Tukio la Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kudaiwa kumlawiti Mwanafunzi, Padri asimulia kilichotokea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi - Sinza, Padre Josephat Celestine Muhoza amesema kuwa Kanisa lao lina taarifa kuhusu tuhuma za mlinzi wao mmoja anayetambulika kwa jina la Baraka kudaiwa kuhusika na tukio la kumlawiti Mwanafunzi wa darasa la Tano mwenye umri wa miaka 14 anayesoma moja ya Shule iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia madai hayo amesema kuwa alipata taarifa kutoka kwa watendaji wa kanisa hilo kuwa mlinzi anadaiwa kumbaka Mtoto ambaye ni Mwanakwaya katika Parokia hiyo.

Amesema “Mimi sikuwepo (siku ya tukio) nilienda Jumuiya nilipofika mhasibu akanitumia meseji akinifahamisha kuwa mlinzi anatuhumiwa kumlawiti mtoto, nikamuuliza imetokea wapi, akaniambia kwenye vyoo vya Kanisa.

“Akasema inadaiwa mlinzi aliingia huko na kumfanyia kitendo hicho, nikaona hii ni habari kubwa na mbaya kwa kuwa hapa ni Kanisani na aliyefanya ni mlinzi wetu, nilichofanya cha kwanza ni kupigia kampuni yake ya ulinzi kwakuwa sisi tunamfahamu yeye kupitia kampuni, kwahiyo nikawapigia nikawapigia na kuwasimulia tukio.”

Amesema kuwa kampuni hiyo ya ulinzi ya Multi-Lion Security Limited haikutoa ushirikiano wa haraka, amedai baada kuona hivyo aliamua kutoa taarifa Polisi ambao walifika kanisani hapo kufuatilia suala hilo.

Amesema baada ya askari Polisi kufika waliondoka na mtuhumiwa pamoja na mtoto ambaye alidaiwa kufanyiwa kitendo hicho, pamoja na Mama yake mzazi kwa ajili ya hatua za kuchukuliwa maelezo.

"Lakini kabla ya askari kuja nilimuita huyo mlinzi Baraka nikamuuliza unahusika na madai haya, akasema hajafanya kitendo hicho nikamwambia unafahamu ukubwa wa hiki unachotuhumiwa nacho? akasema ndio lakini akasema hajatenda tukio hilo," amesema Padri huyo.

Amesema alipozungumza na Mama mzazi wa Mtoto huyo alisema alifika kanisani kutokana na kuona mtoto wake amechelewa kurejea nyumbani tofauti na ilivyozoeleka, anasema Mama alidai alimkuta mwanae analia na akamwambia amefanyiwa kitendo kiovu na mlinzi.

Pia amesema mfanyakazi wa mazingira kwenye parokia hiyo, alitoa taarifa kuwa akiwa anaenda kubadilisha nguo chooni alisikia sauti ya mtoto 'unaniumiza unaniumiza'.

Amesema kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo alilazimika kutafuta usaidizi kwa kukimbilia nje kumuita sister ambaye anahudumu kwenye parokia hiyo, lakini baada ya kushindwa kumpata sister aliwapata wengine lakini walipoenda kuangalia hawakuona mhusika ndani vyoo hivyo.

Amesema kwa mujibu wa mkataba wao na kampuni husika ya ulinzi unaelekeza watawajibika juu ya mlinzi wao ikitokea ametenda makosa mbalimbali yanayokiuka utaratibu na kinidhamu na kisheria.

Amesema baada ya kufikisha taarifa hizo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi hajui rasmi hatua nyingine zinazoendelea baada ya hapo isipokuwa amekuwa akisikia yanayoendelea ikiwemo mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana.

Kuhusiana na mtoto huyo amesema amekuwa akiimba kwaya kanisani na kuwa anawafahamu pamoja na Mama yake ambao ni Wanaparokia.

Pia soma:
- Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza

- Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie
 
Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi - Sinza, Padre Jophat Selestine Muhoza amesema kuwa Kanisa lao lina taarifa kuhusu tuhuma za mlinzi wao mmoja anayetambulika kwa jina la Baraka kudaiwa kuhusika na tukio la kumlawiti Mwanafunzi wa darasa la Tano mwenye umri wa miaka 14 anayesoma moja ya Shule iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia madai hayo amesema kuwa alipata taarifa kutoka kwa watendaji wa kanisa hilo kuwa mlinzi anadaiwa kumbaka Mtoto ambaye ni Mwanakwaya katika Parokia hiyo.

Amesema “Mimi sikuwepo (siku ya tukio) nilienda Jumuiya nilipofika mhasibu akanitumia meseji akinifahamisha kuwa mlinzi anatuhumiwa kumlawiti mtoto, nikamuuliza imetokea wapi, akaniambia kwenye vyoo vya Kanisa.

“Akasema inadaiwa mlinzi aliingia huko na kumfanyia kitendo hicho, nikaona hii ni habari kubwa na mbaya kwa kuwa hapa ni Kanisani na aliyefanya ni mlinzi wetu, nilichofanya cha kwanza ni kupigia kampuni yake ya ulinzi kwakuwa sisi tunamfahamu yeye kupitia kampuni, kwahiyo nikawapigia nikawapigia na kuwasimulia tukio.”

Amesema kuwa kampuni hiyo ya ulinzi ya Multi-Lion Security Limited haikutoa ushirikiano wa haraka, amedai baada kuona hivyo aliamua kutoa taarifa Polisi ambao walifika kanisani hapo kufuatilia suala hilo.

Amesema baada ya askari Polisi kufika waliondoka na mtuhumiwa pamoja na mtoto ambaye alidaiwa kufanyiwa kitendo hicho, pamoja na Mama yake mzazi kwa ajili ya hatua za kuchukuliwa maelezo.

"Lakini kabla ya askari kuja nilimuita huyo mlinzi Baraka nikamuuliza unahusika na madai haya, akasema hajafanya kitendo hicho nikamwambia unafahamu ukubwa wa hiki unachotuhumiwa nacho? akasema ndio lakini akasema hajatenda tukio hilo," amesema Padri huyo.

Amesema alipozungumza na Mama mzazi wa Mtoto huyo alisema alifika kanisani kutokana na kuona mtoto wake amechelewa kurejea nyumbani tofauti na ilivyozoeleka, anasema Mama alidai alimkuta mwanae analia na akamwambia amefanyiwa kitendo kiovu na mlinzi.

Pia amesema mfanyakazi wa mazingira kwenye parokia hiyo, alitoa taarifa kuwa akiwa anaenda kubadilisha nguo chooni alisikia sauti ya mtoto 'unaniumiza unaniumiza'.

Amesema kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo alilazimika kutafuta usaidizi kwa kukimbilia nje kumuita sister ambaye anahudumu kwenye parokia hiyo, lakini baada ya kushindwa kumpata sister aliwapata wengine lakini walipoenda kuangalia hawakuona mhusika ndani vyoo hivyo.

Amesema kwa mujibu wa mkataba wao na kampuni husika ya ulinzi unaelekeza watawajibika juu ya mlinzi wao ikitokea ametenda makosa mbalimbali yanayokiuka utaratibu na kinidhamu na kisheria.

Amesema baada ya kufikisha taarifa hizo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi hajui rasmi hatua nyingine zinazoendelea baada ya hapo isipokuwa amekuwa akisikia yanayoendelea ikiwemo mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana.

Kuhusiana na mtoto huyo amesema amekuwa akiimba kwaya kanisani na kuwa anawafahamu pamoja na Mama yake ambao ni Wanaparokia.

Pia soma:
- Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza

- Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie
Kanisa limeshanajisiwa hilo... Lifungwe
 
Ndani ya Kanisa hili, hii michezo kwa sasa ni kitu cha kawaida sana.

Pariko aweke msimamo wake juu ya ushauri wa papa, kuwabari au kutobariki.

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi unamzuiaje Mwanaume Rijali, anayekula vizuri haswa KUOA?
Martin Luther alikuwa Padri lakini akaona asiwe mnafiki mbele za Mungu

Mungu alimfanya Mwanaume asimamishe na kutoa mbegu na akasema::

" Zaeni mkaijaze Nchi"

Eti leo Binadamu wanawazuia wanaume kuoa Wanawake...Ndio sababu Ushoga na Ulawiti haviishi kwa hawa Mapadri
 
Mimi cha kunishangaza aliepiga sim sio padre na pia yule kijana wa usafi baada ya kusikia saufi chooni mtoto akiwa analalamika unaniumizawa. Akamfuata katekista wakamfuatilie kasema mda wangu wa kazi umeisha. ..... Kitendo cha mlinzi kuoga choo cha watoto na kufanya kitendo hicho ni cha kushangwa sana na pia hao watoto wenzao, watuatiliwe jamani.
 
Back
Top Bottom