Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 255
- Thread starter
- #41
Na wewe ni walewale msioona hata jambo zuri ambao kila kukicha ni kulalama tu utadhani hata kwenye familia yako unatimiza wajibu na majukumu yako sawasawa, mi nilidhani kama kweli wewe ungelikuwa muungwana; japo huoni jitihada zozote za kulipatia ufumbuzi tatizo la foleni walau ungeanza hata kwa kupongeza jitihada za upanuzi wa barabara, Eti watanzania wanapenda kushabikia...
Usiwe na mpapatiko wa moyo, nyie ndo huwa mnasubiri ama kuombea mtu aharibikiwe ndo mcheke na kusema mambo kibao!! kuondoa watu elfu moja karibu na mia tano kwenye ruti za kila siku za barabarani na kuwapitisha kwenye reli unaona ni kitu kidogo? Fly overs sawa lakini unaanzia wapi kwanza? wewe mbona una hisia za kusukuma gari ukiwa umelipanda? ni laziama uwe na pa kuanzia,achana na ujinga wa kukatisha watu tamaa hata kwa juhudi thabiti zinazooonekana bayana!
Mabasi yaendayo kasi yataleta ushindani wa kibiashara hata kama hawatazuia wasafirishaji binafsi, mwisho wa siku watayapunguza magari yao kama si kuyaondoa kabisa barabarani maana kila mtu atahitaji kuwahi kazi zake hawezi kusubiri gari ambalo lina vituo lukuki.
Hapo kwenye Bluu ndo umenidhihilishia una roho ya kwanini, kumbe suala hapa si Reli au mabasi yaendayo kasi bali unaumizwa na umaarufu na utendaji unaokubalika na wengi wa hao mawaziri wawili, chuki zingine ni za kijinga, unajieleza undani wako bila kutambua YAMTOKAYO MTU KINYWANI NDIYO YAUJAZAYO MOYO WAKE!! SHAME ON YOU...
Naona sasa unataka kunisaidia kufikiria.