Kama hamtojali naomba Ufafanuzi wa haraka juu ya haya mambo Matatu tu ya Umuhimu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
1. Je, ukiwa na Akaunti ya Benki fulani ila hukuitumia kwa miaka kati ya 5 hadi 10 ukitaka Kuendelea nayo inawezekana (japo najua itakuwa Imeshafungwa) Kuihuisha au Kuiamsha (Activate) au uachane na haya yote na Ufungue tu Akaunti mpya?

Tafadhali Wataalamu / Wabobezi wa Benki GENTAMYCINE naomba Msaada wenu wa Kiufafanuzi wa haraka na Nitawashukuruni.

2. Je, ukiwa na Akaunti kutoka Benki zetu za hapa Tanzania (Local kama NBC na CRDB) unaweza kuzitumia kwa Kuingiziwa Pesa zako (Mshahara) ukiwa unafanya Kazi nje ya Tanzania na ukazitoa ukiwa huko huko?

3. Naomba kujua Nchi (hasa za hapa Afrika Mashariki) ambazo Benki hizi Mbili za NBC na CRDB zina Matawi yake huko na unaweza bado ukaendelea Kuzitumia hata ukiwa huko huko Kimajukumu.

Natanguliza Shukran kwa Ufafanuzi.
 
Account ikiwa domant then siku ukaamua iendelee kuitumia kinachofanyika wanakata monthly charges zote za miezi yote uliyo Dodge
Si sio afya Kwa kuirudia Tena kama ulidodge miaka 5
Let say monthly charges 2700×5×12
So utaona gharam ni kiasi gan

Kuhusu kulipwa mshahara bank A iliyopo Tanzania na ww inafanya kazi nchi ya ughaibuni nayo pia ni gharam kubwa kwako kui endesha hiyo account at the same time kui maintain

Chukulia mfano unaishi south Africa currency Yao Rand na unalipwa Kwa Rand then account Yako huk nyumbni ni Tsh

So gharama zitakiwa kubwa na utashidwa kuzimud

Then hakuna campun itakubali kulipa amount kwenda nchi nyingine coz utakuwa unakimbia Payee

Na isitoshe campuni nyingi zinalipa mishahara Kwa internet banking system so kwao ni changamoto
 
1. Kwa huo muda wa miaka mitano na zaidi, Bora ufungue akaunti nyingine tu.

2. Benki zetu hazipo nchi nyingi za Afrika Mashariki. Nachofaham KCB na Equity ndio wamejitahidi kuwepo Rwanda, Burundi, Sudan, Uganda, Kenya, na Tanzania.

3. Ikiwa unalipwa pesa ya nchi husika, ni rahisi zaidi ukiwa na akaunti ya hiyo sarafu. Mfano kama upo Kenya, kuwa na akaunti ya KSH.

Mambo ya akaunti ipo nchi Gani na wanalipaje itategemea na sera na aina ya mwajiri.
 
Back
Top Bottom