Kama Kanisa Katoliki ni Kanisa dola, kwanini tusiamini tukio la kutokea Bikira Maria watoto wa Fatima ni la kupangwa?

Mimi ni mkatoliki ila hili tukio la bikira maria kuwatokea watoto wa fatima kule ureno linafikirisha sana.

Kwanza mkuu wa kanisa katoliki yani papa ni Rais wa Vatican pia kama nchi kamili yenye kiti UN. Sasa tukio la kule ureno mwaka 1919 la bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta sio tukio la mchongo? Kwa maslahi mapana ya kanisa katoliki duniani?

Natambua tukio hili lilitokea Portugal na sio Vatican. Pia natambua mkataba wa Mussolini kuitambua Vatican kama nchi pale Roma Italy. Ila pia tutambue serikali zote duniani zina haya matukio ya kupangwa (staged). La fatima nahisi lilipangwa!
...Yaani jambo la Mwaka 1919 linakusumbua Mwaka huu wa 2023, Ndugu yangu ???
Mbona Mambo mengi TU ya kuweza kufikirisha Akili Yako ??
Haya, tufanye kuwa.lilipangwa, So ???
 
Padre Pio naye ni wa mchongo? Lourdes je? Kata ticket uende Portugal ukaangalie vielelezo viko vingi tu. Au vitafute vingine kwenye mitandao.

Kumbuka maneno ya St. Thomas Aquinas... "To the one who has no faith, no explanation is possible and to the one who has faith, no explanation is needed". "Mwenye imani hahitaji maelezo mengi yoyote, kwa asiye na imani hakuna maelezo yoyote yanayoweza kumtosha!"

Kuhoji ni mwanzo mzuri wa imani, Mungu akujalie imani thabiti.

______________________________
 
Povu la nini! Sema ni nani anamfahamu kwa sura bikira Maria hadi aseme katokewa naye?
Kama umesoma au kufuatilia hiyo habari ya Mama Maria kuwatokea hao vijana,usingeuliza swali kama hilo.Ina maana hujui unachokiuliza ila unataka majibu tu na ubishani.
NB:Hayo mambo siyo ya imani yako.Kama ambavyo uzi umeletwa kishari,ni vema ukajishikiza na kupenda kuyajua zaidi yakuhusuyo.
 
Mimi ni mkatoliki ila hili tukio la bikira maria kuwatokea watoto wa fatima kule ureno linafikirisha sana.

Kwanza mkuu wa kanisa katoliki yani papa ni Rais wa Vatican pia kama nchi kamili yenye kiti UN. Sasa tukio la kule ureno mwaka 1919 la bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta sio tukio la mchongo? Kwa maslahi mapana ya kanisa katoliki duniani?

Natambua tukio hili lilitokea Portugal na sio Vatican. Pia natambua mkataba wa Mussolini kuitambua Vatican kama nchi pale Roma Italy. Ila pia tutambue serikali zote duniani zina haya matukio ya kupangwa (staged). La fatima nahisi lilipangwa!
Hili tukio limetokea kwenye community kubwa, lilianza kuwa maarufu mitaani na serikali ya huko ilikuwa haitaki Ukristo kuenea. Serikali ilitumia njia zote kuzuia hizi taarifa na kumuonya paroko wa eneo hilo kulifatilia. Paroko alipowaita watoto kuwahoji aliwaomba wasiendelee kulieneza ili Kanisa lisifungiwe na serikali!

Wakati Paroko na wale watoto wakiendelea na mahojiano wakavamiwa na serikali wote wakakamatwa na Kanisa likafungwa kwa amri ya serikali. Wale watoto wakapelekwa gerezani kuwa interogated na kutishwa kuuawa ila waseme walizusha kutokewa na Bikira Maria!

Moja ya kutaniko la Bikira Maria na wale watoto walimuomba afanye muujiza ili watu waamini. Bikira Maria akawahaidi siku na muda wa kukutana ili afanye huo muujiza. Baada ya shinikizo la wananchi wale watoto wakaachiwa na ikafika hiyo siku!

Siku ya tukio walikusanyika watu zaidi ya 70 elfu kushuhudia vikiwemo vyombo vya habari maarufu huko, viongozi wa serikali ambao walienda ili muujiza usipotokea kama walivyotarajia waongee na wananchi kuacha imani potofu.

Ghafla eneo hilo ilinyesha mvua kubwa, muda ukawa unaenda, watu wakaanza kubeza na wengine kuanza kuamini wale watoto wazushi! Ghafla mvua ikakata na jua kuwaka! , Eneo zima likakauka na watu wote walionyeshewa kukauka kama mvua haikunyesha!

Hapo kidogo watu wakashtuka kinachotokea. Wale watoto pekee wakamuona Bikira Maria na kuanza kuongea nae huku wengine hawaoni wala kuelewa. Baada ya mazungumzo wale watoto waliomba tena muujiza ili waaminike. Ndipo wakaona Bikira Maria akinyoosha mkono kuelekea kwenye jua na ghafla jua huku likizunguka likaanza kushuka kwa kasi duniani!

Kile kitendo kilishuhudiwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa serikali! Watu wote wakaanza kukimbia wengine wakipiga magoti wakifikiri ni mwisho wa dunia. Then lile jua likaanza kurudi mahala pake huku Bikira Maria akitoweka pia. Ndipo tukio hili " Sun miracle" , "Sun dance" likawa kubwa dunia nzima na kuripotiwa na vyombo vya habari ( Picha chache zilizopigwa eneo la tukio zipo google).

Prophecy zote alizosema Bikira Maria kwa wale watoto zilitokea, ikiwemo vita ya dunia kufikia ukomo, Papa kupigwa risasi, lakini pia Papa na maaskofu kutakiwa kufanya ibada maalum kwaajili ya Urusi otherwise huko mbele yatatokea machafuko makubwa ( Hili hakuna Papa aliyetimiza). Yapo mengine yaliyosemwa ila inasemekana Kanisa limegoma kutangazwa ikiwemo kutokea Papa atayekuwa mpinga Kristo.

Hili tukio lilitokea mwaka 1917 lakini Kanisa lilikuja ku approve ni muujiza mwaka 1930.
 
Mimi ni mkatoliki ila hili tukio la bikira maria kuwatokea watoto wa fatima kule ureno linafikirisha sana.

Kwanza mkuu wa kanisa katoliki yani papa ni Rais wa Vatican pia kama nchi kamili yenye kiti UN. Sasa tukio la kule ureno mwaka 1919 la bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta sio tukio la mchongo? Kwa maslahi mapana ya kanisa katoliki duniani?

Natambua tukio hili lilitokea Portugal na sio Vatican. Pia natambua mkataba wa Mussolini kuitambua Vatican kama nchi pale Roma Italy. Ila pia tutambue serikali zote duniani zina haya matukio ya kupangwa (staged). La fatima nahisi lilipangwa!
Amini unachotaka kuamini.
 
Kama umesoma au kufuatilia hiyo habari ya Mama Maria kuwatokea hao vijana,usingeuliza swali kama hilo.Ina maana hujui unachokiuliza ila unataka majibu tu na ubishani.
NB:Hayo mambo siyo ya imani yako.Kama ambavyo uzi umeletwa kishari,ni vema ukajishikiza na kupenda kuyajua zaidi yakuhusuyo.
Labda nikuulize ndugu yangu,inaonekana unauelewa mzuri kwenye mambo ya ukatoriki,Bikira Maria alikufa bila kuwa na mume na watoto yaani hakuzaa,au alizaa?
 
Mazee hivi unajua maana ya King James Bible?na Bible ambazo sio za king James?hakunaga Bible moja authentic...Bible zote zimeongezwa na kupunguzwa kulingana na wahusika walitaka nini
Safi, hivi ndivyo ninavyopenda... Twende kwa hoja! King James version ni moja ya tafsiri tu ambazo zinatofautiana na nyingine kwenye maana ya baadhi ya maneno. Je, ukweli unaweza potoshwa? Ndio inawezekana, hakuna sehemu ya maisha ya Binadamu ambayo shetani hajaingia. Ila sasa leta hoja ya kwamba jambo flani kwenye Biblia ni uongo ndio tuanzie hapo kujadili. Hakuna kitu kwenye Bible kinaweza pingwa kwa hoja kuwa ni uongo. Natural theology and philosophy can easily prove that.
 
Mimi naamini kipindi hicho kulikuwa na teknolojia ya kupiga picha?sasa huyo bikira Maria alikuwa mwafrika,mchina,Mzungu,Muarabu,au mreno?au alikuwa anafanana na yale masanamu yake yaliyokuwepo kabla yake hajatokea?
 
Yesu

Yesu alikuwa na wadogo zake?ina maana Yosefu alizaa naye?
Unapouliza wadogo zake unamaanisha nini?Wa kuzaliwa na mama mmoja au watoto wa ndugu zake wengine?Katika Biblia sijaona sehemu inaeleza hivyo kwamba Yesu alikuwa na ndugu wa tumbo moja.
NB:Unaruhusiwa kuleta habari za kuzusha ili tufurahi.
 
Mimi naamini kipindi hicho kulikuwa na teknolojia ya kupiga picha?sasa huyo bikira Maria alikuwa mwafrika,mchina,Mzungu,Muarabu,au mreno?au alikuwa anafanana na yale masanamu yake yaliyokuwepo kabla yake hajatokea?
Hawawezi kukujibu zaidi ya kukutolea povu tu,hakuna mtu anayejua Yesu au Mama yake wakoje hivyo mtu anapodai ametokewa anashangaza sana maana hata kama ni imani basi ni ya ajabu!
 
Back
Top Bottom