Jumba la kifahari la Mwenyekiti Mbowe lazua maswali ndani ya Chadema

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika ndani ya Chadema kufuatia baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kuona nyumba ya kifahari anayoishi Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambayo ameijenga hivi karibuni huko Machame.

Sintofahamu hiyo imekuja baada ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kupokea taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe weekend hii aliwaita baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu (Heche, Lema na Msigwa) kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa nyumba hiyo mpya ya Mbowe ambayo ameijenga kwa miezi 3 tu.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu wamehoji Mwenyekiti Mbowe amepata wapi hela za kujenga nyumba ya kisasa ya ghorofa kwa miezi 3 tu, tena wakati ambao shughuli za chama zimekwama kuendelea kwa kisingizio kuwa ruzuku imeisha mpaka watakapoingiziwa tena Disemba 2023.

Hoja yao inaonekana ina mashiku kwa sababu, ndani ya Chadema wenye mamlaka ya kuidhinisha pesa kutolewa (Signatories) ni watatu tu Mwenyekiti Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salim Mwalimu na Mjumbe wa Baraza la Udhamini Mzee Mtei.

Hii inaonesha bado hakuna kuaminiana baina ya Mwenyekiti Mbowe na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ukiwatoa wale wanaokula nao sahani moja (Lema, Msigwa, Heche, na Salim Mwalimu) na wengi wanachojiuliza inawezekanaje Chama kikose hela ya mafuta ya Chopa halafu Mwenyekiti anazindua nyumba yenye thamani ya Milioni 500.

Ndugu zangu tuendelea kufuatilia kwa karibu, ndani ya Chadema kuna Bundi anazengea na muda si mrefu tutaanza kusikia vilio vya kuomboleza kwa sababu najua Tundu Lissu hawezi kukaa na kuyafumbia macho yanayoendelea mle ndani.
 
Hapo ulipomweka Mzee Mtei story yote inakosa mashiko.

Mzee Mtei kwasasa ni mzee sana hata kuota jua anasaidiwa kutoka nje ndio itakuwa kusign Chq.

Story nyingine tafuteni njia bora ya kutunga.
 
Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika ndani ya Chadema kufuatia baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kuona nyumba ya kifahari anayoishi Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambayo ameijenga hivi karibuni huko Machame...
Uongo wa kijinga.
 
Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika ndani ya Chadema kufuatia baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kuona nyumba ya kifahari anayoishi Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambayo ameijenga hivi karibuni huko Machame...

Panganeni kwenye hiyo propaganda, Kila mmoja wenu akileta mnaishia kijichanganya. Kubalianeni nani alete Uzi wa hiyo propaganda kisha wengine msaidie kwenye post.
 
Mbona wabachadema hawaonyeshi kusumbuliwa na hili swala
 
Usidhani Freeman Mbowe Maisha kayaanza jana Bwashee

Wakati John Komba rip Mwenye ghorofa pale tangibovu akiwa mwalimu wa Shule ya Msingi huyo Freeman Mbowe alikuwa Mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania
 
Kwa mjengo huo si Rais wa nchi. Mkimpasha IKULU si atajenga HEKALU.

Mmmmmmm, mwenzangu subiri kidogo, Muda wako bado. Ngoja kwanza Fly over, Mwendokasi na SGR ZIKAMILIKE kwanza. Ndio baadae uje utafune pesa za wananchi.
 
Back
Top Bottom