Kama Kanisa Katoliki ni Kanisa dola, kwanini tusiamini tukio la kutokea Bikira Maria watoto wa Fatima ni la kupangwa?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,456
31,024
Mimi ni mkatoliki ila hili tukio la bikira maria kuwatokea watoto wa fatima kule ureno linafikirisha sana.

Kwanza mkuu wa kanisa katoliki yani papa ni Rais wa Vatican pia kama nchi kamili yenye kiti UN. Sasa tukio la kule ureno mwaka 1919 la bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta sio tukio la mchongo? Kwa maslahi mapana ya kanisa katoliki duniani?

Natambua tukio hili lilitokea Portugal na sio Vatican. Pia natambua mkataba wa Mussolini kuitambua Vatican kama nchi pale Roma Italy. Ila pia tutambue serikali zote duniani zina haya matukio ya kupangwa (staged). La fatima nahisi lilipangwa!
 
Kumekucha
FB_IMG_1683107648424.jpg
 
Padre Pio naye ni wa mchongo? Lourdes je? Kata ticket uende Portugal ukaangalie vielelezo viko vingi tu. Au vitafute vingine kwenye mitandao.

Kumbuka maneno ya St. Thomas Aquinas... "To the one who has no faith, no explanation is possible and to the one who has faith, no explanation is needed". "Mwenye imani hahitaji maelezo mengi yoyote, kwa asiye na imani hakuna maelezo yoyote yanayoweza kumtosha!"

Kuhoji ni mwanzo mzuri wa imani, Mungu akujalie imani thabiti.
 
Mimi ni mkatoliki ila hili tukio la bikira maria kuwatokea watoto wa fatima kule ureno linafikirisha sana.

Kwanza mkuu wa kanisa katoliki yani papa ni Rais wa Vatican pia kama nchi kamili yenye kiti UN. Sasa tukio la kule ureno mwaka 1919 la bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta sio tukio la mchongo? Kwa maslahi mapana ya kanisa katoliki duniani?

Natambua tukio hili lilitokea Portugal na sio Vatican. Pia natambua mkataba wa Mussolini kuitambua Vatican kama nchi pale Roma Italy. Ila pia tutambue serikali zote duniani zina haya matukio ya kupangwa (staged). La fatima nahisi lilipangwa!
Kwani kuna mtu amekuzuia kuamini unavyoamini?
 
Hata haya mambo ya kutangazwa mtakatifu ni "mchongo", utakuta mtu yupo motoni ameungua kama mkaa ila katangazwa mtakatifu. Vatican ni serikali na Yesu hakuja kuanzisha serikali za kidunia. Kwa kutumia akili ya kawaida ukatoloki ni "mchongo".
 
Back
Top Bottom