Kama Lowassa ni Msafi, Nani Mchafu CCM?

Ng'wamapalala

21st June 2015 12:30
#1
JF Gold Member
jfgold.png
Array


Join Date : 9th June 2011
Location : Kijijini Bariadi
Posts : 6,068
Rep Power : 22086386
Likes Received4668
Likes Given3795


[h=2]
icon1.png
Makongoro Nyerere: Edward Lowassa ni muongo, fisadi na alituiba pesa kupitia Richmond[/h]
Wakati akiongea na baadhi ya wanachama wa CCM wa wilaya ya Shinyanga Mjini, Makongoro Nyerere amemshutumu vikali Edward Lowassa na kusema ndiye mmojawapo wa wale walioliingiza hasara taifa kwa kuiba pesa za watanzania kupitia mradi wa Richmond Development Company LLC.

Makongoro amedai hata kama Lowassa aligawana na rafiki zake pesa za Richmond, basi yeye atakuwa alichukua pesa nyingi kuliko rafiki zake.

Makongoro ameenda mbali zaidi na kudai, kundi linaloongozwa na Edward Lowassa ndilo linakisumbua sana chama kutokana na pesa za ufisadi ambazo wanazitumia kuwahonga baadhi ya wananchi, wanachama na wajumbe wa vikao vya CCM.

Makongoro amewaasa wanachama hao kuhakikishwa wanashikamana ili kupambana na kundi hili dogo la watu wenye ukwasi mkubwa ndani ya CCM ambalo limekigeuza chama kuwa pango la wezi na vibaka.

Makongoro alikaririwa akisema, ''Maovu ya wezi na vibaka ndani ya CCM yamekifanya chama kionekane kama ni chama cha mafisadi na wezi, huku heshima ya wanachama wake ikishuka ndani ya jamii''.

''Wanachama wote wa CCM tunaonekana kama ni wezi kwenye jamii kutokana na maovu ya wachache ndani ya chama'' alisema.

Makongoro alimalizia kwa kuwaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu utakaokutana Dodoma tarehe 12-13 Julai kuhakikisha wanawaondoa wezi na vibaka ndani ya CCM, kinyume cha kufanya hivyo watakuwa wamekikabidhi chama kwa wezi na vibaka.

Aliwaambia, Katiba ya CCM imesema Wajumbe wa Mkutano Mkuu ndiyo mabosi wa CCM. Hakuna mwanachama au kiongozi wa CCM iliye juu ya Mamlaka ya Mkutano Mkuu.

Video ya aliyoyasema Makongoro Nyerere inapatiakana hapa,


 
Lowasa amekuja UKAWA sawa,linaweza lisiwe tatizo sana.Nilichokitarajia mimi kukisikia ni Lowasa akifunguka kwa Watanzania

Lowasa aseme ile Richmond ilikuwa ya nani.Anasema alitolewa kafara,je huyo aliyemtoa kafara ili yeye apone ni nani?

Watanzania wana hofu..Wanahofu kumtoa fisi aliye half way kushiba na kumuweka fisi mwenye njaa


Lowasa funguka otherwise wengine tunaendelea kuamini wewe ni mwizi...Haitoshi tu kutuambia twende mahakamani...Ueleze what happened
 
Back
Top Bottom