Kama Kanisa Katoliki ni Kanisa dola, kwanini tusiamini tukio la kutokea Bikira Maria watoto wa Fatima ni la kupangwa?

Mazee hivi unajua maana ya King James Bible?na Bible ambazo sio za king James?hakunaga Bible moja authentic...Bible zote zimeongezwa na kupunguzwa kulingana na wahusika walitaka nini
Kama kungekuwa na uwezekano huo basi biblia zote zisingekuwa na neno sabato.Maana 90% ya wanaoitumia biblia hawaitaki amri ya nne ya kutunza sabato
 
Kwa ujumla ukristu ni mchongo. Mungu wa kweli hawezi kumtoa mwanae kafara, wala hana mtoto, ulikuwa tu mchongo uliochongwa na wenye akili.
 
Yaani, wasabato wao njia ya kujipatia waumini , ni kulipiga mawe kanisa katoliki.

Na ndio maana miaka 50 ijayo inakadiriwa kuwa uislamu itakuwa ndio dini kubwa duniani, nikafanya utafiti, nikagundua kuwa waislamu Wana madhehebu tofauti, lakini sijawai KUONA muislamu wa dhehebu Fulani anasimama na kumtupia mawe muislamu wa dhehebu linguine, na kusema hamia huku,
Wao mtu akibadili Imani nyingine kuja uislamu haijalishi dhehebu gani kwao ni fulaha.

Lakini wakristo kazi kunyang'anyana waumini wao kwa wao,

Sasa wasabato kikundi Cha wahuni kutoka wahuni Kama kina William Miller, Helen G white, Joseph Bates, na Hiram edson , wanajifanya wanaijua Sana, hawajui biblia ni Nini, ilitoka wapi kwa Nini imeandikwa, je iliandikwaje, kipindi inaandikwa taaluma ya kuifadhi maandishi ilikuaje

Kazi yao ni kutafsiri uongo wanaijua kutoka na upeo wao kuwa mdogo na kukosa maalifa ya theology, basi wanaongea wanavyotaka. Wao na waganga wa kienyeji hawana tofauti, tujua mwaka 1847 wahuni wao kina William Miller walisema ndio ujio wa Yesu, na Yesu hakufika. Kazi yao ni kusema kanisa katoliki ni wapinga Kristi,
Wakati wapinga Kristi ni mtu yeyote au Imani yeyote isiyoamini katila Kristo, Kama dini na serikali duniani ni katoliki tu.

Hawajawaona wahindu na dini ya serikali ni Hindu na mungu wao anajulikana mungu ram,
Hawajui Anglican kwa U.K ni dini rasmi ya kiserekali, hawajui Kama uislamu ni sehemu ya dini na serikali pia kwa maadhi ya mataifa ya kiarabu, hawajui Kuhusu budha Asia ya kusini na japani huku, hawajui Imani ya mungu dragoni na inchi ya kuchina,

Ndio maana inapasawa kuwe na sheeia bila kupitia mafunzo ya theology degree na kuendelea hupaswi kuwa kiongozi wa dini katila ukristo, sio kwa kuwa unakua kusoma na kuandika , unakura ugali na maharage unaibuka wakatoliki ni dini ya kuhini ya shetani, hata maana ya ushetani hujui,
Yaani mnakaa kupitia muongozo wa Helen G white Kama muongozo wa kutafsiri bibla.
Kwa hiyo Imani zingine zinazopinga Kristosio Imani za wapinga Kristo, yaani wasabato nyie.

HISTORIA YA WAADVENTIST WASABATO
By binemtonzi s thomas
MAFUNDISHO MAKUU SITA YA KISABATO
Mafundisho yanayomuhusu Mungu
Mafundisho yanayomhusu mwanadamu
Mafundisho yanayohusu kanisa
Mafundisho yanayohusu wokovu wa mwanadamu
Mafundisho yanayohusu Maisha ya kikristo
Mafundisho yanayohusu matukio ya siku za mwisho

JINSI KANISA LA WAADVENTIST LILIVYOJULIKANA
Kanisa la waadventist Wasabato linajulikana kwa jina la Unabii kuwa “kanisa la masalio” [remnant]
Kwa mujibu wao; limesalia kutoka makanisa yaliyoiangusha kweli chini na kuingiza mapokeo [makanisa ya Babeli]
Limesalia katika kutembea kwenye mapito ya zamani ya neno la Mungu (yer 6;16)
Limesalia katika kuubiri ujumbe wa Malaika watatu (ufu 14;6-12)
Limesalia katika utunzaji wa amri za Mungu, likikazia Zaidi amri ya siku ya saba, sabato[kuto20:1-17, ufu 14:12]


CHIMBUKO LA KANISA LA MASALIO
Kwa mujibu wao; kanisa lao limetokana na utimilifu wa unabii wa Math 24:20-30
Watu wa mwanzo walianza kuulinganisha unabii huo na; tetemeko la Lisbon- 1755, Jua kutiwa giza – May 19, 1780, Kuanguka kwa nyota- 1833

UAMUSHO MKUBWA [ GREAT AWAKENING] UF 10:9-10
USA
Vikundi mbalimbali vya uamsho na matengenezo vilianzishwa USA na EU. Kiongozi mkubwa alikuwa ndugu William Miller. Alikuwa, mkatoliki, akaacha ukatoliki akawa mwanajeshi. Baadae akaacha jeshi akarudi kumtumikia Mungu katika kanisa la Baptist.
Kupitia kusoma kwake bible Dan 8:13-14. Aliamini patakatifu ni hapa duniani, ambapo kwa sasa pamechafuliwa na dhambi, kwa hiyo yesu anakuja kupatakasa na kukomesha dhambi.
Utabiri wa majuma sabini kitabu cha Daniel 9;24-27, juu ya Mungu kwa mataifa ya Israel



HESABU YA SIKU 2,300 [UF 10;10]
Alipofanya hesabu ya siku 2,300 za kutakaswa kwa patakatifu, aligundua kuwa siku hizo zinaisha katika tarehe 22, oct, 1844.
Akatangaza msimamo wa Imani yake ya kwamba yesu atakuja kutakasa dunia mwaka 1844. Akasababishwa waUSA wengi kujiandaa kumpokea Yesu tarehe hiyo. Na waamini wengi walitengwa na makanisa yao kwa msimamo wa Imani hiyo.
Hujumbe huo uliwaandaa watu wapatao 50,000 kwa ujio wa Yesu. Na hao walikuwa waadventist wa kwanza lakini hawakuwa wasabato. William Miller alifariki mnamo mwaka 1849, bila kushuhudia kurudi kwa yesu mara ya pili.


KUKATA TAMAA KUKUBWA (THE GREAT DISAPPOINTMENT)
UF 10: 9-10- KITABU KICHUNGU
Yesu hakurudi mwaka 1844, kama ilivyotarajiwa. Wengi wakakata tamaa , na wengine wakarudi katika makanisa yao ya awali
Wachache wakabaki na Imani hiyo.
Miongoni mwa waliobaki alikuwamo Hiram Edson, Joseph Bates, Ellen Harmon, James White, Fredrick Wheeler, na Rachel preston.

KUTIMIZWA KWA UNABII WA UFU 10:11 (UNABII MWINGINE)
Hiram Edson alisema kuwa alionyeshwa katika ndoto, kuwa Yesu anatoka katika chumba cha patakatifu pa kwanza tarehe 22, Oktoba, 1844, na kuingia katika chumba cha patakatifu pa pili kwa ajili ya kuendesha hukumu, na ndipo atakuja kuwachukua watu wake.
According to father titus amigu. Katika njozi yake, aliona hekalu mbingini, mfano wa hekalu duniani. Hekalu hilo lilikuwa na sehemu mbili; patakatifu na patakatifu pa ptakatifu, yaani saw ana ilivyokuwa hekalu la wayahudi. Hivyo hiyo tarehe 22/10 / 1844 ni kwamba kristo alitoka patakatifu na kuingia patakatifu pa patakatifu, na atabaki hadi siku ya kurudi duniani. Humo yesu yupo anafanya hukumu ya upelelezi. Na ni fundiusho la kisabato hata sasa. Ufunuo 21;22, NAMI SIKUONA HEKALU NDANI YAKE, KWA MAANA BWANA MUNGU NI MWENYEZI NA MWANAKONDOO, NDIO HEKALU LAKE.
Njozi ya hiram iliaminisha kuwa kumbe ilikuwa sahihi, tofauti ilikuwa ni tafsiri.





NJOZI YA UTUNZAJI WA SABATO
Kutoka kundi lililoitwa moyo na majibu ya maombi yao.
Kupitia maono yar oho mtakatifu, Mungu akawafunulia utunzaji wa sabato ya siku ya saba, jumamosi.
Takribani watu wapatao 40 ndio waliamua kutunza sabato wakingoja marejeo ya Yesu mara ya pili.
Wafuasi wengi wakaongezeka USA na EU, kuamini fundisho hili. Na kukahitajika viongozi kusimamia kundi hili, na kuimarisha Imani yao kwa kuitofautisha na Imani nyingine.
HEREN HARMON [heren G white], ambaye baadae aliolewa na James white, alisaidia utekelezwaji wa jambo hilo, na kuweka kuwa mfumo.
MAONI YA JOSEPH BATES
Joseph bates Mmarekani alikuwa baharia. Alipstaafu akahamia kuishi Jimbo la Massachusetts, Fair haven. Alisoma maandishi ya Thomas Prebble kuhusu Sabato, alishawishika kuamini sabato ya wayahudi ilikuwa sabato ya kweli ya kuaminiwa na watu wote.
Akaandika kijitabu kinaitwa The seventh Day Sabath, a Perpetual sign., na aliandika vitabu vingine vingi kuhusu sabato.
Alitafsiri kuwa jumapili ni siku ya alama ya mnyama; na siku ya sabato ndio siku ya mhuri wa Mungu kwa watu wake waliowaaminifu (ufu 7:4). Miongoni mwa wafuasi waliomfuata Joseph bates na Ellen harmon, na mme wake James white.



MAONO YA HEREN HARMON [ born 1827]
Alizaliwa Portland na alikuwa mmethodist.na alijiunga na uadventist 1940 na 1942 kwa kusikiliza mafundisho ya William miller.
KWA MUJIBU WAKE; Mungu alimpatia maono yafuatayo;
Kuna utaratibu mbinguni, na Mungu anafurahishwa na juhudi za watu wake za kuanzisha mfumo wa utaratibu kwa ajili ya kazi yake hapa duniani.. “nilionyeshwa kwamba ni lazima kuwe na utaratibu katika kanisa la Mungu; na Mfumo huo unahitajika ili kupeleka mbele ujumbe wa mwisho wa rehema katika ulimwengu. ( 1T uk 191, church heritage uk 41)
NJOZI YA KUTAMBULIKA KWA JINA SDA CHURCH
Mwaka 1860 walikubaliana kuanzishwa kwa jina la dhehebu. Kwa msaada wa Ellen G. White jina la Seventh Day Adventist Church (SDA) lilipitishwa.1T UK 224.
Mwaka 1963, general conference ya kwanza ilikutana na kupitisha rasmi jina la Seventh day Church.
MAONO NA CHUKI ZA BI HELENI WHITE DHIDI YA KANISA KATOLIKI
Bi Helen alidai kwamba alipata maono mengine; ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika hekalu la mbinguni, kwanza kabisa aliingizwa patakatifu na baadae patakatifu pa patakatifu pa patakatifu ambapo aliona amri kumi za Mungu zikiwa ndani ya sanduku la agano.
Bi Ellen White anasema alipong’aza macho yake kwenye sanduku la agano la humo hekaluni, aliona amri ya sabato ikiwa imezungukwa na utukufu nah apo eti akang’amua kwamba amri ya kushika sabato ilikuwa ni kubwa Zaidi.
UDHAIFU WA BI ELLEN WHITE
Aliona hekalu mbinguni, lakini mbingun I hakuna, heakalu
Kwa Ushahidi kuwa Yesu yupo patakatifu pa patakatifu akifanya hukumu ya upelelezi, kama ilivyoaminishwa, Bi heleni hakusema tena kama alivyopelekwa patakatifu pa pakatifu alionana na Yesu.
Bi Ellen White ndie aliewapandikiza wasabato chuki dhidi ya kanisa katoliki.
Katika machapisho ya vitabu vyake; kama vile vita kuu, Afya na raha,na siri ya ushindaji, amelitukana kanisa katoliki na kulituhumu limehusika na maovu mengi, kama vile, kubadilisha siku ya sabato, na kuiondoa amri ya sabato. Wakatoliki ni waabudu sanamu, wakatoliki wanamuabudu bikira maria, wakatoliki wanamuabudu Papa, na kumsema ndio mnyama anaetajwa katika kitabu cha ufunuo 13:1-18, wakatoliki wanafundisha mambo ya kidunia badala ya mambo ya ufalme wa Mungu. Wanashitakiwa kuongeza vitabu kwenye biblia.
UDHAIFU WA WASABATO KATIKA KUISOMA NA KUITAFSIRI BIBLIA
Wasabato wanapoisoma biblia wanaitafsiri kwa kurejea mafundindisho na maandiko ya bi Ellen G White badala ya kuifuata biblia yenyewe inasema nini.
Mbinguni hakuna hekalu; ufunuo 21;22.
Amri kuu kuliko zote ni amri ya upendo na sio amri ya sabato kama bi Ellen G White alivyodai. Mt 22;34-40.
VIELELEZO VYA NEMBO YA KANISA
BIBLIA ILIYOWAZI (2TIM 3;16)
MIALE YA MOTO. Mistari mitatu ya miale ya moto huwakilisha ujumbe wamalaika watatu (ufu 14;1-12)
Msalaba; kanisa huamini kuwa kafara ya kristo ndio kiini cha ukombozi wa mwanadamu
Ramani ya ulimwengu; injiri ya marejeo ya Yesu kristo lazima ihubiriwe katika ulimwengu wote.


KUANZISHWA KANISA LA SDA TANZANIA
Lilianzishwa mwaka 1903, na mjerumani Richard conradi.
 
Hata haya mambo ya kutangazwa mtakatifu ni "mchongo", utakuta mtu yupo motoni ameungua kama mkaa ila katangazwa mtakatifu. Vatican ni serikali na Yesu hakuja kuanzisha serikali za kidunia. Kwa kutumia akili ya kawaida ukatoloki ni "mchongo".
Hata huo moto wenyewe upo basiii???
 
Back
Top Bottom