Mo Dewji nakupasulia huu Ukweli ambao GSM wa Yanga SC nae naomba auchukue juu ya Uwekezaji Simba na Yanga

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,030
GENTAMIYCINE nilidhani ukiwa Tajiri basi hata na Uwezo wako wa Kufikiri nao unakuwa ni wa Kitajiri ( nikimaanisha ni mkubwa ) kumbe hali ni tofauti kabisa.

Matajiri Mohammed Ghullum Dewji wa Simba SC na Gharib Said Mohammed wa Yanga SC kwa Historia Kubwa ya Simba na Yanga hasa katika Siasa za Tanzania zilizo chini ya Chama Tawala CCM sahauni kupewa 100% ya Umiliki wa Vilabu hivi Viwili.

Mohammed Ghullum Dewji ( Mo Dewji ) unataka Taasisi za Serikali zifanye haraka na kukupa Wewe 100% ya Umiliki wa Simba SC? Unachekesha kweli kweli Tajiri Wewe unayependa Kukurupuka pindi tu Ukivurugwa Kichwa chako.

Yaani unataka Vyombo vya Serikali vihalalishe 100% Umiliki wako wa Klabu ya Simba ili uweze kuwa na Ushawishi mkubwa kwa Wapenzi, Mashabiki na Wanachama ambao ni Wengi kuliko hata Wanachama wa CCM wapatao Milioni 8 hadi 10 kiasi kwamba huko mbeleni nawe ukiamua Kugombea Urais au ukitumika na Chama cha Upinzani basi uweze kutumia Ushawishi wako mkubwa kwa wana Simba SC na uwaambie wasiipigie Kura CCM na Wawapigie Wapinzani kisha CCM ing'oke mazima Madarakani?

Hivi Mo Dewji unataka kuniambia hili huliui au? Na kama hulijui basi naamini sasa kuwa Mwenyezi Mungu huwa hakupi Vyote na kwamba kakupa Utajiri mkubwa ulionao na kakunyima Akili ila kanipa GENTAMIYCINE Utajiri mkubwa wa Akili ila kaninyima Fedha kama zako.

Mo Dewji wa Simba SC na GSM wa Yanga SC leo hii GENTAMIYCINE nawahakikishieni hapa hapa JamiiForums kuwa Umiliki ambao mtapewa juu ya hivi Vilabu utakuwa ni wa 60% tu ila siyo wa 100% kama utakavyo Mo Dewji na Uotavyo nawe pia GSM kwa Yanga SC.

Mo Dewji ili uamini hiki ninachoandika hapa kuwa Vilabu hivi Viwili vikongwe na vikubwa nchini Tanzania ni Mali za Kudumu za CCM ni kwamba ndani ya Klabu ya Simba SC umechomekewa TISS Agents Watatu ( nawahifadhi Kimaadili ) huku huko Yanga SC nako pia nawe GSM nakuambia katika Uongozi wako wa sasa kuna TISS Agents Wanne ( nawahifadhi Kimaadili ) na Wote hawa wamekuwa penetrated huko ili Kuwaueni Wawekezaji na Matajiri kama nyie na kama ni Faida Kwao Serikali na Chama Tawala au ni Tishio Kwao ili wawakabili upesi.

Mo Dewji au nawe unataka sasa Kutulazimisha akina GENTAMIYCINE tufunguke hapa sababu Kuu zilizokufanya sasa Makazi yako mengi yawe huko UAE na Ulaya na ukwepe sana Kukaa nchini Tanzania kwa muda mrefu hasa kwa Awamu hii ya Sita ya Mama tofauti ulivyokuwa ukitamba katika Awamu ya Tano ya Hayati? Tafadhali usitulazimishe tukasema hapa ambayo yanatakiwa kuwa ni ya SIRI tu kwa sasa sawa?

Halafu ulichokiandika leo Mtandaoni Kwako ni kama vile ni Kutusanifu na hata Kutudhalilisha wana Simba SC wote kwani unataka upewe 100% ya Umiliki wa Simba SC wakati hadi leo hii hata hiyo Shilingi Bilioni 20 unayosema Umewekeza Simba SC hainokekanj kuanzia Benki zote wala katika Vitabu vya Wahasibu wa Simba SC ( kwa Lugha nyepesi ni kwamba Umetudanganya ) na hujaiweka hiyo Fedha ila badala yake Wewe na Familia yako ndiyo mnafaidika na Timu ya Simba SC na hasa Nembo yake na Mtaji wako mkubwa wa Sisi Mashabiki wa Simba SC ambao tunakupa Ushirikiano mkubwa sana wa Kununua na Kutumia Bidhaa zako.

Mo Dewji kwa Maandalizi ya Simba SC yetu sasa kuelekea Ligi Kuu ijayo ya NBC, Michuano ya Super Cup, Usajili mzuri unaoendelea na Klabu Bingwa Afrika ijayo Mimi GENTAMIYCINE sitaki nianze Kukusiliba ( Kukukosoa ) nisije Kuharibu na Kukuvunja Moyo kwa Uwekezaji wako mkubwa ila nawe pia nakuomba acha kupenda Kukurupuka, Kutuvuruga wana Simba SC na kila mara kutaka kutuweka Roho Juu utadhani tuna Mgonjwa aliyeko ICU Muhimbili National Hospital ambaye anataka Kukata Roho ila Madaktari bado wanapambania Uhai wake

Na kwa Taarifa yako Mo Dewji wakati ukijidanganya kuwa Sisi wana Simba SC bila Wewe Simba SC yetu haiendi unajidanganya mno kwani ukimtoa Tajiri mkubwa Tanzania Mzee Bakhressa anayeitaka Simba SC kwa Mtajj wa Shilingi Bilioni 50 yuko Tajiri Mwingine wa Kichina ambaye yuko tayari muda Wowote ule Kuwekeza Simba SC kwa Mtaji wa Shilingi Bilioni 80 na najua huyu Mchina ulishapewa Taarifa zake na Chawa zako Wakuu Murtaza Mangungu na Salim Abdallah Mhene 'Try Again' ila umeamua tu Kujizima Data ( Kujitoa Akili ) kwamba hujui.

Mo Dewji ili ukiamini hiki nilichokuandikja na Kukufafanulia hapa kuhusu Vilabu vya Simba na Yanga kuwa ni Mali za CCM na Serikali na kwamba kamwe hutopewa 100% Umiliki wake hebu nenda Kawekeze zako Ihefu FC au Gwambina FC GENTAMIYCINE nakuhakikishia ukiomba hata Kesho Umiliki wa Jumla ( 100% ) wa Klabu hizi utaruhusiwa Siku hiyo hiyo kwakuwa ni Vilabu vya Kawaida, Vichanga na havina Historia Kubwa, Pana na Tukuka ya Ukombozi na Siasa za muda mrefu za nchini Tanzania kama zilivyo Simba na Yanga ambazo ni Mtaji mkubwa wa Chama Tawala CCM na Serikali katika Ushawishi wa Kimaendeleo na ule wa Kipropaganda.

Ni matumaini yangu makubwa kabisa GENTAMIYCINE kuwa nyie Matajiri Wawili Mo Dewji wa Simba SC na Wewe GSM wa Yanga SC hii Elimu yangu Kubwa niliyowapa hapa na huu Ufafanuzi wangu Kuntu ( wa Kina ) utawasaidieni na Siku zingine ( hasa Wewe wa Kulialia Mo Dewji ) utabadilika na kuelewa kuwa Serikali na CCM zina Mkono mkubwa ndani ya Simba na Yanga kuliko Fedha zako ulizonazo.

Genius la Kizanaki, Kimakuwa na Kitutsi GENTAMIYCINE "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" limemaliza kutema Madini yake kwa Tajiri wa Kulialia Mo Dewji na Tajiri Mvumilivu GSM.
 
Kumbe malalamiko yote yale kisa kanyimwa 100%

Mo nilidhani ana akili lakini kama ni hivi basi nae ni ling'weng'we 😂 😂 😂

Nilikuwaga namchora sana najiuliza hivi huyu anatuoanaje, kisa kasoma huko iST ndo anatuona hatuna elimu ? kile kipindi 2018 alikuwa bizi kwenye press anasema hizo bilion 20 angeweza kununua timu daraja la tatu ufaransa ila kaamua tu kuweka nia hapa Simba, anaongea kirahisi sana utadhani hatuijui nguvu ya hizi timu mbili ni kubwa sana hasa ukizitumia kwenye biashara zako hapa nchini, imefikia kipindi hata hizi energy drinks mtu anachagua kulingana na timu yake na sio ladha ama bei.
 
Amegundua baada ya ligi kuisha mmeanza kunenepa😁😁😁
Anataka yeye ndio awe anabembelezwa kutoa pesa mambo yapo tofauti kwa sasa, anahofia sana timu zikianza kupata pesa zaidi hawata mnyenyekea, saizi yupo desperate kuwahi mapema kabla pesa nyingi hazijaanza kuwatia kiburi zaidi simba,

Timu hizi kwa sasa zinapata dili nono za sponsorship, pesa za caf, n.k.

Kwa sasa ili umiliki asilimia 50 ya hizi timu weka walau 60 Billion na hii ni minimum, mpira wa hapa kwetu unakuwa kwa kasi mno kwenye vilabu hivi kuingiza mkwanja, kwa kasi ya sasa ya makampuni kuweka mizigo kwenye timu hizi ili kupenya zaidi kwenye masoko, natabiri 2025 kila timu za hawa watani zitakuwa zinaingiz bilioni 10 kila mwaka kwa mambo ya sponsors tu, 2025 hapo tutaanza kushuhudia wachezaji wanaletwa hapa wanakunja milioni 50.
 
Kama hizo timu ni mali za CCM/serikali sasa kwa nini hao wamiliki wajifiche? Huo ndio uswahili Mo hautaki . Klabu zisipokuwa na wadhamini/wawekezaji zinapitia njaa Kali halafu hao unaosema ni wamiliki hawatoi hata mia. Sasa hiyo historia wanayoimiliki Kwa hizi timu Kwa nini wasiibadilishe iwe kwenye asilimia na sio kujificha ficha.

Sio kila mwekezaji wa simba na Yanga lazima awe mtanzania, sasa Kwa nini muwazie mtaji wa kisiasa tu kwa hizi timu, kama sio uswahili ni nini?
Kwa andiko lako hili Dangote akisoma kama alikuwa anataka kuwekeza Simba na yanga atasitisha, sababu ni kwamba hakuna uwazi maana hiyo serikali/chama unaosema wanamiliki Simba na yanga kwenye katiba za klabu hawajatajwa popote.
 
Boss,dangote tajiri number 1 africa,muwekezaji mkubwa,unadhani atawekeza simba au yanga bila kujua historia ya timu,tamaduni zake??..kama mimi tu darasa la 7 najua na naona hizi timu zinatumika kisiasa,ndio dangote asijue?@mandunga
 
Kumbe malalamiko yote yale kisa kanyimwa 100%

Mo nilidhani ana akili lakini kama ni hivi basi nae ni ling'weng'we 😂 😂 😂

Nilikuwaga namchora sana najiuliza hivi huyu anatuoanaje, kisa kasoma huko iST ndo anatuona hatuna elimu ? kile kipindi 2018 alikuwa bizi kwenye press anasema hizo bilion 20 angeweza kununua timu daraja la tatu ufaransa ila kaamua tu kuweka nia hapa Simba, anaongea kirahisi sana utadhani hatuijui nguvu ya hizi timu mbili ni kubwa sana hasa ukizitumia kwenye biashara zako hapa nchini, imefikia kipindi hata hizi energy drinks mtu anachagua kulingana na timu yake na sio ladha ama bei.
Sahihi kabisa mkuu
 
"Genius la Kizanaki, Kimakuwa na Kitutsi GENTAMIYCINE "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" limemaliza kutema Madini yake kwa Tajiri wa Kulialia Mo Dewji na Tajiri Mvumilivu GSM."
 
Boss,dangote tajiri number 1 africa,muwekezaji mkubwa,unadhani atawekeza simba au yanga bila kujua historia ya timu,tamaduni zake??..kama mimi tu darasa la 7 najua na naona hizi timu zinatumika kisiasa,ndio dangote asijue?@mandunga
Wengine wanaweza wasijue utajiri sio shule wananwatu wao huwatumia kufanya analysis

Ila hili sakata la simba na yanga kuachiana kubeba makombe huwa inanipa wasiwasi kuna siasa ndani yake

Yani akibeba mwenzake 4yrs au 5yrs unaona na pacha wake anaachwa naye atabeba kwa miaka ayliyobeba mwenzake
 
Boss,dangote tajiri number 1 africa,muwekezaji mkubwa,unadhani atawekeza simba au yanga bila kujua historia ya timu,tamaduni zake??..kama mimi tu darasa la 7 najua na naona hizi timu zinatumika kisiasa,ndio dangote asijue?@mandunga
Ndio maana nikasema huo ni uswahili na hakuna mwekezaji ataweka hela zake kwenye uswahili sababu huko kutumika na kumilikiwa na wanasiasa hakupo wazi.
 
Back
Top Bottom