MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI katika hiyo field anayiongelea.
Hajui kitu, na taabu kubwa ni kuwa hajui kuwa hajui kitu!
 
Duh! Kichwa cha habari na mada mbona haviendani. Hakuna uhuni hapo. Ulizotaja wewe ni changamoto. Mtoto akizaliwa si anaanza kwanza kukaa, kutambaa, kutembea mwisho anakimbia. Hizo route mbili ni mwanzo tu. Haiwezekani kuanza route zote kwani kuna gharama za kufufua mabehewa, route zenyewe, kulipa mafundi n.k. Hizo treni zitasaidia sana sisi wanyonge tunaopoteza masaa mawili kutoka nyumbani hadi mjini hata kama foleni hazitapungua tautawahi kazini. Ubaya wake uko wapi? Binafsi naona hii inastahili pongezi. Ila wana JF acheni kutukana katoa mawazo yake tumkosoe tu bila matusi.
 
Watu mmempaka sana Paul Kijoka, lakini katika undani na mantiki ya hoja yake alikuwa na hoja yenye kuhold water. Hebu someni tena uzi wake "critically" hafu muangalie kama kweli mmemtendea haki huyu kamanda. Hoja zenyewe ni hizi Mmemtendea haki kweli? Haya aloyasema hayana ukweli au umaana katika utekelezaji? guys, you must always think big and avoid being myopic. Siyo kumshambulia tu mtu bila hoja ya maana badala ya kupangua hoja kwa kutumia hoja!!!!
[/LIST]

Watu kama wewe JF mmebaki wachache sana. Kamanda Paul kaandika vizuri. Ila hakua sahihi kuwabeza akina Mwakyembe. Magufuli na Mwakyembe wamethubutu hawajaweza. Ila well done Mwakyembe na Magufuli.

Kuhusu parking mjini, hivi hakuna wakala au taasisi au chombo kinachoratibu ubora wa majengo? Kwanini majengo yajengwayo town, kariakoo nk hayana Parking?. Kweli tunahitaji mzungu aje atwambie hili?.

Hoja za Paul ni nzuri. Fly overs zinakuja ndugu Paul. Hoja zako zote zipo kwenye pipeline!. Hoja ya majengo yenye parking city center hamna kaka maana wala rushwa washakula rushwa!
 
Last edited by a moderator:
Hujui usemalo. Kama unajua, basi wewe roho ya korosho. Kama si roho ya korosho, wewe ni sadist. Kama si sadist, mradi wako wa dala dala unakufa na huna njia nyingine ya kupata pesa. Nakushauri ubuni mradi mwingine.

Hivi umewahi kutoka nje ta Tanzania ukaona wenzetu walivyopiga hatua katika matumizi ya public transport? Hata hivyo nakushukuru kwa kuonyesha matatizo ya watu waliokulia eneo moja tu la nchi au DSM.
 
we unatokea kundi gani mkuu?
maana hao uliowataja sidhani kama ni threat kwa kundi lolote la Urais.
 
Hizo treni mbili kati kati ya jiji hazina msaada wowote katika kutatua tatizo la msongamano wa magari Dar es salaam, watu wanashabikia na kumfanya mwakyembe popular bila sababu, ifanyike master planning mpya ya usafiri wa umma dar es salaam na suluhisho ni kuwa na trains za kwenda kasi na trams sio hayo mabehewa ya mwaka 1947

Nyamtoroka,

Unashauri ifanyike master plan mpya ya usafiri na hapo hapo unasema suluhisho ni treni za kwenda kasi na trams.

Wakati tunasubiri hizo treni na trams kuna ubaya gani kutumia mabehewa ya mwaka 1947???.
 
hujui usemalo. Kama unajua, basi wewe roho ya korosho. Kama si roho ya korosho, wewe ni sadist. Kama si sadist, mradi wako wa dala dala unakufa na huna njia nyingine ya kupata pesa. Nakushauri ubuni mradi mwingine.

Hivi umewahi kutoka nje ta tanzania ukaona wenzetu walivyopiga hatua katika matumizi ya public transport? hata hivyo nakushukuru kwa kuonyesha matatizo ya watu waliokulia eneo moja tu la nchi au dsm.



je ccm ni safi?
Je kuna aliye msafi ndani ya ccm?
 
Usafiri wa treni Tanzania na Mabasi yaendayo kasi ni vitu tulivotakiwa kuwa navyo miaka 30 iliyopita, huu ulikuwa uzembe wa serikali. Kwa wale wanachuo wanajua kama una mtihani amabao hujafanya ni lazima uclear kwanza ndo uendelee mbele.
 
Mkuu mbona hapa we ndo unajionesha ni muhuni ?

wanachofanya mwakyembe na magufuli ni kizuri na nawapongeza kwa jitihada zao kwani hii ni atua moja mbele.baada ya barabara kuwa nzuri ndiyo hatua nyingine itakuwa rahisi kuimplement. kwa sasa kama utasema upunguze magari binafsi yasiingie mjini maana yake ushakuwa umesovu tatizo moja ambalo ni puplic transport.

Kupunguza kuingia kwa wingi magari binafsi ni pamoja na kuongeza fee kwenye packing mfano wenzetu Zimbabwe packing fee mjini kwa saa ni dolari 1 kwa eneo la mita kumi ambapo ukihamisha gari yako kwenda nnje ya hizo mita utalipia tena,pia gari kuingi mjini linalipa dola 1 na kutoka dola moja, hali hii imesababisha kupungua magari binafsi mjini na kuufanya mji upendeze,pia hawana mama nitilie mijini hali inayopunguza watu wasio kuwa na umuhimu kwenda mijini.hali hii haiwezekani kwa sasa hapa tanzania mpanka miundominu yetu iboreshwe kama wanavyojitahidi mwakyembe na magufuli.hongereni sana
 
Du kwa jinsi ulivyo anza mada yako na kuhitimishi inaonyesha ushabiki fulani. Hivi uhuni wa waheshimiwa hao huko wapi,kama kilichofanyika na kinachofanyika ni ktk utekelezaji wa ahadi za serikali ktk kuboresha usafiri. Unaweza kuwa na hoja nzuri kwa viongozi lakini ni vema ktk kuileta na kuijenga uondoe kuongozwa na muhemuko zaidi ili uweze kujipatia fulsa ya utulivu na kujenga hoja yenye mashiko,ikiwa ni pamoja na kutambua kazi nzuri inayoonekana na kuipongeza napia kutoa changamoto ambazo unaziona ambazo kama zikishughulikiwa kulingana na mazingira yaliyopo itaongeza ufanisi. Lakini sio kuanza kwa kukejeri/kutukana mambo ambayo hayana msingi. 'uhuni' kwa viongozi hao sizani kama upo kama ulivyo eleza. Muhimu: viongozi wetu mtambue kuwa mna changamoto ya kuliongoza taifa hili ktk maendeleo na ktk mchakato huo si wananchi wenu wote pamoja na baadhi ya viongozi wenzenu watawaunga mkono. Kikubwa wakati wote mjitahidi kuwa makini na kuhakikisha mko ktk mstari unaotakiwa na taifa lenu na Mungu wenu atawapigania.
 
Sasa Kama yote Hayo Hayakuwepo sasa unategemea nani afanye nini? si Bora wamefikiria na kufanya kitu kinachoonekana!! Ila kwa hela za dart kama zingewekwa kwenye reli!! Dar ingekuwa kama ulaya!!
 
Hizo treni mbili kati kati ya jiji hazina msaada wowote katika kutatua tatizo la msongamano wa magari Dar es salaam, watu wanashabikia na kumfanya mwakyembe popular bila sababu, ifanyike master planning mpya ya usafiri wa umma dar es salaam na suluhisho ni kuwa na trains za kwenda kasi na trams sio hayo mabehewa ya mwaka 1947
Sure mkuu! Bado safari ya UKOMBOZI ni ndefu!!!! Hivi hivi ndivyo tunavyopata Rais kupitia CCM kwa hoja dhaifu sana tena toka kwa WASOMI!
 
Simple! Ndugu Paul Kijoka amka mapema uende pale ubungo maziwa ukawaeleweshe waTZ wenzio ndani ya treni au wanaosubiri treni kwamba hicho "WANACHOSHABIKIA" ni "UHUNI". Then uje utupe majibu!
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom