sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Hatari,hatari kubwa sana kwa serikali,bunge na hata mahakama!Ikiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya viwanda na biashara kwenda kinyume na wajumbe wa kamati na bunge basi hiyo ni hatari kwa usalama wa nchi na mali zake. Kulikuwa na ulazima gani kwa mh.huyu kukubali mwaliko wa bodi ya menejimenti ya TBS kwenda nchini Japan na China wakati kamati ya hesabu za mashirika ya umma ilikwishituhumu TBS kupitia ripoti ya CAG.
Hali kama hii inaweza kuleta mtafaruku mkubwa kwa kamati teule za bunge na bunge lenyewe kutokuaminika mbele ya wananchi.KItendo hiki si kwamba kimelidhalilisha bunge na kamati zake bali pia kimemuondolea rais wetu umakini wa kuwateuwa mawaziri wake bila kuwachunguza.Pia nia aibu kwa chombo cha usalam kinachomsaidi rais na kumshauri aina ya wateule anaotakiwa kuwateua.
Hali imetia doa kwa serikali(power and authourity of appoint) na bunge letu pia.Ni mara nyingi wabunge na wajumbe wa kamati za bunge wameingia kwenye mitego kama hii huku wakijinasibu ni wapambanaji na wenye uchungu na watu wanaofisidi mali za umma.Ndiyo maana nachelea kusema kama mh.Mgimwa naye ameingia kwenye mtego huu basi nchi imekwisha.Kwani ni miongoni mwa watu walionyesha kutopenda kutumiwa kwa maslahi binafsi.
Kinachokera na kusikitisha ni kitendo cha kujaribu kumsafisha bwana Ekelege. Kwa jambo kama hili alilotenda mh huyu na kama kweli ni muumini wa utawala bora basi apime atuachie wizara yetu kabla hajaingiza taifa kwenye janga la uwizi kwa kuwalinda mchwa wasio na huruma na nchi hii.